Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Wana-jf na hasa wale wataalamu wa afya naomba msaada wa ushauri hapa. Jana nilikuwa nacheza na katoto kangu ka miaka 3 seating room na paka wetu ambaye tumekuwa naye kwa takribani miezi 5 sasa na huyu paka amekuwa kama sehemu ya familia yetu kwani hata mwanangu amemzoea utakuta hata akiwa amelala kwenye kitanda chake na paka utakuta amejibanza pembeni. paka huyu tunampa matunzo ikiwemo vacination, kumuogesha kwa dawa na ku-trim manyoya yake after every 3 weeks. alipokuja bibi yake mwanangu (mama yangu) alikuwa mkali sana kuwa si vizuri kumuweka paka karibu yetu kwani manyoya yake ni sumu na yaweza kusababisha matatizo ya kifua yatakayopelekea kukoroma kama paka anavyokoroma...Ndivyo ilivyo??