Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Mfano kitendo cha JK kuyasamehe majizi ya EPA!, kwa mwingine huo ni udhaifu na kwa mwingine ni ushujaa, huruma na upendo!. Wakati mmoja anaona huo ni udhaifu kwa rais kuvunja katiba na kuyasamehe majizi yale kabla hayafikishwa mbele ya vyombo halali vya kisheria kwa mujibu wa katiba, kwa wengine, kitendo hicho cha rais akinatafsiriwa kuwa ni upendo mno na majizi ya pesa nyingi, kufuatia upendo huu, rais ameingia huruma watu hao anaowapenda wasiende kuteseka jela, hivyo akawasamehe kwa upendo na huruma!. Sasa unapomuita rais JK ni dhaifu kwa watu walikula upendo na huruma yake, huku kwao ni kumtukana, ndio maana nikasema Ndungai was right, Mnyika amemtukana rais mwema na mwenye huruma kuwa ni dhaifu!.

Pasco, hapa ninataomba msaada zaidi.... Raisi kuzima swala la EPA, kwa nini tuseme/tuone ni moyo wa HURUMA na si CORRUPT HEART?
Mtu kama Rais si anaapa kuilinda Katiba ya nchi na Katiba imetoa msimamo wa wazi juu ya hatua za kumchukulia mwizi wa kuku na mwizi wa EPA? sasa rais anatoka wapi kuingilia Katiba kwa kuhurumia mwizi wa EPA? Je haya si mambo yanoweza kumfanya baadae akawa kama Mubaraka? Mtu anayempenda mwenzake umwambia ukweli na ukweli kwa raisi wetu, Ndugai na wote wa jinsi hii ni kwamba mambo yanabadilika sana!! mfano mzuri ni chales Taila na Mubaraka
 
ukiwa kiongozi dhaifu na ukathibitika kweli wewe ni dhaifu basi hata uongozi wako utakuwa legelege daima,na hata wasaidizi utakaokuwa nao hawayakuwa tofauti na wewe,JK ni dhaifu kiuongozi na hilo sio suala la kujadili hapa.tusubiri tu hiyo miaka 3 iishe huku nchi ikiendeshwa kama hamna watu makini wa kuiongoza
 
He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

Duh! Siamini kama na wewe Pasco unanunua huo utumbo. Ok, sawa "JK ameangushwa"
sasa itasaidia nini sisi kuorodhesha mapufu yake hapa? Sababu hao "watendaji" aliowategemea ni bado anawategemea....
Kwa maana yako ni kuwa JK yupo chini kaanguka na hatoamka sababu bado yupo na watendaji walewale...
Haitafaa kitu kwa miaka hii 3 iliyobaki.
Pasco na jouneGwalu,
Naomba turejee kwenye hii Makala. Iliandikwa na Rafiki yangu Ansbert Ngurumo tarehe 23/11/2008 akiwa hapa Uingereza masomoni.

Tusilainishwe na tabasamu (2)

MIONGONI mwa wasomaji wa Maswali Magumu waliowasiliana nami wiki hii, yupo mmoja ambaye aliniunga mkono, lakini pia akadokeza:
"Kutoa kashfa binafsi kwa (Jakaya) Kikwete kwa makosa yanayofanywa na mawaziri au maofisa si sawa; ni utovu wa nidhamu na kwenda kinyume cha maandiko uliyonukuu.

Inafahamika anayelikandamiza gazeti la MwanaHALISI na (Saed) Kubenea ni Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni. Kwa nini kashfa zako umpakazie rais?"

Naamini wapo wengine kadhaa wanaofikiri kama Mtanzania mwenzetu huyu. Wana sababu zao. Na wamegawanyika katika makundi kadhaa, lakini makubwa yaliyo dhahiri ni haya matatu.

Kundi la kwanza ni la watu ambao hawataki kabisa kuona wala kusikia rais akihusishwa na uzembe, kashfa, kushindwa, udhaifu au ufisadi wowote katika utendaji wa serikali anayoiongoza. Hawa bado wana imani kwamba rais ni mtu wa pekee na ana uwezo mkubwa na wa pekee, bali wasaidizi wake ndio wana uwezo mdogo. Hivyo, wasaidizi hao ndio wanaoharibu. Na wakiharibu wao, walaumiwe wao; si rais.

Watu wenye fikra hizi ndio wamekuwa wanadai (tuliiona hata kwenye utafiti wa REDET) kwamba umaarufu wa serikali umeshuka kuliko wa rais.
Wanathubutu kumtenga rais na serikali anayoiongoza! Wanajaribu kumtenga na mawaziri wake! Inawezekana? Rais anaongoza serikali ipi, na mawaziri wanaongoza serikali ipi? Kama si kupitia kwa mawaziri na wateule wake wengine, rais anaongozaje nchi?

Kundi la pili ni la wale ambao hawajui kabisa kwamba makosa ya mawaziri na watendaji wengine wa serikali yanamrudia rais.
Hivyo, hawamuoni rais katika wizara za nchi hii na idara zake. Hawamuoni mikoani na wilayani katika matamko na utendaji wa wakuu wa mikoa na wilaya. Nasisitiza: hawajui; si kwamba hawataki. Hawa tutawaelimisha taratibu.

Kundi la tatu ni la wale wanaojua vema uhusiano kati ya rais na wasaidizi wake, lakini bado wamekumbwa na kasumba na ulimbukeni wa kizamani juu ya utukufu na "ufalme" wa rais. Wanaiona taasisi ya urais kama taasisi nyeti isiyopaswa kuguswa – iheshimiwe tu, isiwajibishwe hata inaposhindwa kuonyesha unyeti wake.

Hawa wapo tayari kuswagwa au kuandamana kama kondoo nyuma ya kiongozi ambaye hawajui anaelekea wapi! Utii na ufuasi huu wa kikondoo ndio wanaouita heshima na nidhamu wanayotarajia kila mwananchi awe nayo. Ndiyo maana wanaona kuwa kumhusisha rais na makosa ya mawaziri wake ni kashfa binafsi na utovu wa nidhamu!

Ni bahati mbaya, lakini tunao watu wenye fikra za namna hizi. Tutawakomboaje? Labda tuwahoji kidogo; harakati zao za kupata majibu ya maswali tutakayowapa zinaweza kusaidia kufungua milango yao ya uelewa na ufahamu.

Tutumie mfano wa mwili wa binadamu. Tuseme rais ni kichwa. Mawaziri, wakuu wa mikoa, wakurugenzi mbalimbali kutoka Ikulu hadi idara za wizara, wakuu wa wilaya, wakuu wa vyombo vya usalama, majeshi yote, mabalozi wote nje ya nchi, na wateule wote wa rais tuwafananishe na macho, masikio, midomo, pua, mikono, miguu, na viungo mbalimbali vya mwili.

Kama mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, na wateule wengine wote wa rais ni mikono na miguu yake, tunaweza kujidai tuna akili timamu kwa kuthubutu kuwatenga na rais?

Maana wao ndio mikono anayoitumia kushika; ndiyo miguu anayotembelea; ndiyo macho anayotumia kuona; ndizo pua anazonusia; ndiyo masikio anayotumia kupata habari; na ndiyo midomo yake.

Watu hawa, na vyombo vingine vya dola vinavyomzunguka rais, ndiyo nguvu halisi ya urais wake. Hawa ndio wanaomletea taarifa, ndio wanaomshauri; na baada ya kutafakari taarifa anazopewa nao, anawatuma wale wale na wengine ili kutekeleza makubaliano au hitimisho la ushauri aliopewa. Au anawapuuza.

Ndiyo maana majeshi yamekula kiapo kumtii rais. Mawaziri na wateule wengine wameapa kumtii. Wakuu wa mikoa na wilaya wanaitwa wawakilishi wa rais katika maeneo yao ya utawala. Ndiyo maana kuna Ikulu Ndogo katika maeneo yao ya kazi.

Viapo, utii na mnyororo huu wa kimadaraka kutoka Ikulu hadi vijijini, ndivyo vinamfanya rais awajibike kwa matendo ya wateule wake.
Na kwa sababu ndiye anayewateua kwa mamlaka aliyonayo, na ndiye anayeweza kuwaondoa wasipofanya kazi vizuri, taifa litamwandama yeye anapoendelea kuvumilia makosa yao.

Uchumi ukitetereka, usalama wa nchi ukiwa hatarini, nchi ikikumbwa na njaa, maradhi yakiongezeka na kuhatarisha maisha ya wananchi, elimu ikishuka, walimu na wanafunzi wakinyanyaswa kwa kulalamikia sera au masilahi duni, bei za bidhaa zikipanda hovyo hovyo na kudunisha maisha, miundombinu ikiharibika na kukosa matengenezo, uhusiano wetu na mataifa ya nje ukiharibika, mfumo wa kisheria na kikatiba ukiwa kandamizi, rasilimali za taifa zikiporwa na wageni au wenyeji, zikitungwa sheria mbovu au kandamizi na kama mbaya zilizopo hazifutwi wala kufanyiwa marekebisho, wananchi wakikandamizwa na kunyanyaswa wanapojaribu kuwasiliana, kugoma au kuandamana; anayelaumiwa ni rais.

Sababu kuu ni moja. Ndiye mwenye mamlaka ya juu yanayoendesha taasisi zote kubwa na nyeti; na ndiye anayewateua wasimamizi wa taasisi hizo, washauri wake na waendeshaji wa idara nyeti za serikali.

Ndiye anayepaswa kujenga visheni ya kitaifa, na kwa kushirikiana na wataalamu washauri katika nyanja mbalimbali, kuweka mwelekeo wa kitaifa na kuwatumia watu wenye ujuzi kusimamia na kutekeleza visheni hiyo.

Kama alivyo na mamlaka makubwa ya kuwateua watu hao, ndivyo alivyo na mamlaka makubwa ya kuwaondoa pale wanapodhihirika kushindwa kazi aliyowapa. Wakishindwa akawaondoa, tunaona rais anafanya kazi yake vizuri. Wakishindwa akawavumilia na kufurahia kushindwa kwao, tunaona rais ameshindwa kazi, na anashirikiana na walioshindwa kazi kuhujumu maendeleo ya nchi.

Kama rais asingekuwa na uwezo huu ndani ya utendaji wa wateule wake, basi hata heshima anayopewa isingepaswa kuwapo. Na kama yeye hawajibiki kwa matendo ya wasaidizi na wateule wake – yaani kama wao wana mamlaka yanayoishia kwao, na wanawajibika kwa nafsi zao bila kumhusisha yeye, basi hatuna sababu ya kuwa na rais. Hana umuhimu!

Lakini katiba yetu imemfanya rais kuwa mtu muhimu sana, mwenye mamlaka makubwa sana, kiasi kwamba ingawa maandishi yanasema hakuna mtu aliye juu ya sheria, rais anaishi na kutenda kama mtu aliye nje ya sheria.

Na hii ni sehemu mojawapo ya udhaifu wa katiba yetu ambayo inampa rais mamlaka makubwa mno, kiasi kwamba anafika mahali pa kupuuza na kuviendesha hata vyombo vinavyopaswa kumsimamia na kumwajibisha.

Tazama wabunge wetu wanavyonywea linapofika suala la kujadili makosa kadhaa ya rais! Hivi tujiulize. Kama wabunge wetu wangekuwa hawamwogopi rais, Bunge lingekuwa na msuli wa kuwazuia kujadili hotuba yake aliyoitoa bungeni mwezi Agosti mwaka huu, hotuba iliyoonekana kupwaya na ikabezwa na wengi, wa kwanza akiwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta?

Kwamba hatimaye iliondolewa kabisa katika mjadala wa Bunge, ni dhahiri kwamba mamlaka ya rais yalitumika kudhibiti wabunge wasifukue na kuanika udhaifu wa rais katika hotuba hiyo. Ni udhaifu ulioandaliwa na wasaidizi wake walioandaa hotuba hiyo, lakini pia ni udhaifu wa serikali yenyewe maana hawakuwa na la maana kuliko hilo la kuwaeleza wananchi.

Ndiyo maana licha ya udhaifu wa hotuba hiyo, wale walioiandaa bado wapo Ikulu wanaandaa hotuba nyingine. Rais hana wasiwasi. Ni kazi bure kuwakemea wale kama bosi wao anaona wanafanya kazi nzuri.

Au tujadili kidogo hili la waziri wa habari na MwanaHALISI. Wizara yake ni sehemu ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne. Sheria aliyotumia kulifungia gazeti hilo ni sheria halali lakini dhalimu na katili inayotumiwa na Serikali ya Awamu ya Nne.

Na kabla ya waziri kutoa tamko lake, Ikulu ilishatoa mwelekeo kwa kumtumia Mkurugenzi wa Mawasiliano, Salva Rweyemamu, ambaye alikemea habari liyoandikwa na MwanaHALISI.

Na kuna mambo mawili ya kukumbuka juu ya Salva Rweyemamu. Kwanza, amekuwa Rais wa MISA (Taasisi ya Vyombo vya Habari katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, pia katika tawi la Tanzania).

Bado tunakumbuka matamko mazito aliyotoa akiwa rais wa MISA dhidi ya serikali (ya Mkapa) kwa kufungia vyombo vya habari. Ni mwandishi mwandamizi ambaye baadhi yetu tumepata bahati ya kufanya kazi kwa karibu naye, pamoja naye na chini yake.

Tunajua uwezo wake na uelewa wake wa masuala mbalimbali, lakini hasa ya habari na mawasiliano. Si huyu aliyepaswa kutoa tamko (kwa niaba ya Ikulu) ili kulikandamiza gazeti la MwanaHALISI.

Pili, kwa cheo alichonacho sasa, yeye ni mshauri wa rais katika masuala ya habari na mawasiliano. Maana yake ushauri wake ndio unaweka mwelekeo wa uamuzi na utendaji wa serikali katika suala husika. Na kwa kuwa alishatoa kauli kukemea kilichofanywa na MwanaHALISI, ni wazi kuwa alitumwa kutoa kauli hiyo (kama sehemu ya majukumu yake), na kwamba ofisi inayomtuma ni ile iliyomteua. Kwa hiyo, tamko lolote analotoa Salva ni la rais. Salva alikuwa anaisemea Ikulu.

Kwa hiyo, kama Ikulu imeshatoa kauli, halafu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ikahitimisha kwa kuchukua hatua, tunadhani tuko sahihi kusema mbaya wa MwanaHALISI ni waziri, si rais? Au bado tupo pale pale tulipoanzia wiki iliyopita tunalainishwa na tabasamu?

Na kama Salva huyu tunayemjua kwa miaka mingi amegeuka na kuwa msemaji wa rais katika mambo aliyokuwa akiyapinga kwa nguvu zote, basi kuna mawili.

Kwanza, tutasema kwamba hakuwa mkweli tangu awali; yaani hakutetea jambo aliloliamini kwa moyo wake na akili zake zote. Maana haiingii akilini kwamba sheria hizi na matendo haya yalikuwa dhalimu wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, lakini sasa tunayaona kuwa halali na ya kawaida katika utawala wa Rais Kikwete. Vinginevyo, tukubaliane kwamba tumelainishwa na tabasamu.

