Tujikumbushe baadhi ya Nyimbo na Album Za Muziki wa Kikongo za wakati ule

Public Enemy

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
2,905
3,253
Katika Makuzi, Ama ujana na wengine wenu Ni uzee kabisa mmekua ama timekua tukisikiliza nyimbo za muziki hasa kutoka Nchi ya Kidemokrasia ya Congo. Muziki huu umekua ni sehemu ya Burudani na mafundisho.

Nyimbo Nyingi katika hizo aidha ziliimbwa katika lugha ya Kilingala ama Kifaransa na kwa uchache sana Lugha ya kiswahili.

Nitaanza na Hawa ambao sababu ya kuwaandika kubwa ni familia kumiliki Mikanda yao ya VHS hivyo nimekua nikiwasikiliza na kuwaona kwenye Runinga.

Koffi Olomide -Quartier Latin (Ultimatum) na Loi
Hapa wakitoka Vijana waliokuja Itikisa Afrika baadae kama Fally Ipupa

https://m.youtube.com/watch?v=Qfzrqr4zlxk

Wenge Musica BC BG 4*4- Pentagone(1996)
Humu ndimo walitoka Wanamuziki wakubwa baadae kama Noel Ngiama Makanda almaarufu kama Werrason, Didier Masela, Adolphe Dominguez, baadae Akajiunga J.B Mpiana na Ferre Gola. Baada ya Kutengana Baadae ndipo kukawa na Wenge BCBG ya J.B Mpiana na Wenge Musica Maison Mere ya Werrason, Adolphe Dominguez na Didier Masela.

https://m.youtube.com/watch?v=ZhoUtgpBKBY

Kuna Hili Dude hapa Filandu Ukiwa ni Utunzi wa Blaise Bulla

https://m.youtube.com/watch?v=-4YDsFX3VKQ

Coco Madimba ukiwa ni Utunzi wa Werrason Ngiama Makanda
https://m.youtube.com/watch?v=vxu0Xiki3mY

Dizoizo utunzi wake Allain Makaba

https://m.youtube.com/watch?v=cQBIj26fp2w

Madilu System jina la album Pouvoir ikiwa na Vibao kama Sa Majeste





Wenge El Paris jina la album ni Couvre-Feu, hii Ilikua kama Part B ya Wenge Musica BC BG ambapo Ilikua huko Jijini Paris, Ikiundwa na kuongozwa na Aime Buanga ambaye alienda Ulaya kwa sababu za Kimasomo na wakafanikiwa kutoa album.

https://m.youtube.com/watch?v=0Ziyh3UoYow

Nyboma album nimesahau Jina na isivyo bahati sikumbuki hata Wimbo wake mmoja niliokua nausikiliza enzi hizo kwa sababu nilikua simuelewi.

Mwamba Huyu hapa King Kester Emeneya&Victoria Eleison (DREAM TEAM DREAM BAND) -Mboka Mboka humu ndani vibao ninavyovikubali sana Ni Mifume na Moto na Tembe. Mwamba Ana sauti Moja ya Kipekee sana.



https://m.youtube.com/watch?v=x9b8x2b9RL0

King Kester Emeneya ni Moja ya wanamuziki waliofanya muziki wa Congo ukatoboa nje hasa Paris na Kwingineko

Awilo Longomba- Coupe' Bibamba ambapo kulikua na Vibao vikali kama Coupe Bibamba na Gate le Coin


Awilo Alifanikiwa kutumbuiza katika Tuzo za Kora Music Awards na Kibao chake cha Coupe Bibamba ilikua show moja kali sana.

Empire Bakuba ikiwa na wakali kama Papy Tex , Pepe Kalle (Kabasele Yampanya) na Bileku Mpasi wakiwa na Madamsa wao mbilikimo maarufu kama Emoro album FULL OPTION. Nyimbo zao Maarufu pasipo kuangalia album ni Kama Roger Miller, Yanga Afrika, Full Option, Swabila (pesa wax) Mpenzi Bupe (utunzi wa Papy Tex) pamoja na Hidaya;nyimbo Hizi mbili za Mwisho waliimbiwa Mabinti wa Kitanzania.

https://m.youtube.com/watch?v=NII0zSThFGE

https://m.youtube.com/watch?v=yffmok3VBCU




Extra Musica Etat Major (1998) na Shalai (1999)
https://m.youtube.com/watch?v=SAIbCxVqiDM

Wenge Musica Maison Mere Bendi ikiongozwa na Werrason, Didier Masela na Adolphe Dominguez ambao wawili wa mwisho baadae watatoka na kumuacha Werrason pekee kama kiongozi. - Solola Bien jina la Album ( meaning Speak Properly, Hii ilikua ni diss kwa J.B Mpiana na Wenge BCBG yake) humu ndani Kulikua na Vibao hit kama Solola Bien Yenyewe, Kalayi Boeing na Vita Imana ya Fere Golla. Golla alikuja Kujiunga na bendi hii akitokea BCBG kwa J.B Mpiana.


Album Hii ilikua na mafanikio makubwa na kuibua Vipaji vikubwa kama Rapa wa Bendi Bill Clinton Kalonji.

Wimbo Kalayi Boeing ulifanyiwa remix katika Album hii (orijino ya Huu wimbo Iliimbwa kabla Hawajatengana na J.B Mpiana) na ulikua ni Utunzi Mahiri wa Werrason






Werrason alifanikiwa kuchujua tuzo 2 za Tuzo kubwa za Muziki Barani Afrika KORA AFRIKA NUSIC AWARDS kwa album yake ya Operation Dragon ama Kibuisa Mpimpa



Wenge BCBG ya Jibe Mpiana- Titanic jina la Album akimaniisha Wenge Yao imesambaratika na Kuzama kama Meli ya Titanic baada ya Werrason na wenzake kuunda Kundi jipya la muziki. Wimbo wa Titanic ukibeba jina la Album




Kabla ya Album hii, J.B alitoa album Feux De l'amour ikiwa na Hit song kama Ndombolo, Feux De l'amour, na masuwa



Mwaka 2000 akaja na Album Toujours Humble ikiwa na Hit Songs kama TH, 48 Heures Gecoco,



https://m.youtube.com/watch?v=09JP...URL]https://m.youtube.com/watch?v=OffG5lWdCK4

Tshala Muana Dezo Dezo

https://m.youtube.com/watch?v=0wfWPRXHodY



Gatho Beevens Azalaki Awa



Mbilia Bell Nadina

https://m.youtube.com/watch?v=2GkKKGIKIfg

Zaiko Langa Langa na Proverbes 22:1

https://m.youtube.com/watch?v=k7EIgHneiv8

Papa Wemba akiwa na Viba La Musica



Yolele

https://m.youtube.com/watch?v=QemzwQ839tE
General Defao-General Defao mzee wa Kibinda Nkoi

https://m.youtube.com/watch?v=_7XcNAOfjZY

https://m.youtube.com/watch?v=8QdjDV1dsaM

Tuongee na Nyingine hata Zile za Nje ya Congo. Karibuni.
 
Hii Thread imebuma . Nitakuwa nakuja kuiangalia Kila siku na ku comment neno mwenyewe
 
Back
Top Bottom