Mawaziri waghushi vyeti

Kuwa na PhD feki ni kosa lakini ni zaidi ya kosa kwa mtu aliyekabidhiwa jukumu la kuongoza nchi yetu KUKURUPUKA na kuteua VIHIYO hao kuwa mawaziri wetu.Tukumbuke kwamba "Dr" Nchimbi na wenzake HAWAKUJITEUA KUWA MAWAZIRI bali WALITEULIWA NA Dr (wa heshima) Jakaya Kikwete.Najua two wrongs do not make a right na hapa sitetei hawa Vihiyo bali namlaumu huyo aliyewateua pasipo kuangalia rekodi zao sahihi.Leo tunafahamishwa kuwa tuna mawaziri wenye elimu feki,kesho tutasikia tuna mawaziri wenye uraia feki.Hii nchi ni kama inaning'inia kwenye utandu wa buibui....

By the way,hivi hakuna mamlaka inayomshauri Rais kuhusu anaotaka kuwateua (i mean kumshauri baada ya kuwafanyia sort of profiling...vetting)?


.....Mlalahoi....ukisikia jinsi SIASA inavyochukua uzito kuhusiana na hizi teuzi.....unaweza kuichukia siasa ya Tanzania maisha yako yote.......wee si umemsikia Kingunge anasema MASLAHI YA CHAMA KWANZA.......kwi kwi kwi kwi kwi......na teuzi zinakuwa hivyo hivyo MASLAHI YA CHAMA KWANZA............
 
Inabidi tuwe waangalifu kwenye msamiati. Kughushi cheti kinachosema una sifa fulani wakati huna ni kosa la jinai. Naamini tatizo tulilonalo dhidi ya hawa Mwaziri wetu na Wahadhiri wa Mzumbe si la kughushi.

Accreditation is a relative term. Different bodies have different sets of accredited universities. Labda tunazungumzia accreditation ya TUC. Sasa hao TUC wameshasema shule zipi ndio accredited?

Sidhani kwamba tatizo tulilonalo na hawa vihiyo wetu ni la kusoma kwenye vyuo ambavyo sio accredited. Ni tatizo la kujipatia cheti cha kusema una digrii fulani kwa kununua hicho cheti, na kwa kutosoma kwa kiwango ambacho angalau kinakaribia kweli kilele hicho cha elimu .

Nafahamu, kwa karibu, watu wawili waliojipatia PhD kwa njia hii feki. Wa kwanza alikuwa na MSc ya Mahesabu. Aliwasiliana na PWU, na baada ya kuandikiana kwa miezi kidogo, na bila kusoma Mehesabu zaidi, aliwatumia fedha walizotaka, nao wakamtumia "cheti cha PhD" ya Mahesabu toka PWU. Ngazi yake ya Mahesabu ilibaki pale pale kwenye MSc yake, lakini tangu siko hiyo alidai ana PhD.

Wa pili ana MBA. Anafanyakazi kwenye cho kikuu cha binafsi. Miaka michache iliypita chuo hicho kiliamua ukiwaandikia ukajieleza uzoefu wako na kulipa gharama zinazotakiwa basi wataangalia kama unastahili PhD. Alifanya hivyo na wakampa PhD (ya uzoevu wake). Hakusoma zaidi. Hakuna cha thesis wala cha nini.

Mimi najua mtu yoyote mwenye PhD ya PWU ni kihiyo wa kununua digrii.

Sasa mwajiri wa kihiyo aidha ni kihiyo (kwa kushindwa kugundua vyeti feki) au ni mshirika wa makusudi katika kosa kubwa. Inabidi serikali ingoe vihiyo wote kwenye ajira yake. La sivyo tutajenga uzoefu mbaya.
 
Haya mambo tumeshayaongelea toka miaka ileeeeeeeeee!

Tulianza nayo BCS tukaja na Mzumbe na dreee feki na VC wao na PHD feki, akaja Nungwi kapinga weeeeeeee.

Mpaka tunakosa la kuongeza. Kwenye jukwaa la elimu kuna topic kuhusu hili nadhani ni topic ya 2006 kama sikosei.

Swali ni kuwa kama sisi raia wa kawaida tuliona hili 2005 je serikali yenye Usalama wa taifa na dola kamili hawakuliona hili?

Something is terribly wrong within the system!
 