Pili, wadhifa wake wa sasa unampa fursa ya kuathiri mambo mengi ndani ya serikali katika sekta ya habari na mawasiliano. Ni fursa ya Salva kutekeleza kwa vitendo, tena kwa kasi na ari mpya, harakati alizokuwa anaziendesha kwa makongamano na matamko makali akiwa rais wa MISA au mkurugenzi wa Habari Corporation.

Kama hadi sasa ameshindwa kubadili mwelekeo wa serikali katika masuala nyeti kama hayo, huku akiwa mshauri wa kiongozi mkuu wa nchi ambaye ‘akipiga chafya mawaziri wanaugua mafua,' basi huu ni ushahidi mwingine kwamba nguvu ya bosi wake ni kubwa mno na hashauriki wala habadiliki kwa yale asiyotaka.

Ndiyo maana Salva na waziri wa habari wamejikuta wakiimba wimbo ule ule dhidi ya MwanaHALISI – wimbo wa serikali, wimbo wa bosi wao.
Ni hatari kama wapo wananchi wanaodhani kwamba rais ni mtu siyepaswa kuhusishwa na uamuzi na vitendo kama hivi.

Kama asingehusika, angewakemea Salva na Mkuchika; angebatilisha uamuzi wa wizara kulifungia gazeti; angewachukulia hatua kali wahusika; na kwa mamlaka aliyonayo, tayari angekuwa ameelekeza mabadiliko ya haraka yafanyike kufuta sheria dhalimu na kandamizi. Ni kwa nini tunalainika hovyo hovyo na kushindwa kufikiri kwa kina?

Itaendelea Jumapili ijayo.

Mwisho wa kunukuu!

TUMBIRI (PhD, University of Hull, UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Wakati mwingine huwa najiuliza sana, huenda huyu bwana (JK)hana akili timamu!

1, hasimamii kile anachokisema (kwa ufupi ni muongo)
2, ni mtu kigeugeu
3, anajifanya msikivu sana kumbe mnafiki.
4, ni mdini mkubwa.
5. hajui ni kwanini yupo ikulu na wala hajui majukumu ya mtu anayefika ikulu ni yapi. (anafikiri ikulu ni dangulo au soko la maharamia)
 
critic nyingine kwa rais wa Nne ni kutokumulika kwa karibu kule katika halmashauri zetu hapa nchini,ambako ndio fedha za watanzania zinapotea bila habari.wale aliowatimua juzi ni trela tu.azimulike halmashauri kule ndio kuna uozo uliotukuka


Aidha mimi rais wa tano,namshauri akumbuke ahadi yake kwa watanzania kuwa "IM SMILING BUT FIRM IN SERIOUS ISSUES"
 
kasoro nyingine ya Mh rais wa Nne ni kuwaamini wasaidizi wake kwa asilimia mia moja,hii ni dosari kubwa sana.

Rais wa tano nasema hili si lakufumbia macho.akumbuke kuwa hakuna binadam aliekamilika asilimia zote,hivyo ajitahidi kuwa anawakumbusha mara kwa mara wafanye kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu pamoja na kujali haki na wajibu.
 
kasoro nyingine ya Mh rais wa Nne ni kuwaamini wasaidizi wake kwa asilimia mia moja,hii ni dosari kubwa sana.

Rais wa tano nasema hili si lakufumbia macho.akumbuke kuwa hakuna binadam aliekamilika asilimia zote,hivyo ajitahidi kuwa anawakumbusha mara kwa mara wafanye kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu paumoja na kujali haki na wajibu.
jadi..umeshasema binadamu tunamapungufu, sasa nayy c ndo pungufu lake au umemtoa kwny ubnadam?
 
H wana JF. kumbe inafaa kusoma kwa makini kabla ya kuchangia. All the best!
Mkuu Baba Gaston, kwanza karibu sana jf, pili hongera kwa kukubali kuwa mvumilivu wa kutafuta ufahamu kwanza, kabla hujaanza kuchangia, natamani wana jf wengi wangekuwa kama wewe, mautumbo mengi humu jukwaani yangepungua!.
 
