TRA ya Kitilya imeoza kwa rushwa

the circus

Member
Oct 24, 2011
71
59
Wana Jf nimeikuta hii michuzi lakini mwenyewe kaweka mambo huwezi kucopy text toka kwenye blog yake
Harry-Kitilya.jpg

By US Blogger

Ankal Michuzi, naomba unipe nafasi kuandika kidogo juu ya mambo niliyokumbana nayo ili wa-Tanzania hasa waishio nje ya nchi waelewe hali halisi jinsi inavyosikitisha na kukatisha tama.

Viongozi wamekuwa na safari za kila siku na wamekuwa wakihalalisha gharama za safari zao ya kwamba wanahimiza uwekezaji na sisi wana diaspora tumekuwa tukiambiwa tujenge nchi kwani hakuna tuliyemuwachia nchi atujengee.

Kwa heshima na taadhima baadhi yetu tukaitikia wito. Mimi nikajikusanya na wenzangu ili tuanzishe mradi ambao ulikwa na malengo ya sisi wanasiriamali tupate faida kwa ajili ya juhudi zatu na pia wenzetu wa nyumbani wapate ajira. Tulifanya utafiti wa kisayansi na mtu yoyote amabaye angeona business plan yetu na ni mtalamu wa biashara angeamini kabisa tumejitahidi. Biashara yetu ilikuwa ijishughulishe na ununuzi wa bidhaa kutoka mbalimbali na kupeleka nyumbani.

Wakati tunasafarisha mzigo tulishafanya utafiti wa viwango vya kodi, TRA wenyewe walishatupa makadirio ya kodi kutikana na invoices zetu. Baada ya mzigo kufika Dar es Salaam biashara yote iligeuka na kuwa janga, kwanza TRA walitupatia viwango vya kodi kama jinsi tulivyotarajia, baada ya siku 2-3 clearing agent wetu anatuambia ya kwamba wame ‘uplift’ thamani na hivyo kodi inaongezeka kwa asilimia 100, tukahoji kwa nini iwe hivyo tukaambiwa ya kwamba tathmini ya kwanza hailingani na ‘minimum values’ za TRA wakati ni haohao TRA ndio waliotoa makadirio ya kodi ya awali (preliminary).

Agent wetu anasema hakuna namna kwani hata mtu uki appeal inachukua muda mrefu, nilivyojaribu kuangalia online namna yak u appeal harakaharaka hakuna maelezo yoyote, nikajaribu kuwasiliana na watumishi wa TRA ninaowafahamu nao pia wakasema kama kuna mtu ame uplift hakuna namna. Sasa kama bidhaa inatarajiwa kupatya faida ya kama 20% utawezaje kupata faida endapo kodi inapandishwa kimchezomchezo.

Tukasema haya maji tumeyavulia nguo sasa tunaoge, tukakubali kulipa hiyo kodi. Kam hiyo haitoshi wakati wa kukagua hakuna lolote jipya lakini mkaguzi naye akasema anaongeza kodi. Pia tulikuwa na bidhaa chache amabazo thamani yake haizidi hata $150, bidhaa hizo zilikuwa kama sample kwa wateja wetu kwa hiyo hatukuziweka kwenye invoice, jamaa wa TRA wakadai hilo ni kosa na adhabu yake ni dola $10,000. Hawa jamaa hawana hata ubinaadamu, wao lengo lao ni kukomoa tu na kujifanya Miungu watu. Wana ubinafsi wa hali ya juu na wala hawajali ya kwamba wakimfilishi mjasiriamali atawacha kufanya biashara na wao mapato yatapungua, wanaangalia wakomoe leo bila ya kujali mapato ya kesho.

Yote haya wanayafanya kwa lengo la kushawishi rushwa na online hakuna namna ya kuwasiliana harakaharaka na wakubwa ili waingilie kati. Matokeo yake ni kwamba tumejikuta tumelipa asilimia 500 ya makodi kulinganisha na mahesabu yetu wakati timu yetu ya biashara ina mpaka wahasibu wanaofanya kazi marekani katika taasisi muhimu. Yaani elimu ya mtu haina thamani yoyote katika kufanya biashara Tanzania, ili ufanikiwe inabidi uwe mtoa rushwa vinginevyo ni kupoteza muda.

Nimewasiliana na baadhi wa wafanyabiashara waliofanikiwa na kuwasimulia na wanasema hayo ndio mambo ya kawaida na kwamba ‘huku hakuna formula’. Sasa nchi ambayo mambo yanakwenda kijanjajanja sisi diaspora tutawezaje kuchangia maendeleo kama TRA kazi yao ni kukomoa tu watu. Nimejikuta nalipa kodi zaidi ya hata gharama za kununulia bidhaa.

Mimi nashauri viongozi waache mara moja kushawishi wajasiriamali kuwekeza nchini na kupoteza hela za safari za nchi mpaka hapo vyombo husika vitakapokuwa tayari kufanya kazi na diaspora.

Katika nchi za ulaya na marekani ukinunua chochote hata kama ni gari ama nyumba unapata makadirio ya kodi na wakati wa kulipa unalipa mpaka cents kama jinsi ilivyo makadirio, kufanya hivyo hakuhitaji fedha kwa hiyo umasikini sio sababu, tatizo letu ni kwamba hakuna utamaduni wa uadilifu na watumishi wa Serikali wameweka ubinafsi mbele na uwajibikaji pia hakuna.

Leo tumesoma ya kwamba Serikali inataka kukopa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, kama TRA kazi yao ni kuuwa biashara kwa nini Serikali isifilisike?

Ujanja unaofanywa na TRA sio kubadilisha rate ya kodi kwani rate inapangwa na sheria, wanapowakaba watu ni kwenye thamani ya mali, nunua mali ya $1 lakini ikifika kwenye kupiga hesabu za kodi wao wanakwambia tunaanzia na $5 na unajikuta unalipa mara tano ya ulichotegemea ama unalazimika kuacha mzigo wago uwe mali ya TRA ili wapige mnada na hapo wanashirikiana na marafiki zao kupata makontena ya watu kwa bei ya kuokota wakati mwenye mali ameshakula hasara

Ushauri wangu wa bure kwa wajasiriamali wanaoishi nje ya nchi hasa wale ambao wana matatizo ya moyo ama blood pressure ni kwamba kama kama rushwa kwako ni mwiko na ni dhambi usipoteze muda wako na biashara za Tanzania zinazohusu kuingiza bidhaa, TRA watakuliza na wanaweza kukuua kwa heart attack.

Usblogger11@gmail.com

Kuna Maoni 26 mpaka sasa.

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 09:05:00 PM 2011

Hiyo ndio hali halisi ya uingizaji bidhaa, jamaa wa TRA wanafaidika kwa kukomoa wafanyabiashara na hawana hata chembe ya ubinadamu wao wanatizama mifuko yao wala hiyo uplifted usifikiri inakwenda serikali bali hiyo ni kwa ajili yao. makaratasi wanayaandika upya na wanalipa serikali ile bei ya mwanzo waliokuambia kilichozidi ni makato yao. Tena usiombe ukakutana na wale wamama ndio ujue utajuta kuingiza mzigo. mie kidogo niache RaV 4 yangu pale lakini ndio hivyo. Jamaa wametengeneza mazingira ya rushwa na kudhulumu watu. wafanyabiashara wadogo wala usiingize mzigo pale utaweza kujinyonga. watu wengi washajuta..hii serikali haina macho wala masikio kwasababu tushalalamika sana lakini hakuna mabadiliko..au labda na sisi tuanze kuchukua sheria mikononi...

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 09:27:00 PM 2011

Nimegundukua kitu kimoja hapa TZ. Mtu akisema ukweli kuhusu nchi yetu ilivyooza watu (baadhi) wanakuwa na hasira na kuanza kuongea maneno ya ajabu. Juzi hapa kuna jamaa mmoja alitoa maoni yake juu ya customer service TZ watu wakabisha tena kwa hasira wakati aliyoyazungumza yule jamaa ni ya ukweli kabisa na yapo hapa TZ tunayaona kila siku. Sitashangaa na tuhuma hizi alizotoa USblogge kupingwa na baadhi ya watu wasiopenda kuambiwa ukweli. TZ has to change for real, Kikwete inabidi awe dikteta kubadilisha hii nchi, tunakwisha jamani na hizi dhuluma za kila kukicha. Kikwete uko wapi babaaaa?

Zak Anasema:
Thu Dec 29, 10:00:00 PM 2011

Ndiyo maana bongo haiendelei!

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 10:07:00 PM 2011

Mdau, nakubaliana na wewe 500%.

1. Mimi baada ya kutua tu ng'ambo nikafanya shopping ya zawadi kadhaa na kuwatumia watu wa nyumbani. Cha ajabu, nililipa kodi mara nne ya gharama nilizotumia kununua zawadi zenyewe. Toka wakati huo nimeacha kabisa kutuma zawadi nyumbani. Cha ajabu, waafrika wengine wanashangaa inakuwaje nalipa zaidi kiasi hicho wakati wao wakituma zawadi makwao ni kupeta tu.

2. Baada ya kuji-establish huku na kujenga mtandao na watu wenye akili na uwezo, nikawashawishi tukawekeze Tanzania. Jamaa wakakubali na tulitimiza taratibu zote. Kasheshe likaja kwa TRA, wazungu walikiri hawajawahi kufikiria kunaweza kuwa na ushenzi wa namna hiyo duniani katika uwigo wa uwekezaji. Mimi mwenyewe, japo nilihisi kungekuwa na mambo hayo, sikudhani yangekuwa kiasi hiko. Tuligairi kuwekeza bongo, na sasa biashara zetu zinashamiri vilivyo nchini Botswana na Kenya, mwakani tunafungua matawi Uganda na Zambia. Ila Tanzania marufuku, kamwe!!! Na nimekuwa balozi mzuri sana kuwashauri watu huku wajiulize mara kumi kumi kabla ya kuamua kwenda na kuwekeza Tanzania. Kwa ufupi, Tanzania stori nyingiiii, ila vitendo ni vya kikatili kupitiliza, hata mkoloni asingetubana namna hii.

3. Mwaka jana mmoja wa wakurugenzi wenzangu alifunga safari kwenda kutalii Tanzania. Yaliyomkuta hataki hata kutuambia kiundani, anachosisitiza ni kuwa mgeni yeyote anayerudia kwenda Tanzania kwa mara ya pili hawezi kuwa na akili sawa. Anailalamikia sana sekta ya huduma katika utalii.

...Tanzania yetu ndio nchi ya salamaaaa....!

Makaramu Anasema:
Thu Dec 29, 10:19:00 PM 2011

Dah,kwanza pole sana ndugu yangu.Pili...nashukuru kwa ushauri wako,,,mimi ni diaspora niko Ulaya,,,nilikuwa najiuliza na kupanga biashara ya kufanya form next year.Nikawa nimeamua kuwa nanunua bidhaa huku tena mpya na kwenda kuuza nyumbani,lakini sasa nimekoma baada ya kusoma makara yako hapa.Sitafanya biashara na TZ.Nitajaribu Nchi zingine,,,,,make kuna nchi zingine kidogo sheria inafanya kazi na hakuna rushwa za kijinga kama za kwetu.ASANTE SANA NDU,NAKUTAKIA MWAKA MPYA WENYE KHERI NA BARAKA,,,NA PIA KWAKO KAKA MICHUZI HAPPY NEW YEAR.

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 10:23:00 PM 2011

MDAU SIO WEWE TU WATU WOTE WA NJE HILO TATIZO LINATUHUSU.YAANI YOTE HIO NI KWAMBA UNALAZIMISHWA UTOE RUSHWA.MIMI NIMEKWAMA NA MZIGO WANGU DAHACO, JAMAA ANANAMBIA KAMA NIMETOKA ULAYA HIII NI BONGO! WATAKULA POLISI AU KWA KIKWETE?

YAANI SIO SIRI INAKATISHA TAMAA HATA RAIS ANAPOKUJA KUTUPA DOMO ETI MSISAHAU BONGO MATOKEO YAKE NDIO HAYO, nIMEPELEKA USED REFRIGERATORS 40ft CONTAINER AMBAZO NI 100 units, NIMEFANYA MAONGEZI KABLA NA TRA WAKANIHAKIKISHIA NI 5 MILLIONS SHS, SAWA NIMEJIFUNGA MWANAUME MZIGO KWANZA PAPER WORKS ZAKE, NI TAYARI MILLION 2. WAKAJA SASA WAZEE WA KALAMU IKAFIKA MILLION 11,500,000/= SAWA KUTOA MZIGO MPAKA UNAFIKA NYUMBANI ZINGINE MILLION 3, HIO NI PAMOJA NA RUSHWA ASKARI BARABARANI, DORIA NA MENGINE MENGI TU HATA KAMA UNAKARATASI ZOTE NI LEGAL. FAIDA NILIOKUWA NIKITEGEMEA NI HIO MILLION 7 AMBAYO IMEKWISHA NA MINUS JUU. KWA KWELI INAKATISHA TAMAA WALA WABONGO MSIMSIKILIZE HUYO RAIS WETU NA POROJO ZAKE ZA KUTUVIKA VITAMBAA HAKUNA LOLOTE LA MAANA HUKO

Buckinghamshire Anasema:
Thu Dec 29, 10:24:00 PM 2011

Ndugu yangu US blogger, mimi mambo ya Tanzania nchi yetu tuipendayo nilishayasema mno humu mpaka mwisho nimechoka. Ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Sisi tumelogwa, na aliyetuloga alishakufa. Ndiyo maana watu tuliopata nafasi ya kuishi ughaibuni na kuzoea systems za huku tunasita kurudi nyumbani au ku-invest huko (Tanzania). Nchi inanuka rushwa, wizi nje nje, hakuna principles wala kanuni rasmi za biashara, alimradi shida tu. Mimi nimeshaamua, bongo ni kuja likizo kumsalimia mama tu. Kama ni biashara, kazi, au proper safari holiday ya kuangalia wanyama nitaenda Masaai Mara (Kenya) au visiwa vya Bermudas ambako wanajua maana ya Customer Service ni nini.

