Masoud Kipanya Uhuru Umezidi Mipaka

View attachment 387395
Huyu ni mtu mbaya sana ata kama ni uhuru wa vyombo vya habari hii ni too much. Hiyo katuni alikua anamaanisha nini!! si ni matusi kabisa haya. Huwezi fanya uhuni kwenye gazeti kubwa kama mwananchi tena kwa kutaka kufupisha kitu ili liwe tusi na jina la Rais likiwemo hapo hapo.

Huyu mtu ni jipu ashauriwe kufanya kazi kwa weledi wataaluma yake aache kuleta uhuni wa kijiweni kwenye magazeti.

Na hilo ndo jukumu la katuni. Kukufanya ufikirie. Sasa kwa akili yako wewe umefikiria hivyo. Kwa nini mnafanya mambo kwa hisia? Yaani you are so insecure! WE ARE ALL ALLOWED TO THINK DIFFERENTLY.
 
Una watoto hapo nyumbani wa darasa la tano wape wafupishe hyo katuni. Ninachotaka ujue ni kwamba hiyo katuni haijakaa vizuri kama ww unavyoenda direct kusema UKM
Sina mtoto wa Primary school,
Oh, pole sana, yawezekana najibishana na walosoma Memkwa!
 
kipanya amezinguaa...
Jinsi swali alivyoweka ndo tatizo... Angeuliza tu "JINA LA MAANDAMANO YA UVCCM" na sio kifupi.
 
View attachment 387395
Huyu ni mtu mbaya sana ata kama ni uhuru wa vyombo vya habari hii ni too much. Hiyo katuni alikua anamaanisha nini!! si ni matusi kabisa haya. Huwezi fanya uhuni kwenye gazeti kubwa kama mwananchi tena kwa kutaka kufupisha kitu ili liwe tusi na jina la Rais likiwemo hapo hapo.

Huyu mtu ni jipu ashauriwe kufanya kazi kwa weledi wataaluma yake aache kuleta uhuni wa kijiweni kwenye magazeti.
Tuweni wakeli kabisa toka mioyoni mwetu, tusi liko wapi hapo? Tusiongozwe na hisia mbaya na za kichochezi kwa maslahi ya kujipendekeza tu. Yeye kauliza swali, na hata kama asingeuliza bado kusingekua na tusi, tuacheni kuchonganisha watu. kama huna cha kuandika kaa kimya
 
Kufanyaje mbona hatukuelewi mleta uzi ?! Au unamlisha maneno
Yeye mbona aewalisha maneno UVCCM?Ni wapi UVCCM walisema maandamano yao yataitwa kwa neno hilo?wale wengine wanaongea kwa vinywa vyao kwamba neno ni UKUTA.
Mkuu acha kutetea mambo ya hovyo hovyo,wachora katuni mahiri huzingatia kuelimisha na kuburudisha bila kuleta confussion na unnecessary misunderstanding,kwa yeyote mwenye akili timamu hapa jina la mheshimiwa Rais limedhalilishwa na ndio sababu watu wanakosoa,nae kama ni muungwana na mwenye kujitambua ni vyema aombe radhi kwa hilo.
 
Umoja. Kumpongeza. Magufuli. Kifupi chake ni ukakasi kukitamka!!. Hasa ukiamua kuchukua herefi mbili za mwanzo kwa kila neno.
 
Back
Top Bottom