Maskini mwananchi limekuwa gazeti la propaganda la CCM

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
321
448
Paragraph hii nimei copy kutoka kwenye gazeti la mwananchi:

Septemba 4, mwaka huu Tendwa alitishia kukifuta Chadema baada ya matukio ya vurugu katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika Iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi.

kama mwandishi angekuwa fair ingesomeka hivi:

Septemba 4, mwaka huu Tendwa alitishia kukifuta Chadema baada ya polisi kuifanyia vurugu CHADEMA bila sababu za msingi katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika Iringa na (polisi) kumwua aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi. Naomba tujadili-jazba weka pemebeni.
 
Waandishi wetu nao wana safari ndefu ya kujipigania.

Sikuamini jana kuona Channel Ten ambao ndio wafiwa kumwalika kamanda wa polisi wa usalama barabarani kwenye Baragumu na kushindwa kuunga mkono chama cha waandishi wa habari cha mkoa wa Iringa kususia kazi za jeshi la polisi
 
Muanzisha thread umegusa swala la msingi sana,waandishi wengi ndivyo wanavyoandika!!
 
paragraph hii nimei copy kutoka kwenye gazeti la mwananchi:

septemba 4, mwaka huu tendwa alitishia kukifuta chadema baada ya matukio ya vurugu katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika iringa na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten, daud mwangosi.

kama mwandishi angekuwa fair ingesomeka hivi:

septemba 4, mwaka huu tendwa alitishia kukifuta chadema baada ya polisi kuifanyia vurugu chadema bila sababu za msingi katika mikutano yake ukiwamo ule uliofanyika iringa na (polisi) kumwua aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten, daud mwangosi. Naomba tujadili-jazba weka pemebeni.

tendwa hakutaja chama wala eneo la virugu wewe ndio hukumsikia, usilazimishe watu waelewe unavyojisikia wewe
 
Hili ndio gazeti nililodhani haliegemei upande wowote,na kama imeshakuwa hivi nitafanya kama nilivyopiga marufuku tbc maishani mwangu.

Pili waandishi wengi wa habari wanatumiwa na mafisadi hivyo sigemei kwa njaa zao kuwa na misimamo ya pamoja
 
Tangia gazeti la Mwananchi wakanushe ile habari ya Membe na Mabalozi, nilishalishushia hadhi yake.
 
Waandishi wetu nao wana safari ndefu ya kujipigania.

Sikuamini jana kuona Channel Ten ambao ndio wafiwa kumwalika kamanda wa polisi wa usalama barabarani kwenye Baragumu na kushindwa kuunga mkono chama cha waandishi wa habari cha mkoa wa Iringa kususia kazi za jeshi la polisi
alafu hawa waandishi wetu wanajipambanua na kutaka waheshimiwe kama mwandishi mwenzao Jenerali Ulimwengu lakini ukweli unabaki palepale kuwa Tanzania waandishi ni tatizo kubwa mno.
Uwezo wao wa kuchanganua masuala ni mdogo mno na inaweza kuwa aibu zaidi huko mbeleni tukigundua kuwa nao wanafuta 'maelekezo' ya wakubwa zao kama polisi ambao wanafuata amri za wanaowatuma.

Kwa kusisitizia hoja ya mleta mada, hapa jf kuna picha na video nzuri kabisa zilizoonyesha askari na wananchi waliokuwa wakikutana wakiwa wanaongea na kubaduilishana mawazo kwa amani na utulivu kabla ya mkutano lakini mara amri ilivyotoka ya kuwaamuru polisi waue ndio vurugu zikaanza mpaka wakamuumiza na askari mwenzao then mwandishi anasema cdm!

 
Tendwa hakutaja chama kwa jina (Japokuwa aliilenga CHADEMA). Pili kwa habari hiyo bado haijahamisha imani yangu kwa Gazeti Mwananchi.
1.MwanaHalisi (Lipo Moyoni)
2.Tanzania Daima
3.Mwananchi
4.Raia Mwema
5.The Citizen
6.Mtanzania
 
Kama alimaanisha Chadema, kwanini asingekifuta CCM Kwanza? Halafu yeye ni "mlezi wa vyama vya siasa" ametoa ushauri gani kwa mwanaye huyu(CDM) na ukaonekana ukaidi usioweza vumilika? Hapa lazima mtoto (CDM) atamgeuzia kibao baba(Mlezi) wake ambaye ni Tendwa.
 
'Fair' maana yake aipambe CDM? Ndio maana nchi hii ni masikini ikiwa akili zenyewe ziko hivi.
 
Hilo ni gazeti ambalo nilishalisahau kama Uhuru

Nimetembelea mtandao wao muda si mrefu nimekuta habari ya kwanza isema wabunge wa CDM wapelekwa polisi Igunga kwa kumshambulia DC, nikajiuliza ilikuwa maksudi au tatizo la kiufundi? hii habari ni mwaka jana sept 17- 2011.
 
Msiwe mnarukia fani za watu nakuanza kuandika kama mnavyotaka wenyewe. Hapo mwandishi anakosa gani? Kama hujui sera ya gazeti hilo unaweza kusema mnavyojaribu kusema humu ndani kuhusu story hiyo.

Hata kama mwandishi aliandika hivyo na kama Tendwa alisema hivyo; kuna kosa gani mwandishi kuandika kile kile kilichosemwa?

Hiyo ni story iliyobeba kilichosemwa na aliyeibeba story yenyewe (Tendwa) na si makala iliyoandikwa na mwandishi binafsi kwa mawazo na utafiti wake binafsi. Acheni kutuzengua nyie. Huwezi kujua au kuelewa kila taaluma.
 
Mimi nimeicopy kutoka gazetini, mwandishi ndiye anayelazimisha watu waelewe kuwa chadema ndio waliofanya vurugu kitu ambacho sio kweli maana kama ni kweli angeweka picha kuthibitisha kitu ambacho hawezi maana hakikuwepo kabisa- hivi watu wanafungua tawi tena ni wa chama kimoja na mtazamo unaofanana, je, watafanyianaje fujo? Tafakari.
 
Tendwa hakutaja chama kwa jina (Japokuwa aliilenga CHADEMA). Pili kwa habari hiyo bado haijahamisha imani yangu kwa Gazeti Mwananchi.
1.MwanaHalisi (Lipo Moyoni)
2.Tanzania Daima
3.Mwananchi
4.Raia Mwema
5.The Citizen
6.Mtanzania

Mkuu kwa hili tuko pamoja kwani hatuna haja ya kuchukia chombo cha habari kwasababu hakijakwandika vizuri.
Hata mie magazeti haya nayakubari.
Chadema tu huru kwa vyombo vya habari pls.
Peoplessssssss power!!!!!
 
Back
Top Bottom