Mapungufu katika interview ya Koffi Olomide na Clouds Media leo ni haya yafuatayo...

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,033
  1. Hakukuwa Na Mpangilio Mzuri Hasa Wa Maswali KUNTU Na Ya Kina Ambayo Yangewajenga Watu.
  2. Mtangazaji Muongozaji Hudson Kamoga Kuzidisha KIMBELEMBELE Ili Aonekane Yeye Mjuaji Pekee.
  3. Mtangazaji Mgeni Dakota Kutopewa Wasaa Murua Na Kamoga Kuuliza Maswali Kwa Koffi.
  4. Interview Ingefanyika Kwa Kilingala au Kifaransa Kisha Kungekuwa Na Mkalimani Ambaye Nilitegemea Angekuwa Ni Christian Bella Ambaye Alikuwepo Back Stage Hapo Studioni Ingekuwa Nzuri Zaidi.
  5. Interviewers Wenyewe Kutaka UFAHARI Wa Kujifanya Wanajua Kuzungumza Kiingereza Ambako Wote Wawili WALICHAPIA KUNAKOTUKUKA Kwa Hicho Kiingereza Kwa Mfano Hudson Kamoga Aliuliza Nanukuu " What Education Are You " Na Mwishoni Dakota Nae AKAJICHANGANYA Kwa Kuuliza Nanukuu " Between Fere Gola And Fally Ipupa Which One Is The Best For You ". Watakaonibishia Hili Waende Wakaulizie Footage Ya Hii Interview Ili Wajiridhishe.
  6. Interviewers Wote WALIZIDIWA Na Kitu Kitaalamu Na Hasa Kisaikolojia Kinaitwa Inferiority - Superiority Complex Ambapo Wote Kwa Pamoja ( Nikimaanisha Kamoga Na Dakota ) Walikosa SELF ESTEEM ( Kujiamini ) Na Muda Mwingi Walijionyesha Kama Vile Wanaogopa Na Kujishtukia.
  7. Hakukuwa Na PREPARATION Ya Kutosha Kabla Ya Kuamua Kufanya Interview Na Baba DIDISTONE ( Koffi Olomide ) Na Kuna Wakati Koffi Olomide Alikuwa Anaonekana KUBOREKA Fulani Hivi Hadi Akawa Anachati Lakini Shukrani Kwa Tu Kwa HESHIMA Kubwa Aliyonayo Kwa Brother Joseph Kusaga Na Mwanamuziki NGULI Kwa Sasa Tanzania Christian Bella Ambaye Ndiyo Alikuwa Anamchangamsha MOPAO Vinginevyo Kwa Ninavyomjua Koffi Alivyo Na Nyodo ( Maringo ) Na Dharau ANGESHAONDOKA Pale Studioni.

Otherwise Tunawashukuruni Tu CLOUDS MEDIA GROUP Kwa Kumleta KOFFI OLOMIDE Ila Ushauri Wangu Tu Mzuri Na Mkubwa Kwenu Ni Kwamba Siku Nyingine Mkiwa Mnataka Kupiga PESA NDEFU Na Kupata Watu KIBAO Mleteni Mwanamuziki Jean Bedele Tshituka Mpiana ( JB Mpiana ) Na Bendi Yake Nzima Ya WENGE MUSICA BCBG Nawahakikishieni Kuwa HAMTAJUTIA Kumleta ILA Kwa Koffi Olomide Leo MTAPIGA Tu Hela Kiasi.

Fanyeni Mpango MUMLETE JB MPIANA Muone Kazi Na Nitakuja Hata Na POPOMA Wangu Mkuu Humu nifah Tuje TUYAKATE Na TUSEREBUKE Na Tambueni Kuwa Hapa Nchini Tanzania Kati Ya Watanzania Milioni 48 Hivi Ni Kwamba Watanzania Milioni 40 Nzima Ni WAPENZI Na WASHABIKI Wa JB MPIANA Na Kundi Lake Zuri Na La KUTUKUKA La WENGE MUSICA BCBG Na Hao Milioni 8 Waliobaki Milioni 2 Mbili Mbili Ni Wa Koffi, Werrason, Fally Na Fere.
 
Hiv kuna siri gan kat ya haya maneno; KUTUKUKA, POPOMA. au swaga tu??
 
Pale Clouds nafikiri hata akina Kusaga wameshaling'amua hili kwamba watangazaji wao wengi ni VILAZA na more worse ni too much know..!!
 
Kwani waumini wa nabii Fulorah mnaruhusiwa kushabikia muziki ya kidunia?
 
