Matokeo ya sensa: Tanzania ina watu 44,929,002!

wewe hujawajua wvikwazo vya maendeleo ya taifa hili.KAA KIMYA,
YAAN MTU SOHESABIWA NDO KIKWAZO CHA MAENDELEO NA UNAAMINI HILO KAKA/DADA?

Kwa namna fulani anaweza akawa sahihi... mfano mdogo tu hapo home kwenu, hivi kama hujui mpo wangapi unaweza ukajuwa unune mchele/unga kilo ngapi ili utowatoshe wote? Sasa expand haya maelezo kwenda kwenye madawa, idadi ya hospitali, wapi pajengwe hospitali ya kutibu magonjwa gani, wapi pajengwe shule ngapi, wapi panahitaji ambulensi ngapi...etc...etc
 
nimehuzunishwa na star tv na itv badala ya kurusha tukio hili la kitaifa wao wanasubiri uzinduzi wa ilani za ccm
 
Kweli Zanzibar ni mzigo kwetu. HAWA ndo tunawapa 50:50 katika wajumbe wa Tume ya katiba na wabunge kibao? Bora waende zao wawe kama Somalia au Chad

ZNZ ni kadogo with a lot of potentials. Ndio maana Mainland hawataki kuiachia! Hivi wewe na Nyerere nani ana akili zaidi?
 
taarifa kutoka kwa mtonyaji anasema sensa ilikuwa na kipengele cha dini ila kilikuwa kimefichwa. Naskia matokeo ni kwamba waislam ndio wengi, hasa wale wa suruali fupi
 
huu usanihi utaisha lini jamani,hata kwenye mambo ya msingi? yaani kutangaza nako uzinduzi?kwanza matokeo yenyewe si ya kweli.
 
Hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma, ilifaa wahusika wakutane na vyombo vya habari tu, then taarifa zingetufikia badala ya kufanya sherehe zisizo na maana
 
hahahahah wamesema wenye suruali fupi wako wangapi???
taarifa kutoka kwa mtonyaji anasema sensa ilikuwa na kipengele cha dini ila kilikuwa kimefichwa. Naskia matokeo ni kwamba waislam ndio wengi, hasa wale wa suruali fupi
 
walijuaje kuwa wazanziba wako 1,303,568 mbona mimi sikuulizwa kama ni mtanganyika ama mzanziba..
 
Assallam alleykum ni neno la kiarabu lenye maana ya "Amani iwe juu yenu" kwa hiyo ni kama kutakiana amani. Ila bwana yesu asifiwe ipo too specific na haiwezi kutumiwa sehemu nyingine.

Too specific vipi mkuu? Mungu kupewa sifa ndio too specific?!
 
Kuna shida kidogo kwenye hii idadi. Kwa muda mfupi tu niliochunguza kuna familia tano ambazo watu wa sensa hawakufika kabisa. Je kwa nchi nzima watakuwa wangapi?
 
kaka naona hukuwa na ratiba ya shughuli hiyo na hii inatokana na kuvamia shughuli za watu, si kweli kwamba shughuli ilitakiwa kuanza saa mbili kama ulivyotangaza. rais alifika saa 4 na dadika 17 kwa hiyo alikawia (na si kuchelewa) dakika 12. muda mwingine tuwe tunaongea ukweli wa mambo.... angalia viambatanisho ndo utaona namna ulivyo muongo.... limekushuka!!!!!!!!!!!

Ratiba ya Uzinduzi.JPG Kuwasili Mgeni Rasm.JPG


Leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar Rais Jakaya Kikwete atazindua matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwezi August, 2012.

Nimeona nifike mwenyewe pasipo kupenda baada ya lengo langu la kupata huduma kwenye ofisi za umma leo kushindwa baada ya kutokukuta wahusika karibu wote kisa ni kwamba meagizwa wote waende kuhudhuria tukio hili tena wamepewa na posho!!

UPDATES
*Tukio lilitakiwa lianze kufanyika toka saa mbili asubuhi lakini mpaka sasa(saa nne na nusu) rais hajafika japokuwa watu wameshafika, hakuna cha maana zaidi ya burudani nzito ya Muziki inayoporomoshwa kwa fujo(Kama Bonanza)

*Rais ameshafika na tukio limeanza kwa mratibu wa sensa kitaifa na mwakilishi wa UNFDA kutoa hotuba fupi.

*Waziri wa fedha Mgimwa, Balozi Seif Idd, Pinda nao wametoa hotuba za shukrani na mchakato wa sensa ulivyokwenda.

*Rais sasa anaongea, anasema matokeo ya leo ya sensa ni ya awali(General) mengine yatoka baadaye mwezi wa Pili mwakani(Details eg. Ratio of male and Female) kisha mwezi wa nne(At district level)

Tanzania ina jumla ya watu 44,929,002!

- Tanzania Bara 43,625,434
- Zanzibar 1,303,568
 
Back
Top Bottom