Masters degrees za Mzumbe University zinaua ubora wa elimu

Nijikweze nini sasa, hutaki kuamini au hupendi kuona kuwa mimi ni Alumnus wa Mzumbe halafu naikandya Alma mater yangu? Nitabaki kuwa Alumnus wa Mzumbe lakini nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Usome Mzumbe.. Utambe.. Tehhhhh
Mzumbe hatutoi vilaza kama ww
 
Baada ya pilika za kutwa nzima naamua kupitia jamii forum!!! among other thing nimekutana na argument zinazochekesha sana kutoka kwa masterz holder, very goodluck nimekutana pia na kijakazi wangu ambaye amepost mengi tu juu ya uelewa wake katika level ya masterz japo aliishia darasa la saba na sasa nimemuendelezea anatarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne mwakani. Binti huyu amekuwa akishinda mtandaoni kutwa nzima hata majukumu yake hatekelezi tena. WARNING be carefully unaeza ukapoteza muda kuargue na mtu huyu. Kaaazi kwenu.

Kumbeeeeeee daahhhhh
 
Nawaomba uongozi wa Mzumbe University mfikirie upya hizi degree za masters mnazozitoa huko mitaani/Centres za mikoani. Mnaua ubora wa elimu nchini. Si jambo jema academically, mtu wa Advanced diploma kusoma masters bila basic degree! Nimeona products wenu wana mapungufu mengi! unawaona kabisa kuwa kuna vacuum upstairs with regard to professionalism worth of Masters degree level. Re-think your programme.

Sasa mmebatizwa kwa kuitwa "MAHARAGE YA MBEYA" kuwa yanaiva haraka/mapema! Nipigeni madongo, lakini ngoja niliseme
sijaelewa watanzania wengi mna vipimo gani kupima hichi chuo ni bora au sio bora.Mtu akiwa na perfomance nzuri haimaanishi kuwa chuo alichosoma kilifundisha sana,ni bidii ya mtu mwenyewe katika kujifunza.kwani waalimu wanakupa percentage ndogo sana ya ufahamu,percentage kubwa unatafuta mwenyewe.
what matters, ni jinsi gani utaweza kui-defend degree yako,au masters yako mbele ya pennel.camon! mind you! it has absolutely nothing to do with any university,it is all about yourself with the capacity of knowledges you have.
 
Well said, just a simple question: If it is a matter of bidii ya mtu" kujifunza, as per your contention that the place/university of learning does not matter: SWALI- University of Oxford, Massachussets Institute of technology (MIT), Havard University, Cambridge, London University just to mention a few hazina tofauti na Mzumbe University. Nijibu!
 
Mimi nimeconclude kwa kusema

nijuavyo mimi hapa Tanzania.. Mzumbe university.. Ndo chuo kinachoongoza kutoa elimu bora katika fani zake inazojivunia ambazo ni

finance, accounts & management science (public administration, health services management, human resources management, local government management, public services management, records and archives mgt)

na kama mnabisha angalieni hali halisi ktk soko la ajira wanavyopeta

si hizo tu...

Hata ktk fani zingine kama BBA, PROCUREMENT, Production and operations mgt, economics... Mzumbe ni baba lao

hawa wanafunzi wa hasa wa udsm wanaleta propaganda za kiwehu sana..... Baada ya kuon hawaifikii mzumbe ktk hzo kozi tajwa hapo juu

mamia ya wanafunzi kila.mwaka wanashindwa kugraduate mzumbe... Maana kuna mtu karopoka hapo juu kuwa ukidahiliwa mzumbe lazima utamaliza.. Jambo ambalo si la kweli

kuhusu RESEARCH..... kwa kweli anayepondea jambo hili kwa mzumbe ni zaidi ya uonevu.
Kwa sababu nijuavyo mimi...

Chuo kikuu mzumbe ni chuo pekee kjnachotoa mda wa mrefu kwa ajili ya kufanya research kwa first degree........... Research ni kitu ambcho kinazingatiwa sana kwa mwanafunz wa degree ya kwanza na ndyo maana inakuwa ni rahisi sana kwa mwanafunzi aliyegraduate first degree mzumbe kufanya vzuri ktk masters degree

wanaanza kufundishwa theories kwa semwster nzima..... Then mwaka unaofuata unatakiwa utafute mada ambyo ungependa kuifanyia research..then unaandika proposoal.... Then unatakiwa ukafanye research for whole semester.... Then uandae report.. Na hatimaye kuisubmit kwa supervisor.. Na hatimaye kuipresent kwa oral presentation

hatua hizi zote unakuwa bega kwa bega na supervisors wako.. Both internal and external supervisors... Na kila hatua kuna marks zake... Kwa hyo sijaona mantiki ya kusema mwanafunzi wa mzumbe hajui kuandika dissertation......

UKIONA mwanafunzi wa masterz anashindwa kuandika dissertation basi ujue huyo first degree alisoma ktk vyuo vingine.. Na si mzumbe

msingi wa research ni first degree na syo second

NB. Udhaifu wa mwanafunzi mmoja huwezi kuutumia kama hitimisho kuwa chuo ni kibovu

juzi hapa PSRS walitangaza kaz za auditors na HR 101

cha kushangaza zaidi ya 70 % waliofanikisha wametoka Mzumb

MTASUBIRI SANA.. na propaganda zenu zitaishia baharini

kuna jamaa niliwahi kukutana naye akasema anatamani apate japo CERTIFICATE ya MZUMBE......... lakn alishindwa

kuhusu muda wa research unavyodai unasoma theory mwaka,, then next semester unaanza kutafta title uifabyie kazi ukiwa bega kwa bega na supervisors sio jambo geni saaana la kujisifu maana ndio maana halisi ya research.. Lazma mtu usome theory na ukianza research lazma kwanza title yako ikubalike ndio uanze kazi ya kuandika proposal nayo ikubalike ndio uendelee na research tena kipengele hadi kipengele unakuwa na supervisor.. Sasa ntashangaaa kama kuna mtu ana first degree na hajaptia hali hiyo,, hicho ndio nlifanya mimi na sijasoma MZUMBE. Upo apo???
 
Nawaomba uongozi wa Mzumbe University mfikirie upya hizi degree za masters mnazozitoa huko mitaani/Centres za mikoani. Mnaua ubora wa elimu nchini. Si jambo jema academically, mtu wa Advanced diploma kusoma masters bila basic degree! Nimeona products wenu wana mapungufu mengi! unawaona kabisa kuwa kuna vacuum upstairs with regard to professionalism worth of Masters degree level. Re-think your programme.

Sasa mmebatizwa kwa kuitwa "MAHARAGE YA MBEYA" kuwa yanaiva haraka/mapema! Nipigeni madongo, lakini ngoja niliseme

Wanaposema Advanced Diploma ni equivalent to degree huwa wana maanisha nn???
 
Tuwe na discussion ya kuelimishana. Usitukane. Nimetoa ninachokiona ofisini. Sijui Bunju ni nini lakini unajaribu kutukana (Mimi nimemaliza basic degree 1980 UDSM, sijisifu ila naona mapungufu). Mimi naona graduates wa hizo masters wanatia mashaka sana. Tunao maofisini can not even make a good english sentence, hao wa advanced diploma! Kuna ambao wana Basic degree, unaona kuna tofauti kubwa, they are doing good.

Umepigwa bao kwenye mpunga huna lolote ww,mwenye masters ya mu anavuta mkwanja mrefu kuliko ww mwenye basic degree ndo maana unakuja na argument za kipuuzi tu.mtu mzima ivyo
 
Acheni kusema kitu usichokijua mtoa maada, mimi ni mwanafunzi nasomea Project planning Management (Master), sasa msoto wa huku najuta kwa nini nimekimbilia kujitesa, maana ni mchaka mchaka wa hatari ni Elimu quality.

NB. Tujifunze kuandika jambo tulilofanyia utafiti na sio kwa kusilkia, na kama wewe ni free-rider sema na sio kuharibu image ya Chuo. Pia sifia chako na si cha jirani.
 
Mzumbe University ni chuo kikuu jamani siyo Institute kama Ifm kwa hiyo mkieshimu sawa!!!&??
 
