Mashindano ya 'U-Miss' Yamezidi. Michezo Mingine Tumeisahau?...Twisted Priority?

Ukiangalia nchi za skandinavia utakuta kitu miss fulani hakina nguvu vile, ni kajikitengo fulani tu kananako fadhiliwa na makampuni pamoja na maduka ya mavazi na urembo. Nchi hizo bajeti zao za michezo ziko juu kuliko, kwanini basi wanafanya hivyo? kuimarisha, kulinda na kujenga mazoea ya michezo, kwasababu ndo msingi wa afya ya raia wa na viongozi wa kesho. bongo kulikoni?
 
Ukiangalia nchi za skandinavia utakuta kitu miss fulani hakina nguvu vile, ni kajikitengo fulani tu kananako fadhiliwa na makampuni pamoja na maduka ya mavazi na urembo. Nchi hizo bajeti zao za michezo ziko juu kuliko, kwanini basi wanafanya hivyo? kuimarisha, kulinda na kujenga mazoea ya michezo, kwasababu ndo msingi wa afya ya raia wa na viongozi wa kesho. bongo kulikoni?

Hapa ndo utapata jibu kwanini bongo na nchi za Africa hasa kusini mwa jangwa la Sahara tunaongoza kwa ngoma.
 
Usiwalaumu hao ma-binti.... Sio kosa lao. Jinsia yao ndio inayowaponza.

Do you know anything about " Carrot and Stick" ?

Hujawahi kuona kwamba kila kabla ya mashindano, walimbwende huonyeshwa zawadi gani watapata pindi watakaposhinda ? Wake up!!!!!!!!!!!
 
Kiufupi sipendi kuwalaumu walimbwende wetu la hasha, nichangamoto fulani tu. Je nini kimefanya mashabiki wa michezo ya ukweli, ambayo ni kipimo cha vipaji na juhudi za washindani, wakahama na ghafla kuanza kushabikia ulimbwende? Je ni ngono? je wabongo tunapenda bongo kiasi hicho? maana yake kila kukicha muheshimiwa fulani mgeni rasmi? au mi ndo nimelewa?
 
Kila kona ninayo angalia nchini Tz, jambo lolote linalo husu burudani na michezo limetawaliwa na walimbwende na Lundanga wao.

Nnavyo kumbuka mambo haya hayana hata miaka kumi nyuma, cha ajabu ma miss wetu wameua michezo mingi ya maana kama netiboli, basket, kuogelea pamoja na michezo mingine mingi ambayo watu wanajipima juhudi na vipaji vyao. "
Hebu thibitisha hapo kabla ya kuendelea kumwaga pumba...
 
Hebu thibitisha hapo kabla ya kuendelea kumwaga pumba...

Kama mpaka leo hujui kama kenya kwenye mashindano ya Golden league duniani wamewasilishwa na zaidi ya wanamichezo 200, tanzania 0. Kwenye kwenye world championship germany kenya zaidi ya 80. bongo 5. hii inaonyesha wewe ni mmoja kati ya hawa (i) inaonekana wewe sio mwanamichezo kwani ungekuwa mmoja basi ungegundua kuwa huo mchezo wako umeathirika kwa kukosa ufadhili. (ii) Mmoja kati ya wadhadhili ambao wamejijengea ngome za kuendelea kuvitafuna binti vyao. Utapata ushahidi zaidi only if you identify yourself.

madai yao ohh tunatangaza nchi yetu kiutalii, eti michezo mingine imeshindwa BUT IF YOU LOOK CAREFULLY NEITHER HAS ULIMBWENDE.
 
We are heavily investing in Ngono or things that are associated with it. If you want to gain on your business do that. Get some and loose some for a long term. We are sending to trash can things which are important and promoting things which are not important. Bottom line Miss Tanzania beauty pegeant is all about sex and manipulation for women to men, its all about prostitution.Sorry if this sounds disturbing but its true.
 
