Mangula: Najuta kuishi jimbo la Halima Mdee

Ungefanya utafiti kidogo ungejua kuwa jimbo la kawe halitakuwa chini ya chadema tena kwa sasa mdee kachuja sana hana uwezo wa kuutisha hata mkutano wa hadhara akapata watu.

Hapo kwenye kolezo umesema kweli kabisa mkuu kwani siyo tabia ya chama chake bali kile unachokishabikia ndo kinatisha mikutano kama kilivyofanya kule Arusha,Morogoro na kwa Mwangosi.
Unaposema akipita Tegeta na Kunduchi anaona aibu hakuna alichofanya unamaanisha nini.Wewe ulitaka afanye nini ambacho hakufanya mbona unatia aibu ndg yangu?Au ulitaka ajenge barabara ,apeleke umeme ,akununulie viroba,akupe kibali cha kuua Tembo ilhali vyote hivyo vipo mikononi mwa chama chako?
 
msameheni bure huyu mzee "wazee wa mtandao" walishamtupa kando kitambo. kwaiyo bado anaweweseka. hajakaa sawa bado.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.
Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata na wilaya zote za jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wa CCM.
“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende,” alisema.

Maswali yangu kwake ni haya:
-WanaCCM pekee wa jimbo la Kawe wanatosha kulirudisha jimbo CCM ktk sanduku la kura?
-Kwanini awe mwongo asisngizie kuumwa,kwani hana demokrasia ya kukataa kwenda kwenye kikao?

-Kinachomsababisha ajute ni kipi?

kawaida ya wana ccm kusema uongo,sasa mtu mzima na umri wake anasema uongo jee watendaji wake serikalini?Mawaziri,wabunge ,ma RPC,ma CCM karibu wote wanaishi Kinondoni,Kawe dijui kwa nini hawapataki temeke,labda kigamboni watahamia
 
"Wise men speak because they have something to say; fools because they have to say something"-Plato
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.
Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata na wilaya zote za jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wa CCM.
“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende,” alisema.

Maswali yangu kwake ni haya:
-WanaCCM pekee wa jimbo la Kawe wanatosha kulirudisha jimbo CCM ktk sanduku la kura?
-Kwanini awe mwongo asisngizie kuumwa,kwani hana demokrasia ya kukataa kwenda kwenye kikao?

-Kinachomsababisha ajute ni kipi?
aende Bunda
 
Ungefanya utafiti kidogo ungejua kuwa jimbo la kawe halitakuwa chini ya chadema tena kwa sasa mdee kachuja sana hana uwezo wa kuutisha hata mkutano wa hadhara akapata watu.

Simiyu Yetu aka gamba mharisha hovyo,una uhakika na unenayo au mnajipa matumaini ya mgonjwa wa ukimwi kupona,hahahahaaa kapokee buku saba upelekee watoto.
 
Last edited by a moderator:
Alimpigia kura ?

Chanzo cha ugumu wa maisha ni bosi wake mkubwa.

Sisi tulioko huku nje ya kidogo ya nchi ya tz tusemeje

ilogwe
 
hivi CCM wanawaza kwa kutumia nini? Hivi kweli kila mtu akianza kujitenga kwa kigezo cha vyama tutafika mbali? Kuna kosa gani kuishi jimbo la Mdee? Au hao wanaoishi huko wamekosa nini? kwahio wao wanastahili yeye ndio hastahili? mmmmhh huyu mzee tangu aoe naona nguvu zimempungua................
 
Arudi kijijini alikotoka sijui anafanya nini hapa, kila siku anaagiza mafaili ya watuhumiwa wake yafunguliwe lakini hatuoni action yoyote. Anazeeka vibaya

Uko sahihi arudi kijijini kulima viazi. Yeye alidhani ni kazi rahisi kuongoza chama kilichotwaliwa na mafisadi na wauza unga. Sasa anatafuta ajenda nyingine baada ya kushindwa kukisafisha chama kama alivyoahidi
 
Huyu mzee juha kabisa......hivi hajui kuwa Mabalozi wa G20 wote mbunge wao ni Mdee? Mbona hawalalamiki? Halafu nani alimwambia kuwa ataitwa kwenye mkutano ili akatae?
 
Back
Top Bottom