Kwani tulimuomba kuwa kiongozi wetu, mbona nyie watu mnajaribu kumpamba ? Rais maana yake ni nini ? ni kiongozi anayepashwa kutuonyesha njia, ndio maana tunamlisha na kumtunza maisha yake yote hili yeye akae atafakari awe makini , afikiri badala ya sisi na kutuonyesha njia ya kutupeleka kwenye neema na maisha bora. Sasa kama anashindwa anakaa kufanya nini, kama hawezi kuongoza vizuri anataka nini . Si apishe wenye uwezo wakafanye kazi , sio kutupotezea miaka kumi kwa kucheza kiduku.Jamani watanzania watu wenye uwezo mbona wapo kibao.Kwa nini mnataka kumpamba Kikwete kuwa ni mtu makini ? kafnya nini cha maana ?
Mkuu Omukajunguti, lets be fair, hivi ulitaka rais wako afanya nini zaidi hiki alichofanya?, njia si ameshatonyesha ya kuelekea kwenye maisha bora?, au unataka akubebe mpaska akufikishe hapo?. Anayeshindwa kufikia maisha ni aliyekuonyesha njia au aliyeshindwa kufika?.

Si tumemchagua wenyewe?, na baada ya miaka mitano, tukaridhika na utendaji wake, tukamuongezea mingine!. Hi kiukweli ukishachaguliwa kuwa kiongozi unajipima mwenyewe au unapimwa na waliokuchagua?. Kama sisi tuliomchagua mwanzo na baada ya miaka mitano tukampima tukamuona anaweza, tukamuongezea, wewe ni nani wa kumuuliza ajipime na kuwapisha wengine?.

Hivi katiba yetu ndivyo inavyosema tukishamchagua rais, ajipime, akijiona hawezi apishe?.
 
Mkuu Omukajunguti, lets be fair, hivi ulitaka rais wako afanya nini zaidi hiki alichofanya?, njia si ameshatonyesha ya kuelekea kwenye maisha bora?, au unataka akubebe mpaska akufikishe hapo?. Anayeshindwa kufikia maisha ni aliyekuonyesha njia au aliyeshindwa kufika?.

Si tumemchagua wenyewe?, na baada ya miaka mitano, tukaridhika na utendaji wake, tukamuongezea mingine!. Hi kiukweli ukishachaguliwa kuwa kiongozi unajipima mwenyewe au unapimwa na waliokuchagua?. Kama sisi tuliomchagua mwanzo na baada ya miaka mitano tukampima tukamuona anaweza, tukamuongezea, wewe ni nani wa kumuuliza ajipime na kuwapisha wengine?.

Hivi katiba yetu ndivyo inavyosema tukishamchagua rais, ajipime, akijiona hawezi apishe?.


Mkuu unachosema ni kweli, lakini tatizo ni kwamba ukiangalia mazingira ya kisiasa ya Tanzania, mtu akichaguliwa na CCM kugombea urais ni kama automatic anakuwa Rais, hata kama wengine hawakumtaka. Wananchi tunategemea rais aweke mazingira na njia zinazoweza kutumiwa kwa haki na watu kuiendeleza. So far JK na serikali yake wameshindwa katika hilo. Walichofanya ni kwamba wanatumia njia wanazoweza kuzitumia kuwawekea fursa watanzania kwa manufaa yao binafsi. Huko ni kuwa na uwezo wa kujineemesha na kutokuwa na uwezo wa kuendeleza nchi na wananchi.

Kuna maswala mengi ambayo tunaweza kumjudge Kikwete na serikali yake. Tuangalie macheche....kesi ya akina Zombe, mpaka sasa hakuna kinachoendelea kesi imetupwa, hadi siku ndugu watakapoamua kuchukua sheria mkononi. Kumbuka keshi ya Dito iliendeshwa kihuni huni tu...kuna mifano mingi.