Kiukweli kabisa Tanzania ni mabingwa wa kupoteza mielekeo kwa kutekwa na kasumba potofu, suala la kutelekeza michezo mingine yyt na kushikilia "washinda njaa" ni ufinyu wa mawazo na kutokuwa na upeo sahihi wa malengo na mipango thabiti, kuwasaidia hawa nadhani ni kuanzisha kampeni ya kurudisha michezo katika hatua za chini za elimu kwa kuhakikisha inatekelezeka na kudhaminiwa kwa mamilioni kama yale yanayotupwa kwenye ulimbwende.
 
mie hapa sina hata cha kuongezea ,
hawa mamiss wenyewe hata 20 bora huwa hawaingii ,ila afadhari yao wanaenda kuosha macho
 
Kiukweli kabisa Tanzania ni mabingwa wa kupoteza mielekeo kwa kutekwa na kasumba potofu, suala la kutelekeza michezo mingine yyt na kushikilia "washinda njaa" ni ufinyu wa mawazo na kutokuwa na upeo sahihi wa malengo na mipango thabiti, kuwasaidia hawa nadhani ni kuanzisha kampeni ya kurudisha michezo katika hatua za chini za elimu kwa kuhakikisha inatekelezeka na kudhaminiwa kwa mamilioni kama yale yanayotupwa kwenye ulimbwende.


point taken yaani hapa umesema kweli kijana
 
Kila kona ninayo angalia nchini Tz, jambo lolote linalo husu burudani na michezo limetawaliwa na walimbwende na Lundanga wao. Nnavyo kumbuka mambo haya hayana hata miaka kumi nyuma, cha ajabu ma miss wetu wameua michezo mingi ya maana kama netiboli, basket, kuogelea pamoja na michezo mingine mingi ambayo watu wanajipima juhudi na vipaji vyao. Swali langu ni kwamba hao mamiss, ukiondoa kujishindisha na njaa, wana kitu gani cha maaana sana mpaka taifa zima likayafumbia macho michezo yoooooote na kumwaga mamia ya mamilioni kwa watu ambao wanajishindisha na njaa? Je hao wafadhili wanaingalia riadha ikifa kibudu? na mbona tangu hapo kale hakuna la maana tulilo liona ambalo wamelifanya hao washinda njaa wetu? Je watanzania tumesahau kuwa riadha inauwezo wa kuitangaza nchi kuliko huo ulimbende uliojaa majungu na unyanyasaji wa kijinsia? Hivi ni vigumu kuiga Msumbiji ambayo ulaya inajulikana kwaajili ya mtu mmoja tu Maria Mutola? Kenya je? Jamaica nayo? namaliza kwa kumnukuu mwanafalsafa aliposema "haiwezekeni mkawa hamjalewa"




wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi ..
 
wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi ..

Partly, nakubaliana na wewe mh. Kiongozi,

Ndio maana kila kijana mdogo siku hizi uswahilini wanawaza kufakamia fani za bongo fleva, miziki ya bendi wenye muelekeo wa ki-congo, kunyonga viuno, n.k.

Lakini kwa upande mwingine nadhani taifa letu halina mipango madhubuti ya kimaendeleo na jamii inachokionesha ni ktk tu kudhihirisha hilo. Taifa linaloongozwa na watu wasio na dira wala fikra zenye kujenga ni vigumu sana kwa mambo kama haya kutojitokeza. Serikali zote makini duniani zinachunga sana nguvu kazi zao, hususan vijana na ndio maana wanajaribu kuweka rekodi za unemployment na hizo takwimu zinawagusa na kuwafanya wakune vichwa kila siku. Na ndio maana umesikia majuzikati hapa Obama ameongeza kodi kwa matairi kutoka China ili kulinda makampuni ya kimarekani yasiathirike. Amefanya hivyo kwa sababu ya ushauri wa kitaalamu no matter how controversial it is seems. Kinyume chake, kwa Tz sidhani kama kuna takwimu zozote unaweza ukaziita za kuaminika kuhusu unemployment. Pia sidhani kama kuna mikakakati yeyote ya kutengeneza nafasi za ajira. Ni hobelahobela.

Ni majuzi tu hapa Waziri Kapuya, alipoamua kuudhalilisha uprofesa wake na kusema eti tayari ajira zaidi ya milioni moja zimetengenezwa na serikali ya awamu ya nne. Pia hata mkuu wa kaya alizungumzia eti kuongezeka kwa ajira za u-housegirl kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya wabunge. This is laughable.Hii ni aibu na inaonesha viongozi wetu ni vichwa boga.

