DOKEZO Maringo, Kawe kuna wenzetu wanaziba mitaro ya barabarani kwa viroba ili wapate maji ya kumwagilia maua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kawe.jpg

Maringo.jpg

Eneo la Kawe katika Kituo cha Daladala cha Maringo kuna hali ambayo imekuwa ikinikera kwa muda mrefu, mitaro inayopotisha maji inazibwa kwa makusudu kwa kutumia viroba na vijana wanaofanya biashara ya kuuza maua ‘original’, yaani yale maua halisi, wanafanya hivyo ili wapate maji ya kumwagilia maua yao.

Taarifa hii tumeshaitoa kuanzia Ofisi ya Kata hadi wahusika wa Ofisi ya Mazingira Wilaya ya Ilala lakini jibu tulilopewa ni kwamba maua hayo yanayopandwa yanapendezesha mji, hivyo ni lazima yawepo.
Maringo1.jpg

Maringo2.jpg
Inapotokea kuna mamlaka zinafanya mchakato wa kusafisha mitaro hiyo baada ya muda wahusika hao wa maua wanarejesha viroba vyao, kibada zaidi ni kuwa mvua zikinyesha hawavitoi hivyo viroba, kwa hiyo maji yanaoverflow na kusambaa juu.

Kingine kinachokera zaidi kuna wenzetu kadhaa walishawahi kulalamika juu ya tabia hiyo inayofanywa na wenzetu hao wa maua, wakaanza kuwatishia maisha kuwa wanwaharibia biashara wakati ukweli ni kuwa wao ndio wanachangia uharibifu wa mazingira na hawachukuliwe hatua.

Naheshimu biashara na ajira yao lakini basi wazingatie usafi wa mazingira, kwani maji hayo ya mtaroni yanaposambaa kwenda sehemu nyingine hasa kwenye makazi ya watu ni hatari kwa afya kwa kuwa si masafi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom