Mawaziri wa JK: Ngeleja na apartment ya $350,000

Hivi 'Uwaziri' ni DEAL?

unless i have missed your point.....lakini literally nadhani hii kitu ni DEAL. tena kubwa!

maana JK amekaririwa akisema endapo mawaziri hawatateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, basi kungekuwa na uwezekano wa baadhi ya watu kutogombea ubunge kabisa.
 
I am sorry but this is the reason our dear TShs keeps on trailing behind major currencies daily. Jana tumeambiwa Maige ametoa CASH US$ 400k, leo Ngeleja 350k. Hawa ndio waliopaswa kusimamia our currency! Malima kaibiwa US$ 4k (petty cash) na Mbunge aliyeibiwa Dodoma alichotwa 0.6k. Governor wa Central Bank anasema haijalishi. Kwa nini wasihalalishe wote tukatumia dollar tu?

Wa-TZ mtajiju
 
Heshima kwako Invisible,

Mkuu wangu unajua magonjwa ya moyo tiba sahihi na za uhakika zinapatikana India bahati mbaya mimi si mteule wa Rais nina uhakika nikiugua leo nitakimbizwa Selian or KCMC nikakumbane na maDr wenye hasira za kusengenywa na mkuu wa Kaya kwenye kile kikao cha Wazee wa Dar sijui hatima yangu itakuwa vipi ?.

Kila kukicha unakumbana na ufisadi uliotamalaki kila kona hakuna wizara yenye nafuu ukitia mguu Uchukuzi ubongo lazima uchezee ukiulizia Mali asili na Utalii ndiyo kumeoza kabisa Madini na Nishati utaratibu wa kupelekwa India haukwepeki.Naomba mnapoanzisha threads mtoe taadhari msije mkapelekwa mahakamani kwa kusababisha vifoo vya ghafla.
 
I am sorry but this is the reason our dear TShs keeps on trailing behind major currencies daily. Jana tumeambiwa Maige ametoa CASH US$ 400k, leo Ngeleja 350k. Hawa ndio waliopaswa kusimamia our currency! Malima kaibiwa US$ 4k (petty cash) na Mbunge aliyeibiwa Dodoma alichotwa 0.6k. Governor wa Central Bank anasema haijalishi. Kwa nini wasihalalishe wote tukatumia dollar tu?

Wa-TZ mtajiju

Ni wajukuu wanachuma kwenye shamba la bibi yao. Hakuna anayewazuia (what an undefended wealth of Tanzania!)
 
Aaaaaaaaaaaa, hii nchi inaenda wapi sasa! Ngeleja huyu alokuwa wakili wa vodacom, mhhhhhhhhhhhhhhh!

Ni kijana wa Rostam, ni yeye Rostam alihakikisha amempeleka vodacom ili awe informer wake kutoka Managment kuhusu vodacom as he is one of the main shareholder, I hope he had about 26% shares or so. Alipoona ameshaandaa njia akampa hela ya kampeni akagombee ubunge na alipopata RA alichagua wizara kadhaa ambazo ni lazima zishikwe na vijana wake na Nishati na madini ni mojawapo? Kwa mantiki hiyo Mwamvita Makamba amechukua nafasi ya uinformer kwa RA na kwa jinsi RA alivyo smart akahakikisha na Ikuku anawaweka Salva na Makamba ili apate mengi ya nchi!! Nchii hii inahitaji mabadiliko na mabadiliko ya uongozi!!!
 
Mkuu si matatizo ya wasukuma, siCeM hakuna msafi mimi nakwambia hivi ni vifaranga tu.. mengi huyajui. Kuna siri kubwa ya siCiyemu kukataliwa mwanza.. mengine naogopa kuyaandika humu

Unaogopa nini??? Kama unajua madudu yao we andika tu.... Otherwise unajidai kujua while hujui.... Sidhani kama hilo ni kubwa zaidi ya kutokua na Imani na Waziri mkuu.... na watu wamemwambia na Sahihi waliweka bila kusahau such a move had an Initiator...
 
Obe, kwenye hizo picha wewe umeiona popote hiyo figure ya dola 350,000? Au kwa vile aliyebandika ni Invisible kwa hiyo hakuna hata haja ya kuhoji?

Kweli Watanzania hatuna attention to detail.

Muwe mnasomaga kwa umakini, Sireem ndiye kasema huyo Msomali wa African Village anauza kwa bei hiyo kwa apartment
 
Jamani mbona mkataba uko wazi tu kwamba jamaa anamiliki floor na si appartment nzima, je huu ni kuchafuana au kitu gani?.

Halafu hiyo figure ya dola 350000 mmeipata wapi?- je mna uhakika aliinunua kwa bei hiyo?- je hakubargain?- je mwishowe alitoa cash kiasi gani?.

No way, siziungi mkono sera za ngeleja, lakini hii thread ni half information and hence half the truth!
 
Sasa kama bosi wao anahusishwa na kale kalodge ka Serengeti, hawa wadogo ndo wanajifunza huko..bila ya wananchi kuamka mapema kwa sauti moja kuwapinga hawa jamaa lazima tutakula wa chuya..!
 
Muwe mnasomaga kwa umakini, Sireem ndiye kasema huyo Msomali wa African Village anauza kwa bei hiyo kwa apartment

Sasa hapa sijui nani anahitaji kusoma kwa makini!

Angalia nani kaanzisha mada na angalia kichwa cha mada kinasemaje! Ebo!!!
 
Jamani mbona mkataba uko wazi tu kwamba jamaa anamiliki floor na si appartment nzima, je huu ni kuchafuana au kitu gani?.

Halafu hiyo figure ya dola 350000 mmeipata wapi?- je mna uhakika aliinunua kwa bei hiyo?- je hakubargain?- je mwishowe alitoa cash kiasi gani?.

No way, siziungi mkono sera za ngeleja, lakini hii thread ni half information and hence half the truth!

Thank you Gamba La Nyoka!!
 
Watu tunalala giza kumbe jamaa anajipigia dili kwa kutumia giza eti umeme wa dharula kumbe wanavuna mapene.
Hawa adhabu ni moja tu kunyongwa hadharani kama China
 
narudia kusema JK anajua hao ni wezi, lakini anakosa nguvu ya moyoni kuwashughulikia, Usafi wake akiwa wizara ile unampunguzia nguvu ya kutenda dhidi ya huyo Bwana, sanjari na hawa mapapa wengine kama kina Maige.

UWAZIRI NI UDOKOZI, UWAZIRI NI WIZI , UWAZIRI NI UMILIONEA.
 
Back
Top Bottom