Mazishi ya wanapinduzi wa Nyamongo, TARIME

Watanzania,
Kuweni na kili hata kidogo za kufikiri vityu kabla hamjaandika upuuzi kama huu.
Hivi ktk akili zenu mnaweza kunambia tukio lolote hapa duniani ambalo watu zaidi ya 800 hadi 1,000 waliweza kuvamia sehemu ili wakaibe?.. Huu wizi gani kama sii kukosa sababu za maana ktk kujenga hoja...

Kisha ebu twambieni wana Mapinduzi huwa na alama gani? na lini haswa mtaondokana na hizi akili za kitumwa kiasi kwamba shirika la Nje Barricks mnalibeba kwa mabaya mengi walokwisha wafanyika wananchi iwe Bulyanhulu au Tarime ati kwa sababu ya ushabiki wa chama.. Hii akili kweli halafu nyie wenyewe wepesi kudai nchi yetu sio maskini na mkiorodhesha madini tulonayo kama sababu. leo wametokea watu wakasema - Hapana, basi wameisha kuwa maadui zenu kwa sababu chama cha Chadema kinawakilisha madai ya wafiwa.

Mbona hamkusema haya wakati Tundu Lissu alipokuwa akiwawakilisha wananchi wa Bulyanhulu na kama sikosei akatiwa ndani na kutushiwa kunyang'anywa liseni yake? Yameishia wapi ya Bulyanhulu ambapo leo tunapokea ruzuku ya asilimia 1.1 toka mauzo ambayo leo hii dhahabu ni chumi bora kuliko hata mafuta!

Acheni wakuu zangu kushabikia vitu pasipo kufikiria na hawa jamaa zetu wamekufa mashujaa kwa sababu sisi sote hapa ni MInafiki, woga na wenye kuitikia ewallah bwana kama watumwa wa kimawazo. Hakika kama kuna mijinga duniani basi Tanzania tumezidi na ndio maana tunatawaliwa na tutazidi kutawaliwa kitumwa kwa sababu ya khanga na Tshirt...

Mkuu Mkandara, mimi sishabikii haya mauaji hata kidogo lakini najiuliza, wakati sisi tunapigwa na kuuliwa na kufanyiwa vitendo kadhaa vya kudhalilishwa na Majeshi ya kivamizi ya Tanganyika, nyinyi mlikuwa wapi na haya msiyashupalie?

Au sisi si watu?

Nyinyi si ndio mliokaa mkitucheka na kutukebehi na kutuita wakorofi?

Sasa kibao kimewageukia, ndio mnalalama sio?

Basi hio ndio CCM yenu, Chama cha Magamba.

Na bado mtauliwa sana tu!!

Lakini poleni "wapiganaji"
 
Any loss of life is regrettable. Inabidi kufanyika uchunguzi kujua mazingira ambayo watu hawa walifariki. Je, walipigwa risasi wakiwa ndani ya eneo la Barrick? Je, polisi walikuwa na jinsi nyingine ya kuwazuia isipokuwa kuwapiga risasi? Je, ni kweli walipigwa risasi mgongoni wakati wanakimbia?

Pia tukumbuke kuwa ule ni mgodi wa dhahabu, hivyo lazima ulindwe kama inavyolindwa benki au kampuni yoyote yenye mali. Sasa watu kama walivamia ndani ya mgodi kwa lengo la kuiba gold ore na wakapigwa risasi napata ugumu kuwatetea na kuwaita "wanamapinduzi."

we unajua maana ya mapinduzi?Hayo madini sisi tunaliwa na mabepari wa ndani na nje hivyo tunapata kiduchu tu,Hivyo hao wenzetu walikuwa wanapindua huo udhalimu wa kutuibia mali zetu na kuonyesha kua hiyo dhahabu hata sie tunaitaka na ndio maana Mungu akaiweka iwe tz nasio usa au huko canada upo hapo?
 
