Ayub Ryoba wa TBC fanya kazi punguza uchawa

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,240
TBC redio ni shirika la umma kwa ajili ya kuhabarisha wananchi na hasa wa hali ya kawaida bila kujali itikadi zao za kisiasa. Aidha shirika linapaswa kutoa habari na burudani kwa nchi nzima.

Jambo la kusikitisha haki hii ya kupata habari na burudani haiwafikii Watanzania walio wengi kutokana na uwezo mdogo wa mitambo inayotumika. Hii si sawa kabisa kwani Watanzania wengi hawatendewi haki. Na hii inatokana na uongozi wako mbaya na usio na viwango.

Bw. Ryoba ukiwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika unapaswa kijirekebisha haraka sana. Kwa sasa unatumia zaidi ya nusu ya muda wako wa kazi kufanya uchawa badala ya kusimamia utendaji na ufanisi wa kazi.

Vitu unavyotakiwa kuvifanya haraka iwezekanavyo ni kwanza kuongeza mtandao wa usikivu (coverage) wa chombo hiki cha umma na pili kuboresha usikivu. Mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe hakuna wanachonufaika kutokana na chombo hiki cha umma. Mtandao wa redio hii haufiki maeneo mengi na unakofika usikivu ni dhaifu sana.

Muda mwingi umekalia kupiga siasa na kufanya uchawa. Kama unataka kufanya siasa achia ngazi wengine wapige kazi. Ujumbe wangu kwako ni " Punguza uchawa piga kazi"
 
Mbaya zaidi amekifanya kituo cha TBC kama mali yake binafsi!
 
uyo alinfanyaga niichukie tbc siangaliag ad leo enz za magu alikua nabkpnd chake sjui bado kpo ad leo kile knafanana na medan ya siasa yan nikusifia sifia kupamba watawala pk unajiulz this broadcasting chanel au chanel yakupamba viongoz
 
Ryoba shughulikia usikivu wa TBC achana na uchawa!
 
Back
Top Bottom