Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Watu hawaelewi wanafikiri ni kuzuiliwa kwenda US tu - hii ngoma inakwenda mbele zaidi kwamba US haitapokea traces zozote za ndugu zako wa damu, watoto wako, mzigo ama order yoyote toka Marekani kwa jina lako milele - hadi watakapoifuta hatua hii

Kumbuka kwamba hii ni individual - hata ukiacha kazi serikalini leo bado adhabu ipo palepale mpaka itakapotenguliwa ! - kwa hiyo kama ulikuwa na mtoto wako, ndugu yako wa damu anasema unakwenda na maji - jiandae kumpokea
watu hewa wamezuiwa kwenda marekani? Siamini Taifa kubwa hivi linashindwa kutoa taarifa kamili. Naipenda Marekani na siamini taarifa hii! It is too low!
 
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."

View attachment 1681412

Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
___________________________________________________

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.

Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.

Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.

Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.

Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.

''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo

Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.

BBC.
 
Lkn katiba inasema Mnataikiwa muheshimu UHURU WA MTU WA KUJIELEZA,JE KWA KUFANYA HIVYO HUONI WAMEENDA KINYUME NA KATIBA.

KWANI HAKUNA ALIYE JUU YA KATIBA.
Ndio maana Trump hajafungwa jela kwa tuhuma za uchochezi.Angekuwa yupo Tz angeitwa centro.

Trump alikuwa anawachochea wafuasi wake wafanye fujo.Aliwachochea wafuasi waje wakanye mavi katika jengo la bunge.Ndio maana kafungiwa.
Wamebugi awa lini na lini magu akaenda nje ya nchi
JE Bashite?
 
Ndio maana Trump hajafungwa jela kwa tuhuma za uchochezi.Angekuwa yupo Tz angeitwa centro.

Trump alikuwa anawachochea wafuasi wake wafanye fujo.Aliwachochea wafuasi waje wakanye mavi katika jengo la bunge.Ndio maana kafungiwa.

JE Bashite?
Ulichokiandika una uhakika nacho? Trump kesi yake ipo senate na lazima safari atapatikana na hatia. Halafu Attorney General wa DC anamchunguza kuhusu kesi nyingi na hiyo ya uchochezi sasa ihvi muda usiozidi saa moja na nusu atakua raia wa kawaida subiri utitiri wa kesi
 
Mimi nasema hivi pale Marekani hakuna aliye juu ya sheria.Ata ukiwa Rais ukivunja sheria unashughulikiwa.

Kuna nchi zingine unakuta Rais anavunja sheria na anakiuka katiba na hakuna chochote kinafanyika sababu kuna watu wapo juu ya sheria
 
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."
Pompeo kagusa pasipo gusika.
=====
 
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."

View attachment 1681412

Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
___________________________________________________

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.

Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.

Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.

Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.

Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.

''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo

Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.

BBC.
Haina noma Pompeo nae kapigwa stop asikanyage China
 
Waulize Iranians, Zimbabweans, North Korea etc nini maana ya vikwazo vya waAmerica . Wala usiombe wakaenda deep

Odhis *
Sasa hizo nchi ulizozitaja hapo ni zimekewa vikwazo vya kiuchumi nchi kama nchi(yaani serikali kuu) na siyo viongozi mmoja mmoja.

Taarifa ya leo inasema inawawekea vikwazo vya kusafiri(kuwanyima visa ya kuingia marekani) baadhi ya maafisa wa serikali waliohujumu uchaguzi.

Kwa hiyo lazima utofautishe nchi kama nchi kuwekewa vikwazo na kiongozi mmoja mmoja kuwekewa vikwazo.

Mfano : Paul Makonda alipotangaza mashoga wote wa dar wakamatwe, marekani iliamua kumwekea vikwazo vya kusafiri yeye kama yeye na siyo serikali kuu.
 
Waulize Iranians, Zimbabweans, North Korea etc nini maana ya vikwazo vya waAmerica . Wala usiombe wakaenda deep

Odhis *
Sasa hizo nchi ulizozitaja hapo ni zimewekewa vikwazo vya kiuchumi nchi kama nchi(yaani serikali kuu) na siyo viongozi mmoja mmoja.

Taarifa ya leo inasema inawawekea vikwazo vya kusafiri(kuwanyima visa ya kuingia marekani) baadhi ya maafisa wa serikali waliohujumu uchaguzi.

Kwa hiyo lazima utofautishe nchi kama nchi kuwekewa vikwazo na kiongozi mmoja mmoja kuwekewa vikwazo.

Mfano : Paul Makonda alipotangaza mashoga wote wa dar wakamatwe, marekani iliamua kumwekea vikwazo vya kusafiri yeye kama yeye na siyo serikali kuu
 
Back
Top Bottom