Mimi siku zote husimamia haki na daima huwa upande wa wanyonge dhidi ya maovu. Ila kamwe siwezi kuunga mkono uvamizi wa mgodi wa North Mara na kuwaita waliouwawa wanamapinduzi -- hapa tunachezea maana halisi ya wanamapinduzi.

Wote hapa hatujui nini haswa kilitokea, lakini based on police statements ni kuwa kundi la watu 800 mpaka 1,000 walivamia mgodi wa North Mara wakiwa na mapanga, marungu na silaha zingine za jadi wakawa wanataka kuiba gold ore kwa lengo la kwenda kuiuza na kujinufaisha wao wenyewe.

Sawa, wananchi wa Nyamongo wana manung'uniko yao ya muda mrefu kuhusu mwekezaji kupewa eneo hilo lakini kisheria Barrick ni mmiliki halali wa mgodi huo. Hivyo watu 8 au watu 800 wakiingia ndani ya mgodi huo kinyume cha sheria kwa lengo la kuiba mawe ya dhahabu watu hao ni wezi au wavamizi tu, kamwe si wanamapinduzi.

Ni kama wewe ukiwa na shamba lako lenye hati umeuziwa na serikali ya kijiji, umejenga ukuta na kuweka geti. Sasa wakaja wanakijiji 800 na kuvamia eneo hilo kwa lengo la kuiba ng'ombe wako utawaita hao wanakijiji wanamapinduzi au wezi? Ndiyo maana wengine wameweka vibao kwenye mashamba yao kuwa "Trespassers will be shot!"

Kama wanakijiji wa Nyamongo wana malalamiko kuhusu mgodi huo ni vyema CHADEMA na wanasiasa wengine wakawafundisha utaratibu mzuri zaidi wa kudai haki zao, si kuvamia na kuiba mawe ya dhahabu kwani Barrick watakuwa na haki ya kulinda mali zao.

Nadhani polisi walitumia excessive force kama wanavyofanya kila siku wanapouwa watuhumiwa wa ujambazi au wananchi wasio na silaha kwenye maandamano kama ya Arusha.

Hatuwezi kuunga mkono uvunjaji wa sheria hata kama wananchi hawa wana madai halali, pia serikali itaonekana ni ya kipuuzi mbele ya wawekezaji wa kimataifa kama itashindwa kulinda mali za wawekezaji kutoka kwa wavamizi.
Mkuu, hivi kweli taifa hili tumekosa viongozi serikalini wenye akili ya kuwawekea raia mazingira mazuri DHIDI ya wawekezaji uchwara, hadi CHADEMA ndo itegemewe kuwafundisha raia hao taratibu??? Halafu bado tunasema tuna serikali iliyotokana na wananchi??? Na kwa nyie wenye kufuata utaratibu tuambieni serikali hii imefika wapi na suala la mgodi huu huu kutiririsha sumu kwenda mto unaotumiwa na wananchi hawahawa. Nani amewajibishwa na sheria?? hawa raia walilipwa fidia gani? nani alikuwa na wajibu wa kuwalinda....? maswali ni mengi mno...
 
Hivi kumbe Nyamongo ni mali ya Barrick?? Na je wana Nyamongo waende wapi? Hivi kweli naweza kuja leo katika kiwanja chako na kuweka uzio wa chuma na jeshi na kusema yaliyomo ni mali yangu. Ushindwe na Barrick yako!!

Nilifanyaga a little research on Barrick on my "conflict resolution class" Kuna mengi niligundua kwenye hii kampuni na kwakifupi kila mahala wanapowekeza lazima kutokee mapambano na wenyeji. Ofcourse "African governments" huwa zina side na wao. Hizi ni baadhi ya links you can get the picture of the company. In simple terms I can say mahali walipowekeza Barrick (hasa nchi maskini) it is always their way or no way.

http://www.geography.ryerson.ca/jmaurer/811CONGO.htm

http://tools.morningstar.co.uk/t92wz0sj7c/stockreport/default.aspx?tab=3&vw=story&SecurityToken

In Papua New Guinea: Barrick Gold vs Indigenous Peoples : Climate and Capitalism

Barrick Gold makes it big in Africa | 03 March 2011 | www.commodityonline.com | 3

Sorry if that is too much info, but just wanted to give a clear picture of how Barrick operates.

http://www.geography.ryerson.ca/jmaurer/811CONGO.htm
 
Mimi siku zote husimamia haki na daima huwa upande wa wanyonge dhidi ya maovu. Ila kamwe siwezi kuunga mkono uvamizi wa mgodi wa North Mara na kuwaita waliouwawa wanamapinduzi -- hapa tunachezea maana halisi ya wanamapinduzi.

Wote hapa hatujui nini haswa kilitokea, lakini based on police statements ni kuwa kundi la watu 800 mpaka 1,000 walivamia mgodi wa North Mara wakiwa na mapanga, marungu na silaha zingine za jadi wakawa wanataka kuiba gold ore kwa lengo la kwenda kuiuza na kujinufaisha wao wenyewe.

Sawa, wananchi wa Nyamongo wana manung'uniko yao ya muda mrefu kuhusu mwekezaji kupewa eneo hilo lakini kisheria Barrick ni mmiliki halali wa mgodi huo. Hivyo watu 8 au watu 800 wakiingia ndani ya mgodi huo kinyume cha sheria kwa lengo la kuiba mawe ya dhahabu watu hao ni wezi au wavamizi tu, kamwe si wanamapinduzi.

Ni kama wewe ukiwa na shamba lako lenye hati umeuziwa na serikali ya kijiji, umejenga ukuta na kuweka geti. Sasa wakaja wanakijiji 800 na kuvamia eneo hilo kwa lengo la kuiba ng'ombe wako utawaita hao wanakijiji wanamapinduzi au wezi? Ndiyo maana wengine wameweka vibao kwenye mashamba yao kuwa "Trespassers will be shot!"

Kama wanakijiji wa Nyamongo wana malalamiko kuhusu mgodi huo ni vyema CHADEMA na wanasiasa wengine wakawafundisha utaratibu mzuri zaidi wa kudai haki zao, si kuvamia na kuiba mawe ya dhahabu kwani Barrick watakuwa na haki ya kulinda mali zao.

Nadhani polisi walitumia excessive force kama wanavyofanya kila siku wanapouwa watuhumiwa wa ujambazi au wananchi wasio na silaha kwenye maandamano kama ya Arusha.

Hatuwezi kuunga mkono uvunjaji wa sheria hata kama wananchi hawa wana madai halali, pia serikali itaonekana ni ya kipuuzi mbele ya wawekezaji wa kimataifa kama itashindwa kulinda mali za wawekezaji kutoka kwa wavamizi.
1. ni lini police statement zikawa za kweli?? walivyoua wafanyabiashara wa mahenge na kupora mali zao, Si zombe alitoa statement kuwa wameua majambazi; na police ni professional,na kudai hawana mashaka na hilo, mbona tume ya raisi ilisema vingine?
2. serikali yoyote makini inajua majukumu yake, nayo ni kuwa ipo madarakani kwa maslahi ya wananchi walioipa dhamana. kwa hiyo kudhulumu ardhi ya wananchi bila fidia, na kuwaua bila hatia kwa kisingizio cha kulinda mali za wawezkezaji, ni kutokuwa makini kwa viongozi, upstairs hakuna kitu!!!
 
Haiwezekani kamanda goigoi akaongoza askari wakakamavu. Kiongozi wa magamba ni mwerevu kufikia hilo linaloendelea hapa bongo.
 
Hawa common criminals wanaitwa wapiganaji na mashujaa, kule Pemba na Unguja walipoandamana kwa kupinga matokeo, wakaitwa wakorofi.

Hivi hawa CHADEMA watakuwa lini?
Ndugu angalia chuki zako zisikupofushe.. Chadema iliyokuwa inaiunga mkono Cuf iliwaita wafuasi wa cuf wakorofi??
 