Acheni kusema kitu usichokijua mtoa maada, mimi ni mwanafunzi nasomea Project planning Management (Master), sasa msoto wa huku najuta kwa nini nimekimbilia kujitesa, maana ni mchaka mchaka wa hatari ni Elimu quality.

NB. Tujifunze kuandika jambo tulilofanyia utafiti na sio kwa kusilkia, na kama wewe ni free-rider sema na sio kuharibu image ya Chuo. Pia sifia chako na si cha jirani.

Huyu jamaa muongo sana haijui mzumbe, kuipata upper 2nd tu hawezi.
 
Umepigwa bao kwenye mpunga huna lolote ww,mwenye masters ya mu anavuta mkwanja mrefu kuliko ww mwenye basic degree ndo maana unakuja na argument za kipuuzi tu.mtu mzima ivyo

Ndio maana nasema Masters za Mzumbe ziko below standard. Just look at you shallow argument! We are not discussing what you call "mpunga", we are trying to make a point with regard to academic credibility of masters offered by Mzumbe university particularly the so called Executive Masters!
 
masters za mzumbe, hasa campus ya Dar es Salaam ni janga kubwa sana yaani ni lipua lipua hata waajiri wengi sasa wameanza kuzititlia shaka kwa kweli ni weupe mno kichwani, TCU hebu chunguzeni hili mkianza na mzumbe Dar Campus
 
Ni kweli kuna wasiwasi mkubwa wa viwango vya Masters zinazotolewa na baadhi ya vyuo vya Tanzania hususan Mzumbe, Tawi la Dar es salaam. Ila sikubaliani na mtizamo wake kuwa udhaifu huo unatokana na sababu kuwa husaili wahitimu wa Advanced Diploma. Advanced Diploma kwenye fani nyingi inakua na uzito sawa na digrii. Nasema fani nyingi kwa sababu kuna fani kama Udaktari, uhandisi nk ambazo curricular ya Advanced Diploma hutofautiana sana na ile ya Shahada. Ila kuna fani kama Uhasibu ambazo kimantiki kwa vyuo kama IFM kilichobadilika ni jina tu kutoka Advanced Diploma kwenda Shahada ila masomo ni yale yale na miaka ni ile ile. Hoja yangu hapa ni kwamba tatizo sio wahitimu Advanced Diploma wanaosajiliwa kwani kuna hata wenye shahada waliosajiliwa Mzumbe na wamefanikiwa kupata Masters ila ubora wa hizo Masters haupo. Unasikia mtu anafanya utafiti na kuandika (kiwa) thesis ndani ya wiki moja na anapitishwa angali hata kilichoandikwa hakijui vizuri. Ukweli ni kuwa hizi Masters zimerahisisha sana wajanja wa mji hasa wale wavivu wa kusoma kuboresha cv zao kwenye makaratasi lakini kwa wale ambao hawakuwa na ajira hazijawasaidia chochote. Pia walioko kwenye ajira hazijasaidia mwajiri. Naamini tatizo liko kwenye mfumo mzima wa vyuo. Naamini utawala wa hivi nyuo unafahamu hilo ila unafumbia macho kwa kuwa unahitaji hela (ada) za hawa watu ili kujiendesha.
 
Nawaomba uongozi wa Mzumbe University mfikirie upya hizi degree za masters mnazozitoa huko mitaani/Centres za mikoani. Mnaua ubora wa elimu nchini. Si jambo jema academically, mtu wa Advanced diploma kusoma masters bila basic degree! Nimeona products wenu wana mapungufu mengi! unawaona kabisa kuwa kuna vacuum upstairs with regard to professionalism worth of Masters degree level. Re-think your programme.

Sasa mmebatizwa kwa kuitwa "MAHARAGE YA MBEYA" kuwa yanaiva haraka/mapema! Nipigeni madongo, lakini ngoja niliseme
Maharage Ya Mbeya ndio yapi
 
Hivi kweli Mzumbe wameanza hayo mambo du hatari sasa tutaenda wapi kila chuo kinamatatizo!
 
Back
Top Bottom