Mapenzi na ng'ombe

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Bw. Masanja alikuwa na kawaida ya kuamka asubuhi mapema kukamua maziwa ng'ombe wake kabla ya kuelekea kibaruani. Ilitokea siku fulani alidamka asubuhi sana na bahati mbaya siku hiyo ilikuwa ni takriban mwezi mzima tangu alipokula penzi kwa mara ya mwisho na mke wake japo mke wake alikuwa haishi kumpapasapapasa usiku bila mafanikio. Kama kawaida yake, alipoamka alikwenda moja kwa moja zizini na kumfunga ng'ombe tayari kwa kuanza kukamua maziwa. Bahati mbaya siku hiyo ng'ombe alicharuka na kuanza kumfanyia fujo Mzee Masanja kwa kutumia mkia wake. Kuona hivyo, wazo likamjia Mzee Masanja. Alichukua kamba nyingine akashika mkia na kuubinua kwa juu kisha akaubana mgongoni mwa ng'ombe kwa kufunga vizuri kwa kutumia kamba. Baada ya kufanikisha zoezi hilo, aliamua achimbe dawa kwanza kabla ya kuendelea na zoezi la kukamua manake alikuwa amebanwa sana. Jamaa akaona bora akojoe kwa pembeni tu akiwa palepale amesimama na ng'ombe. Ooooohhhh, ghafla mke wake alitokea ghafla na bahati mbaya alimkuta Masanja akiikung'uta bunduki yake kuelekea usawa unapoanzia mkia. Lahaulaaah, mke wa watu alianguka chini palepale na kuzimia! Alipozinduka alimgeukia Masanja na kumwambia yaani mume wangu imefika mahali unafanya mapenzi na ng'ombe!!! Ndiyo maana sasa umeishiwa hata hamu ya kulala na mimi!! Mzee Masanja wa watu alijaribu kujitetea lakini wapi hatimaye ndoa ilivunjika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom