Matatizo ya kifamilia

kalukamise

JF-Expert Member
May 4, 2011
683
189
MATATIZO YA KIFAMILIA
Basi sikiliza kisa hiki.
"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane, aliyekua na binti mkubwa tu na tukaamua kuoana. Baadaye baba
yangu akamuoa binti yangu wa kambo hivyo huyo binti yangu, wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa
mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama, mkwe wa mkwe wake.

Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa kambo, alipata mtoto wa kiume. mtoto huyo wa kiume alikua ndugu
yangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile, alikua ni mtoto wabinti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu
wa mke wangu na mimi nikawa babu yake mdogo wangu.

Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu, tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana ambaye ni ndugu
wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake. Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kua
shemeji wa mtoto wangu ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi
ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wabinti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa
kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.

SWALI.
Je, unadhani mpaka hapo wewe una matatizo ya kifamilia?
Acha kulalamika
 
Mkorogano mkubwa sana huo.
 
Back
Top Bottom