Mange Kimambi: Mwanaharakati mwiba wa Serikali ya Magufuli

Mange Kimambi: Mwanaharakati mwiba wa serikali ya Magufuli
Ikiwa ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu Rais John Magufuli wa Tanzania aingie madarakani, rais huyo ameonesha kutokusita kukabiliana na wapinzani wake, kuanzia wanasiasa na hata viongozi wa dini.
Rais Magufuli amethibiti shughuli za kisiasa za wapinzani. Mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa vyote vimezuiliwa, huku viongozi wote wa juu wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema wakiwa wanakabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani ikiwa ni pamoja na makosa ya kusababisha vurugu.
Serikali ya Rais Magufuli, ambaye ni muumini mzuri wa kanisa Katoliki, imetishia kuzifutia usajili asasi zote za kidini ambazo aidha zinajihusisha na siasa au kuzungumzia siasa katika mahubiri ya ibada

Lakini sasa rais huyo anakabiliana na upinzani mkubwa katika utawala wake kutoka kwa mwanaharakati wa kisiasa ambaye ushawishi wake bado unawashangaza wengi.
Mange Kimambi, mwanamitindo aliyebadilika kuwa mwanaharakati wa siasa, ndie muasisi wa maandamano yanayaopangwa nchi nzima kupinga kile anachokiita kuwa ni muendelezo wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uminywaji wa haki za kiraia nchini Tanzania.
Mange, akiwa na wafuasi karibu milioni mbili kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambaye miaka miwili iliyopita aliutumia ukurasa wake Instagram kumuunga mkono Rais Magufulu wakati wa kampeni za urais, leo hii anautumia ukurasa huo huo kuitisha maandamano makubwa ya kumpinga Magufuli na serikali yake.
Mange ni mama wa watoto watatu anayeishi nao Los Angeles, nchini Marekani. Harakati za mama huyo kumpinga Rais Magufuli zilianza kwenye mitandao ya kijamii takribani miezi sita tu baada ya rais huyo kupinga kuonyeshwa mubashara kwa shughuli za bunge kwasababu za kiuchumi.
Wafuasi wake, wengine wakiwa watumishi wa umma, wamekuwa wakimtumia taarifa mbali mbali zikiwemo zile zinazoaminika kuwa nyaraka nyeti za serikali, kufichua kile wasichokubaliana nacho juu ya mwenendo wa serikali. Wapo wengi pia ambao wamekuwa wakimtumia picha na taarifa kuonyesha hali duni ya huduma za kijamii katika maeneo yao.
Mange ni mmoja wa watu wa kwanza nchini Tanzania miaka ya mwanzo ya 2000, ambapo alitumia kurasa zake kuzungumzia maisha yake na marafiki zake pamoja na mitindo ya mavazi. Lakini Mange alizungumzia pia habari binafsi mbalimbali za watu maarufu waishio ndani na nje ya Tanzania, wakiwemo walimbwende, wanamuziki na waigizaji filamu.
Wengi wanaamini habari hizi ndizo ziliwavutia watu wengi kuanza kumfuata katika kurasa zake za mitandaoni.

-Wakati ambapo shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani zimedhibitiwa na watu kadhaa wamekamatwa na kushtakiwa kwa kuikosoa serikali kwa namna ambayo mamlaka haikupendezwa nayo, ukurasa wa Instagram wa Mange umefanyika sauti kuu kwa wakosoaji wengi wa serikali ya Rais Magufuli
Wakosoaji wa serikali na wanaharakati wa haki za binadamu wameendelea kuonya kwamba haki za kisiasa na uhuru vyombo vya habari na watu kujieleza vimeendelea kuminywa nchini Tanzania. Hata hivyo serikali imekuwa ikitupilia mbali madai haya.
Mara ya mwisho wafuasi wa upinzani walipoandamana mwezi Februari, makabiliano yao na polisi yalisababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilline ambaye inaelezwa kuwa alipigwa risasi kwa bahati mbaya.
Ikiwa maandamano haya yatafanyika ama la, ni jambo ambalo wengi wanasubiri kuliona. Lakini muitikio wa serikali katika kuapa kudhibiti maandamano haya umetafsiriwa na wengi kuwa ni mafanikio ya ushawishi wa Mange kupitia ukarasa wake wa Instagram tu, jambo ambalo vyama vingi rasmi vya upinzani nchini Tanzania vimeshindwa kulifanya.

