aende akafanye nini na ni "matumbili" yamekufa? Yaani unataka aache starehe zake aende porini kisa kuna "tumbili" wamepigwa risasi?hv wazir wa mambo ya ndani kwa nini ajaenda tarime mbona waziri mkuu kimya hv yupo?
Tangu tukio la mauaji lilipotokea kila mtu amajiuliza ni kwa nini Polisi wanakuwa makini kiasi hicho kuhakikisha kwamba Barrick haisogelewi!
Habari mbaya kabisa niliyoaambiwa toka Ukuryani ambayo inaonekana ni taarifa toka ndani ya Barrick wakikerwa na uhusiano wao na wananchi wanaowazunguka ni kwamba, Mauaji hayo yanachochewa na mishara inayotolewa na Mgodi kwa mkuu wa Mkoa, Mkuu wa polisi wa Mkoa, Mkuu wa wilaya na OCD. Yawezekana na wengine weeengi.
Hawa watu yasadikiwa wana mgawo kila mwezi ikiwa ni shukrani kwa ulinzi wanaoutoa ktk mgodi.
Lakini pia Pale Musoma mjini, Mkuu wa polisi anatoa nafasi kwa askari kwenda kulinda Nyamongo kama zawadi maana kila anayekwenda kulinda pale anapewa shiling 40,000 kwa siku. Pesa hizi hutolewa na mgodi. Tofauti na malindo mengine ambayo askari huambulia mkono mtupu au kwa faida kidogo ya shilingi 20,000 au 25,000.
Sasa kumbe amani ktk eneo la Nyamongo inaondoa uhalali wa askari kwenda kuvuna pesa mgodini na njia pekee ya kuweka mazingira ya umuhimu wao kuwa mgodini ni wao kupiga raia, na sasa kuuwa ili mgodi uone umuhimu wa wao (askari) kuwa pale na hatimaye wakuu wao waendelee kupata kipato cha ziada toka mgodini.
Naweza amini. Taarifa hii inanifanya nianze kuunganisha matukio ya nyuma mpaka leo hii;
-Kwa nini Mh. Sitta alikuwa makini kiasi kile ktk kumumdhibiti Mh. Cheyo wakati akichangia mjadala wa matukio ya tindikali ya mgodi wa Barrick?
-Kwa nini tarrifa ya kamati ya Bunge iliishia uvunguni bila hata muelekeo?
-Kwa nini Waziri wa mambo ya Ndani, Kagasheki anashindwa kuwa makini kuieleza hali halisi ya ubovu wa maamuzi ya askari uliopelekea mauaji hayo?
-Kwa nini Rais na waziri Mkuu wake wako bubu bila hata la kuonyesha masikitiko ktk tukio hili?
Watu wanaolipwa na Barrick ktk nchi hii wanaweza kuwa ni wengi na hasa kwa kuzingatia matukio mabaya ya Barrick yaliyowahi kutokea ktk Dunia hii.
wezi wanapewaga milioni tatu kila mmoja na jeshi la polisi???
<br />
<br />
We makalio kweli,Tundu lisu amehangaika sana na nyamongo.na watu wanamjua sana nyamongo,sasa wewe cjui unachukulia tukio la jana ndo kisa? Kwanza hamna mkurya Mwenye MAWAZO LEGEVU kama yako. We umenunuliwa,af huna sifa za kukaa majukwaa kama haya mana maneno yako yanalijazia jukwaa nzi,na kama unavojua feni zimezima kutokana na mgao wa umeme kwaiyo ni vizuri ukalale au ukatafute gazeti la udaku usome.