Angalia issue ya EPA, Kagoda, Kiwira, Radar, ndege ya Rais, Richmond etc etc etc...yeye kama rais anatakiwa kushughulikia maswala haya, hata kama mengine hayakutokea wakati wa utawala wake. So far inaonekana kuwa yote hayo hajashughulikia na hana nia au hana uwezo wa kuyashughulikia.

CCM kama chama kwa sasa kiko in shambles, kila mtu ni msemaji ni muongeaji, cabinet same same waziri huyu anasema hili mwingine anasema lile.......manaibu waziri sasa wanaonekana kuwa ni play boys, hakuna nidhamu na maadili.

Uchumi nadhani kila mtu anaweza kuwa shahidi hakuna haja ya kuelezea.

Tunatakiwa kukumbuka kuwa unapoamua kudeligate power ujue kuwa, yule unayempaka kazi akifanya vizuri credit ni kwako, lakini akifanya ovyo responsibility bado iko kwako. Kusema kuwa washauri wa JK ni wabaya it is absolutely **** since those washauri are his appointees. It is only an idiot who will argue in that line, because the government bureaucracy does not work that way.

Ni kweli naibu waziri akichukua changudoa au akifumaniwa, au Waziri Mkuu akiongopa, au baraza zima la mawaziri kutokuwa na nidhamu, kweli si kosa la rais, lakini anawajibika moja kwa moja kutokana na kuteua madudu, na kuchangia kwa kiasi kikubwa kuteua watu ovyo, na bila kuweka rules za kulinda integrity ya serikali, the responsibility goes all the way up to the top. Tumesikia mara nyingi Obama akisema "as commander in chief the responsibility is mine", Bush alipoingia mkenge wa kusema Iraq inasilaha za sumu na kufanywa asome maneno ya uongo, alisema wajibu ni wake. McCain alaiposhindwa urais kutokana na chaguo baya la VP, hakumlaumu Steve kwa kumchagulia S Palin, alisema kuwa ni yeye ameshindwa. Kuna mifano mingi tu. Kwa hiyo hoja ya kuwalaumu washauri, wasaidizi, na aliowateua ni ufinyu wa akili.

We may have voted for JK, we may have voted for CCM, but that does not change the fact that there is a big mess that needs cleaning. Let's call mess a mess, not a miss.
 
"Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!."

MTOA mada asante kwa ku post hii. Lakini npenda kusema kuwa katika mfumo wa uongozi uliopo Tz ni vigumu rais aliyeko madarakani kutenda vile anavyotaka kwa sababu rais aliyepita nyuma yake anakuwa bado na mamlaka nyingi tu: mojawapo ni kuwa na ukaribu zaidi na viongozi wa vyombo vya dola, mbili ni kuwa na timu kubwa ya watendaji watekelezaji wa majukumu kwenye nyidhifa nyeti (wakurugenzi). hawa ndo watekelezaji wa majukumu ya kila siku ya serikali. kwa mtindo huo rais aliyeko madarakani anakuwa hana ubavu wa kuporomosha maswahiba wa rais aliyeondoka labda awe kichaa fulani. JKN aliweza kwa sababu waliondoka hawakupendwa (wakoloni)
Suala la EPA- siyo rais hivyo, kwani waliohusika walikuwa ni mawahiba wa rais Mkapa ndo kipindi ambacho ufisadi huo ulipotokea na yeye kuhusishwa na KIWIRA- wanaharakati walipohoji JK akasema " mwache mzee wetu apumzike kwa amani" kwani nini kauli hii? wenye akili alijua sababu yake-Kulindana. JK angechukua maamuzi makali -hata BM angejikuta anahusika. HAwakutaka haya yabainike.
kikatiba rais ndo mtendaji wa mwisho lkn ikitumika vibaya nchi itayumba tu, lkn pia isipotumika nchi itachechemea kama hivi sasa.
USHAURI: Kama nchi ni lazima tuwe na msimamo wa kitaifa-hakuna kulea ubovu wa mkubwa aliyepita-ikibainika achukuliwe hatua hata za kimahakama. Hii itawafanya watendaji kuwa waoga hivyo kuwa wadilifu. wataogopa kutenda ufisadi kwa kuw ahakuna kigogo cha kuegemea pindi mambo yakifumuka. HUU NDO UKWELI.
Tazama influence ya JKN wakati wa utawala wa AHM. Uhuru wa rais ulikuwa wapi? Mikonini mwa JKN. Hii ndo Tz. Katiba mpya utumike kuweka wazi kuwa ubaya/uovu wowote ukitendwa mtendaji bila kujali nafasi yake atapambana na mkono wa sheria. Nchi itanyooka. Sababu ya viongozi wakubwa kumiliki maeneo wasiyomudu kuyatunza kwa kisingizio cha kuandalia maisha watoto na wajuu wake, kitaisha, uadilifu utarudi bila kushikiwa fimbo
 