Chadema muache mambo yenu ya hovyo ule msiba hauwahusu kabisa ni wa watu wa Tarime na wamefariki sio kisiasa mbona mnaleta siasa Chadema za kujinufaisha kupitia misiba ya watu! Nani kawambia walio kufa ni Chadema hadi mlete majitu yenu ya akina Lissu huku Tarime! Tunataka haki kwa wana tarime kupata mapato ya mgodi,lakini sio kutuletea siasa za Kishamba!
 
Mkuu Mkandara, mimi sishabikii haya mauaji hata kidogo lakini najiuliza, wakati sisi tunapigwa na kuuliwa na kufanyiwa vitendo kadhaa vya kudhalilishwa na Majeshi ya kivamizi ya Tanganyika, nyinyi mlikuwa wapi na haya msiyashupalie?

Au sisi si watu?

Nyinyi si ndio mliokaa mkitucheka na kutukebehi na kutuita wakorofi?

Sasa kibao kimewageukia, ndio mnalalama sio?

Basi hio ndio CCM yenu, Chama cha Magamba.

Na bado mtauliwa sana tu!!

Lakini poleni "wapiganaji"
Ahaa! hivi waziri wa mambo ya ndani ni nani vile na anatoka wapi....... Asante mheshimiwa umeeleweka!!!
 
Chadema muache mambo yenu ya hovyo ule msiba hauwahusu kabisa ni wa watu wa Tarime na wamefariki sio kisiasa mbona mnaleta siasa Chadema za kujinufaisha kupitia misiba ya watu! Nani kawambia walio kufa ni Chadema hadi mlete majitu yenu ya akina Lissu huku Tarime! Tunataka haki kwa wana tarime kupata mapato ya mgodi,lakini sio kutuletea siasa za Kishamba!
Irina riyu nehe urirusiri mbane....?! Rengera whiki iga nkhe mugutuna???
 
Chadema muache mambo yenu ya hovyo ule msiba hauwahusu kabisa ni wa watu wa Tarime na wamefariki sio kisiasa mbona mnaleta siasa Chadema za kujinufaisha kupitia misiba ya watu! Nani kawambia walio kufa ni Chadema hadi mlete majitu yenu ya akina Lissu huku Tarime! Tunataka haki kwa wana tarime kupata mapato ya mgodi,lakini sio kutuletea siasa za Kishamba!

Hilo jina unalotumia si la sehemu unayotoka, kule Tarima hakuna watu wenye spirit za kike naza kikahaba kama unazoleta wewe hapa. tutakugecha.
 
Hilo jina unalotumia si la sehemu unayotoka, kule Tarima hakuna watu wenye spirit za kike naza kikahaba kama unazoleta wewe hapa. tutakugecha.
Unafikiri kwa kutumia sehemu ya kutolea uchafu ya nyuma? Tarime yote ni Chadema? Hatutaki mrete siasa na jambo hili Chadema! Uchungu wa kufiwa ni wa wana tarime siasa za Chadema zinaingiaje hapa?
 
Unafikiri kwa kutumia sehemu ya kutolea uchafu ya nyuma? Tarime yote ni Chadema? Hatutaki mrete siasa na jambo hili Chadema! Uchungu wa kufiwa ni wa wana tarime siasa za Chadema zinaingiaje hapa?

Tarime hakuna anaezaliwa na spirit za kike na za kinafki.
 
we unajua maana ya mapinduzi?Hayo madini sisi tunaliwa na mabepari wa ndani na nje hivyo tunapata kiduchu tu,Hivyo hao wenzetu walikuwa wanapindua huo udhalimu wa kutuibia mali zetu na kuonyesha kua hiyo dhahabu hata sie tunaitaka na ndio maana Mungu akaiweka iwe tz nasio usa au huko canada upo hapo?

Tz au Tanganyika Mkuu?

Kwani sisi tunafaidika nayo vipi Zanzibar?

Si mnajua kutukalia kwa mabavu tu?

Mimi nataka hao Barrick waichukue yote ubakie udongo mkapakasie mikeka tu.

Daini Tanganyika yenu sio kudandia vya watu.
 
Back
Top Bottom