Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Kibaya zaidi hii clip uionayo hapa juu Azam wameiachia kwenye social medias baada ya kusikia malalamiko kwani kwenye live TV interview ilipofikia kocha kutoa lawama na kutishia kutoshiriki tena basi kwa haraka walikatiza interview ya kocha na kuweka tangazo ili tuhuma alizokuwa akitoa zisisikike.
Huku ni kuonyesha udhaifu wa soka na pia vyombo vyetu vya habari hasa kile cha tibisii, asam na wengine wanaoripoti.Imagine huko Rwanda mashabiki wanaoamini timu yao kupokwa ushindi bado tena wanaona kocha wako akizimiwa live interview watajisikiaje?
Yani ung'olewe meno halafu upewe bisi za kutafuna?
Tanzania inawezekana tumekuza matangazo tu ya mipira na viwanja ila soka bado sana kutokana na kubebana. Hayo mafanikio tunayosema Simba na Yanga wamepata kimataifa yamechangiwa na wachezaji wa kulipwa wa kigeni na sio wazawa wanaobebwa na ndiyo maana upande wa Taifa Stars isiyo na professionals wa kigeni bado tunajikongoja.
Ingependeza kiungwana referee wa mechi ya jana apewe adhabu stahili na pia TFF kuiomba radhi club ya APR ya Rwanda na Rais Kagame ambaye pia tunategemea kumfungia yule refa kutokanyaga Rwanda.
Azam TV pia ambao licha ya kutangaza mechi hiyo ni wadhamini pia wa APR wanapaswa kuomba radhi kwa kukatiza interview live katika Televisheni ili malalamiko ya Kocha yasisikike.Azam wamekuwa maduwanzi, hata kurudia lile goli kwenye kila angle wamekataa na ukweli ni kwamba sasa hivi ili kombe ni kama bonanza la CCM ambalo mshndi ni timu ya Mbunge aliyeandaa Bonanza.
Tujitathmini na Tukuze Soka kiuhalisia sio kwa upendeleo wa home team jambo ambalo limeonekana kukua mizizi hata kwenye ligi ya bara hasa kwa timu kubwa na hata ziitwazo ndogo zikiwa viwanja vya nyumbani na kwa matokeo mengi tuliyoshuhudia katika mchezo wa Boxing kutoa ushindi fake kwa mabondia wa nyumbani.
Kisiasa tupore ushindi, kimichezo nako tupore ushindi tunaenda wapi? Kila kitu sisi ni rafu?
Tubadilike.