Elections 2010 Matusi au 'tuhuma' katika kampeni?

jamani, sasa sijui hawa CCM wanataka kampeni zifanyikeje. Kampeni ya uchaguzi maana yake ni kwa mgombea kunajinadi ubora wake kwa wapiga kura na vile vile kuwaonyesha wapiga kura udhaifu wa mpinzani wake, ndivyo ilivyo duniani kote. Udhaifu mkubwa wa CCM ni rushwa na kuongoza nchi vibaya; sasa utawaonyeshaje wanachi udhaifu huo iwapo kufanya hivyo itatafsiriwa kuwa "siyo lugha ya kistaarabu"?

Angalia kampeini za Obama zilivyokuwa

 
Last edited by a moderator:
kuna ambalo amekosea hapo?.....me i see GREEN.....! GREEN LIGHT......GREEN MEANS GO.....KINANA GO.....TALK POINTS NOT PEOPLE...WHAT WILL YOU DO...AND NOT WHAT OTHERS DIDNT.....! TALK WHAT GOOD YOU DID.....AND NOT WHAT OTHERS FAILURES....!
MWANAMUME RIJALI HUZUNGUMZIA ATAKAYOMFANYIA MWALI SIO KUONGELEA MADHAIFU YA WANAUME WENGINE.....AONGELEAYE MADHAIFU YA MWINGINE HUYO DOMO ZEGE HANA SERA...(HATA KAMA MADHAIFU KWELI YAPO)

Wewe hujui maana ya kampeini za ushindani; unadhani ni enzi za chama kushika hatamu.
 
Kusema kuwa Mkapa na Lowassa walishiriki katika upangaji na uporaji wa fedha za EPA si lugha ya kistaarabu. Kusema kuwa Kikwete alisaini mikataba mibovu ya madini mwaka 1994 si lugha ya kistaarabu. Kusema kuwa Kikwete amesema atawalipa fidia wahanga wa waliozikwa hai
katika mgodi wa Bulyankulu si lugha ya kistaarabu. Kusema kidumu chama cha mapinduzi ni lugha ya kistaarabu. Mmeelewa?

Ndiyo Mkuu
 
Haya yanayotafsiriwa na tido kuwa ni matusi ndio sisi wananchi tunataka kusia. Ccm kama chama kilichoshikilia dola kilichakachua waliokwapua pesa za Epa na kwa sababu wao ndio walioshika hatamu walijua basi hakuna mahali watakapohojiwa. Sasa tunawaomba wanasiasa wayalete yote yaliyochakachuliwa na serikali kwenye mahakama ya wananchi ili tuyatolee hukumu hapo tarehe 31.
Tido anatakiwa kufahamu kuwa raia wana uelewa na wanaweza kupambanua lipi ni lipi bila kuhitaji tafsiri pori anayotaka kuwalisha.
 
Siku zote mnasema chama ni safi ila baadhi ya watu chamani ndio mafisadi. Sasa wale baazi yunu ndani ya chama wanapotajwa mnalia lia. Ccm acheni kutuchanganya. Tena chadema waelezeni wananchi wahoji zile pesa za Epa zilizodaiwa na Kikwete zimerudishwa, alifanya hivyo kwa mujibu wa sheria ipi na kama kweli walirudisha ni kina nani na ziko wapi.
Ccm siku ya kwanza tu wanalia kama vitoto, hii ndio inayotuzihirishia wananchi kwamba chama ndio fisadi na wala sio mtu mmoja mmoja kama walivyotaka kutuhadaa.
Chadema mnapaswa kuelewa kuwa adui yako pale unapomkanyaga akalia sana ndio pagonjwa, hivyo unatandika sana eneo hilo mpaka apoteze network.
 
Hivi kumbe maana ya kuleta vile vi-bylaws vya maadili ya kampeni ilikuwa ni kuhahakikisha CCM haikashifiwi? Hlafu kama ni kashfa mbona mkutano wa kampeni wa CUF ulikuwa unafanafana vijembe kama huo wa CHADEMA. Hivi si ni hawa walisema hawaiogopi CHADEMA kulikoni tena?
 
Hivi kumbe maana ya kuleta vile vi-bylaws vya maadili ya kampeni ilikuwa ni kuhahakikisha CCM haikashifiwi? Hlafu kama ni kashfa mbona mkutano wa kampeni wa CUF ulikuwa unafanafana vijembe kama huo wa CHADEMA. Hivi si ni hawa walisema hawaiogopi CHADEMA kulikoni tena?
CUF ni CCM B
 
hivi huyo kinana ana akili kweli? kesi ya EPa zilizo mahakamani ni za akina Maranda nk, za wale walio tajwa jangwani zao bado hazijafikishwa mahakamani, hivyo hakuna utata wowote. (kwani kagoda imefikishwa mahakamani? kwani RA, EL amefikishwa huko?
 
3. CCM haiwezi kuongelea mambo yaliyo Mahakamani

Wewe ''al shabab'' acha danganya toto. Na huko kwenye mahakama unajua wazi jinsi mgombea wenu alivyojijengea himaya. Asilimia kuwa ya Majaji kawateua yeye.
 
CHADEMA endesheni kampeni zetu vivyo hivyo; onyesheni madhambi yote ya CCM bila kumezea kitu. Ukaimua kupiga nyani usimwangalie usoni. Atakayesema hayo ni matusi aende mahakamani, na kama TBC wametumwa wasionyesehe mikutano yenu, nyie pelekeni mikutano hiyo hivyo hivyo ilivyo kwa wananchi moja kwa moja huku huku mkiwasisitiza wasisikilize tena vyombo vya habari kwa vile vimefunikwa na ufisadi kuficha ukweli huo kwa niaba ya CCM; hatua hiyo pia inaweza kusaidia kuua message za CCM zitakayokuwa zinatumwa kwa kutumia vyombo hivyo.
 
Lugha ya Kistaarabu ni Ipi? Hivi Mwizi utamwitaje?

Kwa hawa wa EPA utawaita kama vile JK alivyowaita alipohutubia Bunge Aug 6 2008: "Waliolipwa na BoT." Hivi kwa nini CCM wanapenda sana kudai lugha laini kuelezea kila madhambi makubwa dhidi ya wananchi wanayofanya nyuma ya mapazia endapo yanagunduliwa? Muibe nyie halafu mseme "Jamani, basi muwe wastaarabu kuelezea wizi tuliofanya! This is a really f****** country!!!

Kama mna ubavu si mpelekeni Marando mahakamani kama mlivyofanya kwa Mrema mwaka 1996 kuhusu ile kesi ya Mil 900. Maneno maneno ya nini? Mnataka kujenga hoja gani hapa kwa kusema kusema tu? Mnavyowakebehi wapinzani majukwaani na katika magazeti mliyoyanunua mnafikiri ni sawa? Ama kweli mkuki kwa nguruwe!!
 
Mi nadhani ni bora Chadema wakaachana na hayo matangazo ya TBC -- wawe wanawaumbua CCM majukwaani tu, nchi nzima, na ujumbe utafika. Nilijua tangu mwanzo kwa CCM kukazania maadili ni jitihada za kutaka madhambi yao yasimulikwe, hakuna kingine. Mmekaa madarakani miaka na miaka, sasa mnataka msisemwe madudu yenu mliofanya? Mimi nadhani viongozi wa Chadema muwe tayari kupelekwa mahakamani na serikali ya CCM. Msiogope kitu. Mwaka huu CCM lazima ivuliwe nguo zoote!!!! Wananchi tumechoka kuibiwa -- halafu mwaleta visingizio mara maadili, mara ustaarabu, mara ushahidi!!!! Usanii tu mnaofanya kutafuta kinga ya madhambi yenu -- hamna hata haya?
 
CCM wanaweweseka tu. Wanasisitiza maadili na ustaarabu, huku wao daima sifa hizo hawana -- tumeona juzijuzi tu ktk michakato yao ya uteuzi. Si wangeanzia kwao basi? Charity begins at home.... Safari hii nguo zote chini.....
 
MjasiliaMali Mzawa!

.
Wapinzani wa kweli jukwaa hili la campaign ndio uwanja sahihi wa kuyahubiri madhambi ya ccm, maana wanayo.
Kama ccm wangetaka siasa za kistaarabu walipaswa kuuacha wizi wa kodi ya wananchi, ama kuwashitaki wakwapuaji mfano wa Kagoda, Richond, deep green, tangold, meremeta, inport support nk.
Ccm wasitarajie makamanda wa ukombozi wa wananchi watatumia lugha ya kisanii kama wao. Hapa ni nyundo juu ya kidonda mpaka kieleweke.
Kama ccm wangelikuwa wastarabu wangemzushia Bashe kwamba sii raia? Haya ndio matusi!!
 
C C M ni wapika MAJUNGU Dr Slaa alipowataja MAFISADI wengi walisema watamshitaki kwani kuna hata mmoja alijitokeza baadae wale wote waliomtishia kumshataki sasa kesi zao zinaunguruma Mahakama ya Mkazi Kisutu

Tido hana lolote nae ni mmoja wao tuu CHADEMA walikuwa wanawajulisha UMMA CCM wavyoikwapua nchi yeye ansema MATUSI kwani yeye ndio amepewa jukumu na NEC kuto tafsiri ya meneno ambayo yanatumiwa katika kampeni ya VYAMA..? Kwanza waajiri wake wa zaman BBC watakuwa wamefadhaishwa sana na kile kitendo chake.
 
Mwaka huu imekula kwao..na Mbowe aliwatahadharisha kuwa hizo ni rasha rasha tu, mvua ya gharika inafuata.
 
....na kama TBC wametumwa wasionyesehe mikutano yenu, nyie pelekeni mikutano hiyo hivyo hivyo ilivyo kwa wananchi moja kwa moja huku huku mkiwasisitiza wasisikilize tena vyombo vya habari kwa vile vimefunikwa na ufisadi kuficha ukweli huo kwa niaba ya CCM; hatua hiyo pia inaweza kusaidia kuua message za CCM zitakayokuwa zinatumwa kwa kutumia vyombo hivyo.

Sasa hata magazeti ya Tanzania Daima,Raia Mwema na Mwanahalisi hayapatikani huku kwetu vijijini na kwenye net vile hayapo....sasa tutapata habari vipi?...inaonekana ITV wako CCM....msaada unatakiwa haraka sana wa kuweza habari besides za CCM
 
Back
Top Bottom