Buckinghamshire

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 10:41:00 PM 2011

HAO NDIO TRA (TANZANIA ROBBERY AUTHORITY) pole bwana, tushazowea hayo mambo kwa sisi tunaoka nje

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 10:58:00 PM 2011

kwanza pole sana ndugu yangu hiyo ndio hali halisi kabisa ya hapa nyumbani

Buckinghamshire Anasema:
Thu Dec 29, 11:04:00 PM 2011

Kuna wakati niliwahi kuandika makala humu yenye title 'Nchi Yetu Ni Kichwa Cha Mwendawazimu' lakini ikapuuzwa. Hata hivyo leo nasisitiza tena, japokuwa Tanzania ninaipenda lakini ukweli ni kuwa nchi yetu ni kichwa cha mwendawazimu.

Hatuhitaji ujuzi wa sayansi ya roketi kudhibiti uchafu na ubadhirifu unaofanyika pale longroom (TRA). Lakini why toka nikingali mtoto nikiishi TZ mpaka leo hii niko overseas bado tabia yao ni ile ile? Hiyo ina maana AMA viongozi wa nchi hawajui kazi yao, au wao nao pia wanakula nao hao wabadhirifu wa TRA!

Cha kusikitisha ni kwamba hata kila baada ya uchaguzi hakuna bunge hata moja linaloraise hiyo issue... Wabunge wetu nao (wote wa upinzani na wa chama tawala nao pia wanatafuta kula tu) alimradi total chaos. Anyway mimi kama nilivyosema, nilishasema sana mpaka nimechoka, bongo mimi basi, hata mama watoto nitatafuta huku huku :)

Pole sana US blogger, baadae nitakuemail.

Buckinghamshire

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 11:09:00 PM 2011

You are off the hook if you do your things right and play no poker games with TRA.
When you think you are smart and want to conceal some financial deal with TRA- thats when problem begins.

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 11:17:00 PM 2011

US Blogger, a house divided can not stand. It is the government versus the government. And it is the government by the people for the people. So why blame the government if "by the people" is incompetent. No president in the world can supervise everything. I think TRA jobs in Tanzania have sworn to corruption and destruction of the country. It is a people's choice. Let go!

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 11:18:00 PM 2011

Yaani huu mswada ni wa maana sana na unaumiza wadau wengi wenye nia nzuri ya kuanzisha maisha yao. TRA kweli kuna WEZI wa kutupa. Uaminifu hakuna na kila mtu anataka kujinufaisha yeye mwenyewe kupitia JASHO la wavuja jasho.

Ustaarabu kwao ni Msamiati ambao hauleweki na hata kwenye kamusi zao haupatikani. Hawa wafanyakazi mafedhuli wa TRA wanashindwa kuelewa kuwa hawa watu wa kawaida(na Wajasilimali) wanajitahidi kuanzisha/kuendeleza maisha yao, na kulisha/kuelimisha na kuvisha familia zao.

KWANINI ubeberu wa namna hii? Mnaonesha nini na mnashawishi vipi watu wasitoe Rushwa ama kutumia njia za mkato????? Tanzania itakuwa lini????

Huu ni uozo unaonuka kabisa!!

Mdau na Mkereketwa!!

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 11:28:00 PM 2011

Bongo mwisho. Lakini kwanini mpate taabu wakati huko mliko mnaweza fanya biashara. Kuna vijana hapa UK wamefungua Pub wanaalika kina Kopa, Diamond, na wengine kupiga muziki. Kuna Serengeti anasafirisha mizigo, kuna Wakenya wanalinda. Biashara za nyumbani ni kuliana pesa tu. Kama unataka kuliwa pesa zako basi fanya biashara TZ wakati wewe unaishi ughaibuni!!

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 11:32:00 PM 2011

baba karibu mjini.. ila nakushauri usiskilize maneno ya maagenti kwani wao lao ni moja na watu wa TRA wakikwambia kodi wame 'uplift' waambie sawa mi na appeal as long as you have your supporting documents usiskilize hizo stori za kuchukua muda mrefu ni sound tu za kutaka uwape hela wenzio tunakomaa nao mpaka sa ivi wameshatuzoea michezo ka hiyo hawatufanyii..