Koffii Charles Antonio Olomide! Ekotikee acha moto uwake baba! unataka kutuambia watanzania wote mil 48 Hata watoto ni mashabiki wa Sebene za Kofi na Fall?
 
ili kuthibitisha maneno yako basi tupia kibao kinachotamba cha jb Mpiana mukulu papa.
 
Wivu usio na tija na kutaka kuchonganisha watu bila sababu za msingi! Kwa nini interview iwe kilingala wakati kofie yupo hapa kwetu! Umemsikia mwenyewe kama anashangaa kwa nini tunahusudu kingereza kuliko kiswahili amabacho yeye anakichukulia kama lugha ya afrika nzima! Na kama interview ingekuwa katika kifaransa au Lingala ina maana vijana wetu wangekuwa watazamaji tu kwani muongozaji, muhojiwa na mkalimani wote wangekuwa wakongomani! Kwa nini hupendi vijana wetu wakwae jukwaa kubwa kwa kufanya mahojiano na mwanamuziki mkubwa wa kiwango cha dunia! Wacha hizo! Jifunze " to give credit where it is due"

Vijana wamejitahidi sana under the circumstances, quality ya kiingereza cha Kamoga kimekidhi mahitaji ya shughuli na ndio maana Kofie alikuwa anamuelewa spot on bila pardon pardon nyingi.
 
umesikikia.. Kwahiyo utakuwepo leo Escape one au wivu umekuzidi

Kuna Mtu Wangu Wa Karibu Kaniletea Tena VIP Ticket Ili Nijumuike Nae Leo Lakini Nimemtoa " Baru " Nimemfukuza Na Hata Kama Kusingekuwa Na Kiingilio Nisingeenda. Koffi Olomide Hajui Kuimba Na Kibaya Zaidi Si Mzuri Ktk " Live " Shows Kama PAPA CHERI JB MPIANA Na Bendi Yake Nzima Ya WENGE MUSICA BCBG Na Kama Hamuamini Nyie au Wale Mtakaokwenda Leo Hapo ESCAPE One Kesho Mtaniletea MREJESHO Na Kukubali Hiki Nilichowaambieni.

Angekuja JB Mpiana Hata Kama Ningekuwa MAHUTUTI Kitandani Ningemwambia Israeli Asiniue Kwanza Hadi Nikacheze Mziki ( Sebene Na Rhumba ) Na Wenge Musica BCBG Chini Yake BIN ADAM JB MPIANA Huku Show Nzima IKINOGESHWA Na RAPA Mahiri, Fundi, Mtundumtundu Na Mwenye Udambwidambwi Mwingi Aitwae Pitshou Lisimo Gentamycine. Ukiwa Na Bendi Halafu Ukampata Rapa Kama Antibiotique Gentamycine ( Pitshou Lisimo ) Kila kukicha Shows Zako ZITAFURIKA Kwa Kujaza Watu.

Mimi Ni Disciple Mtiifu Wa JB MPIANA Na Wenge Musica BCBG Nzima Na Huyo Koffi Wenu Shughulikeni Nae Nyie MAPOPOMA Wenzie Na Kuna Kibao Kipya JB MPINA Anaenda Kukipakua Tarehe 25 Wakati Wa Sikukuu Ya Noel ( Christhmas ) Na Nina Uhakika KITAMFUNIKA Huyu Koffi Wenu Na Mtaisahau Hii " SELFIE " Yenu. Msikae Mbali Na Mtamkubali Tu JB Mpiana Na Wenge Musica BCBG Yake.
 
ili kuthibitisha maneno yako basi tupia kibao kinachotamba cha jb Mpiana mukulu papa.

Mtafute Mkongo ( Mzairwaa.... ) Yoyote Aliye Karibu Nawe Kisha Muulize Ni Mtindo Gani Ambao Sasa DRC Nzima, Bandal Nchini Angola, Rwanda Na Burundi, Cameroon, Ivory Coast, Congo Brazaville, Paris, Brussels, Canada, Marekani, South Africa Na Zambia Unaotamba Na Umekuwa GUMZO Kama Siyo Wa " MBUNDA " Na " ROTA ROTA " Wa Kwake JB MPIANA Na Kundi Lake Zima La Wenge Musica BCBG. Ukitaka Kuijua Kazi Ya Huyo Rapa MAHIRI Na Asiye Na Mfano Sasa DRC Nzima Pitshou Lisimo Gentamycine Antibiotique Tafuta DVD Yoyote Ya " Live " Ya Wenge BCBG Ya JB Mpiana Uiangalie Na Utarudi Kunipa Mrejesho. Ukiona Nampenda Mtu au Kitu au Jambo Fulani Jua Ya Kwamba Ni Kizuri Na KIMETUKUKA Na Kwamba Hata Mwenyezi Mungu Nae AMEKIPENDA.
 
Back
Top Bottom