Ruvuma: Shule ya msingi Ngingama ina walimu wawili

Nedd Ludd

Senior Member
May 16, 2023
135
245
Shule ya Msingi Ngingama, yenye wanafunzi zaidi ya 400 iliyoko wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma ina walimu wawili wa kuajiriwa na mmoja wa kujitolea, hivyo wanafunzi wanatumia muda mwingi kucheza badala ya kusoma.

Kutokana na changamoto hiyo, wazazi, wanafunzi na walimu wameomba walimu waongezwe katika shule hiyo.

Chanzo: ITV 22/01/2024

Hii kata bila kupinga imetengwa sana kwani hata Mbunge mwenyewe huwa hatembelei hii kata, utasikia kafika anaishia maeneo ya kimkakati zaidi, ila hili jambo si sawa hata kama hii kata ya LINGA ina idadi ndogo zaidi ya watu katika jimbo la Nyasa basi isitegwe kiivyo.

Eng. Stela Martin Manyaya.
 
Duh..hatari hii ama kuna wachawi sana huko kuna sehem wananchi wanawaroga sana walim.Ww mwalim kalala ndani asubuhi anajikuta yuko nje atakaa hapo.
 
Duh..hatari hii ama kuna wachawi sana huko kuna sehem wananchi wanawaroga sana walim.Ww mwalim kalala ndani asubuhi anajikuta yuko nje atakaa hapo.
Hamna kitu kama hicho, watu wa kule ni wakarimu sana, kama mwalimu anaweza hata hasitimie pesa yake kununulia chakula, wananchi wakawa wanampa chakula.

Changamoto kubwa ya kijiji hicho ni mtandao, yote hayo ni jukumu la Serikali.
 
Back
Top Bottom