Masikini TBC

Borakufa

JF-Expert Member
May 26, 2011
1,503
390
Heshima kwenu wakuu!

Tido Muhando alipofanyiwa zengwe TBC wengine tulijua nini kinafuata! Shirika hili ambalo ni mali yetu sisi wananchi lilisimama katika kutoa haki japo lilikuwa likibanywa kwa njia moja au nyingine wakati wa ukurugenzi wa Tido Muhando. Kweli alikuwa na mapungufu yake kama binadamu, lakini kwa kiasi kikubwa wananchi wengi waliridhika na utendaji wake.

Ni wiki mbili tu tangu kuteuliwa mkurugenzi mpya huwezi kuamini sifa za TBC kwisha kabisa! wanaripoti uongo mtupu na habari za upande mmoja tu. Hivi ndivyo ilikuwa asili ya TBC. Ilitumika kuwadanganya wananchi huko nyuma ili tutawaliwe wanavyotaka watawala kandamizi.

Ninachotaka kusema hapa namshauri yule ambaye bado anafikiria kuwa eti bado anaweza kulitumia shirika la habari ambalo linaendeshwa kwa fedha zetu sisi wananchi eti kutudanganya kwa faida ya tumbo lake kama ilivyokuwa RTD na TVT. zama za zidumu fikra sahihi zilishapitwa na wakati.

Wito kwa mkurugenzi mpya wa TBC namsihi kuachana na mpango wake wa kutuchakachulia habari kwani kufanya hivyo atakuwa analipwa fedha zetu kwa njia haramu.

Tafakari chukua hatua!
 
mfano ile habari ya nyamongo wealiyorusha bila upande wa pili,walionesha kiwango kikubwa cha kushuka kitaaluma.

TBC wasibobadilika,watajisoma kwenye historia
 
Hilo kila mmoja alilijua. Kibaraka mkubwa wa CCM huyu Mshana. Utamu wa TBC umeisha kabisa, kama radio uhuru ya CCM.
 
mfano ile habari ya nyamongo wealiyorusha bila upande wa pili,walionesha kiwango kikubwa cha kushuka kitaaluma.

TBC wasibobadilika,watajisoma kwenye historia

Umeona eeh!
 
Natoka sasa kusikiliza/kutazama tarifa ya habari tbc yani ni msiba, habari zote muhimu ambazo inaionyesha vibaya serikali wameipotezea duuh!!
 
TBC hawana muda. watakuwa kicheko cha dunia before december 2011.
 
hv bado mna tune hiyo station?mm nilisha delete kabisa haipo kwenye luninga yangu,inanijazia channel tuu
 
kusema ukwel wameshuka kiwango sijui habar wanatafutiwa na wachina yan hamna kitu sasa ITV,STAR TV, CHANNEL TEN na MLIMAN wapo juu lakn TBC KUSHINEHI kabisa
 
hawa jamaa bado wanadhani tupo kwenye zile enzi za RTD yaani radio moja tu wakisema wao ndiyo basi hakuna sehemu nyingine ya kupata habari. sasa watasoma na kuonyesha habari zao na kusikiliza na kutazama wao wenyewe. sisi nyumbani kwetu anaangalia baba peke yake hata mama yangu amewapiga chini na bado tunamsomesha baba naye awatose. kuna TV na radio kibao za kitaifa na kimataifa

Tatizo lao wanadhani mabadiliko yanaweza kuiwa muda wote, dawa ya mabadiliko ni kujiandaa na kukop nayo
 
Watakapo kuja elewa kuwa ukweli hauchakachuliki itakuwa too late maana hivi sasa habari yao kwisha kabisa
 
MUKAMA ALIPOANZA ZIARA MIKOANI WALIMWONYESHA KILA SIKU. Tangu azomewe kule Mara nyumbani kwao ambapo alizaliwa hawajarusha tena. Sijui kama ziara imeishia wapi, waendelee kutujuza Mzee wa gamba kafikia wapi.
 
hv bado mna tune hiyo station?mm nilisha delete kabisa haipo kwenye luninga yangu,inanijazia channel tuu

Haswaaa na mimi nimeifuta juzi, nimeamua kubadilisha decoder ya easy tv baada ya kuona startimes bado inachembechembe za u tbc ccm!

Kwakweli inakera sana kuona chombo cha umma kinatumikia chama kimoja cha siasa ilihali tz kuna vyama vya siasa zaidi ya kumi? Na zaidi inatumikia chama ambacho walipa kodi wamekikataa kwa kura halali, chenyewe kikalazimisha kwa kura za kichina pale Kijitonyama !!!
 
mfano ile habari ya nyamongo wealiyorusha bila upande wa pili,walionesha kiwango kikubwa cha kushuka kitaaluma.

TBC wasibobadilika,watajisoma kwenye historia

Umeona eeh!

Sio muda mrefu toka sasa, itakuwa kama radio uhuru
Time will tell
 
Back
Top Bottom