Masaki flats bounce back

Nakumbuka Mgambo walibomoa, kama kawaida walichukua vitu vyote maana zile ghorofa zilikuwa zimekamilika na kilakitu ndani.

Manispaa aina uwezo wakulipa zile gharama.
 
Hii nchi haitakiwi kuendelea kuongozwa na hawa wacheza sanaa wanaoona hakuna shida hela za walipa kodi kutumika bila mpangalio.

Wao wanatoa vibali vya kujenga na kubomoa! Umeona wapi hiyo!
 
• Adaiwa kuitia hasara serikali bil. 8

na Mwandishi Wetu, Tanzania Daima

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ametajwa tena kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni nane kutokana na amri aliyoitoa akiwa madarakani ya kubomoa jengo la ghorofa lililopo kiwanja namba 383, Barabara ya Toure, Masaki, Dar es Salaam.

Lowassa, alitoa amri hiyo kwa Manispaa ya Kinondoni mwaka 2006, akidai kuwa majengo hayo mali ya Kampuni ya Empire Properties Ltd, yalikiuka taratibu na sheria za ujenzi mijini.

Hii ni mara ya pili katika siku za hivi karibuni Lowassa kutajwa kuisababishia hasara Serikali ya Awamu ya Nne kutokana na baadhi ya maamuzi aliyokuwa akiyafanya.

Kwa mara ya kwanza Lowassa alitajwa hivi karibuni wakati Kamati ya Bunge inayoshughulikia Hesabu za Serikali, ilipokutana na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini.

Wakati wa kikao hicho, kamati hiyo ilielezwa kwamba mwaka 2007 serikali ilitumia zaidi ya sh milioni 11 kwa ajili ya kuwaleta na kuwagharimia wataalamu kutoka Thailand kwa ajili ya kutengeneza mvua hapa nchini.

Juzi, Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi jijini, iliuamuru uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuilipa fidia ya sh 8,047,814,000 Kampuni ya Empire Properties Ltd, kwa kuvunja majengo yake yaliyokuwa kwenye ujenzi Masaki.

Kutokana na amri hiyo ya mahakama, baadhi ya viongozi wa Manispaa ya Kinondoni waliozungumzia hukumu hiyo kwa sharti la kutokutaka majina yao yachapishwe gazetini, walisema akiwa Waziri Mkuu, Lowassa aliamuru majengo hayo yabomolewe kwa vile yalikiuka sheria ya ujenzi mijini.

"Hayo ni maamuzi ya kukurupuka, tuliwahi kukaa kwenye vikao hapa wilayani, baadhi ya madiwani na wataalamu, tulipinga kabisa uamuzi wa kubomoa ghorofa hilo, lakini wengi tulihofia kuingizwa kwenye mkumbo wa ufisadi maana tusingeeleweka.

"Nasema hivyo kwa sababu wapo maofisa wa ardhi waliofunguliwa kesi kwa kutoa kibali namba 00000600 cha ujenzi huo kihalali, walishapima wakaona panafaa. Leo tizama kiasi cha fedha za kulipa fidia, ni nyingi sana," alisema mmoja wa madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.

Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni mwaka 2006 iliamua kubomoa jengo hilo lililopo kwenye kiwanja namba 383 Barabara ya Toure na Mtaa wa Mwaya huko Masaki, kwa madai kuwa yalijengwa bila kuzingatia kanuni za ujenzi mijini.

Taarifa za awali zinaonyesha Kampuni ya Empire Properties Ltd kabla ya ujenzi wa majengo hayo iliwasilisha kwenye halmashauri maombi ya kibali cha ujenzi yakiyoambatana na michoro kwa ajili ya uendelezaji wa kiwanja hicho ikiyoonyesha kusudi la kampuni hiyo kujenga ghorofa nane.

Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni baada ya kupitia michoro hiyo iliyowasilishwa na kwa kuzingatia matumizi ya mipango miji, iliidhinisha michoro hiyo na kutoa kibali cha ujenzi mwaka 2004. Kibali hicho kiliruhusu ujenzi huo. Kesi ya kulipwa fidia kwa Kampuni ya Empire ilisikilizwa na Jaji Aghaton Nchimbi na kutolewa uamuzi Januari 8, mwaka huu.


h.sep3.gif
I conclude, Kweli huyu ni mtaaalamu wa kushughulikia fedha za umma

blank.gif
 
Tulilijua hili mapema..tuwaachie wananchi waamue wenyewe..

ila naona wananchi wameshachoka
 
Hii ndo gharama tunayoilipa kwa Kikwete kukaidi wosia wa Baba wa Taifa, Nyerere! Lowassa ni mpenda pesa, PERIOD!
 
Yule jamaa angeendelea kuwa PM kwa miaka miwili zaidi sijui tungekuwa wapi?
 
Jengo hili liko jirani na anakoishi EL kwa sasa hapa jijini. Inasemekana alilitaka sana eneo hili kama anavyofahamika kwa UCHU wake wa vitu vitatu, namely, PESA, ARDHI na MADARAKA. Wahindi hawa wakamzidi kete. Hata hili nalo hatuna ushahidi wa kumfikisha mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka?
 
Wakati tafakuri ikifanyika na huku tukisubiri wajuzi wa sheria kutujuza kama anaweza kufikishwa mahakamani au la, kuna yale ambayo yanaweza kufanyika bila kusubiri.Wale watumishi wa Manispaa au wizara husika ambao wamebainika kumshauri vibaya au kumpotosha kwa makusudi wanazo lawama za kujibu na hatua kali za kisheria na za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.

Hawa kama custodians wa records na issuers wa permits hizo walijua au walipaswa kujua kwamba ujenzi ule ni halali na unaoendana na mipango miji. Angalau Kenya wanajaribu kuchukua hatua dhidi ya watumishi wao japo ni kwa juu juu na selectively.

Hata hivyo jazba aliyoonyesha Mkubwa huyu wakati wa kuamuru kubomolewa kwa majengo yale inaleta hisia kwamba hazikuchochewa na ukuikwaji wa sheria za ujenzi na mipango miji peke. Zilionyesha mtu mwenye personal interest na kilichojitokeza pale.

Ni kama vile opportunity ilijileta ili yeye aitumie ku-settle scores. Wataalam wanaweza kutuambia fidia hiyo ni proportion kiasi gani katika pato letu la taifa na tungeweza kupata huduma kiasi gani kama zingetumika kwa ajili ya umma wa Watanzania!
 
Najua wengi mmeshasahau na labda hata wengine hawajui kiliwahi kutokea. Baada ya jengo la Chang'ombe Village kuporomoka na kuua kulifuatia soul searching na kuanza kubomolewa kwa majengo mbalimbali mengine yakidaiwa yalikuwa yanajengwa kinyume cha sheria na bila ya vibali husika. Mojawapo ni jengo lililokuwa pale Masaki (kona ya Mwaya na Toure)..

Sasa habari ambazo zimeanza kutiririka siku hizi chache ni kuwa wamiliki wa jengo hilo wameshinda kesi?? na Manispaa ya Kinondoni itajikuta inawalipa fidia. More info to come.. (i'm going to sleep!)


Uzuri wa serikali yetu inajiandaa kushindwa kesi hata kabla ya kesi yenyewe kunanza. Ndio maana katika kesi mia inashinda moja, 99 inapoteza. Huu ni mradi mwingine uliobuniwa kuzitafuna kodi za wananchi.
 
Uzuri wa serikali yetu inajiandaa kushindwa kesi hata kabla ya kesi yenyewe kunanza. Ndio maana katika kesi mia inashinda moja, 99 inapoteza. Huu ni mradi mwingine uliobuniwa kuzitafuna kodi za wananchi.

Very true...
 
hawa wakubwa wote bwegez tuuu. wanajifikiria wenyewe tu!!!
Tuwafanyejee wakubwaa hawa wanaojiona wao ndo SERIKALI!!!!

Je wapi nguvu ya mahakama katika kuzuia uharibifuu unaopelekeaa serikali kuwajibika kwa kulipaa???Nina maana court order ya kuzuia kuvunjaa haikuwapoo au mlalamikaji aliona wamalize kuvunja then ashtaki alipwee upyaa jengoo??
 
Haya ndio mazao tunayovuna kwa kukubali kuwachagua viongozi wasio fuata sheria.
 
wale wamiliki au mmiliki atalipwa 8bil kama fidia usumbufu wote etc, remember hela hii itatoka mfukoni mwako! aaghrrrrrrrrrr!!
 
Kama serikali/halmashauri itatakiwa kulipwa itabidi waliohusika na uzembe ndio walipe ,au hii itashindikana vp!?
 
Yule jamaa angeendelea kuwa PM kwa miaka miwili zaidi sijui tungekuwa wapi?
Magazeti yetu yanaamini hayauzi bila richmond/lowassa/rostam.
Hivyo mtu mwenye akili yake anaweza kuutwisha uamuzi wa serikali [cabinet decision] kwa mtu mmoja??? basi kama kuna mtu wa kutwisha bora angebebeshwa rais.
 
Hold on!

Ina maana alivyosema tu libomolewe, basi wasaidizi wake, manispaa husika, n.k vilifuata u amri blindly bila kupinga au kushauri??
 
Back
Top Bottom