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 11:37:00 PM 2011

Ndugu yangu uliyoyaandika kwakweli yote nisawa yamewatokea wengi na watu wameandika kila sehemu na wamelalamika kila kona mimi mwenyewe niliingiza gari nikawapa kila kitu na wakaenda mpaka company nilionunua gari wakaapewa kopi za risit kwamba bei nisawa lakini wakanipangia bei yao wanayotaka wenyewe nikalipa %110 kwakweli inasikitisha!
Nakuhusu webside unazosema ziko mapambo tu wala hazifanyi kazi na simu zao sizo!
mimi nilitaka kutapeliwa kiwanja changu nikaingia webside ya wizara ya Ardhi nikaandika email na nika wapigia hakuna anaepokea na email mpaka leo sijajibiwa!
chakuchekesha nikwamba viongozi wako wapi?Hawasomi magazeti watu wanavyofanyiwa?wananchi wananyanyasika sana viongozi hakuna Tanzania wenzetu kenya kwakweli wanaendelea vizuri ukilinganisha na sisi!Na nikweli sisi tunapenda nchi yetu lakini viongozi hawako pamoja na sisi na pia watanzania wenzetu waliokuwa tanzania wanakuwa kama na wivu hawatusaidii chochote kushirikiana kujenga nchi yetu kwa pamoja!
sisi tunajitahiid lakini sidhani kama watoto wetu watakuwa na mioyo kama yetu!Tunahitaji viongozi Tanzania kwa kila sekta kwakweli kuanzia raisi mpaka mesenja!

Anonymous Anasema:
Thu Dec 29, 11:39:00 PM 2011

Nakubaliana kabisa na mdau hapo, nilipeleka vitu Tanzania inaishia kuletewa kodi ambazo bei ya vitu haiwiani, 5 times most likely. TRA Tanzania watakuua

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 12:00:00 AM 2011

tra ni washenzi na wauaji hasa kuna mzee mmoja anaitwa mwaseba yeye ndio anajifanya tra ni ya kwake.

hawa ma clearing nao huwa ni waizi wakubwa mno shenzi zao.

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 01:50:00 AM 2011

Ni kweli kabisa ndugu zangu, mimi nimejionea mwenyewe, & we have to do something !. Ngoja tuanze sasa na hii dawa ya kuwataja hapa hadharani kwa majina sasa maana tumechoka sasa !!!, kuna mzee mmoja yupo TRA ya pale manzese anaitwa Mr. Bungenyi !!!, huyu mzee na najua pia wapo wengi sana wa namna hiyo !!, ni rushwa tu !, wanawajengea wananchi makusudi mazingira ya rushwa !!,jamani TAKUKURU mpo wapi ???!!!!!.We are tired kwa kweli !!! wizara zote za serikali zinanuka rushwa !!!, God will punish u one day !!!, leaders ( Viongozi ) !!!!!

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 01:59:00 AM 2011

Poleni ndugu zangu kwa yaliyowakuta. Viongozi wanalijua hili lakini 10%je?wanatumwa hao kutekeleza kazi yao,mwisho wa siku wanagawana, kwanza hakuna kiongozi anayelipa hayo makodi sijui mavalue, nyie wadanganyika ndio mnaolipishwa, Gari au mzigo ukifika bandarini na ni wa mkubwa, inapigwa simu tu hapo gari inatoka. Cha muhimu ni kwamba sasa hivi mfumo wa sheria Tanzanania umekuwa mzuri, jamani si tutumie recoding device kuwarecord tu, peleka kwenye dola tuone kama haki haitatendeka. Tuna simu hizi siku hizi unaweza kurecord video, peleka kwa pilato tuone kama haki haitendeki!!!kabla ya kuipeleka huko tuwekee kwenye blog hapa tuone wanavyoomba na kupekea rushwa, alafu huyo hakimu tuone asitende haki.
Hiyo ndio miaka 50 ya uhuru wa kuiba bila woga.
Mungu tubariki watanzania, maana tukisema ibariki nchi, nchi nadhani imeshaoza na tumelogwa, achilia mbali ni nchi ya kina nanii tu.

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 02:53:00 AM 2011

pole sana mdau..
aisee Bongo kama unataka mambo yako yaende vizuri we jifanye **** flani ndo hutasumbuliwa sana.ukijifanya we ni mtu honest wallah itakula kwako.
TRA ni mbwa maaana nikiwa likizo dukani kwa mzee jamaa sometimes huwa wanaingia hadi kwenye droo kuhesabu pesa ili kuona kama ziko sawa na hizo ulizoandika kwenye risiti.Sasa sheria gan inasema hivyo kama sio wizi tu?
We dawa kula na wakubwa tu....

