Matokeo ya Uchaguzi Igunga: Radio One

Status
Not open for further replies.
Habari hizi ni za kweli kabisa CDM imeshinda Igunga nimewasiliana na mtu ambaye yupo kwenye chumba cha kuhesabia kura, kwa sasa kinachofanyika toka usiku ni kuingiza matokeo kwenye zile computer za Riz One ili ichakachue. Mkurugenzi amesema matokeo saa 8 na watumishi wa Halmashauri ambao wana umri mkubwa(wazee) washeambiwa warudi majumbani kwao kwa kuwa hawana uwezo wa kukimbia hali itakapokuwa ngumu baada ya kuchakachua matokeo.
 
Chadema inasemekana imeshinda kwa kura zaidi ya 3000 na CCM kuangukia pua na ndiyo maana hadi sasa NEC haijatoa matokeo rasmi. Dr Kafumu haamini macho yake na amekataa kusign.

Ngoja tusubiri saa 8 ifike
 
Ataamini vipi na akipiga hesabu hela zote alizoiba kwenye miataba ya kifala ya madini zimeyeyuka na ubunge hakuna,zaidi my wife wake alijinyenyekesha kiasi cha kupiga magoti jukwaani lakini hakuna kitu..

Kalaghabaho!!!!
 
Nikamwelewa Dr Kafumu kukataa kusaini kwa point 2.
1. alisha somo Twitter ya Zitto akikiri Chadema imeshindwa
2. FFU wamewadhalilisha tena waislamu maana katika kupiga mabomu na kumwaga maji ya washa washa vijana kadhaa wa kiislamu wamepoteza baraghashia zao na wanawake wachache wa kiislamu waliokuwa wanapita karibu wamefunuliwa hijabb na hivyo kudhalilishwa kidini. Astaghafululah!!! Takbiri, Takbir!!!!

Astaghafululah! Masheikh tutakutana kesho kutoa tamko rasmi. BAKWATA hatutamtambua mbunge atakayetangazwa.
 
Bado wa cuf hatujamsikia....... Cuf Wapi? Sema kitu..... cuf wameshinda kwa ngapi?
Aisee tuache porojo waungwana Tunahitaji matokeo ya kuaminika..... hatutaki tetesi sasa... maana mtatuua wengine kwa presha
 
Nikamwelewa Dr Kafumu kukataa kusaini kwa point 2.
1. alisha somo Twitter ya Zitto akikiri Chadema imeshindwa
2. FFU wamewadhalilisha tena waislamu maana katika kupiga mabomu na kumwaga maji ya washa washa vijana kadhaa wa kiislamu wamepoteza baraghashia zao na wanawake wachache wa kiislamu waliokuwa wanapita karibu wamefunuliwa hijabb na hivyo kudhalilishwa kidini. Astaghafululah!!! Takbiri, Takbir!!!!

Kuhusu zitto kukiri kushindwa, hili ni uharifu wa kimtandao, watu wameingilia akaunti za watu kama regia fb, zitto twita, nape jf hata mimi ni hacked lakn najaribu kupost
 
Hebu tuwe serious na tuache ushabiki, Zitto amekiri CDM kushindwa kwa Kupata 45% na CCM 49% . Kama naibu katibu mkuu wa chama anakiri kushindwa nyie data hizo mnazitoa wapi?
 
Hebu tuwe serious na tuache ushabiki, Zitto amekiri CDM kushindwa kwa Kupata 45% na CCM 49% . Kama naibu katibu mkuu wa chama anakiri kushindwa nyie data hizo mnazitoa wapi?
acha kuleta habari za vijiweni, Zitto ndiye mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi? umelipwa bei gani kwa kazi hii ya kuandika habari ya Zitto, Zitto, Zitto- unakera watumiaji wa mtandao huu.
 
Mimi nilishangaa jana watu kuanza kupata matokeo masaa mawili tu toka vituo vifungwe wakati baadhi ya vituo vilikuwa bado hata kuanza kuhesabu. Hii ni mara ya kwanza kwa CCM kuanza kutangaza ushindi kabla ya tume, wamejitahidi kuwaandaa watu kisaikolojia nasikitika hata Invisble nayemwamini aliingia kwenye mtego huo, sikumwelewa alikuwa na maana gani aliposema ubishi umeisha angali akijua yale matokeo yalikuwa hayana reliable source
I have updated the 1st post. Hopefully ubishi umeisha!
Sasa kuna watu wakishirikiana na mods wanataka watuaminishe Zitto kakubali matokeo hadi mods wameipa Title ya Breaking News na coverage kubwa. Tafadhali tusijirahisi hivyo kugandamiza demokrasia next time hatutaaminiwa.
 
'Subira yavuta heri, ila kwa hili.. Mh! Nadhani subira yavuta shari'
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom