Maoni ya wananchi: Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar es Salaam

Hongera Arusha Mambo, leo redio imetulia, poleni kwa usumbufu wa internet jana na juzi,
big Up
 
Hongera Arusha Mambo, leo redio imetulia, poleni kwa usumbufu wa internet jana na juzi,
big Up
Duh kuna siku nime tune Arusha Mambo nikawa nasikia jamaa wanaongea kwenye simu. Wanaagana na kuambiana kesho wataonana. Nusura nisikie mambo yao mengine!
 
Tumechoshwa na poroja za CCM kwani uanze usianze sie tushazoea foleni yetu period
 
Miongoni mwa nyenzo rahisi na za uhakika katika sekta ya usafirisjhaji ni reli. Kwa njia hii ni rahisi zaidi kusafirisha mizigo mikubwa na mzito kwa haraka na ufanisi zaidi, hali ambayo huchangia kwa kasi zaidi kukuza uchumi katika taifa lolote lile duniani.

Nchi zote zilizopiga hatua ya maana katika maendeleo, zimejikita sana katika kusimamia na kuelekeza nguvu zote katika usafiri wa reli kwa kuwa ndiyo ukombozi wa kweli katika usafirishaji.

Tanzania tumejaliwa kuwa na reli kuu mbili, ile ya Tanzania na Zambia (Tazara) na Reli ya Kati. Kwa sasa itakuwa ni kujidanganya kusema kuwa zinatoa huduma kwa kiwango kilichotarajiwa ndiyo maana shughuli kuu ya usafirishaji wa mizigo na abiria imehamia barabarani.

Ukiitazama Reli ya Kati inatia huruma; mabehewa yamechakaa, vichwa vya treni (injini) ndiyo usiombe kabisa, lakini kikubwa zaidi hata njia yenyewe (reli) nayo iko hoi.

Hali imesababisha huduma zitolewazo na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuwa duni sana kiasi cha kushindwa kabisa kuvutia wateja wa maana.

Siku hizi nchi hii imekuwa ni soko kubwa la malori ya mizigo, siyo kwa sababu mizigo imeongezeka sana, la hasha, ila kwa sababu barabara imebakia kuwa njia pekee ya kusafisha mizigo na abiria.

Tangu juhudi za kubinafsisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuwa TRL zishindwe kuleta tija yapata miaka mitano hivi iliyopita, taifa hili limejaa malumbano ya nani kafanya hiki au kile kiasi cha kufikisha shirika hilo hapo lilipo leo.

Bila kumung’unya maneno, waliofikisha TRL hapo lilipo leo ni sisi Watanzania; ni sisi ambao tulipata fursa ya kuajiriwa ndani ya shirika hili, badala ya kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii, tulishiriki kwa njia moja au nyingine katika kulihujumu. Kwa maana hiyo Watanzania wanapaswa kujilaumu na kujilaani wenyewe kwa kuua TRL.

Hata hivyo, pamoja na majuto haya, tunafarijika sasa kusikia kwamba zipo juhudi za kweli kabisa za kubadili hali ya mambo. Akiwasilisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Uchukuzi bungeni jana, Waziri wake, Dk. Harrison Mwakyembe, aliweka bayana mikakati ya kufufua Kampuni hiyo.

Pamoja na mambo mengine alisema katika mwaka wa fedha wa 2012/13 serikali imetenga Sh. bilioni 104 kwa ajili ya kufufua kampuni hiyo.

Aliainisha kazi zitakazofanyika kuwa ni pamoja na kujenga upya njia ya reli, kufufua injini na mabehewa ya mizigo na abiria, kulipa madeni makubwa iliyokuwa inadaiwa kampuni hiyo ili kujijenga upya na kwa kasi na morali mpya.

Katika hotuba hiyo waziri huyo alisema watakarabati injini nane, kutoa malipo ya awali kwa injini mpya 13, mabehewa mapya 22, kukarabati ya mzigo 125 na kununua mapya 274, sambamba na kufufua reli katika jiji la Dar es Salaam.

Waziri huyo alisema kwa Dar es Salaam Sh. bilioni 4.75 zimekwisha kupatikana kwa ajili ya kufufua njia ya reli, injini tatu na mabehewa 14 ili kusaidia usafiri kwa jiji hilo na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

Kwa macho na tathmini ya aina yoyote malengo na mipango hii ni vitu vikubwa, ni kujitoa kwa nguvu zaidi kurejesha huduma ya usafiri wa treni katika heshima inayostahili kwa ajili ya kusaidia uchumi wan chi hii. Tunapongeza hatua hizi na kumtia moyo waziri wake na wizara nzima kwa ujumla kusimamia kazi hii kwa ufanisi mkubwa.

Tunasema bila kujibidiisha kujenga miundombinu yetu, hakika hakuna Mgeni kutoka kokote atakayekuja kusaidia kazi hii, kwa maana hii tunaunga mkono juhudi hizi za kuthubutu, tunawatia shime wote wenye wajibu wa moja kwa moja katika kufanikisha kazi hii wafanye biadii ili kufikia malengo tarajiwa.

Hata hivyo tungependa kutoa angalizo kwamba katika utekelezaji wa miradi mikubwa kama hii, walaghai wenye mioyo ya kifisadi hawakosekani, ni kwa maana hiyo tunawataka wote wenye dhima ya usimamizi kuwa macho kuhakikisha kwamba malengo haya yanafanikiwa na hivyo kuleta Mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini. Kila la heri Wizara ya Uchukuzi.




CHANZO: NIPASHE

 
Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe amesema huduma za treni Dar es salaam kwa kuanzia zitakua kutoka stesheni ya reli Dar es salaam hadi Ubungo maziwa ikiwa ni kilomita 12 pamoja na Mwakanga hadi Kurasini kupitia stesheni ya Dar es salaam kilomita 34.5.
Amesema “kazi ya ukarabati wa njia na injini tatu za treni na mabehewa 14 ya abiria imeanza na inatarajiwa kukamilika oktoba 2012 ambapo huduma hii itaanza kwa kuwa na treni mbili ambazo zitatoa huduma asubuhi na jioni kuanzia jumatatu mpaka jumamosi”

Dr Mwakyembe amesema Treni hizo zitasimama kwenye vituo sita ambavyo ni stesheni ya Dar es salaam, Kamata, Buguruni kwa Mnyamani, Tabata Matumbi, Mabibo na Ubungo Maziwa na kila treni itakua na mabehewa sita yenye uwezo wa kubeba abiria waliokaa na waliosimama elfu moja kila safari na inakisiwa treni hizo zitaweza kusafirisha watu elfu kumi na sita kwa siku.

Baada ya kusema hayo, Dr Mwakyembe amewasihi wafanyabiashara kuwekeza kwenye mradi wa maegesho ya magari kwenye eneo la eka nne Ubungo lililotengwa kwa ajili ya watu wanaotoka Kibaha, Kimara, Kiluvya, Mbezi Luis na kwengine kwa ajili ya kupaki magari yao Ubungo kisha kupanda treni kwenda stesheni ya Dar es salaam.


Kwa upande wa reli ya Tazara ukarabati wa injini tatu na treni za mabehewa 14 unaendelea na unatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu ambapo huduma hiyo ya treni itakua na njia mbili, Mwakanga kwenda Yombo mpaka stesheni ya Tazara ikichukua dakika 30 alafu njia ya pili Mwakanga kwenda Yombo mpaka Kurasini ikichukua dakika 40, itakua na vituo 14 ambavyo ni stesheni ya Tazara, kwa fundi umeme, Yombo, Kwa Limboa, Lumo, Kigilagila, Barabara ya Kitunda Kipunguni B, Moshi Bar, Majohe, Shule ya sekondari Magnus, Mwakanga, Chimwaga, Maputo, Mtoni relini, Kwa Aziz Ally relini hadi Kurasini.

My Take:
- Tumeanza vizuri kuhusu hili, naamini reli ni njia mbadala, nafuu, rahisi na ya haraka katika usafirishaji. Ila kuna maswali yakujiuliza kuhusu usafiri huu, usalama wake ukoje? (tumeskia ajali za treni zinavyoua maelfu ya watu kwenye nchi za wenzetu).
- Je kwa watanzania waliojizoeza kwenda na magari binafsi mpaka mjini wapo tayari kubadilika na kuacha magari yao majumbani au vituoni na kisha kuingia kwenye treni (Mind set change)?.
- Je kuna mpango mbadala (plan B) kwa vyombo ya usafiri (public transport) tunavyotumia sasa hivi? Kama ikitokea abiria wakihamia kwenye treni ni wazi kwamba daladala zitakosa abiria, kama hakuna mbadala kwa daladala basi tutegemee hujuma za mara kwa mara kwenye reli na treni zetu.
 
Treni kwa Jiji la Dar es Salaam ni hasara Dar es Salaam hakuna watu wa hivyo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hawazidi hata milioni 5 kuna miji ina watu mpaka milioni 7 mpaka 10 lakini hakuna Treni, tatizo la Dar es Salaam ni barabara kubwa zimeingiliana barabara ya Kawawa, Barabara ya Morogoro, Barabara ya Mandela, Barabara ya Nyerere, kunatakiwa kujengwa Fly-over crossing kwenye mataa..

