Status
Not open for further replies.
Mleta uzi hao wote ambao umewataja ndiyo wanarudi ktk baraza la mawaziri!
Serikali ya ccm haina jipya
 
Wewe unataka tuwapange vilaza ili waboronge!!! tangu lini CDM wanaombea serikali imara ya CCM. umewataja wote imara wasiwekwe sasa unataka tumuweke mbowe lissu sugu au?? acha kumpangia yeye ndio Rais wewe kausha hata akimpanga ambaye hafai yeye ndio atawajibika sio wewe
 
Kwa namna yoyote nkiangalia list ya wabunge wa CCM, naona kabisa hawa hapa wanatokelezea kny Cabinet yake
1. Prof. Muhongo (japo ana arrogance na dharau)
2. Mwakyembe
3. Maghembe (Ndio pekee toka north anayeeleweka)
4. Mwigulu
 
Naomba asimsahau Prof Majimarefu kwenye wizara ya Utamaduni na Michezo maana huyu prof ana ufahamu na mambo ya soka kwani ni kada mzuri wa klabu ya Simba,pia katika utamaduni prof ni mganga mzuri wa tiba za jadi
 
Hali ya Kisiasa

1. Mgogoro wa Zanzibar ni jukumu lako kwa sasa halikwepeki. Tafuta wasuluhishi wawili (kutoka Bara na Visiwani) wakusaidie kulishughulikia hili

2. Katiba mpya ya JMT ? pengine si ajenda ya chama chako kwa sasa lakini linahitaji dhamira yako ? chonde chonde litendee haki taifa hili



Mfumo na Uendeshaji wa Serikali

3. Uza mashangingi ya Serikali na ubakize machache tu kwa shughuli muhimu. Watumishi wa Serikali wakopeshwe magari na wapewe mafuta ili kuokoa fedha nyingi mno zinazopotea kiholela.

4. Rejesha nyumba za Serikali kwani wananchi wengi hatuna imani kuhusu dhamira, mantiki na umuhimu wa kuziuza nyumba za Serikali

5. Punguza sana idadi ya Wizara na Mawaziri ili kupunguza gharama

6. Boresha kipato cha Watumishi serikalini ili kuwaongezea morali

7. Toa fursa katika vipindi tofauti mikoani ukutane na wananchi wenye matatizo uwasikilize ana kwa ana, mmoja mmoja (uwe rais wa wananchi)

8. Misamaha ya kodi ni donda ndugu linalohujumu Taifa mapato, dhibiti hili kwa nguvu zako zote.

9. Panua wigo wa vyanzo vya mapato ya Serikali ? hili ni muhimu sana

10. Dhibiti safari za nje zisizo za lazima kwa Viongozi waandamizi wa Serikali


Rushwa na Ufisadi

11. Mahakama ya Rushwa na Ufisadi ianzishwe kama ulivyoahidi
12. TAKUKURU ipewe mamlaka ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani bila kibali cha DPP

Afya, Maji na Mazingira

13. Karabati hospitali za umma (Taifa, Mikoa, Wilaya) ziko katika hali mbaya (Zahanati kwa kila kijiji inawezekana!)
14. Imarisha Hospitali ya Muhimbili ikidhi viwango vya kimataifa ili kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi
15. Panua wigo wa Mfuko wa Bima ya Afya ili ijumuishe wananchi wote (Rwanda wameweza hili) watakaochangia kiwango nafuu
16. Miji na Majiji ni machafu mno (taka ngumu na maji taka), imeshindikana kubadili hali na inaelekea hakuna suluhisho, inabidi tuzoe uchafu ? tunaomba wahusika wageuke taka
17. Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto iboreshwe kwa nguvu zote
18. Serikal igharimie magonjwa hatarishi ikiwemo saratani na UKIMWI
19. Matumizi ya mifuko ya plastiki yapigwe marufuku (Rwanda, Zanzibar imewezekana)
20. Anzisha Mfuko wa Maji Vijijini ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika maeneo yote

Elimu

21. Wanafuzi wengi wa elimu ya juu hawakupata mikopo kwa mwaka2015/2016? litatue hili kwani ni aibu
22. Elimu ya bure hadi kidato cha nne iwe kweli na yenye ubora
23. Shule ziimarishwe kwa kupatiwa madarasa, maabara, vitabu, walimu na lishe muafaka

24. ?One Computer, One Pupil? ? tujenge taifa la kisasa na linaloendana na mabadiliko ya nyakati kimaendeleo

25. Anzisha Kamisheni ya Taifa ya Ushauri kuhusu elimu

Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda

26. Fufua kilimo cha mazao asilia (mkonge, kahawa)
27. Anzisha Mfuko wa Taifa wa Kilimona Mifugo utakaotoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
28. Imarisha na jenga miradi ya umwagiliaji na majosho ya mifugo
29. Imarisha vyama vya ushirika na viwezeshe kujitafutia masoko
30. Futa kodi zote kandamizi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
31. Anzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi
32. Weka kodi nafuu na shindani kuhamasisha wawekezaji


Miundombinu na Uchukuzi

33. Punguza gharama za vifaa vya ujenzi ili wananchi wengi wamudu kujenga nyumba bora
34. Fufua Shirika la Ndege la Taifa (ATC)
35. Imarisha miundombinu ili kuondosha misongamano katika majiji na miji mikubwa (Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha)
 
Magufuli akitaka mambo yaende vizuri awaweke benchi wote uliowataja aje na mawaziri wapya kabisa tofauti na waliokuwa mwanzo.
 
Wewe unataka tuwapange vilaza ili waboronge!!! tangu lini CDM wanaombea serikali imara ya CCM. umewataja wote imara wasiwekwe sasa unataka tumuweke mbowe lissu sugu au?? acha kumpangia yeye ndio Rais wewe kausha hata akimpanga ambaye hafai yeye ndio atawajibika sio wewe

Taabu za serikali mbovu wawajibikaji ni sisi na ndio tutakaoteseka
 
Hatupokei ushauri kutoka chadema.hamna nia njema nyie mnataka asifanye vizuri muanze kubinua midomo yenu.asante kwa ushauri ila hautazingatiwa.
 
Wewe unataka tuwapange vilaza ili waboronge!!! tangu lini CDM wanaombea serikali imara ya CCM. umewataja wote imara wasiwekwe sasa unataka tumuweke mbowe lissu sugu au?? acha kumpangia yeye ndio Rais wewe kausha hata akimpanga ambaye hafai yeye ndio atawajibika sio wewe


Kwa sasa tunajenga nchi mkuu, maslai ya taifa kwanzaa
 
Mimi namkubali Prof Muhongo kwa sababu ni mtu wa facts, anaongea kitu ambacho kipo direct. Kuhusu kuthamini wawekezaji wa ndani sio kwamba hawathamini ila ni ukweli ulio wazi kwamba sekta ya nishati na madini inahitahi wawekezaji ambao wako full competent. Mfano kipindi cha mzozo wa vitalu vya gesi alitaja technical and financial requirements ambazo mwekezaji anatakiwa kua nazo ili apate kitalu.. Akasema anayeona ana qualify basi aende ofisini. Na kuhusu kutetea, ni kawaida waziri yupo upande wa serikali na lazima atetee serikali yake.

Mkuu nchi zote duniani zilizo endelea zimejengwa na wazawa, watajiri wa huko waliwezeshwa wakaweza watu wakapata ajira na kujenga nchi yao.

Kwenye madini tumewapa hao wazungu ambao unasema wanauwezo lkn sasa tunashuhudia tunaachiwa mashimo, Tanzania kwanza...
 
MMILIKI.gif
 
Wote ondoa ila prof.muhongo muache
. Ni mtu makini, mkali, anunuliki, msomi na anaogopeka uliza mameneja wa Tanesco, watakuambia. Huwa hana utani, ni the strongest candidate.
Mi ni ukawa pure
 
HAPA KAZI TU,wale wanao subili kubebwa kipindi chao kimekwisha,haijalishi ulitembea nchi zima na MH kwenye kampeni.WATANZANI tunahitaji watendaji kazi ambao siompaka wasukumwe kufanyakazi za maendeleo kwaTaifa letu.
 
Mkuu nchi zote duniani zilizo endelea zimejengwa na wazawa, watajiri wa huko waliwezeshwa wakaweza watu wakapata ajira na kujenga nchi yao.

Kwenye madini tumewapa hao wazungu ambao unasema wanauwezo lkn sasa tunashuhudia tunaachiwa mashimo, Tanzania kwanza...

Bila shaka wewe utakuwa ni mzee machache
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom