Matokeo ya sensa: Tanzania ina watu 44,929,002!

[h=5]Sensa ya Tz kwa mwaka 2012 ni watu milioni 44,929,002
Uzazi wa mpango hureeee![/h]
 
Nimemsikia mkuu wa kaya akisema eti tukiendelea kuzaliana wengi serikali itakuwa na mzigo wa kuwahudumia watanzania. Kumbe anafanya makusudi kuweka baraza la mawaziri kubwa huku akijua wao ndo wanaotumia rasilimali zetu pamoja na watoto na ndugu zao.
 
Nilihesabiwa na mhudumu wa guest tena aliniambia nijaze nionavyo maana walimkabidhi fomu naye hajui kusoma wala kuandika. Taarifa hizi zina mapungufu na Mkulu kazoea kuzindua vitu 'fake' ovyo kama alivyofanya kwa upimaji ukimwi na kupewa majibu 'fake' hapahapa Mnazimmoja
 
Watanzania tumetakiwa tupunguze kuzaana na kuongeza juhudi katika kufanya kazi.
Hakuna haja ya kupunguza kuzaliana wakati tuna rasilimali za kutosha!kikubwa ni namna gani nzuri ya kutumia vizuri hichi tulichonacho kwa faida ya wote!
 
Tupo milion 44 laki 9 ishirin na 9 elfu na 2, Tanzania bara watu milion 43 laki 6 ishirin na 5 elfu na mia 4 thelathin na 4. Zanzibar watu milion 1 laki 3 na elfu 3 mia 5 na sitin na 8

Tanganyika 97% wakati Zanzibar ni 3% ya wakazi wa Tanzania ipo haja ya kutafakari namna ya kugawana fursa za uwakilishi na raslimali
 
Mh! Haya matokeo sidhani Kama ni realistic nahisi kuna Watu hawajahesabiwa hapa Maana approximately ni 45 mill tu ist possible kuna ongezeko la Watu mill 5 tu tokea sensa uliyopata?
 
Assallam alleykum ni neno la kiarabu lenye maana ya "Amani iwe juu yenu" kwa hiyo ni kama kutakiana amani. Ila bwana yesu asifiwe ipo too specific na haiwezi kutumiwa sehemu nyingine.

Then Jesus came to them and said, "All authority in heaven and on earth has been given to me. Mathew 28:18
 
Matokeo yanzazinduliwa jamani kuna nini katika nchi hii! mie nilitegemea yatangazwe kama wanvofanya kwa matokeo ya mitihani sasa duuu!

Na kama wanazindua watakaa siku ngapi hapo mnazi mmoja wakiendelea na maonyesho au uzinduaji kaaaaaaaaaazi kweli kweli!

Walitaka kuwatangazia waliogoma kuhesabiwa kuwa sensa haikuathirika pamoja na mgomo wao.!
 
najiuliza sana,tena sana

kwani asalaam aleykum ni ishakua salam official ya kiserikali??
Kwa maana karibia wazungumzaji wote nimewaskia wakija na salam ya namna hii
kuna nin hapo??

Ingekua inasemwa bwana yesu asifiwe sana then ikabaki hivyo hivyo haitaleta ukakasi??

umeonaee,hata mimi nimejiuliza kama ww mkuu,kazi bado ipo.
 
Back
Top Bottom