Hali ni ya kusikitisha na kwa jinsi uzalishaji wa nguvukazi yetu inavyozidi kuwa hoi, hali ya uhalifu inaongezeka, na utegemezi wa misaada unaongezeka, maradhi, umaskini, ukosefu wa elimu n.k. ktk jamii vinazidi kukita mizizi. Mustakabali wa nchi yetu unazidi kuwa kizani.
 
kila kona ninayo angalia nchini tz, jambo lolote linalo husu burudani na michezo limetawaliwa na walimbwende na lundanga wao. Nnavyo kumbuka mambo haya hayana hata miaka kumi nyuma, cha ajabu ma miss wetu wameua michezo mingi ya maana kama netiboli, basket, kuogelea pamoja na michezo mingine mingi ambayo watu wanajipima juhudi na vipaji vyao. Swali langu ni kwamba hao mamiss, ukiondoa kujishindisha na njaa, wana kitu gani cha maaana sana mpaka taifa zima likayafumbia macho michezo yoooooote na kumwaga mamia ya mamilioni kwa watu ambao wanajishindisha na njaa? Je hao wafadhili wanaingalia riadha ikifa kibudu? Na mbona tangu hapo kale hakuna la maana tulilo liona ambalo wamelifanya hao washinda njaa wetu? Je watanzania tumesahau kuwa riadha inauwezo wa kuitangaza nchi kuliko huo ulimbende uliojaa majungu na unyanyasaji wa kijinsia? Hivi ni vigumu kuiga msumbiji ambayo ulaya inajulikana kwaajili ya mtu mmoja tu maria mutola? Kenya je? Jamaica nayo? Namaliza kwa kumnukuu mwanafalsafa aliposema "haiwezekeni mkawa hamjalewa"

bila hao tutaishi vipi mkuu...........ndo malimwengu hayo
 
Naunga mikono na miguu hii hoja,kwakweli tanzania tunainvest pale pasipotakiwa nahii ni kwa sababu tu ya upenzi wa ngono si kingine,hao vodacom wanadhamini ujinga huo usioletea taifa hili hata dola moja???!!hakuna lolote kina Lundenga wachawi tuu,wekeza katika riadha,ngumi,jamaa wakienda nje tunapata foreign exchange! hawa mamis wanaleta nini?zaidi ya kufyonza,na mapedezee wanaanza mbio za kuwafukuzia na kumwaga tu mihela,huoni hii ni hasara kwa taifa kuliko faida?Ningekuwa mkuu wa kaya ningeyapiga marufuku,hayana faida,anayepinga aorodheshe hapa faida ya haya mashindano!
 
Kusema miss TZ ni about sex is "myopic" Washindi wanapata zawadi kubwa including magari na wengine nyumba na hata advertisments and wengine through that wamekuwa models and they are getting good contracts and earning their living. Hii ni fani na haina uhusiano wote na sexy. Sexy inahusisha mwanaume na mwanamke na hivyo huwezi kusema mashindano ya u-miss is about sex, la hasha. Be positive so long something has also positive impact in the society. We can't remain the same forever men....
 
mie hapa sina hata cha kuongezea ,
hawa mamiss wenyewe hata 20 bora huwa hawaingii ,ila afadhari yao wanaenda kuosha macho

Exactly mama wa kwanza! Nasi tunapeleka watalii nje ya nchi! Ubunifu wa hali ya juu.
 
Kama mpaka leo hujui kama kenya kwenye mashindano ya Golden league duniani wamewasilishwa na zaidi ya wanamichezo 200, tanzania 0. Kwenye kwenye world championship germany kenya zaidi ya 80. bongo 5. hii inaonyesha wewe ni mmoja kati ya hawa
Sina hakika sana katika Golden League, lakini kwenye World Championship 2009, Tanzania iliwakilishwa na wafukuza upepo 10. Hii pekee inanipa picha jinsi gani una uelewa mdogo wa michezo hapa Tanzania. Kwa kukusaidia tembelea link ya IAAF kujua ni kina nani walituwakilisha huko. Na ili kuondoa ukungu machoni mwako kuhusu mchezo huo hasa wakati wa mashindano hayo ya Berlin 2009, jaribu kuungana na wanaJF ambao walijadili kwa kina ushiriki wa watz huko katika linki hii.

Aidha katika ushiriki wa Golden League Zakia Mrisho pichani chini alishiriki na kuweza kupata matokeo mazuri kuliko alivyoshiriki katika Ubingwa wa Dunia.
610x.jpg


Kati ya wakimbiaji kumi waliokwenda Ujerumani, makimbiaji watano walijikita katika mbio za marathon na kama uliweza kufuatilia matokeo yake unayajua. Kama kawaida ya mchezo huu na mengine sababu za kushindwa ziliwekwa wazi kama zinavyochambuliwa na Father Kidevu.
(i) inaonekana wewe sio mwanamichezo kwani ungekuwa mmoja basi ungegundua kuwa huo mchezo wako umeathirika kwa kukosa ufadhili.