Swali ni kuwa kama sisi raia wa kawaida tuliona hili 2005 je serikali yenye Usalama wa taifa na dola kamili hawakuliona hili?
Something is terribly wrong within the system!

Jibu la swali lako ni kwamba hao wenye hivyo vyeti feki ni sehemu ya hiyo serikali na Usalama wa Taifa! Unataka wajishughulikie wenyewe? Hukuona hii ishu haikutakiwa Bungeni? Kuna kitu kinaitwa "vested interests".

Mnaotaka Elimu ya Kweli msotee vyeti vyenu. Serikali hii ya sasa ni ya wanastarehe ambao wanataka vyeti, lakini bila jasho. Wanavinunua.
 
Haya mambo tumeshayaongelea toka miaka ileeeeeeeeee!

Tulianza nayo BCS tukaja na Mzumbe na dreee feki na VC wao na PHD feki, akaja Nungwi kapinga weeeeeeee.

Mpaka tunakosa la kuongeza. Kwenye jukwaa la elimu kuna topic kuhusu hili nadhani ni topic ya 2006 kama sikosei.

Swali ni kuwa kama sisi raia wa kawaida tuliona hili 2005 je serikali yenye Usalama wa taifa na dola kamili hawakuliona hili?

Something is terribly wrong within the system!

Kweli kaka, mimi naona tunazunguka, tatizo ni pengine usalama wa taifa wamelala, au hawajui wajibu wao, au hawasikilizwi. maana Kikwete kuteua lazima usalama wa taifa wawapeleleze hao watu, ama sivyo ndiyo hayo unachagua watu kama hawa, au kama yule mkuu wa wilaya aliyepiga walimu bakora!
 
Tufike wakati tujiulize GPA ya Mkulu ikoje?. Kwa nini hakufanya Masters. Majibu ya maswali hayo yatathibitisha kwamba shule nene sio issue, issue ni kuwa mpiga domo mzuri wa kuinadi ilani ya uchaguzi kwa wananchi na CCM itaendelea kutawala milele!.

Mhhh Pasco, hapo umenivunja mbavu!! Kama kuna mwenye data atueleze jamani. Tunaweza kuwa tunamwonea mzee wa watu kwa kutegemea mambo makubwa kumbe yeye aliibuka na PASS ya kubangaizia!! Hapa naomba kieleweke kwa Mkulu kwanza:rolleyes:
 
Sina uhakika na hili lakini nilipopita kwenye blog ya January Makamba niliona kama Mh.Anthony Diallo anajitambulisha kama Dr.Anthony Diallo! Kuna yeyote mwenye kuweza kuthibitisha kama huyu jamaa naye anajiita Dr. Diallo kwa maana ya Phd? nachofahamu mimi alikuwa anafanya masters kwenye phoenix university na chuo kingine cha aina hiyo cha australia miaka ya 2004-2005 sasa hili la Phd limenistua kidogo.
 
Dr. Aisha Kigoda..... huyu ni clinical officer lakini anapenda aitwe dr. si sahihi
 
Hayo ndo mambo ya Tanzania bwana.Lakini viongozi wakae chonjo make watanzania walioongozwa na baba wa taifa sio wa sasa hivi.Kwa sasa watu wanajua kinachoendelea ingawa shule za kubabaisha.Kufikia mwaka 2020 wabongo wengi watakua hawadanganywi tena.
 
Dr Nchimbi E
Dr Matayo David Matayo
Dr Mary Nagu
Dr Makongoro Mahanga
Dr Kamala D

Mbona wapo wengi is more than 4 waliofichwa majina hapo!!

Mkuu Masanilo, kama unawafahamu hao wengine waanike hapa ndugu, pia ingekuwa vyema kama ungeeleza kwa nini vyeti vyao ni feki e.g labda nao walipata hizo Doctorate huko PWU etc.
 
Hili ndilo tatizo la TAALUMA zisizo na BOARDS zilizosajiliwa kisheria kama ilivyo kwa wahasibu na NBAA na wahandisi na ERB.
 
Ninavyofahamu Dr. Mathayo hana Degree kutoka huko PWU bali Orange Free State RSA. Sasa kama kweli ni feki basi atakuwa amefoji cheti maana OFS ni one of the best universities in RSA hivyo hakuna cha kununua cheti pale.
 
Ninavyofahamu Dr. Mathayo hana Degree kutoka huko PWU bali Orange Free State RSA. Sasa kama kweli ni feki basi atakuwa amefoji cheti maana OFS ni one of the best universities in RSA hivyo hakuna cha kununua cheti pale.

Hajawahi register for PhD pale...kama unataka mtetea tuandikie tittle ya Thesis yake. Mkuu tuliishafatilia pale hakuna mwanafunzi wa aina hiyo. Sasa unataka kusema cheti katoa wapi? na hakuna PhD ya miaka 2! puuuuuh
 
hiii ni so kweli kweli ..... hapa inatakiwa iundwe tume huru ambayo kazi yake ni kupitia wizara moja baada ya ingine ili wawabaini hao wanaofoji then wawataje live then wawafungulie mashataka na kupewa kifungo hata cha mwaka mmoja itatosha maana watu qwengi wana sifa hawapati kazi kumbe kuna watu wamejipatia kwa kufoji THIS IS UNJUST AND VERY UNFORTUNATE IT OCCURS IN OUR BELOVED COUNTRY (WADA NGANYIKA)....
MPKA YESU ARUDI NDIO HAKI ITATENDEKA VINGINEVYO NI FULL LONGOLONGO KWA KWENDA INFRONT
 
Kosa ikiwa wametumia vyeti hivyo kujipatia vyeo , na zaidi ikiwa wametumia vyeti hivyo kujiongezea mshahara maana baadhi ya vyeti vinakusaidia katika kuongeza mshahara sasa hawa ni mafisadi waliondani ya mishipa ya Taifa wao wamekuwa kama wadudu wa HIV wanaua tu ,hakuna wa kuwatibu,ni kuwapiga na chini CCM ili kupunguza kasi ya madudu haya.
 
Tatizo tulilonalo juu ya hivi vyeti feki ni kwamba, wengi walionavyo ni wanamtando wa CCM ambao ndio waliompigia debe muungwana kuwa Rais na hao vihiyo sasa wengine ndio mawaziri wake na wapambe wake!! Sasa kuwaumbua inakuwa shida kwani maana yake muungwana lazima atengane na maswahiba wake na ndio maana hata kule bungeni Sitta mara nyingi, juu ya ubabe wake hawa vihiyo anawaogopa sana kwani wanaweza kumuangusha!! Mfano mzuri ni wakati wa uchaguzi wa wajumbe wa baraza la kutunga sheria la Afrika Mashariki; katika uchaguzi ule Sitta alialifiwa kuwa kulikuwa na candidates wa CCM ambao walikuwa na vyett feki vya PH.D [ Masaburi, Sigara, Mafwenga na Nangale] lakini kwa unafiki na ufisadi wa CCM no effort was taken to certify the authenticity of their degrees na wawili kati yao VIHIYO ndio wakachaguliwa kutuwakilisha wananchi kwenye EALA!! Hii yote ni kwa kulindana kwa ccm hivyo kutuaibisha mbele ya wenzetu waganda na wakenya ambao wanashangaa kuona nchi yenye BRAINS ikiwakilishwa na watu wasioweza kujenga hoja ikaeleweka in defence of their motherland!! Nategemea huyu Prof. Nkunya na taasisi yake hawatarudia makosa ya wenzao ya kutolifuatilia tatizo hili to its logical conclusion.
 
Nani anakumbuka ile story ya yule dada alijifanya daktari na kwa muda mrefu aliendelea kufanya kazi ya udaktari kule Dododma miaka mingi kidogo iliyopita?
Alikuwa anafanya hata operations na kazi za ku prescribe dawa kwa wagonjwa.
Alikuwa anafanya hata round kwenye ward za wagonjwa.
Mungu saidia Tanzania maana kila tapeli ana practise utapeli wake katika nchi yetu na hakuna anayeshituka.
 
Nimeambiwa hatimaye Kamala kafanikiwa kupata Ph.D inayotambulika kutoka Hull university.

Sina uhakika sana ila inaelekea baada ya scandal kuanza akajiandikisha kimya kimya na ameonekana akitembelea hicho hicho mara nyingi.

Wenye taarifa zaidi mnaweza kutujulisha. Kule bungeni bado hajaweka hiyo taarifa. Labda anasubiri watu wamshambulie ndio atoe ushahidi wake, au anasubiri 2010 wapinzani wake wakija na tuhuma ndio ataoe ushahidi wake.
 
Back
Top Bottom