Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani October 28, 2012

Kwakweli matokeo hayaridhishi.. pamoja na hila zote za waoM hilo haliwezi kua utetezi maana hakuna aliekua hajui mbinu zao na kama hatuwezi zikabili hizi mbinu kwenye kata 29.. twawezaje kuuaminisha uma kwamba tutadhibiti nchi nzima? Nahitadi CDM mje na majibu.

Nahitaji pia mje na analysis ya maana ikiwa ni pamoja na idadi ya kura zote zilizopigwa katika hizi kata na kiasi CDM imepata ili tuweze jitathmini ingekua uraisi tungekua wapi.. pia tuweze kutathmibni chama kimekua kwa kiasi gani na ukilinganishwa na rasilimali zilizoelekezwa kwenye kukucha chama katika kata hizo. Mweze kutuenzela na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wenu, ni nini fundisho na nini mikakati yankujirekebisha.

Tumeongeza kata lakini ukweli ni kinyume cha matarajio. Narejea kauli ya mkiti.. tutazoa kata 20 kati ya 29... aje hapa yeye au Mnyika msemaji wa chama atuambie Kulikoni?

Uwajibikaji kwanza....

Sitaki kupinga hoja yako ni nzuri, lakini tunapo sema cdm watuambie sababu za kushindwa ni zipi, hapo kidogo napata taabu, kwa sasabu cdm ilivyo kwa sasa inajengwa zaidi na wanachama wake wote kuliko kutegemea viongozi pekee, mimi ni mmoja wa wanachama niliyekuwepo kwenye michakato ya kampeni wilaya ya mbozi na cdm tumepoteza kata zote mbili

Kwa uchaguzi ulivyokuwa ni zaidi ya kupiga kampeni tu, kuna mambo mengi yanayopelekea kukosekana ushindi, 1. Rushwa 2. Uelewa mdogo wa wapiga kura(mfano: watu wengi utakuta wanakuambia mama yako hata kama ni mbaya uwezi ukamkataa) 3. Vitisho ( watu wamepigwa na kulazwa hospitali) 4. kukosekana kwa utawala bora ( jeshi la polisi na baadhi ya viongozi wa serikali kusaidia ccm) na mengine mengi, tusilaaumu sana zaidi ya kujipanga kama watanzania wote kwa ujumla tujipange katika katiba mpya haya mambo yawekwe sawa
 
Aisee ccm wanambinu nyingi za kujipatia ushindi ambazo ni kama za shetani.ili kuishinda inatakiwa mbinu za ziajda.katika kata nyingi walizo shinda ccm walitumia mbinu zifuatazo 1 walikuwa na orodha ya wapiga kura katika kata ambayo walikuwa wanamfuatilia mtu mmoja moja nyakati za usiku na kumwachia kitu kidogo 2 kuwahonga wapiga kura pombe hasa wa vijijini 3 kuwatiya woga wananchi kuwa wasichaguwe vyama vya upinzani vitaleta vita hapohapo wao wenyewe wanageuka kwa kutumia vijana wao wanawashambulia wananchi majira ya usiku ambao wanajitambulisha kwao kuwa wao ni chadema au chama chochote cha upinzani.wakisha fanya hivyo wanakuwa watu wakwanza kwenda kulalamika polisi.4 kutumia jeshi la polisi kuwatisha wananchi .mara nyingi jeshi la polisi linakuwa lipo mahali hapo kwa ajili ya usalama lakini ccm wanageuza nakuwaaminisha wananchi kuwa polisi wameletwa na wao kwa ajili ya kuwalinda wananchi ili wasiendelee kushambuliwa na chadema 5 wanatumia uelewa mdogo wananchi.wanachi wengi wako vijijini ambao wengi wao tangu kuzaliwa kwao wao wanacho kijuwa ni ccm tu hakuna kitu kingine. Kundindi hili lina watu wengi na ni vigum kulibadilisha na ccm imelifanya kuwa mtaji mkubwa sana kwa kutumia ujinga waliyonao.wengi wakundi hili ni wazee,watu wamakamo na waumri wakati kundi ambalo ni la wapiga kura lakini ni wagum kuiacha ccm.dawa yakufisha hili kundi ni kutowa elimu kwa vijana na kundi la watoto wanao onekana kuwa wapenzi wa vyama vya upinzani.
 
