Elections 2010 Matusi au 'tuhuma' katika kampeni?

Nakubaliana na Mhe. Kinana kwamba Watanzania wengi si mabwege any more. Labda waliobakia mabwege ni wale wanaodhani sisi Watanzania hatujui kwamba CCM ikiongozwa na wale waliotajwa na Slaa pale Mwembe Yanga mwaka 2007 na waliotajwa tena na Mabere Marando juzi, walikwapua fedha za EPA na kuzitumia kwa Uchaguzi Mkuu wa 2005.

Nikiwa nimebahatika kuwa Muasisi wa hiki chama, na Mwenyekiti Taifa wa kwanza, natamka kwamba Jukumu kuu la CHADEMA na Mgombea wetu wa kiti cha u-Rais sasa ni kuelimisha umma wote juu ya ukweli wa UFISADI huu na kuwapa ujasiri wananchi wawakatae wale wanaodhani sisi ni mabwege.

HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!!!
 
Mimi ni mwanachama wa CCM , hili la kulia lia na kutojibu tuhuma linanipa wasiwasi kodogo.
Uongozi wa Chama Tawala unatakiwa ujibu tuhuma na si kuzifunika kwa maneno mazuri.
Tuhuma hizi vile vile ieleweke kuwa ni zinawahusu watu binafsi ambao wana uhusiano mkubwa na Chama, kwa nini watu hawa wasichukuliwe hatua?
 
CCM wapuuzi tu. wamezoea kupambwa na kusifiwa kinafiki. Wamekaa uchi halafu wanataka tuwapambe kwa kuwaambia kuwa wamejisetiri kwa kuvaa nguo nzuri sana!! Hapana hii haiwezekani. Tukiwaacha na sisi tutaonekana vichaa. Lazima tuwambie wamekaa uchi ili wakavae. Wezi lazima tuwaambie ni wezi. There is nowhere under the sun a black colour can be seen as white neither can the white colour be seen as black.
 
Huyu msomali asitubabaishe, yeye siyo raia kwani wakati ule suala la uraia wake lilipoibuka faili likaibiwa hapo uhamiaji na ndiyo ikawa mwisho wa sakata hilo,lakini ajue kuwa watz bado tuna kumbukumbu nzuri tu kuwa Kinana siyo raia. Kikwete na genge lake wanahusika na wizi wa EPA, kama wanabisha waende mahakamani
 
Katika Taarifa ya Habari ya Channel 10 na TBC1 Meneja wa Kampeni wa CCM Abdulhaman Kinana amedai:

1. CHADEMA wamevunja maadili waliyosaini kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu

2. Marando ni Mwanasheria Kaongelea mambo ya EPA yaliyo mahakamani kinyume na Ethics za Taaluma

3. CCM haiwezi kuongelea mambo yaliyo Mahakamani

4. Ni vema kutumia lugha isiyo ya matusi ili hata baada ya uchaguzi viongozi waendelee kuongea pamoja badala ya kukwepana.

5. Mbatia wa NCCR-Mageuzi naye anadai vyama viongelee hoja na si Watu - Kuzindua Kampeni baada ya Ramadhani (Mfungo)

Mimi sijui kama kuna kesi ya EPA dhidi ya CCM imefunguliwa. Ninachojua ni kuwa kuna individuals wamefunguliwa kesi.Marando ameituhumu CCM, so kwa vile hakuna kesi ya EPA dhidi ya CCM, matamshi ya Marando hayawezi kuathiri kesi zlizoko mahakamani ambazo haziihusu CCM. More particurlary kawataja Mkapa, Lowassa na JK, hawa hawana kesi iliyoko mahakamani. Ina maana hata JK asiongelee vita dhidi ya rushwa kwa vile kuna kina Mramba na Mgonja kesi zao ziko mahakani? Sijui huyu Kinana anafikiri kwa kichwa au anatumia nini. Huyo ndio manager wa kampeni wa kikwete, well, kweli sijui kama tutafika
 
