Marafiki wanaoishi DAR... Sio kabisa

Utani unaokaribia na ukweli sio mzuri hata kidogo! Yote tisa, kumi pale anapojifanya yupo bze lunch tym ili aonekanae amekosa muda wa kwenda kula kumbe hana mambo!!! Mitaa mingine; sio fair kabisa kuweka ofisi; eti unakuta msosi wa bei rahisi ni wali wa sh.1,500/=!!! heri nimeondoka kwenye ofisi ya mitaa ile!
Maeneo gani tena hayo!! mana posta vyakula vy buku kibaao.
 
Kaka maisha ya Dar si sawa na ya kwenu ulikotoka, kukaribisha mgeni ni mzigo mzito sana. Watu tunawakimbia hata ndugu sembuse wewe rafiki!
 
Kaka maisha ya Dar si sawa na ya kwenu ulikotoka, kukaribisha mgeni ni mzigo mzito sana. Watu tunawakimbia hata ndugu sembuse wewe rafiki!
<br />
<br />
nani kasema mie nakuja hamishia shda zangu kwako... Acheni hzo.. Twaja tukijua mko hooii..
 
<br />
<br />
preta mm nakuja mjini next week na hela yangu ya mavuno,naomba nikutafute unionyeshe mji 2le bata,nipm pls

HUNA lolote kijana, uma laya tu unakusumbua! Preta ni mke wa mtu huyo; shauri yako! Kama kweli hauna nia mbaya, mtumie kwanza viroba viwili vya mchele na debe moja la viazi mbatata!
 
mkuu dar kubwa sana na pilika ni nyingi sana, wala usiwalaumu wapwa zako...
 
Wana JF ... hili limekaa vipi?.. Mie nimetoka Mkoani nimekuja Jijini(DAR).. kwa Mapumziko kidogo, kusalimia ndugu na marafiki zangu....
sasa jamani ugumu nimeukuta ktk ishu moja... Rafiki zangu wa Ukweli,,nimesoma nao kabisa,,,tumeishi pamoja chuoni... tumekula bata(kujirusha) pamoja wakati nipo nao chuo...!!! Maajabu nimewatafuta niwaone wamekua watu wa ma promise yasiyokua na fulfilment... Sasa mie nikajiuliza hawa vijana wanaoishi dar... wanatuchukulia vipi sie tunaotoka Mkoa... wanadhani ua tunakuja lia NJAA..kwao auuu??? Acheni ujinga bana, tunakuja na hela zetu za mavuuno ...!!!

Mhhh,Uzoefu wangu ni kwamba Dar ni dunia nyigine...Watu wanaishi kama wako kwenye machimbo ya mawe na huko kwenye mashimo Oxygen haitoshi....Ni jambo linalositikisha ila kama mtu ni mwelewa na mwepesi wa kusoma mazingira, unaweza kuwapotezea na kusubiri hadi waje mikoani..Kuna baadhi ya washikaji heshima imerudi mara tu baada ya kutemblea huku mikoani na kupigwa dinner na mazaga zaga mengine!

...e bana wee...ni ukweli usiopingika. Taratibu ule utamaduni tuliokuwa nao wa 'kuwakarimu' wageni unaanza kutoweka.
Hata mimi nime li experience hilo Dar, afadhali kidogo waliopo Arusha, angalau wanajitahidi kukufata huko ulipo.
Sijui wa mwanza wakoje?...

Waliopo Dar utawasikia lawama zao siku ukiondoka japo walijua upo mujini...
kukimbiana noma wakuu, kupigika kimaisha ni jambo la kawaida, kukutana na mgeni wako muhimu,
hata mki share 'kijoti' cha maji ya uhai powa tu....

...kwa faida ya vizazi vyetu na vijavyo,....maisha mnayoyakumbatia sio.
 
Mimi nafikiri njia ile uliyotumia kuwatafuta (simu,sms,e mail) ndiyo hiyo hiyo ungetumia kuwalaumu ili ujumbe uwafikie walengwa directly.
 
DC nimependa maelezo yako.... but umeniacha njia panda hapo... heshima imerudi kivipi?? yaaani akukimbie alafu akija kwako mkoani ndo heshima irudi (au in the sense majumbani mwao mwa ukweli??)

Unajua ADii, binadamu tulio wengi tunapenda kulipa mabaya kwa mabaya...Binafsi niko tofauti. Kwa wale ambao tumekutana huku mikoani, mie nimetoa muda wangu na resources nyingine kuwa-entertain...Baada ya hapo ndiyo nimeanza kuona mabadiliko kiasi kwamba hata nikiwapigia ninapokuwa mujini Dar wanajitahidi tunaonana au wanatoa sababu zinazoeleweka.....


Ujumbe...Be yourself and revenge not!
 
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia,
alitoka siku moja, porini kutembelea,
akayaona matunda, mtini yameenea,
mtini yameenea, sungura nakuambia............
........................................
..................................

Sungura karuka ruka, mtini akarukia,
mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
kwenye mti akatoka, pembeni akasogea,
pembeni akasogea, sungura nakuambia!

Dah!! e bana nimesahau muendelezo wa hili shairi; wadau naomba mnikumbushe basi!! Au kwenye vitabu vya watoto wa siku hizi hamna hili shairi? manake nataka nifikie pale ambapo baada ya mzee sungura kuruka sana na kushindwa kuyapata matunda; mshikaji ikabidi aponde "sizitaki mbichi hizi!"

Yaani JF hii...ni zaidi ya kila kitu...ni Full package!!

Ahsate kwa kutukumbusha enzi zile za Kibanga ampiga Mkoloni!!
 
Dar watu wanatoka majimbani mwao saa kumi na moja wanarudi saa tatu usiku utaonana nao saa ngapi? Usiwalaumu kaka Ingekuwa Arusha ningekukirimi. Karibu sana Arusha kaka
 
Naturally....hakuweza kufanya mawasiliano vizuri na wakongwe...mbona wako wengi tuu...aaah sion hata sababu ya kuwataja...maana hata mzee wa kaunta anajulikana
Watu wa JF mbona wapenda meeting new members... you know the wrong JF members basi....lol
 
UKIONA hivi sasa nina uso wa bashasha ni kwamba nipo mitaa ya posta ambako ugali mchicha robo napata kwa sh.350/=!
mh! 350!! embu niagizie mana kuna kadada saa z lunch huwa kananiganda ganda nikapeleke huko..
 
preta mm nakuja mjini next week na hela yangu ya mavuno,naomba nikutafute unionyeshe mji 2le bata,nipm pls

usijali mpendwa.......wewe na mimi.....mimi na wewe......wewe cheza na PM yako tu.....
 
.....usafiri kaka,mpk wafike huko kwako siku inakuwa imeisha!hiyo ndio daslam bana
 
Pole sana Data watu wanakimbizana na maisha...kama bado upo DSM omba kampani ya JF membaz ..hautajutia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom