Maoni ya wananchi: Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar es Salaam

SERIKALI KUHAMIA DODOMA: Rai hii imekuwa ikitolewa mara nyingi na viongozi mbalimbali wa chama (CCM) na serikali mpaka imeoneka kuwa porojo miaka nenda rudi tangu enzi za awamu ya kwanza ya mwalimu, fedha nyingi za walala hoi zimetumika kwa ajili ujenzi na uboresha wa makao makuu ya nchi Dodoma. JE MPAKA SASA SERIKALI INASUBIRI NINI? Na je kuna sababu za msingi serikali kuu kushindwa kuhamia Dodoma? Natumaini sasa ni wakati wa kuacha porojo, ni wakati wa serikali kufanya kwa vitendo ili KUPUNGUZA MSONGAMANO NA FOLENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM. Na pia kwa USALAMA wa nchi si sahihi serikali kuendelea na jiji la Dar es salaam kuwa kitovu cha utawala (administration centre) mimi binafisi sioni sababu za msingi, sijui wadau mnasemaje?
 
mbali na purukushani za kibiashara za dar es salaam, lakini huu mji unaonekana kuwa na 'uswahili' mwingi ambao unakuwa kikwazo kikubwa kwa watu kufikiri kwa uhalisia.
Nadhani Dodoma bado ni sehemu nzuri kwa watu wenye nia njema ya kuongoza nchi na sio ajabu viongozi wanangangania Dsm kwa maana nia yao sio kuongoza nchi bali kufanya biashara. Huwezi kuamini hata 'viti maalumu' wote wamejirundika DSM na wengine wanafikia hata sehemu ya kuuza madawa.
Tunaweza kwenda kujifunza kutoka Nigeria walivyoweza kutoka Lagos na kuhamia Abuja.
 
Nashangazwa sana na namna ambavyo serikali inatumia gharama kubwa kutengeneza barabara ya magari yaendayo kasi kwa kisingizio cha kuondoa foleni dar.

Hivi serikali haijui ni kitu kinachosababisha foleni au makusudi tu na utumiaji mbaya wa fedha za maskini wa nchi hii!?

Hata mtoto wa darasa la kwanza anafahamu kuwa tatizo la foleni dar linasababishwa na sehemu zenye taa za kuongozea magari (Traffic light), kinachofanyika sasa ni kutuaminisha kua daladala zinasababisha foleni, jambo ambalo si la kweli.

Tujitafakari upya!
 
hapo umesema hawalioni hilo sijui ni tanroad or wzr ya ujenzi na uchukuzi ,baada ya miaka miwili watakuja na plan hio tena wakati unakaribia uchaguzi
 
Tatizo linalowasumbua viongozi wa serikali yetu ni kutokua na Future Strategic Plan! Haiwezekani barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa baada ya muda fulani zinavunjwa na mfano wa barabara hizo ni Kawawa road na morogoro kuanzia Ubungo mpaka kuelekea mbezi, zilijengwa miaka kumi iliyopita leo zinavunjwa kupisha mradi wenye manufaa kwa wachache. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi
 
Ni mtazamo wangu ambao naona ndiyo suluhisho la foleni Dar ktk kipindi hiki ambacho strabag wanajenga barabara, mimi naona kama hauna ulazima sana kwenda na gari town acha gari home panda daladala acha aibu, kwa wale wanajiona mabosi kodini teksi basi.

Tatizo kila mtu anataka aonekana ana gari mjini au kazini.Mimi sioni raha kwa kuendesha gari kwa foleni kwanza matumizi ya mafuta ni makubwa, barabarani mateso yaani shida tu.

Kwa ktk kipindi hiki kama hauna umuhimu sana wa kwenda na gari town au sehemu nyingine tumia basi au taxi.

Huo ni mtazamo wangu, sijui nyie mnaonaje.

Natanguliza salam.
 
calculate uone unatumia mafuta ya shilingi ngapi kukaa kwenye foleni na kama unataka kufatilia issue au kazi unajikuta instead ya kufanya shuguli tatu unaishiwa kufanya moja tu...unaingia sehemu saa nne kurudi saa moja jioni.
 
wakuu naomba kuweka historia sawa, hivi juzi rais JK alivyotembelea banda la Ardhi University si alisema foleni za Dar es Salaam zinatokana na trafiki? ...au nilimsikia vibaya?
 
Uko sawa kiongozi ila naomba kuongezea wazo hivi,

Barabara kama zingekuwa zipo kila mtaa mfano nyumba zilitakiwa zipeane migogo na mbele yake zipite barabara ambazo ni za mitaa smart kama za wilayani meatu zingesaidia kupata shortcult way kuingia barabara kuu na siyo ilivyo sasa.

Ugawaji wa ploti bado hauna utaratibu maalum maana ramani za wasomi wetu huletwa baada ya laia kujenga bila kufuata mpango wa kitaalam.

Tukifanikiwa kutengezeza barabara za juu bado tunachangamoto kwa matukio ya haraka kama moto na jinsi ya kuyafikia ktk nyumba zetu ambazo wasomi wetu waliosoma ili kupata ajira na siyo kutenda kazi zao kwa ufanisi hawawasilrishi lamani katika maeneo mapya ambayo watu hukimbialia kujenga kwa kasi. Na matokeo yake hutoa ofa kama njugu wakisubiri magufuri aje kujigamba kubomoa nyumba za wahanga wakusababishiwa na Serikali sikivu yenye watu sikivu waliojaa rushwa na uvivu utadhani watoto wa mama mmoja.

Tuige basi japo sehemu zingine zilizopata lamani miaka ya nyuma ambazo zko ktk hata wilaya zetu ili Dar nayo ipanuke.

Think big.
 
Si UCLAS tu yenye suluhu za traffic jam pia hata UDSM nk. Weak linkages kati ya tafiti za vyuo na governance ya serikali inapelekea udumavu wa maendeleo yetu. Pili kupoteza masaa ya wakati wa kufanya kazi kwa ajili ya movements za hapa na pale ni ongezeko la umasikini na kero kazini hadi kwenye familia. Wafanyakazi wakitoka makazini wanasubirisha foleni kwa kukaa bar wengine migahawani nk hili ni janga kwa watoto kutoonana na wazazi wao kwa kuchelewa kurudi na kuondoka majogoo. Hapana not after 50+ ya uhuru. Tafiti zitumike kutupunguzia adha na kero hii
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom