Masanduku 16 yamekamatwa yakiwa na kura zilizopigwa Arumeru Mashariki

Taarifa nilizozipata hivi punde kutoka kwa mwanaharakati aliyeko Arumeru mashariki ni kwamba masanduku 16 yakamatwa Tengeru yakiwa na kura zilizopigwa. Yamepatikana masanduku hayo 16 yakiwa yameichagua CCM. Mwenye taarifa kamili tafadhali amwage hapa janvini. Photos will be appreciated.

kweli hii mutu mubaya ..hawajaweka hata kura mbili mbili ktk kila box za chadema?
 
Hawa mafisadi hawana mbinu tena!

Habari hii ni ya ukweli kwn nimepokea simu kwa rafiki wangu wa karibu sana na ni mwanasisiem lakini ni jina tu!
Na bila shaka atanipa na picha flu!

Na habari zaidi imeendelea kudodosa ya kwmb zile kura zimetoka mikoa ya kusini na gari aina ya Landcruiser DFP Station Wagon.

Lakini nina hakika ya kwmb mafisadi hawana lolote zaidi ya wizi mtupu!

Ntarudi baada ya muda!
 
Duh Kama ni kweli Hii ni Hatari!! Hawa watu wanahubiri Demokrasia wasioweza Kutekeleza? Kweli Magamba Choka Mbaya!! Sasa ni muhimu watu Kuweka Target Maeneo yote yenye Chaguzi mbalimbali ; Kama Mwanza, Songea na Vijibweni!! Huwa hawa majaluba Huwa wanaficha masanduku porini na wanafanya zoezi la kubadilisha within 2 -3 Minutes!! Kweli hawa watu wanahadaa Demokrasia na Amani ya Nchi
 
With just over 24 hours remaining before the Electoral Commission announces Sumari the vote winner for Arumeru, Magwand@ are resorting to disseminating baseless informations for the sake of justifying their coming humiliating defeat by CCM.
 
Hawa mafisadi hawana mbinu tena!

Habari hii ni ya ukweli kwn nimepokea simu kwa rafiki wangu wa karibu sana na ni mwanasisiem lakini ni jina tu!
Na bila shaka atanipa na picha flu!

Na habari zaidi imeendelea kudodosa ya kwmb zile kura zimetoka mikoa ya kusini na gari aina ya Landcruiser DFP Station Wagon.

Lakini nina hakika ya kwmb mafisadi hawana lolote zaidi ya wizi mtupu!

Ntarudi baada ya muda!

uje na updates!
 
With just over 24 hours remaining before the Electoral Commission announces Sumari the vote winner for Arumeru, Magwand@ are resorting to disseminating baseless informations for the sake of justifying their coming humiliating defeat by CCM.

tulianza na MUNGU na tutamaliza naye
 
With just over 24 hours remaining before the Electoral Commission announces Sumari the vote winner for Arumeru, Magwand@ are resorting to disseminating baseless informations for the sake of justifying their coming humiliating defeat by CCM.
Blockhead at work.
 
Hizi taarifa nimezipokea kwa njia ya simu, ikanifanya ni browse jf kujua kama kuna mwingine mwenye taarifa hizi.
Inaonekana ni kweli, kwani mtu aliyenipigia hajawahi kudanganya.

ikibainika kuwa ni kweli kuna masanduku yamekamatwa, basi watu wa dini zote tutalazimika kutoa shukrani zetu kwa mungu wetu ijumaa na jumapili kwa tukio hili muhimu kwa usalama wa nchi yetu.

sababu kubwa ikiwa hii: kwamba mungu wetu anajibu maombi. tupo ambao tumekuwa tukiombea amani ya nchi yetu
ambayo ufunguo wake hasa upo katika mikono ya watu waliopo katika dola--hususan vyombo vya ulinzi na usalama.
vyombo vya ulinzi na usalama watapohamia upande wa matakwa ya wananchi, watapoanza kupuuza amri za kijinga kutoka chama tawala, amani ya nchi yetu itakuwa tayari imeishapatikana.

Haya masanduku 16 sababu pekee ya kushikwa kwake itakuwa kwamba mtu fulani katika dola amevujisha taarifa ya kuwepo kwake, na hili ni jema sana kwa usalama wa nchi yetu. asante mungu wetu. tunakuomba ee mungu wetu tanzania yetu ibadilike bila damu za watu kumwagika. watie ujasili polisi , watie ujasili mashushu, watie ujasili wanajeshi, watie ujasili tume ya uchaguzi na idara nyingine ambazo umeziweka wewe kwa maslahi ya waja wako katika taifa hili, waweke peupe upumbavu unaotishia kuangamiza taifa letu.

iwezeshe nchi yetu ikazaliwe upya katika amani.
 
mimi nimepigiwa simu na kuambiwa yamekamatwa kia,hii thread inasema tengeru
Hapa mkanganyiko,jamani kama kuna wanao zusha habari kutuchanganya hapa jamvini waache na kama ni ukweli tupeane fact with critical evidens kama vidio na audio ya lusinde matusi
 
Mmeshaanza , mmeona mnashindwa mnaandaa visingizio in advance.

Hata kama kweli masanduku yamekamatwa na kura ndani lakini mwisho wa siku mawakala wenu watakuwepo pale kituoni watahesabu masanduku na kuangalia ndani kama yana kitu chochote.
 
Back
Top Bottom