(ii) Mmoja kati ya wadhadhili ambao wamejijengea ngome za kuendelea kuvitafuna binti vyao. Utapata ushahidi zaidi only if you identify yourself.
(i)Ama kweli Nyani aoni kundule, nimejaribu kukuomba uthibitishe ni kwa namna gani mashindano ya umiss yanavyosababisha kuanguka kwa riadha, na umeshindwa kufanya hivyo.

Nilivyokuelewa ni kwamba katika riadha ya Tz inawakilishwa na wasichana pekee, na kurudishwa tena kwa mashindano hayo kumesababisha wasichana kuacha kukimbia na kukimbilia mashindano ya urembo. Hapa kwanza inabidi uombe radhi kwa kudhalilisha mchezo wa riadha ambao una washiriki wa kiume na kike.

Ili kukufahamisha namna gani jamii hii imekuwa ikifuatilia mchezo huo kuanzia kwenye mafanikio yake na matatizo yake nakuwekea linki kadhaa na uzipitie kwa kina kabla ya kukurupuka tena na pumba zako.

Mwaka 2008 mwezi wa tisa, Rais Jakaya Kikwete alionyesha nia ya dhati kwa serikali kusaidia mchezo wa riadha. Chama cha riadha RT, kilitoa nafasi kwa wadau wote wa riadha kutoa maoni yao juu ya kuinua mchezo huu. Awali Rais alikitaka chama hicho kusema kama kinataka kupatiwa kocha wa kigeni. Hata hivyo chama hicho kilihitaji kwanza maoni ya Watanzania juu ya kuufufua tena mchezo huu. Zaidi unaweza kucheki linki hii na kuona jinsi gani wana JF walivyotoa maoni yao.

Hapana shaka wewe nawe uliweza kutoa maoni yako!

Wadau wengi wanajua kwamba riadha imekufa, lakini kifo cha riadha kamwe hakiusishwi na mashindano ya urembo. Ni wale tu ambao wana mawazo finyu kama wewe ambao wanaweza kudhubutu kusema urembo unaangusha riadha hapa Tanzania.

Katika kujadili kufa kwa riadha, maoni mbalimbali yametolewa na kujadiliwa na kuwaachia wahusika kuchukua hatua mahususi na madhubuti ili kufufua mchezo huo. Moja ya tatizo sugu lililoonekana ni uongozi wa mchezo huo kama inavyosomeka katika maoni haya.

Tatizo lingine ambalo limeonekana ni migongano ya idara na mamlaka za serikali katika kuona mchezo huu unakuwa na sio kuanguka. Hii inadhibitishwa na mamlaka ya TRA jinsi walivyoshughulikia suala la vifaa vya michezo vya wanariadha mwaka 2006. Huu ukiwa ni muendelezo wa kukwamisha vifaa vya wanariadha ambapo ulianza tokea kipindi kile Major Juma Ikangaa alipopigwa stop kuingiza benz lake kama zawadi yake kwa kushinda mbio za marathoni huko Japani.

Kuanguka kwa michezo mengine zaidi ya riadha vilevile imekuwa inakuna wadau wengi wa michezo. Mwaka 2008 Gazeti la Tanzania Daima liliandika kwa urefu kadhia hiyo na kupata kujadiliwa hapa JF kama inavyoonyesha linki hii

(ii)Hoja yako ya pili sijaifahamu
 
Hebu thibitisha hapo kabla ya kuendelea kumwaga pumba...

Dah mkuu naona umesahau kidogo juzi kati hapa kulikuwa na mashindano ya ngumi Kitaifa viwanja vya Leaders hakuna hata kampuni lililo zamini wala hata maji ya kunywa nashangaa wamejikita kwenye mashindano ya vichupi na wanayapa kipaumbele sana kuliko michezo mingine.
 
Dah mkuu naona umesahau kidogo juzi kati hapa kulikuwa na mashindano ya ngumi Kitaifa viwanja vya Leaders hakuna hata kampuni lililo zamini wala hata maji ya kunywa nashangaa wamejikita kwenye mashindano ya vichupi na wanayapa kipaumbele sana kuliko michezo mingine.

Kwa kuwa mada hii inahusu warembo, na kwa kuwa warembo ni fani yako, na kwa kuwa kwa mara ya kwanza umepinga warembo kupewa big up. Nimeamua kukupa thanks za nguvu. Hapa na kwenye mchango wako. Thanks!
 
Back
Top Bottom