Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

Wewe ndio wale wale, kwanza jua kukariri ni moja wapo ya njia ya kuelewa, kuna vitu havibadiliki hata aliyesoma miaka 100 itabakia hivyo hivyo, barua ya kikazi lazima anuwani yako iwe upande wa kulia juu na hapo kwenye anuwani yako ndio utaongezea email na namba za simu zako. Sasa hapo unapotetea saini kuwa chini ya jina, mtu mwingine anaweza akaja kuandika jina lake chini yake, saini itakuwa siyo yake tena.

Jaribu kutofautisha kukariri na kufuata utaratibu

Acha kujichanganya aliongelea kuhusu jina na saini nani?
 
Very True Mdau ....Mbwembwe za nini ? badala ya kutoa zile sababu za kidhungu ( I'm looking for a new challenge) yeye anatangaza Njaa lol ! Ajira zenyenye za Bongo ni Last Name yako au kujuana nina Mtoto wangu kahiti...hata hujamaliza utasikia Kamlete , tena mlete kesho asubuhi , Mahusiano Mazuri ni Muhimu sana... acha kazi kistaarabu tu ...

Angeliondoka kimya kimya. Ingelimpa heshima sana. Angalia, kila mtu kamlaumu namna alivyojitangaza kwa dharau (neno kutumika)
 
kwa mimi ambae sielewi sijaona tatizo kabisa ya hiyo barua
mnaoona ina mapungufu yawekeni wazi


Kama huoni tatizo hata tukikueleza hutatuelewa.

Ila kwa ufupi, umeona comment ya mdau kuhusu mahali ilipo tarehe? Umeona mpangilio wa paragraph? Umeona alipoweka jina na sahihi yake? Umeona cheo chake kabla ya kusitisha mkataba wake?

Ngoja niishie hapa ila mambo kama haya na mengine yanayogusa elimu yetu yanadhihirisha kuwa kama taifa tuko katika hali mbaya sana!!
 
Kuna mfanyakazi dada mmoja alikuwa mtangazaji mashuhuri ITV alikufa . Moja wapo ya sad stories about her ni kuwa alikuwa hana mkataba pamoja na kufanya kazi muda mrefu pale!
Aiseee...kama ni kweli Mungu atalipa hapahapa.
 
Kumbukumbu zangu

Mwaka 2005 nilisoma kwenye gazeti moja hivi (sikumbuki) alisema anampango wa kugombea ubunge ifikapo 2015.

Sijui kama bado ana nia hiyo iliyomlazimu aache kazi au kapata shavu kwingine.

ALL IN ALL: Kila la kheri Maulid Kitenge a.k.a Baba Shadya tutakumiss kwenye kioo.

----------------------


attachment.php
attachment.php

Huu mtindo wa kuchakachua "post" za watu wengine mie sijaupenda hata kidogo kwa Modes wa hili jukwaa hapa JF, Heading ya habari niliiweka mimi, maudhui niliweka mimi mpaka jana , ila leo hii iliyo quote leo ndo inaonekana kuwa ndo muanzisha thread... hii sio fair kabisa Mods, eti leo QN OF SHEBA ndio muanzisha mada..... kama uko makini angalia likes zangu hapo na hiyo ya qn of sheba. kuweni muda heshimu mtoa mada na sio kwa kuwa mna uwezo wa ku edit habari na kuipanga (coz ni mod) mnavyotaka basi mna chakachua... sio fair nasema sio fair kabisa.
 
Hakukuwa na sababu ya kuweka siri za mikataba baina yake na mwajiri wake kwenye mitandao. Unless anataka kitu hapo, yaweza kuwa anatuma ujumbe kwa umma kuhusu hali ya hewa IPP kuwa sio nzuri, au kuondoka na mashabiki wake lakini kwa reputation yake hajafanya uungwana.
 
One of my brother amefanya kazi TRA kama senior officer na mshahara mzuri lakini akaacha kazi akapata kazi PPF na sasa ameacha kazi PPF yupo UN wabongo wanadai jamaa ni shushushu kisa wao wamezoea wizi na hawaamini kama kuna binadamu anaweza kuacha kazi TRA na PPF.

Hiyo Ndio inatakiwa ..ukiona umefanya kazi mahala miaka 5 kwenda Juu na HAJALETA impact ..unatakiwa kutafuta kazi mahala pengine ..utakapoweza ku fit ...it's not about money
Ukifanya kazi mahala miaka Mitano na Zaidi ...ukaleta mafanikio pia unatakiwa kuangalia changamoto mpya sehem nyingine ....hata Kama hawalipi kwa Ofa kubwa ..at least wakikupa Ofa sustainable...ni heshima Kuleta impact

Mashirika ya kimataifa ...hata MNCs ukipeleka cv unataka kazi ...umekaa sehem Moja miaka 20 ...na hawaoni ulikuwa unafanya nini Zaidi ya formalities Za vyeo kupanda...kupewi kazi ..wanampa mtu ambaye wanajuwa anaweza Kuleta impact na ame prove sehemu mbili au Tatu
Pia employers wengi serious hawawapi kazi wale ambao wanabadili kazi chini ya miaka Mitano ...kashafanya sehemu mbili hadi Tatu .......hawa Ina maana wana matatizo ...Ndio maana hawakai kwenye kazi muda unaotosha Kuleta mabadiliko ...kumuajiri mtu Kama Huyu ni kupoteza muda
Ni vema vijana WANAoanza kazi wajifunze kujenga carrier Zao ...wakipata kazi hata Kama hazilipi Sana WAWE wanavumilia na kujitahidi kujenga legacy fulani kwa muda wa Kutosha ...hawa automatically wanakuwaga poached ....kwa Ofa nzuri bila hata kuomba.....kuna vijana Leo ni CEO wa makampuni makubwa lakini unakuta walianzia kazi Za door to door marketing ...,managers...hadi wanapanda haraka
 
Huu mtindo wa kuchakachua "post" za watu wengine mie sijaupenda hata kidogo kwa Modes wa hili jukwaa hapa JF, Heading ya habari niliiweka mimi, maudhui niliweka mimi mpaka jana , ila leo hii iliyo quote leo ndo inaonekana kuwa ndo muanzisha thread... hii sio fair kabisa Mods, eti leo QN OF SHEBA ndio muanzisha mada..... kama uko makini angalia likes zangu hapo na hiyo ya qn of sheba. kuweni muda heshimu mtoa mada na sio kwa kuwa mna uwezo wa ku edit habari na kuipanga (coz ni mod) mnavyotaka basi mna chakachua... sio fair nasema sio fair kabisa.

You have a point ..nafikiri tuangalie upya Wakati wa kuunganisha thread ..Huwa inawakatisha baadhi ya members hasa wale wapya tamaa
Mnapounganisha thread mnaweza kubuni namna ya kuwaweka wale wote ...au hata kuwa recognize ...kwa chini kwenye post ya kwanza ya Hiyo thread ...
Mtu aliyetoa most detail information anaweza kupewa lead role Kama mwazilishi au Yule wa kwanza kabisa kuweka hata Kama hakua na taarifa Sana Kama news ni Breaking au Alert
 
Back
Top Bottom