Matokeo Kidato cha Sita: Uongozi wa shule ya Jangwani kubadilishwa na Walimu wa muda mrefu kuondolewa

Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,063
2,985
Wadau,

Habari nilizozipata na ambazo zimethibitishwa na mwalimu mmoja ni kwamba mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani amesisimamishwa kazi kutokana na kufanya vibaya kwa shule hiyo katika matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni.

Aidha walimu wote waliokuwa wanafundisha shule ile wamehamishwa na kutawanywa katika shule mbalimbali jijini dar na wengine mikoani kabisa.

Haya yanatokea huku chama cha walimu na vyama vyote vya wafanyakazi humu nchini vikiwa kimya kabisa kama vile kafukuzwa paka tu.

Wakati sasa umefika kwa vyama vya wafanyakazi kuamka na kutetea wenzao wanaopata matatizo ya kuonewa kama haya.

--------

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametaka uongozi wa shule ya Sekondari Jangwani kufanyiwa mabadiliko na kuwatoa walimu waliokaa zaidi ya miaka mitano wanaojiita 'Wahenga wa Jangwani'

Waziri Jafo ametoa maagizo hayo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar na kutoa siku moja yawe yametekelezwa kwani hajafurahishwa na usimamizi wa shule hiyo

Amesema "Katika taaluma tunasema ninyi mna unyafuzi wa kitaaluma, katika shule yenu, matokeo yenu mabovu sana. Hivi inakuaje mtu uambiwe shule hii ina daraja la kwanza 1?! Jangwani hali yenu ni mbaya"

Aidha, aliongeza kuwa "Jangwani Girls leo hii hakuna kitu. Shule ambayo msichana popote pale Tanzania ndoto yake ni kusoma Jangwani, yenye upako maalum lakini leo inakua ya 3 kutoka mwisho. Hii ni fedheha"

Jafo amesema Shule hiyo ni miongoni mwa Shule chache zenye Walimu wengi lakini imekuwa katika kundi la mwisho “Shule ya Jangwani ina walimu 87, Shule ya Kibaha ina Walimu 52, yenye Walimu 52 inakua ya kwanza kitaifa lakini yenye Walimu 87 inakua ya tatu kutoka mwisho kitaifa”
 
Duuh! Pole sana zimfikie huyu mnyonge (mwalimu). Hivi alitakiwa awafanyie nini hawa wasichana wa Jangwani ili wafaulu?

Hawa wasichana ni wake wa makonda, bodaboda na ndiyo machangudoa wa kila baa na klabu.

Wana simu kali kuliko wazazi wao. Wanatembea na sketi fupi kuliko chupi zao. Wamefanya ngono mara nyingi kuliko wazazi wao.

Hawa wanawezaje kumsikiliza mwalimu wakasoma na kuelewa?
 
Huyo mwalimu wamemuonea tu watoto wa skuizi whasp kwa sana, hasa vile vitoto vya jangwani vikishavaa zile jezi na viraba vyao vyeupe ndio huviambii kitu
Hilo ni jukumu la headmaster kudeal na wanafunzi kama hao, haiwezekani mwanafunzi anaingia kwenye gate la shule akiwa na sim mfukoni halafu headmaster hajui

Hapa lazma nidhamu irudi mashuleni,
 
Back
Top Bottom