Hata kontena kipindi wanakagua huwa wanachukua baadhi ya vitu alafu wanasema eti ni sample.sasa cjui wanajua mwenye mzigo anaviokota?TZ bila rushwa haiwezekaniiiiiii..............................
Davy-muni
Manichester

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 03:02:00 AM 2011

Wenzao huwa wanafukuza wote kisha wanaajiri wengine wapya, nao wakianza kujua mbinu za rushwa tu unatimua wote na kuajiri wapya, yaani unawaweka wafanyakazi mguu ndani mguu nje. Lakini twende mbele na turudi nyuma mnategemea nini ikiwa TRA yote imejaa kabila la wezi watupu? Wizi ni jadi yao na ili uwe mwizi lazima uwe na roho mbaya, roho ya kishetani. Tazama maghorofa yaliyoporomoshwa na wafanyakazi wa TRA? Tazama mahekalu waliyojenga huko kwao? Hiyo lifestyle yao unafikiri wanapata wapi hizo pesa?

Na ni nani anaruhusu hilo suala la kuuplift kodi iliyokwishakadiriwa kama sio kutengeneza mazingira ya rushwa? Na wao wanajua uovu wote wanaoufanya watalaumiwa viongozi, ifike mahala tuwalaumu wahusika moja kwa moja, na ikiwezekana watajwe kwa majina, kuwa fulani kaniomba rushwa nimemnyima, tuone kama hii tabia ya kuombana ombana rushwa haitaisha. Mtu akikuomba rushwa hakuna cha kwenda TAKUKURU wala nini unatoa tu tangazo lako kwenye vyombo vya habari basi, lazima tutengeneze HALL OF SHAME ndio tutaweza kurekebishana otherwise mmhh kumeoza hakufai hata kidogo. Mimi nafikiria mwakani kuhama nchi nikawalee watoto wangu mahali ambako kuna ustaarabu, heshima, utu na kufuata sheria maana wasijeambukizwa uozo bure!!

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 03:08:00 AM 2011

Dah, inasikitisha mno. Kuna jamaa aliandika kitu kama hiki kwamba hatuna customer service na ubabaishaji hapa TZ kumbe ni kweli? Sasa rais wetu kipenzi anafanya nini maana hili suala la TRA ni la muda mrefu sana. Hapa Dar kuna secretary tu wa TRA kajenga bonge la ghorofa kule (jina kapuni), sasa jiulizeni mdada tena secretary ana jumba kama lile analipwa mshahara gani mpaka awe na lijumba kama lile? TRA inabidi ishughulikiwe haraka. Haiwezekani mtu ananunua kitu bei ndogo toka ughaibuni kuleta bongo analipa zaidi ya thamani aliyonunulia. Na ndiyo maana watu wanashindwa kugomboa mali zao pale bandarini mwishowe zinaliwa na jamaa wa TRA. TZ tuamke jamani. Hii serikali ya Kikwete hii?

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 03:16:00 AM 2011

Ngojeni nakuja kuchukua hiyo nchi nitairekebisa, nitaweka ma watchdogo wangu mtu akienda tu kimzunguko out next day maana tunao wasomi wengi kwanini tumtunze huyu mla rushwa, nitawatupa gabage wasahaulike, maana watu tunaleta utani, siyo TRA tu na kwingineko nasikia hata bank kuu, nao wakipelekewa hayo makusanyo ya TRA wanaweka kwenye akauti zao badala ya akaunti ya serikali, nita kula nao sahani moja mpaka watafute kuniua na wala hawata weza nitawafagia wote sitaki uchafu mimi, nataka nchi hiyo niifanye kama Marekani sasa hivi, Ok.

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 03:16:00 AM 2011

nchi imeoza mimi naishi na watu wa nchi za afrika nyingine wao wanatuma mizigo kwao na hata magari wanalipia hela ndogo sana kiasi kwamba utawaonea wivu maana wanatuma kila siku ukiwaambia kodi ya nchi yetu kutuma gari au mizigo wanashangaa

nchi mbovu sana eti wanataka kuiombea ikiwa nchi imejaa rushwa maombi yatafika wapi

Anonymous Anasema:
Fri Dec 30, 04:21:00 AM 2011

Nilikua na mpango mkubwa sana wakupeleka watu TZ ku invest ila nikawa na doubts baada ya kuongea na watu wachache, na sasa najiuliza mara kumi kumi... Nimechanganyikiwa, hawa fellows wanataka kwenda lakini mimi naogopa lawama kwa yatakayowapata! Stressed right out!!! Botswana ni second choice na so far nimesikia mazuri tu, la sivyo kwa Kagame!
MICHUZI: yale yaleeeee.....TRA Inanuka Rushwa!
 
wenzenu TRA wanawatangazia kuwa wamevuka malengo ya kukusanya kodi........unafikiri viongozi wetu vilaza watawapigia kelele tena hao TRA?
 
alafu tunaambiwa ndani ya TRA kuna askari wa usalama wa taifa wa siri! System nzima ni mfu.usalama wa taifa kazi yao nini! Tunajengaje uchumi imara namna hii!
 