Ushauri wangu wa bure kwa Kikwete.
Jibu hoja za Wapinzani wako sasa ili uwe material ya kuchagulika pia jibu sasa ukiwa bado madarakani; vinginevyo utajibu hoja hizo ukiwa mahakamani pale utakapokuwa umeshindwa kwenye uchaguzi. Chonde chonde Rais wangu jibu hoja zile sasa kabla hujachelewa maana baada ya octoba 31, hadhi yako itakuwa tofauti na sasa' Hao wa kina Kinana, Tido Mhando, Reginald Mengi na kila mtu watakugeuka kama walivyo mgeuka Mkapa baada ya wewe kuapishwa.
Jibu hoja za madai ya kushiriki kwenye ufisadi ili wananchi wako tukuone utakatifu wako au unatuacha tuamini ufisadi huu unaotuhumiwa kuwa wa kweli,
Twambie kama wamekusingizia wewe au kama Lowasa, Rostam na Mkapa hawakuhusika!
Hatutaki kusikia Kinana, Tambwe na makamba wakipayuka payuka kwa niaba yako wakati hawajatuhumiwa.
Jibu hoja kwa hoja ili tukuone kama wewe ni Material ya kuchagulika au la! Vinginevyo sisi tutaendelea kuamini kuwa wewe nawe ni mhusika Mkuu wa EPA SCAM wala si benefically tu.
Kalaghabhaho mwanakwetu!
 
kinana ndugu zake wote wapo kule Makuyuni Arusha na ndiko alipoanzia maisha na kuja mjini. Alikuwa mwizi wa wanama pori mpaka leo wale waliokamatwa bandari ya Tanga na kule Thailand na Ufilipino mambo yake hayo na ndugu zake.
 
Nakubaliana na Mhe. Kinana kwamba Watanzania wengi si mabwege any more. Labda waliobakia mabwege ni wale wanaodhani sisi Watanzania hatujui kwamba CCM ikiongozwa na wale waliotajwa na Slaa pale Mwembe Yanga mwaka 2007 na waliotajwa tena na Mabere Marando juzi, walikwapua fedha za EPA na kuzitumia kwa Uchaguzi Mkuu wa 2005.

Nikiwa nimebahatika kuwa Muasisi wa hiki chama, na Mwenyekiti Taifa wa kwanza, natamka kwamba Jukumu kuu la CHADEMA na Mgombea wetu wa kiti cha u-Rais sasa ni kuelimisha umma wote juu ya ukweli wa UFISADI huu na kuwapa ujasiri wananchi wawakatae wale wanaodhani sisi ni mabwege.

HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!!!

Ni kweli kabisa Mzee Mtei!!!

Hakika CCM inavuna matokeo ya kosa la KIFISADI kutumia fedha za EPA .... nafikiri jina zuri la ujinga huu ... Tuuite Ubwege... kwani ndilo jina alililolitumia Kinana...ingawa ninashaka akilitumia Dr slaa litaonekana ni matusi na TBC watazima matangazo.

Ni Ubwege kulea kwa mazoea tu, ufisadi hadi chama cha siasa kitumie fedha za wananchi kwa mtindo wa EPA, MEREMETA,DEEP GREEN na viongozi wa chama hicho wajilinde kwa jeuri ya uongozi tu ....wakitegemea wananchi wanyamaze...kiukweli hakuna mtanzania ***** kiasi hicho...

Jambo la msingi CCM ijitokeze hadharani na kuomba msamaha .... huko ndio kukomaa kisiasa na kuepusha vurugu kwenye Kampeni. Kuomba msamaha, waziwazi ndio msingi wa Kampeni za kiutu na kibinaadamu. CCM Ikiri hadharani kuwa kama chama ilifanya makosa .... Hilo ndilo jambo la kufanya na sio kukimbia kivuli chake kwa hoja laini za kuipaka CHADEMA matope...hilo ni kosa juu kosa la awali.

Nani adangayike?

Hayupo: Hatudanganyiki: .... Tunaitaka CCM kukiri KOSA LA EPA KWENYE KAMPENI ZAKE ZOTE ILI KUBORESHA AMANI YA NCHI KUELEKEA UCHAGUZI...!!!
 
Ukiona hivyo ujuwe kisu kimefika kwenye mfupa.Ukweli siku zote unauma. Ukitupa jiwe gizani ukisikia mtu akilia ujue limetua utosini. CCM habari ndiyo hiyo, nyie ni wezi kupitia vigogo wenu na utawala wenu wa mika mitano iliyopita ni batili.Kama kuna mtu ametukanwa aende mahakamani, acheni utoto huo.
 
Mimi sijui kama kuna kesi ya EPA dhidi ya CCM imefunguliwa. Ninachojua ni kuwa kuna individuals wamefunguliwa kesi.Marando ameituhumu CCM, so kwa vile hakuna kesi ya EPA dhidi ya CCM, matamshi ya Marando hayawezi kuathiri kesi zlizoko mahakamani ambazo haziihusu CCM. More particurlary kawataja Mkapa, Lowassa na JK, hawa hawana kesi iliyoko mahakamani. Ina maana hata JK asiongelee vita dhidi ya rushwa kwa vile kuna kina Mramba na Mgonja kesi zao ziko mahakani? Sijui huyu Kinana anafikiri kwa kichwa au anatumia nini. Huyo ndio manager wa kampeni wa kikwete, well, kweli sijui kama tutafika

Halafu pia Kinana anasema Marando kakosa ethics za ki-uanasheria kwa kuzungumzia habari za kesi mojawapo ya EPA anayeitetea mahakamani -- yaani ni kama vile anatoa siri ya kesi hiyo! kinana afahamu kuwa pengine mteja wake katika kesi hiyo Jeetu Patel kamruhusu kusema hayo kwamba yeye anaonewa tu kupelekwa mahakamani -- lakini wahusika wakubwa waliopnga kukwapua BoT ni hao akina Lowassa, JK, Rostam na Mkapa.
 
Hivi CCM (kupitia mwakilishi wao Kinana) kwa nini isisitize katika makubaliano kati ya UNDP (waliotoa hela za matamnagazo kwa vyama vyote, TBC na vyama kwamba maadili yanayotakiwa ni pamoja na kutokituhumu chama kingine kwa lolote lile? Leo nimemsikia JK akisema huko Rukwa kwamba vyama vya upinzani ni vya msimu tu! Chadema wanaweza kudai hili ni tusi kwani chama hicho kipo daima kinakitia makamasi CCM na kushiriki katika chaguzi na kushinda (eg Tarime in 2008).

Labda JK alikuwa anamaananisha vyama vingine vya akina Mbatia etc.
 
=====

-Alihusikaje na EPA?
-Kwa nini aliamua kuwasemehe anaodai walirudisha fedha za EPA?
[S=4]Mkuu wa nchi kutajwa katika kashfa kubwa namna hii ukakaa kimya si salama hata kidogo. Akanushe na wanaomsingizia wapelekwe mahakamani. Mbona mgombea wa CUF Tanga amekamatwa kwa kumkashifu Kikwete? Mbona Mtikila yuko mahakamani akijibu tuhuma za kumkashifu?

[/SIZE]

Sawia kabisa, ajiteetee sio atetewe na washabiki wake! Namshukuru pia Nd Kichuguu kwa kutuwekea clip ya Obama, kumbe haya yaliyofanywa na Chadema ni ya kawaida kabisa, kwa nini wanataka kutufanya Watanzania mabwege hawa CCM. Hatudanganyiki tena!
 
Mimi ni mwanachama wa CCM , hili la kulia lia na kutojibu tuhuma linanipa wasiwasi kodogo.
Uongozi wa Chama Tawala unatakiwa ujibu tuhuma na si kuzifunika kwa maneno mazuri.
Tuhuma hizi vile vile ieleweke kuwa ni zinawahusu watu binafsi ambao wana uhusiano mkubwa na Chama, kwa nini watu hawa wasichukuliwe hatua?

Muungwana huna sababu ya kutokujibu hoja! Mkapa na Kikwete wajitetee, wajisafisha majina yao. Lakini Mkapa anadaiwa bado ripoti ya mali zake baada ya kuwa Raisi, anaogopa

Hivi na wewe bado ni mwanachama wa CCM! Sikio la kufa mwanangu......
 
Hivi naomba kuuliza jamani! Hivi mtu akiiba kuku anaitwaje, akiiba mfukoni (pick pocket) anaitwaje? akiiba kwa mtutu anaitwaje? akiiba kwa forgery anaitwaje? Akiiba kura anaitwaje? Kiswhili cha majina haya ni nini? Je kuna tofauti kati ya mwizi msomi na asiye msomi? Kuna jina waitwalo wanasiasa na wasio wanasiasa wezi?
Naomba kujulishwa tu!
 
Nimefuatilia malalamiko ya CCM na TBC, nimeona msingi wa hoja zao ni kuwa chama fulani kinakiuka makubaliano ya Kampeni za Kistaarabu. Nimejaribu sana kufikiria walikuwa

  1. wanamaanisha nini walipowataka wenye vyama kusaini makubaliano ya Kampeni na Lugha za kistaarabu?
  2. Je kuna definition madhubuti au orodha ya mambo yaliyo au yasiyo ya Kistaarabu?
  3. Na je hii ni sheria, kwa maana mtu akikiuka anaweza kuhukumiwa?

Mana hili swala litalta mkanganyiko na hata vurugu kubwa sana!
 
Kukosa ustaarabu ni pale tu unposema CCM imekumbatia mafisadi. CUF hakusema hivyo na CCM ikawasfifia, CHADEMA wamelisema hilo wenyewe wanaitwa WASIO NA USTAARABU.
 
unaposema JK anakumbatia majizi na unaposema hela za EPA ndo zlitumika kwenye kampeni za Kikwete 2005 basi hizo sio kampeni za kistaarabu
 
CCM accuses rival party of dirty tricks
Monday, 30 August 2010 10:46


By Beatus Kagashe


Chama Cha Mapinduzi (CCM) yesterday castigated Chama cha Denmokrasia na Maendeleo (Chadema) for allegedly using abusive language during the launch of its presidential campaigns at Jangwani grounds on Saturday.


But the CCM campaign manager, Mr Abulrahman Kinana, told a news conference yesterday that the party was leaving the matter on the hands of the National electoral Commission (NEC) for further actions.


However, NEC director of elections, Mr Rajab Kiravu, told this paper that the Commission would not act until it get a petition from another party.


“We cannot take any action because NEC is not attending ant rally. How can we act on our own while we have no idea what transpired during the rally?” asked Mr Kiravu.


Mr Kiravu advised CCM to lodge a complaint if they want NEC to react.


Mr Kinana blamed Chadema leaders for blatantly attacking the CCM presidential candidate, Mr Jakaya Kikwete.


“We are have been upset by the way Chadema leaders insulted our candidate. It should be understood that CCM has not been taken to court (in relation to EPA cases) and it has no power to decide on those cases,” said Mr Kinana adding those involved in the cases would be dealt with in accordance with legal requirements.


He was reacting to statement by Chadema leaders that a number of CCM leaders have been taken to court in connection with grand corruption cases.


Mr Kinana called political parties to adhere to the code of conduct in which all parties agreed to adhere to the use of civilised language and not to incite people.


“Winning is the vital thing to every political party but let’s seek victory in a civilised manner such that after the election we remain a peaceful country. I people do not want to listen to your policies, don’t retort to insulting other people, you will be putting the country in a collision path,” he said.


He singled out a statement by Mr Mabere Marando who said he has tangible evidence on thefts of billions of shillings from EPA account of the Bank of Tanzania saying as a lawyer he (Mr Marando) was not supposed to publicly discuss the cases that are still in the courts.


Mr Kinana also criticised Chadema presidential candidate Dr Willibrod Slaa argument that CCM has failed in agriculture, education and health.


He called those saying they will provide free education to come out with evidence on how they were going to implement that.



Source: The Citizen
 
Ivi kwa nini Chadema wasifungue kesi juu ya huyu jamaa?Kwani shida ipo wapi? Si wana wanasheria. Kampeni inaendelea, huku wakiwa na kesi na TBC! Tuachwe kunyanyaswa bwana! Kila siku ni kelele tu! Lazima tuonyeshe hawa jamaa kuwa na sasa tuna-action!
 
Back
Top Bottom