Matumizi ya "Dr" kwa wanasiasa wetu ni PhD au vumbi?

dr mary nagu
dr nelson ruta
dr nchimbi
dr makongoro mahanga
msemakweli upo na mafisadi wa elimu?
 
Nakerwa na viongozi na wanasiasa hasa hao wanaotumia initial za "Dr" kwenye majina yao wakati rules haziruhusu.

Nakumbuka TCU iliwahi pia kuweka sawa hili kuhusu matumizi ya hii initial na kusisitiza kama una Degree ya Heshima ya Udaktari basi hupaswi kutumia hii initial ya Dr.

Lakini cha kushangaza aidha wanaitwa na wafuasi wao au wanaojipendekeza au wao wenyewe, lakini wahusika wanakaa kimya tu na kuacha majina yao kutumika hata kwenye vymbo nyeti kama bunge.

Nakerwa na jambo hili linaonyesha dhahiri wanasiasa wetu wasivyo makini na kupenda kusifiwa na kukumbatiwa kwa msifa ya bandia.

Kakamueni PHD tujue kweli na nyinyi ni miamba na mmnazo za kihalali na za kweli sio za kununua kama tulivyoona kwa watu maarufu kama wafanya biashara na viongozi wa dini.

Ulimbukeni uawasumbua wanasiasa na viongozi wetu. Nchi za wenzetu watu wana Phd zao lakini hujikuti wakijiita Dr hata siku moja. Imagine Lyatonga nae ni Dr!
 
Hata Slaa na kale ka JCD kake ka kusoma misa, hapaswi kujiita Dr!
Sijawahi kucheka kama leo........eti ka JCD kake ka kusomea misa .teh-tehe tehe. Wanasiasa wa Tanzania kwa kupenda sifa! hivi mrema anajua neno "PhD" lina maana gani?
 
Wakati nasomea PhD yangu nilikwenda nyumbani kusalimu. Baba yangu akaniambia kuwa kuna mama mmoja anataka kuniona siku nyingi. Alipokuja huyo mama akaanza kunieleza matatizo yake mengi ya kiafya. Ikabidi nimueleze kuwa mimi sio daktari wa kutibu magonjwa bali nasomea udaktari wa filosofia. Nilivyomuona alionekana kuwa hakunielewa vizuri. Vivo hivyo na hao wanaopenda kutumia Dr. kila mahali hawaelewi vizuri maana ya PhD.

Nadhan lengo lako ni kutueleza umesoma PhD ukaamua utupige fix kiaina
 
obama ana phd lakini hatumii DK, raila odinga , kibaki wana phd za honoraria nyingi tu, hata museveni , lakini huwezi sikia dr, museveni, dr,raila huu uzumbukuku ni wa hapa TZ,hata mkapa, nyerere walikuwa nazo lakini hawakupenda huu uzumbukuku wa jk na vilaza wengine.

kuna haja pia ya kufanya vetting ya hivyo vyuo vinavyotoa hizo phd za wansiasa huenda kuna hongo fulani
Mwikimbi Obama hajawahi kuwa na PhD
 
Last edited by a moderator:
Dr Aisha Kigoda, ambaye ni just RMA sijui medical assistant
Dr. Nchimbi.....na PhD yake ya bogus online university
Afadhali hata huyo professor maji marefu labda amekuwa prof. kwa tunguri na miujiza ya ajabu.
 
Na ni mabingwa wa kupiga majungu wasomi wa kweli wanaoingia kwenye siasa kwa kuwaambia humu sio kwenu, nendeni vyuo vikuu, nchi hii haina mahitaji ya viongozi wakuu wenye PhD, lakini ni hao hao ndio wapo mstari wa mbele kwenda kuokoteza PhD majalalani;
 
Na ni mabingwa wa kupiga majungu wasomi wa kweli wanaoingia kwenye siasa kwa kuwaambia humu sio kwenu, nendeni vyuo vikuu, nchi hii haina mahitaji ya viongozi wakuu wenye PhD, lakini ni hao hao ndio wapo mstari wa mbele kwenda kuokoteza PhD majalalani;

ndugu yangu, mbona unanichekesha? waende vyuo vikuu GPA zinatosha? labda unamzungumzia Lipumba na wengine wachache sana!!!
 
Wanabodi,
Nimeshangaa kusikia sifa za Rais wetu zikiongezeka na kuwa kama za maisha bora kwa kila mtanzania.
Kwa kuitwa Mheshimiwa hiyo nikikubaliana nayo kwa kazi kubwa iliyofanywa 2005 ya ushindi wa kimbunga na chaguo la Mungu akawa Rais akaukwaa Uheshimiwa ambao nimesikia hata mbunge wangu na wakuteuliwa ni Waheshimiwa msumari wa mwisho ni diwani wangu Makundi wa mwika naye kwa nafasi ya sasa baada ya kustaafu Jeshi na kura kutotosha ubunge 2010 zikatosha udiwani naye kwa nafasi ya sasa ni Mheshimiwa kutokana na maelezo hayo nakubaliana na Uheshimiwa nimeusikia sana.
Swali langu kwenu ni baada ya kusikia Rais wangu kapiga hatua kuelekea maisha bora kwa kila mtanzania kawa mfano ni Docta.
Hivi itatuchukua muda gani kuwa docta kama yeye
Je? Jk ni docta wa nini falsafa au nini wanajamvi
Inawezekana ukalala undergraduate ukaamka Dr
Kuuliza si ujinga mods naombeni muiche nielimishwe jk ni modal wa sie kujifunza nataka nijifunze hili la taaluma.
 
Back
Top Bottom