Sitaki kupinga hoja yako ni nzuri, lakini tunapo sema cdm watuambie sababu za kushindwa ni zipi, hapo kidogo napata taabu, kwa sasabu cdm ilivyo kwa sasa inajengwa zaidi na wanachama wake wote kuliko kutegemea viongozi pekee, mimi ni mmoja wa wanachama niliyekuwepo kwenye michakato ya kampeni wilaya ya mbozi na cdm tumepoteza kata zote mbili

Kwa uchaguzi ulivyokuwa ni zaidi ya kupiga kampeni tu, kuna mambo mengi yanayopelekea kukosekana ushindi, 1. Rushwa 2. Uelewa mdogo wa wapiga kura(mfano: watu wengi utakuta wanakuambia mama yako hata kama ni mbaya uwezi ukamkataa) 3. Vitisho ( watu wamepigwa na kulazwa hospitali) 4. kukosekana kwa utawala bora ( jeshi la polisi na baadhi ya viongozi wa serikali kusaidia ccm) na mengine mengi, tusilaaumu sana zaidi ya kujipanga kama watanzania wote kwa ujumla tujipange katika katiba mpya haya mambo yawekwe sawa

Kamanda umesema vizuri na mbinu hizo chafu zilifahaika maana hazijaanza juzi wala jana. My concern ni kwamba tulijiandaaje kukabiliana na hujuma hizi? tutawaaminishaje watanzania kwamba tutaweza kabiliana na hizo hila na uelimishaji unaotakiwa kabla ya 2015?

Natambua ni majukumu yetu sote ila mikakati yote ya chama lazima yajielekeze katika kupambana na mbinu hizi na lazima mikakati hiyo ijidhihirishe pasipo shala kwamba inazaa matunda.
 
Mkuu hayo yote yanajulikana, kitu muhimu ni kujipanga vilivyo kwani mashabiki hatukutaraji matokeo hayo, hasa ukizingatia hapa JF washabiki wa CCM hawakohoi na mitaani hapa Dar kama hamna watetezi wa CCM. Hivyo tulitaraji makubwa.

Chadema inahitaji zaidi ya mashabiki sasa hivi. Chadema wanahitaji wanachama ambao wanaweza (a) kutambua viongozi kwenye jamii yao, wenye uwezo wa kuleta mageuzi na kuongoza wananchi kupata madabiliko wanayohitaji na (b) kushawishi na kutia hamasa watu wajitokeze kupiga kura kuchagua wagombea hao. Tuwe sehemu ya mabadiliko na mageuzi tunayotarajia. Pamoja tunaweza. Play your part!
 
Binafsi sina updates zozote za kilichojili jana kwenye zoezi la uchaguzi wa madiwani nchini wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi kutokana na sababu tofauti tofauti. Naomba mtujuze...labda mimi niko nyuma ya wakati. Mniwie radhi.
 
Kwa ukweli hili limethibitika katika uchaguzi wa madiwani ..sehemu ambazo chadema wameshinda kulikuwa na mpasuko au makundi au kutokuelewana katia ya wanachama wa ccm..lakini sehemu zote ambako ccm walikuwa kitu kimoja wamechukua wameweka waa...
Jipangeni upya chadema chama cheni ni kama kampuni ya biashara....m4c ni njia ya watu kujitengenezea ela za michango ya wahisani na wananchi.
 
Cdm endeleeni na m4c arusha mwanza tu...mana ndo mnakoona kunawachama ..... Kata 26 mnatapata 5 nd mnakuja mbele ya watanzania et chama pendwa kinapendwa na chama cha matumaini..hizo ni siasa tu za kwenye vyombo vya habari
 
Kamanda umesema vizuri na mbinu hizo chafu zilifahaika maana hazijaanza juzi wala jana. My concern ni kwamba tulijiandaaje kukabiliana na hujuma hizi? tutawaaminishaje watanzania kwamba tutaweza kabiliana na hizo hila na uelimishaji unaotakiwa kabla ya 2015?

Natambua ni majukumu yetu sote ila mikakati yote ya chama lazima yajielekeze katika kupambana na mbinu hizi na lazima mikakati hiyo ijidhihirishe pasipo shala kwamba inazaa matunda.

Hivi ni M4C au M4D?
Poleni sana.
USHINDI UTAKUJA!
 
Back
Top Bottom