Utawala ukiwa lege lege system nzima inaharibika! Na bado a lot to come,kuna mabomu ni muda tu haujatimia! Rushwa inakoelekea inakuwa very complicated,sio ya kuomba tena bali ndani ya system,urasimu!
 
This is too much....i swear this is too much...we have to do something to stop this...
 
Moja ya sababu kubwa sana ya umaskini, ukwasi wa pesa na matatizo ya uchumi ni TRA kuwa na mfumo mbovu wa kukusanya mapato nafikiri kuliko nchi sana Africa na pia wafanyakazi wameoza kwa rushwa hapo TRA na sijui PCCB inafanya nini? Vigogo na wafanyabiashara wakubwa hawalipi kodi
 
Kitilya na genge lake wana loyalty kwa Basil Pesambili Mramba ; mpaka hapo kesi yake ya rushwa itakapotupiliwa mbali wanakinyongo na Mkweree ndio maana wanahujumu mapato kwa kuendekeza mambo ya rushwa!! Mstaafu Luhanjo alikuwa anafaidika na genge hili na ndio maana akamuingiza mkenge mkweree kwa kumshauri amuongezee muda wa miaka miwili ya contract Kitilya!! Pole sana wadanganyika.
 
CCM oyeeee!

Ndg pamoja na kwamba mzigo wote tunaitwisha CCM/Serikali kwa uzembe, lakini wanaofanya haya ni mimi na wewe tuliokalia hizi office.
Manjonjo ya dini zao na vyama vyao wakifika ofisini wanaweka pembeni ni rushwa kwa kwenda mbele.

Tubadilikeni jamani, tuanze sisi wenyewe kama si hivyo watoto wetu tutawaridhisha nchi hipi? Rushwa, tamaa, ubinafsi, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka ni janga tunaitaji kubadilika.
 
.....Tubadilikeni jamani, tuanze sisi wenyewe kama si hivyo watoto wetu tutawaridhisha nchi hipi? Rushwa, tamaa, ubinafsi, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka ni janga tunaitaji kubadilika......

Mkuu,
Kwa level ya uchafu ilipofikia kwa sasa, kurekebisha inahitaji muda mrefu, moyo na akili kama ya mwendawazimu, ingawa inawezekana. Ni suala ambalo inatakiwa lichukue investment ya muda mrefu sana, kwa maana ya kufundisha uzalendo kwa nchi toka ngazi ya shule za awali kabisa. Uzalendo wa nchi hii umekwisha kabisa, na kwa hali ilivyo sasa Tanzania, ukionekana unafanya jambo kinyume na mazoea (vile inavyostahili lifanyike) , kila mtu anakushangaa. Nakuunga mkono, tuanze sasa mabadiliko hayo
 
Wana Jf nimeikuta hii michuzi lakini mwenyewe kaweka mambo huwezi kucopy text toka kwenye blog yake
Harry-Kitilya.jpg

By US Blogger

Ankal Michuzi, naomba unipe nafasi kuandika kidogo juu ya mambo niliyokumbana nayo ili wa-Tanzania hasa waishio nje ya nchi waelewe hali halisi jinsi inavyosikitisha na kukatisha tama.

Viongozi wamekuwa na safari za kila siku na wamekuwa wakihalalisha gharama za safari zao ya kwamba wanahimiza uwekezaji na sisi wana diaspora tumekuwa tukiambiwa tujenge nchi kwani hakuna tuliyemuwachia nchi atujengee.

Kwa heshima na taadhima baadhi yetu tukaitikia wito. Mimi nikajikusanya na wenzangu ili tuanzishe mradi ambao ulikwa na malengo ya sisi wanasiriamali tupate faida kwa ajili ya juhudi zatu na pia wenzetu wa nyumbani wapate ajira. Tulifanya utafiti wa kisayansi na mtu yoyote amabaye angeona business plan yetu na ni mtalamu wa biashara angeamini kabisa tumejitahidi. Biashara yetu ilikuwa ijishughulishe na ununuzi wa bidhaa kutoka mbalimbali na kupeleka nyumbani.

Wakati tunasafarisha mzigo tulishafanya utafiti wa viwango vya kodi, TRA wenyewe walishatupa makadirio ya kodi kutikana na invoices zetu. Baada ya mzigo kufika Dar es Salaam biashara yote iligeuka na kuwa janga, kwanza TRA walitupatia viwango vya kodi kama jinsi tulivyotarajia, baada ya siku 2-3 clearing agent wetu anatuambia ya kwamba wame ‘uplift’ thamani na hivyo kodi inaongezeka kwa asilimia 100, tukahoji kwa nini iwe hivyo tukaambiwa ya kwamba tathmini ya kwanza hailingani na ‘minimum values’ za TRA wakati ni haohao TRA ndio waliotoa makadirio ya kodi ya awali (preliminary).

Agent wetu anasema hakuna namna kwani hata mtu uki appeal inachukua muda mrefu, nilivyojaribu kuangalia online namna yak u appeal harakaharaka hakuna maelezo yoyote, nikajaribu kuwasiliana na watumishi wa TRA ninaowafahamu nao pia wakasema kama kuna mtu ame uplift hakuna namna. Sasa kama bidhaa inatarajiwa kupatya faida ya kama 20% utawezaje kupata faida endapo kodi inapandishwa kimchezomchezo.

Tukasema haya maji tumeyavulia nguo sasa tunaoge, tukakubali kulipa hiyo kodi. Kam hiyo haitoshi wakati wa kukagua hakuna lolote jipya lakini mkaguzi naye akasema anaongeza kodi. Pia tulikuwa na bidhaa chache amabazo thamani yake haizidi hata $150, bidhaa hizo zilikuwa kama sample kwa wateja wetu kwa hiyo hatukuziweka kwenye invoice, jamaa wa TRA wakadai hilo ni kosa na adhabu yake ni dola $10,000. Hawa jamaa hawana hata ubinaadamu, wao lengo lao ni kukomoa tu na kujifanya Miungu watu. Wana ubinafsi wa hali ya juu na wala hawajali ya kwamba wakimfilishi mjasiriamali atawacha kufanya biashara na wao mapato yatapungua, wanaangalia wakomoe leo bila ya kujali mapato ya kesho.

Yote haya wanayafanya kwa lengo la kushawishi rushwa na online hakuna namna ya kuwasiliana harakaharaka na wakubwa ili waingilie kati. Matokeo yake ni kwamba tumejikuta tumelipa asilimia 500 ya makodi kulinganisha na mahesabu yetu wakati timu yetu ya biashara ina mpaka wahasibu wanaofanya kazi marekani katika taasisi muhimu. Yaani elimu ya mtu haina thamani yoyote katika kufanya biashara Tanzania, ili ufanikiwe inabidi uwe mtoa rushwa vinginevyo ni kupoteza muda.

Nimewasiliana na baadhi wa wafanyabiashara waliofanikiwa na kuwasimulia na wanasema hayo ndio mambo ya kawaida na kwamba ‘huku hakuna formula’. Sasa nchi ambayo mambo yanakwenda kijanjajanja sisi diaspora tutawezaje kuchangia maendeleo kama TRA kazi yao ni kukomoa tu watu. Nimejikuta nalipa kodi zaidi ya hata gharama za kununulia bidhaa.

Mimi nashauri viongozi waache mara moja kushawishi wajasiriamali kuwekeza nchini na kupoteza hela za safari za nchi mpaka hapo vyombo husika vitakapokuwa tayari kufanya kazi na diaspora.

Katika nchi za ulaya na marekani ukinunua chochote hata kama ni gari ama nyumba unapata makadirio ya kodi na wakati wa kulipa unalipa mpaka cents kama jinsi ilivyo makadirio, kufanya hivyo hakuhitaji fedha kwa hiyo umasikini sio sababu, tatizo letu ni kwamba hakuna utamaduni wa uadilifu na watumishi wa Serikali wameweka ubinafsi mbele na uwajibikaji pia hakuna.

Leo tumesoma ya kwamba Serikali inataka kukopa fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, kama TRA kazi yao ni kuuwa biashara kwa nini Serikali isifilisike?

Ujanja unaofanywa na TRA sio kubadilisha rate ya kodi kwani rate inapangwa na sheria, wanapowakaba watu ni kwenye thamani ya mali, nunua mali ya $1 lakini ikifika kwenye kupiga hesabu za kodi wao wanakwambia tunaanzia na $5 na unajikuta unalipa mara tano ya ulichotegemea ama unalazimika kuacha mzigo wago uwe mali ya TRA ili wapige mnada na hapo wanashirikiana na marafiki zao kupata makontena ya watu kwa bei ya kuokota wakati mwenye mali ameshakula hasara

Ushauri wangu wa bure kwa wajasiriamali wanaoishi nje ya nchi hasa wale ambao wana matatizo ya moyo ama blood pressure ni kwamba kama kama rushwa kwako ni mwiko na ni dhambi usipoteze muda wako na biashara za Tanzania zinazohusu kuingiza bidhaa, TRA watakuliza na wanaweza kukuua kwa heart attack.

Usblogger11@gmail.com

Kuna Maoni 26 mpaka sasa.

MICHUZI: yale yaleeeee.....TRA Inanuka Rushwa!
Mambo yote haya yalikuwa yanafanyika geti namba ngapi vile??
 
Back
Top Bottom