Matokeo ya Form four 2007

Hivi Mitihani ya sekondari ni swala la Muungano? Nilidhani elimu ya Juu tu ndo swala la Muungano! Inakuwaje matokeo pia yana shule za Visiwani na Bara?

Naomba mwanga zaidi

Mzalendo, mi binafsi sina hakika ni mambo gani ya Muungano na si yapi ya mmungano..ni mchanyato maalum ambao nahisi wanauelewa wachache sana...labda ndo maana pia hata haya mazungumzo ya CUF na CCM kuhusu 'kero' za Muungano hayaelekei kufikia mwisho!
 
Siku hizi mambo yameanza kubadilika na wengi wanaliona hili. Career na maisha ya ndoa ni mambo mawili ambayo yanahitaji careful balance. Ni vyema kila mtu akalijua jukumu lake katika ndoa na kuheshimiana. Tatizo especially hawa akina dada zetu wanaosoma equality kwenye human rights wanataka wailete hiyo theory nzima nzima ndani ya nyumba na hapo baba anakuwa mbogo. Its hardly possible to apply western theories in our African traditional setting bila kuzifanyia marekebisho kiasi... I guess kama mdada au mama una elimu yako you can careful craft what you want by negotiating with your partner than using threats of "usinibabaishe nazijua haki zangu"..Harafu naturally mwanamke akishamzidi kipato mume lazima mzee awe na inferiority complex. Its natural. So its for mama/dada kukaa na kumuonyesha kwa vitendo kwamba her kipato has nothing to do with their love and life. Lakini wengi wanashindwa. Na walioweza hata ukikutana nao utawajua tuu, they are so intelligent, wanajiamni na wana roho za kimama typical!

So my sisters as we move forward you should balance between the two because your career is very important so is your family life. Its all about genuine compromise.
 
Hivi Mitihani ya sekondari ni swala la Muungano? Nilidhani elimu ya Juu tu ndo swala la Muungano! Inakuwaje matokeo pia yana shule za Visiwani na Bara?

Naomba mwanga zaidi

kiukweli tumeungana kwenye elimu ya juu tu ila kwa hiari yetu tukaomba wenzetu tujiunge nao ktk mitihani tu ya O level na A level

ila tunauwezo kisheria kutunga mithani hio kwa ngazi hiyo.

na nntegemea hilo wizara ya wema inalizingatia hili.

lkn suala haya mambo ya ss kuwa kila uchao kuwa kimeo kuna mkono wa makusudi wazenji tuwabigije hawa wasiwe na sauti
 
Mtu wa Pwani,

Ahasnte kwa ufafanuazi- tu watu wamoja kama Watanzania. Hizo shule silizofanya vibaya- hebu zianike hapa- je ni za Pemba au Unguja?

Sii walisema kuna 2,100 waalimu wako idle Zenj- na hakuna shida ya waalimu?

Waziri wa Elimu Visiwani anasema ni sababu zipi zinafanya matokea haya mabaya?
 
shule zote za unguja na pemba

hilo suala la kusema kuna walimu hawana kazi ni mambo ya kisiasa na mm masuala haya ya kujidai huna shida wakat unazo zinaniudhi ss tuna wahitaji sana walimu lkn si kama wenzetu kwa hiyo isemwe vizuri kuwa tunaweza kujibana ili kupunguza tatizo lenu
 
Matokeo yanaonekana sasa, ingependeza kama wangeweka uchambuzi wa muelekeo, wangapi walijiandikisha, wangapi walifanya, wangapi wamefeli (division 0) wangapi wamepata div 1 2 na 3.Uwiano na miaka iliyopita, regional brakdown, rural urban breakdown, boys /girls breakdown, shule za wavulana /shule za wasichana breakdown, shule za dini breakdown, top 20 and so on.

Hivyo hizi data zingeweza kueleweka zaidi.Walivyofanya sasa wamelundika data tu hata hatujui kama kuna maendeleo mazuri au tunafanya vibaya zaidi kuliko miaka ya nyuma kwa mfano.

Ukiwa na data hizi na database ni kazi rahisi sana kutengeneza hizi analytical breakdowns.
 
Nilipokuwa napitia matokeo ya Form Four leo, nimegundua kuwa shule zetu zinatofautiana sana jinsi watoto wanavyopasi mitihani.

(a) Shule nyingi za wasichana tupu zilifanya vizuri sana kuliko shule nyingi za wavulana tupu na zile za mchanganyiko.

(b) Seminari za katoliki zimeendelea kufanya vizuri kwa jumla.

(c) Shule nyingi zenye kutumia majina ya wanasiasa zimefanya vibaya sana.

Sujaangalia influence ya geographical location ya shule, lakini sidhani kama hii ina effect yoyote.

Kutokana na shule nyingine kupasi kwa kupata divison 1 by 99.9999% wakati kuna shule ambazo zimefanya vibaya sana kwa kupata chini ya Divion III huku asilimia zaidi ya 85% ya wanafunzi wake wakiwa na division IV au F inaonyeshasa kuwa tatizo kubwa katika elimu yetu siyo mfumo wetu wa elimu bali ni namna tunavyoendesha elimu yetu.

Shule ambazo zinafanya vizuri ni zile zinazoendesha elimu katika msingi wa elimu kikwelikweli. Shule ambazo zinaendesha elimu kwa misingi ya kisiasa zinafanya vibaya. Nadhani wakati umefika kwa wanasiasa kugundua hilo.

Kwa maoni yangu, njia ambazo elimu inaendeshwa kisiasa ni pamoja na:

Kuendesha shule bila kuwa na waalimu pamoja na vifaa vya kufundishia kwa nia kuongeza namba kwenye takwimu za serikali.

Wanasiasa kutembelea mashule mara kwa mara ili kupata photo opportunities bila kutambua kuwa maandalizi ya kuwapokea pale shule huchukua muda na raslimali nyingi za kufundishia.

Kutumia waalimu underqualified kielimu na kimaadili na kuwalipa waalimu chini ya mahitaji ya majukumu ya kazi zao kwa lengo la
kuongeza namba katika takwimu za serikali.

Nina imani wana JF wanajua njia nyingine zitumikazo kudumaza elimu kwa sababu za kisisasa.
 
wakati shule ya St. Mary imeanza nilikuwa Mbeya na nina bahati ya kuweza kutembelea shule hiyo. Jambo moja ambalo niwahakikishie kuna nidhamu ya ajabu pale hadi unaweza kukimbia.
 
Mimi nadhani hawa wakatoliki wana kasiri ka aina fulani maana shule zao siyo tu TZ hata US, Uingereza, India nk zinafanya vizuri sana. Wenyewe wanaita "Catholic education". Na nina uhakika hawasali rozali kutwa nzima. Ni nini ambacho tunaweza kujifunza?
 
Jambo moja la wazi katika mfumo wa kikatoliki ni kuwa wanapiga vita ngongo kwa nguvu sana kwa vile watawa wa kikatoliki wanaondesha shule hizo wanatakiwa wasijihusishe na mambo ya kujamiiana kabisa.
 
Asante Kichuguu kwa kujaribu kuangalia trend kwenye haya matokeo.

Ama kweli kuna shule na shule! Sehemu kubwa ya hizi shule zina matokeo ya kila mwanafunzi kupata au Div IV au kufeli! Nimeangalia nyingi sana. Ni shule chache sana zenye angalau nusu ya watahiniwa kupata Div II au zaidi!

Kwa maoni yangu, swala la kufanya vizuri Form 4 ni swala la kitovu cha maendeleo yetu. Kuna mengi yanoyotokea sasa ambayo msingi wake ni hii elimu hafifu katika ngazi hii. Kwa mfano, nimeangalia gazeti la The East African la Jan 28, na mwandishi mmoja (Mohamed Issa Mohamed) ameandika, na nanukuu: "It is estimated that the government will earn $3.5 million in revenue for the current financial year". Huyu lazima atakuwa Mtanzania aliyefeli Hesabu Form IV. Haiwezekani awe Mkenya, kwani wao hawakupitia kipindi cha kuharibu mfumo wa elimu.

Wasichana wakiwekwa mahali ambapo hawaambiwi "hamwezi" kila siku wanafanya vizuri kuliko hata wavulana. St. Francis na Marian College zimethibitisha hilo mwaka hadi mwaka. Kuna wakati watoto wa kike walionewa kijinsia hata na Waziri wa Elimu. Waziri alikuwa anapita mashuleni huku na huko, na anapopumzika analetewa wanafunzi. Sitamtaja jina, lakini ilikuwa wakati wa Elimu ya Ujamaa na Kujitegemea.

Future ya wasichana ni nzuri sana Tanzania. Wameanza kuwa na self confidence ya hali ya juu. Matokea haya ya mitihani yanazidi kuwajengea hiyo self confidence. Itabidi Kanisa Katoliki na wahusika wengine wawatayarishie vyuo vikuu vitakavyowawezesha kuendelea na hiyo hali ya kujiamini. Si vema utoke St. Francis kisha uishie chuo cha hovyo.

Mwishowe, nitoe pendekezo: Si lazima mtu asome diploma au digrii ya ualimu ndiyo aweze kufundisha vizuri. Hizi shule za binafsi zinazofanya vizuri zina waalimu wengi ambao hawajapitia vyuo vya elimu. Tuwe radhi kuruhusu wahitimu wa vyuo vikuu kufundisha bila kusomea ualimu kwanza. Teachers are born; they are not made.
 
Siku hizi mambo yameanza kubadilika na wengi wanaliona hili. Career na maisha ya ndoa ni mambo mawili ambayo yanahitaji careful balance. Ni vyema kila mtu akalijua jukumu lake katika ndoa na kuheshimiana. Tatizo especially hawa akina dada zetu wanaosoma equality kwenye human rights wanataka wailete hiyo theory nzima nzima ndani ya nyumba na hapo baba anakuwa mbogo. Its hardly possible to apply western theories in our African traditional setting bila kuzifanyia marekebisho kiasi... I guess kama mdada au mama una elimu yako you can careful craft what you want by negotiating with your partner than using threats of "usinibabaishe nazijua haki zangu"..Harafu naturally mwanamke akishamzidi kipato mume lazima mzee awe na inferiority complex. Its natural. So its for mama/dada kukaa na kumuonyesha kwa vitendo kwamba her kipato has nothing to do with their love and life. Lakini wengi wanashindwa. Na walioweza hata ukikutana nao utawajua tuu, they are so intelligent, wanajiamni na wana roho za kimama typical!

So my sisters as we move forward you should balance between the two because your career is very important so is your family life. Its all about genuine compromise.

Ninakubaliana na wewe. Lakini ni kwa nini tu, ni responsibility ya mwanamke kumliwaza mumewe pale mamaa anapoleta hela nyingi nyumbani? NI kwa nini mwanaume asijiulize hivi huyu ni mke wangu tu, mimi sijali how much money she makes wala nini? ninampenda yeye na sio hela zake, na hizo hela mimi hazimaanishi kitu chochote kwangu.
Kweli western standards hatuwezi kuzileta nyumbani, lakini hii brutality ya wanaume wa kinyumbani towards wanawake, yaani wake zao ni kama ubao wa kupiga ukiwa uko-frustrated na life in any way, badala ya kuongea na mkeo kumwelezea matatizo yako wewe unamgeuza mpira, just an example.
All in all ninafikiria maybe mila za Jando na Unyago zirudishwe back in a way ziwe zinaendana na hali ya dunia sasa hivi. Watoto wafundishwe sex in a way waelewe sex sio kitu kibaya ila ni kitu kizuri na wafundishe social interaction, maanake jamani ni kweli kabisa gap kubwa sana inaendelea hapa Tz kwani ndoa zinavunjika sana na vijana wengi hawaowi wala kuolewa, au hata wakioa na kuolewa unaona kuna trend mpya ya kuoa/kuolewa na foreigner haswa waarabu na wazungu. Something needs to be done soon wakati ndio bado mwanzo wa tatizo lenyewe.
Kwani kuna fallout kubwa sana ya family katika africa ambayo inatisha sana kwa kweli, sijui future ya black people inaelekea wapi katika hili.
 
Mimi nadhani hawa wakatoliki wana kasiri ka aina fulani maana shule zao siyo tu TZ hata US, Uingereza, India nk zinafanya vizuri sana. Wenyewe wanaita "Catholic education". Na nina uhakika hawasali rozali kutwa nzima. Ni nini ambacho tunaweza kujifunza?

Mzee Mwanakijiji,
Nimesoma shule ya kikatoliki, unaposoma shuleni hapo, sio unafundishwa elimu tu, hapana.Unafundishwa MAISHA!
Namna ya ku-interact na watu, priority katika maisha, tolerance, obidience, determination, perseverance, etc. Yaani unakuta system yote ni kukuandaa wewe uwe responsible na maisha yako mwenyewe, na hapo hapo maisha yako mwenyewe ni elimu, kwa hiyo unakuta wanafunzi wana adabu kama wehu gani sijui, na kusoma ni mtindo mmoja tu, hakuna mchezo, kila mtu ni namba moja darasani. Kwa sababu mtoto yoyote anayepewa responsibility ya maisha yake, anakuwa responsible automatically if they are well prepared.
Sielewi ni kwa nini serikali inashindwa hili kwa kweli, it is just full of propaganda, ili tu wapate vijimisaada koko kila leo tu.
 
Back
Top Bottom