Maskini mwananchi limekuwa gazeti la propaganda la CCM

Pamoja na mambo mazuri (taarifa) kutoka kwa waandishi wetu kupitia vyombo mbalimbali vya habari kutusaidia kujua kinachoendelea kwingineko, lakini tuwe wakweli kuwa tasnia hii bado ina safari ndefu sana hapa nchini. Kiwango chao cha malipo kinashawishi wengi wao kujipendekeza kwa wanasiasa ili waongeze kipato, wengine wanaingia moja kwa moja kwenye siasa - Betty Mkwasa, Muhingo Rweyemamu, Sara Dumba, Halima Kihemba, Novatus Makunga na wengine unatarajia nini katika hali kama hii? Ni wazi kuwa walikuwa bega kwa bega na wanasiasa ndio maana sasa wapo hapo walipo! Tutarajie nini kama sio kusalitiana wenyewe kwa wenyewe?
 
Gazeti la Mwananchi linajitahidi sana kuandika habarai kwa mrengo wa kuwasapoti waTZ na sio watawala ingawajr kuna wakati wana balance mno habari kiasi cha kutojua which is which?
 
Gazeti la Mwananchi ni objective kwa mambo mengi; tusilihukumu Gazeti kwa habari moja tu.

Nilikuwa nalinunua kila siku kwa Kuamini Lipo Objective!! Ila kwa ushabiki Huu wa kushadadia naona sasa wamenikosa!! Bye bye Gazeti la Udaku!!
 
Tendwa hakutaja chama kwa jina (Japokuwa aliilenga CHADEMA). Pili kwa habari hiyo bado haijahamisha imani yangu kwa Gazeti Mwananchi.
1.MwanaHalisi (Lipo Moyoni)
2.Tanzania Daima
3.Mwananchi
4.Raia Mwema
5.The Citizen
6.Mtanzania
Mwe!! hapo namba 6 si ni gazeti la Rostam hilo chini ya usimamizi wa Bashe?
 
Gazeti la Mwananchi wanatakiwa wajipange vizuri, hivi karibuni hawajatulia na wameanza kupwaya na wameanza ushabiki wa kitoto. Kuna toleo moja walionesha ushabiki kwa yangu kwa kutoa picha ya mchezo mmoja ametoka burundi sijui Rwanda kwenye ukurasa wa mbele na nyuma. Nilishangaa sana kwani mchezaji huyo alikuwa bado hajafika hapa nchini na kwa jinsi nilivyokuwa nalipenda gazeti hili niliboreka sana kuona waandishi pamoja na wahariri siku nzima inapita wameshindwa kupata habari ya kipaumbele kiasi cha kwamba wanarudia habari moja tu. Mwananchi mjipange na rudieni zama zenu za jinsi mlivyokuwa mnaripoti uchaguzi mkuu. Uwezo mnao acheni ushabiki na kujibamiza serikalini.
 
Maneno ya mwandishi wa Mwananchi ni nukuu za Serikali na Nape kwamba kila wanacho CDM ni vurugu.
 
Paragraph hii nimei copy kutoka kwenye gazeti la mwananchi:

Septemba 4, mwaka huu Tendwa alitishia kukifuta Chadema baada ya matukio ya vurugu katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika Iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi.

kama mwandishi angekuwa fair ingesomeka hivi:

Septemba 4, mwaka huu Tendwa alitishia kukifuta Chadema baada ya polisi kuifanyia vurugu CHADEMA bila sababu za msingi katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika Iringa na (polisi) kumwua aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi. Naomba tujadili-jazba weka pemebeni.

Katika magazeti yasioegemea upande wowote ni mwananchi,sasa wewe ni kipi sijui walichokezea,ila mwananchi wako vizuri-huo mtazamo wangu.
 
tendwa hakutaja chama wala eneo la virugu wewe ndio hukumsikia, usilazimishe watu waelewe unavyojisikia wewe

ni kweli tendwa hakutaja jina.kwa maana hiyo basi mwandishi kama ni kweli .basi atakuwa ana matatizo tena kubwa tuu
 
Machapisho yake ni kwa gharama za nani?..hii si kodi ya wananchi kweli?
 
Kwa hili la Mwananchi sikubali kuwa ni gazeti la kipropaganda la nyinyiemu, ukizingatia mkurugenzi wa gazeti hili aliondolewa TBC kwa mizengwe kuwa aliibeba CDM 2010, linawezekana ikawa ni oversight ya uandishi.
 
Machapisho yake ni kwa gharama za nani?..hii si kodi ya wananchi kweli?[/QUOTE]

Siyo kampuni ya serikali, MCL (Mwananchi Communication Ltd.) ni kampuni dada na kampuni inayotengeneza magazeti ya The Nation na Taifa Leo nchini Kenya.
 
Machapisho yake ni kwa gharama za nani?..hii si kodi ya wananchi kweli?

Mwananchi Communication Limited (MCL) ambao ni kampuni binafsi ndo wachapishaji wa gazeti la Mwananchi, ni kampuni dada na kampuni inayochapisha magazeti ya The Nation na Taifa Leo nchini Kenya.
 
Hivi gazeti la uhuru bado lipo kweli?
Mkuu lipo ila linaishia kusomwa hapa Lumumba na makada wa CCM waliochoka mbaya ambapo wanapewa bure!

Hata wauza maandazi siku hizi wamegoma kufungashia maandazi wanadai linawakimbizia wateja.
 
Paragraph hii nimei copy kutoka kwenye gazeti la mwananchi:

Septemba 4, mwaka huu Tendwa alitishia kukifuta Chadema baada ya matukio ya vurugu katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika Iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi.

kama mwandishi angekuwa fair ingesomeka hivi:

Septemba 4, mwaka huu Tendwa alitishia kukifuta Chadema baada ya polisi kuifanyia vurugu CHADEMA bila sababu za msingi katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika Iringa na (polisi) kumwua aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi. Naomba tujadili-jazba weka pemebeni.

Mkuu mahali ambapo Fisadi wa SSM ameacha foot prints unategemea pawe safi? Pale yalikuwa makazi ya Rostam Aziz with some ownership kama hajanunua habari Corporation!!!!
 
tendwa hakutaja chama wala eneo la virugu wewe ndio hukumsikia, usilazimishe watu waelewe unavyojisikia wewe

Yaani unatetea hata visivyoweza kutetewa.
Sio lazima ataje chama kwa jina ndio watu waelewe kuwa anasema jambo gani, au wewe unadhani Tendwa anaweza kuifuta CCM ??
Angalia mfano huu:-
Mtu anaweza kusema sentensi ifuatayo '...kiongozi fulani alisema kuwa liwalo na liwe ...'
Katika sentensi hiyo, unadhani kuna jina la mtu limetajwa ?? Ila inajulikana kabisa kuwa kiongozi huyo ni nani, ingawa hakutajwa jina !!!
Upo hapo !!!
 
Mwananchi tunawasheshimu. Inawezekana walijikwaa tu. Wajirekebishe ili waendelee kulinda credibility yao.
aya nenda lumumba kapokee buku 2.unapinga hata unayoyakubali kimoyomoyo.Mwananchi limepoteza mvuto.
 
Back
Top Bottom