Na huu mradi wa mabasi nao wakiumaliza nadhani tatizo la foleni Jiji la Dar es Salaam itakuwa historia, Treni ni mradi mkubwa kwa nchi yetu bado wakazi sio wengi, Dar es Salaam ikifika saa 4 usiku magari na watu hakuna barabarani.

Kama kuna Fly-over crossing mtu unatoka Kariakoo mpaka Ubungo bila kusimama au unatoka Airport mpaka Kariakoo bila kusimama.

Mkuu watu zaidi ya milioni 4 unasema siyo wengi? Unacheza kweli wewe. Miji kama Oslo yenye wakazi laki tano tu ina treni (Metro/Subway), tram na mabasi. Mji kama Berlin una wakazi milioni 4 nenda kaone treni zilivyo nyingi pale. DAR treni si hasara hata kidogo zinahitajika sana tu.
 
Tatizo ni msongamano! Je wanaJF wanaushauri gani juu ya hilo.. sasa mdada tayali umekibilia kwenye kuhukumu... hapana shaka una uwalakini kuwepo hapa JF

Alichosema Mwafrika wa Kike NI KWELI! Hata ukiangalia suala la BRT (Bus Rapid Transit), mradi unaojengwa sasa hivi, unajengwa kwa kuwa kuna "commission" za wakubwa. Siku hizi, hakifanyiki kitu mpaka "tumbo langu lishibe", kwa mujibu wa wadau wenzetu kwenye wizara husika na taasisi za serikali. BRT will be a failure, mark my words! You just cant "import" an infrastructure methodology from a foreign country and expect it to "adapt" to our way of life! IMPOSSIBLE!

Mimi najua nini kinapaswa kufanyika kumaliza kabisa hili tatizo. One technology! Commuter trains: LRT + Monorail!

Nilishawahi kuongea kwa kina na Mhe. Mwakyembe, wakati akiwa Naibu Waziri kule Miundombinu. Sasa yuko Uchukuzi. Aliunga mkono hoja yangu. Tatizo, BRT imefika point of no return. They all know this will be just another white elephant, lakini kwa kuwa kuna ulaji, there's little that can be done. Money has changed hands, contracts have been signed (legal and binding). We will cry dry tears, later, when the BRT ITSELF will be a source of congestion!
 
Last edited by a moderator:
Mimi najua nini kinapaswa kufanyika kumaliza kabisa hili tatizo. One technology! Commuter trains: LRT + Monorail!
Sawasawa Monorail ni suluhisho zuri zaidi, na hasa kama litakuwa na gharama nafuu kwa mwananchi wa kawaida kabisa. Aidha Monorail mara nyingi imekuwa ikutumiwa na watu wengi wa daraja la kati kuliko wale wa la chini, ambao kwa hapa kwetu ndio wengi.

Pengine ufafanue zaidi jinsi monorail itakavyoweza kuwashawishi wenye magari binafsi kutumia aina hiyo ya usafari zaidi ya magari yao!
 
Bongolander,

...thats not an absurd idea...........niliwahi kusema huko nyuma kuwa kuna kitu chaitwa EEE....i.e. Engineering, Education and Enforcement.........kilichokosekana kwetu kuhusu hiyo idea ni hizo mbili "Education & Enforcement".........kinachotakiwa baada ya hapo wahandisi wanatakiwa wa-evaluate the performance ya idea waliyoitoa kama ina-work or not........if it doesn't........ there are plenty other options to play with

Unajua kama kuna tatizo kubwa unatakiwa kuchukua hatua za maana. You are very right, there are plenty of ideas around the issue, but we do not see any meaningful idea being adopted. The idea which can address the problem and not bringing confusion. Hatuwezi kushighulikia mambo kwa mawazo ya miaka ya 60 kwa matataizo ya mwaka 2012.

Dar es salaam si mji mkubwa kama Tokyo au kama Caracas, hili si tatizo la kuwepo kwa miaka karibu 10 bila suluhu.

tatizo moja ni kwamba kila kitu kiko concentrated posta, kama baadhi ya maofisi yangewekwa kunduchi megine temeke na mengine Kimara, kusinge kuwa na one way traffic kama ya sasa. Tungekuwa na mabasi ya abiria yenye kubeba abiria 100 tatizo hili lisingekuwepo. Angalia sasa, ni miaka mingapi tangu post hii iwekwe na nini kimefanyika so far?
 
Alichosema Mwafrika wa Kike NI KWELI! Hata ukiangalia suala la BRT (Bus Rapid Transit), mradi unaojengwa sasa hivi, unajengwa kwa kuwa kuna "commission" za wakubwa. Siku hizi, hakifanyiki kitu mpaka "tumbo langu lishibe", kwa mujibu wa wadau wenzetu kwenye wizara husika na taasisi za serikali. BRT will be a failure, mark my words! You just cant "import" an infrastructure methodology from a foreign country and expect it to "adapt" to our way of life! IMPOSSIBLE!

Mimi najua nini kinapaswa kufanyika kumaliza kabisa hili tatizo. One technology! Commuter trains: LRT + Monorail!

Nilishawahi kuongea kwa kina na Mhe. Mwakyembe, wakati akiwa Naibu Waziri kule Miundombinu. Sasa yuko Uchukuzi. Aliunga mkono hoja yangu. Tatizo, BRT imefika point of no return. They all know this will be just another white elephant, lakini kwa kuwa kuna ulaji, there's little that can be done. Money has changed hands, contracts have been signed (legal and binding). We will cry dry tears, later, when the BRT ITSELF will be a source of congestion!
Mkuu unachoongea sio siri, the whole thing is a failure. Labda tunaweza kunufaika kidogo na barabara, lakini the whole BRT thing kwa Tanzania it is never gonna work, hakuna mtu anayeweza kusimamia na hakuna mtu anayeweza kuendesha, usafiri wa umma Tanzania unatakiwa uendeshwe kwa mtyino wa daladala za sasa kwe na give and take inayofanya mteja na mtoa huduma wategemeane.

BRT itafanya kazi kwa mwaka( the maximum) then utakufa halafu zitaanza issue kama za UDA na KAMATA, huyu kaiba yule kaiba na hakuna atakayechukuliwa hatua.
 
Duuuhh.......Mkuu Bongolander heshima mbele........hebu tuone huo mradi wa BRT.........pengine watajitokeza walio na uchungu wa kudumisha/kusimamia vizuri huu mradi.........mradi huu unahitaji watu SERIOUS kusimamia.....wakileta michezo ya "mpatie shemeji/nepotism"......tumeumia.......

BTW; Ninavutiwa na utendaji wa Dr. Mwakyembe, Balozi Kagasheki, Prof Sospeter, na Dr. Huvisa......angalau naweza sema JK hapo ana mawaziri watendaji na sio blah blah blah..........
 
Last edited by a moderator:
Duuuhh.......Mkuu Bongolander heshima mbele........hebu tuone huo mradi wa BRT.........pengine watajitokeza walio na uchungu wa kudumisha/kusimamia vizuri huu mradi.........mradi huu unahitaji watu SERIOUS kusimamia.....wakileta michezo ya "mpatie shemeji/nepotism"......tumeumia.......

BTW; Ninavutiwa na utendaji wa Dr. Mwakyembe, Balozi Kagasheki, Prof Sospeter, na Dr. Huvisa......angalau naweza sema JK hapo ana mawaziri watendaji na sio blah blah blah..........

Mkuu Ogah, hiki unachosema kuwa kinakuvutia ndio tatizo lenyewe, tunatakiwa kuwa na system ambayo regardless of who is in the office the government, ministry or any department should perform with same speed, strength and effectiveness. Otherwise tunaweza kuwa tunabadilihsa mawaziri kila siku kwa kudhani kuwa tutakuwa na mabadiliko. kama system haifai, bila kujali nani yuko ofisini haitasaidia.

Nakubaliana kuwa mwaziri uliowataja wanatia moyo, may be they are among the best we have seen so far out of our cabinet. lakini ukiangalia vizuri unaweza kuona sana sana ni personality based than institutional based effiency, that is not what our country needs to have.
 
dar sio mahali aisee miundombinu inaliangusha jiji hili...as long as serkali itamiliki usimamizi
 
I agree with many ideas. Only if the government change its mind set (from Mshiko to patriotism and trust) where as the research work such as that of UCLAS, the construction companies such as of Military, and use of foreign may ideas only in advisory might change the situation. This ghost called investor based on foreign tech is chewing us deadly, even the consent of local contractors many of the companies of which I know do not qualify, they are lay people in engineering as I am and they use certificates of competent registered engineers to register their companies with mshiko we end up with poor and serious delays in delivery.

The above must tally with long term vision of the kind of cities we want! see what Paris did recently after realising the changes in the demands in traffic.
 
hapa ni gotera- ethiopia


gotera.jpg
 
Back
Top Bottom