Kwa nini ahurumie majizi asihurumie wananchi maskini walioibiwa hizo fedha na walistahili kupatiwa huduma kwani hawawezi hata kupata mlo wa siku na huduma nyingine za kijamii
 
tatizo kubwa kwa nchi yetu ni 1!! tunaongozwa na sera za vyama lakini hatuna sera za nchi ambazo zinauwajibikaji na utekelezaji!! pia kama ua vission na mission usipotekeleza anayekuwajibisha ni nani!1 taifa letu bado lina changamoto nyingi nduguzanguni!1 lazma tuwe na sera ya nchi ili kila kiongozi anayeingia madarakani aifuate na akishindwa kufulfil anatakiwa ajiuzulu pia attupe dedline ya kuflfill ahadi zake!!
 
Kwa kifupi JK aliingia madarakani kwa nguvu ya watu wengine akina EL, ROSTAM na wenzao. Hao ndio waliokuwa na Maono yao wenyewe na wala si ya JK. Baada ya kulazimishwa kuachana nao ndio ukawa mwisho wa 'maono na mtazamo' wa JK!
 
Kwani mnafikiri JK hafahamu kinachoendelea!!!!!?? Anafahamu sana lakini atafanya nini endapo mtandao wake ndo unaomtesa?? Wakati wa uchaguzi aliwaona watu wazuri (kwa vile walimsaidia kuingia ikulu) na hivyo kulipa fadhila, sasa wanaboronga na hana namna ya kufanya.

Ushauri wangu kwa waTZ ni kufikiria namna gani tutajikwamua kuanzia 2015 na si sasa kwani TUMEKWISHACHELEWA (It is too late). Yote yanayoendelea anayafaham ila hata yeye hana namna, ni sawa na kuona nyumba yako inaungua moto halafu unataka kuuzima kwa maji ya ndoo!!!
 
inawezekana huyu jamaa naye ana mambo yake mabaya hivyo hawezi kuwashtaki wanachama wake ktk uhalifu maana watamtaja.
 
mimi ninaamini hakuna mtu asiye na makosa! lakini yakizidi kipimo hugeuka na kuwa zigo zito. kama ulifumaniwa unakwiba mke ya m2 na wewe mwenyewe akamfumania yule aliyekufumania jana anakwiba ya kwako. Hauwezi kumwajibisha maana utasutwa. Hii ndo mambo yanayomsumbua mkulu
 
"Asiyekubali kushindwa si mshindani"
Inaonekana wanaume tunaendekeza sana kujuana na undugu usiokuwa na Tija.
Wanaume sasa tumeshidwa kuendesha hii nchi, inabidi sasa tujaribu kuikabidhi kwa mwanamke kama walivyofanya Malawi ili tuone kama mabadiliko yatakuwepo.

Tunao wanawake ambao ni wasomi na wasiokuwa na mzaa kazini ambao naamini wanaweza kuleta mabadiliko ya haraka katika mfumo mzima wa uongozi hasa wa kiutendaji.
 
Back
Top Bottom