Kuna wakati unawaza mwenyewe. Then unatoa hoja kwa kufikiria kuwa kila mtu ana mawazo yako. Nakushauri Kamsome Mwanakijiji. Kaandika kisomi zaidi. Wewe ni yule walioshindwa kuandama Ila kukiri udhaifu unashindwa.
 
Kwani na wewe ni GT? Aisee! Sijui na wewe kichwani umejaza nini!!!!
 
Mangekimambi wabongo wasikupoze kiaina, Wanaharakati wamekusaliti!! Hata viongozi na wafuasi wa upinzani unaowapigania wamekusaliti. Sweden wamekaribishwa na Balozi waeleze malalamiko yao, wamegoma, unachopigania hakitafika kwa muhusika Sababu Sweden nao waoga, wamekusaliti!!!

Waaingie Ndani kufanya nini ? Mkishaandamana wao ubalozini ndio walitakiwa kutoka nje Huo ndio utaratibu

Katika macho ya kishabiki kuna watakaobeza yaliyotokea jana na leo
Ila katika macho ya information interpretation kilichotokea ni hatari zaidi
Kushindwa kufanya kazi Kwa Mifumo ya kufikisha malaamiko serikalini Ndani ya ccm na Upinzani, media na hata NGO’s ni jambo la hatari hizi ndio formal democratic foundations and channels
Tumaini la mwisho lilikua la mass kufikisha malalamko kama hili limeshindikana Sasa tujiandaee Kwa matukio yasio ya kawaida wala ya kisiasa
Wale ambao wana uwezo Mkubwa wa kubadili mambo ila sio Wanasiasa walikua na Matumaini mambo yatabafilika kupitia njia rasmi kwakua ineshindikana basi njia watakayochagua ni hatari zaidi ..wengi wa watu kama hao ni hatari zaidi
Tusikebehi kwakua njia inayokuja ni hatari zaidi na ya gharama Sana kukabikiana nayo hata dalili Zimeanza kuonekana

Tuombe Mungu
 
Msimpe Mange ujiko usio na ulazima, yeye anajuwa watanzania wengi ni mazoba na ndiyo maana alitumia njia hiyo (maandamano ya mtandao) kuwalostisha ila bahati mbaya serikali ilimuonyesha kuwa japo watu wake ni mazezeta ila iko tayari kuwaokoa na ndicho ilichokifanya.

Huuu ndio mfano wa uzezeta

Kutumia maBILIONI kutishia watu na kuagiza magari ya lumficha mfalme nani muoga hapo
 
Nilijua tangu mwanzo kuwa maandamano yetu yangefana sana. Na kweli, yamepita mitaa yote kuanzia Facebook, Instagram, JamiiForum mpaka Whatsapp. Sisi sio watu wa mchezomchezo bwana! ...And we will do it again!
 
Waaingie Ndani kufanya nini ? Mkishaandamana wao ubalozini ndio walitakiwa kutoka nje Huo ndio utaratibu

Katika macho ya kishabiki kuna watakaobeza yaliyotokea jana na leo
Ila katika macho ya information interpretation kilichotokea ni hatari zaidi
Kushindwa kufanya kazi Kwa Mifumo ya kufikisha malaamiko serikalini Ndani ya ccm na Upinzani, media na hata NGO’s ni jambo la hatari hizi ndio formal democratic foundations and channels
Tumaini la mwisho lilikua la mass kufikisha malalamko kama hili limeshindikana Sasa tujiandaee Kwa matukio yasio ya kawaida wala ya kisiasa
Wale ambao wana uwezo Mkubwa wa kubadili mambo ila sio Wanasiasa walikua na Matumaini mambo yatabafilika kupitia njia rasmi kwakua ineshindikana basi njia watakayochagua ni hatari zaidi ..wengi wa watu kama hao ni hatari zaidi
Tusikebehi kwakua njia inayokuja ni hatari zaidi na ya gharama Sana kukabikiana nayo hata dalili Zimeanza kuonekana

Tuombe Mungu
Ngoja nikupe Taratibu za maandamano Duniani. Kwanza kuna kueleza nia ya kufanya maandamano. kwa kuomba/kutoa taarifa kwa mamlaka, kuna kupanga mahali pa kuanzia, route na mahali yatakapoishia hayo maandamano, kuna kuandaa kiongozi wa kuyapokea maandamano hayo atakayefikishiwa ujumbe huo. Kukosekana kwa utaratibu huo sio maandamano ni uvamizi na kiongozi aliyevamiwa hawezi kutoka tu kienyeji ati kuna watu huko nje wanapiga kelele.
 
Mange Kimambi: Mwanaharakati mwiba wa serikali ya Magufuli
Ikiwa ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu Rais John Magufuli wa Tanzania aingie madarakani, rais huyo ameonesha kutokusita kukabiliana na wapinzani wake, kuanzia wanasiasa na hata viongozi wa dini.
Rais Magufuli amethibiti shughuli za kisiasa za wapinzani. Mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa vyote vimezuiliwa, huku viongozi wote wa juu wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema wakiwa wanakabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani ikiwa ni pamoja na makosa ya kusababisha vurugu.
Serikali ya Rais Magufuli, ambaye ni muumini mzuri wa kanisa Katoliki, imetishia kuzifutia usajili asasi zote za kidini ambazo aidha zinajihusisha na siasa au kuzungumzia siasa katika mahubiri ya ibada

Lakini sasa rais huyo anakabiliana na upinzani mkubwa katika utawala wake kutoka kwa mwanaharakati wa kisiasa ambaye ushawishi wake bado unawashangaza wengi.
Mange Kimambi, mwanamitindo aliyebadilika kuwa mwanaharakati wa siasa, ndie muasisi wa maandamano yanayaopangwa nchi nzima kupinga kile anachokiita kuwa ni muendelezo wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uminywaji wa haki za kiraia nchini Tanzania.
Mange, akiwa na wafuasi karibu milioni mbili kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambaye miaka miwili iliyopita aliutumia ukurasa wake Instagram kumuunga mkono Rais Magufulu wakati wa kampeni za urais, leo hii anautumia ukurasa huo huo kuitisha maandamano makubwa ya kumpinga Magufuli na serikali yake.
Mange ni mama wa watoto watatu anayeishi nao Los Angeles, nchini Marekani. Harakati za mama huyo kumpinga Rais Magufuli zilianza kwenye mitandao ya kijamii takribani miezi sita tu baada ya rais huyo kupinga kuonyeshwa mubashara kwa shughuli za bunge kwasababu za kiuchumi.
Wafuasi wake, wengine wakiwa watumishi wa umma, wamekuwa wakimtumia taarifa mbali mbali zikiwemo zile zinazoaminika kuwa nyaraka nyeti za serikali, kufichua kile wasichokubaliana nacho juu ya mwenendo wa serikali. Wapo wengi pia ambao wamekuwa wakimtumia picha na taarifa kuonyesha hali duni ya huduma za kijamii katika maeneo yao.
Mange ni mmoja wa watu wa kwanza nchini Tanzania miaka ya mwanzo ya 2000, ambapo alitumia kurasa zake kuzungumzia maisha yake na marafiki zake pamoja na mitindo ya mavazi. Lakini Mange alizungumzia pia habari binafsi mbalimbali za watu maarufu waishio ndani na nje ya Tanzania, wakiwemo walimbwende, wanamuziki na waigizaji filamu.
Wengi wanaamini habari hizi ndizo ziliwavutia watu wengi kuanza kumfuata katika kurasa zake za mitandaoni.

-Wakati ambapo shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani zimedhibitiwa na watu kadhaa wamekamatwa na kushtakiwa kwa kuikosoa serikali kwa namna ambayo mamlaka haikupendezwa nayo, ukurasa wa Instagram wa Mange umefanyika sauti kuu kwa wakosoaji wengi wa serikali ya Rais Magufuli
Wakosoaji wa serikali na wanaharakati wa haki za binadamu wameendelea kuonya kwamba haki za kisiasa na uhuru vyombo vya habari na watu kujieleza vimeendelea kuminywa nchini Tanzania. Hata hivyo serikali imekuwa ikitupilia mbali madai haya.
Mara ya mwisho wafuasi wa upinzani walipoandamana mwezi Februari, makabiliano yao na polisi yalisababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilline ambaye inaelezwa kuwa alipigwa risasi kwa bahati mbaya.
Ikiwa maandamano haya yatafanyika ama la, ni jambo ambalo wengi wanasubiri kuliona. Lakini muitikio wa serikali katika kuapa kudhibiti maandamano haya umetafsiriwa na wengi kuwa ni mafanikio ya ushawishi wa Mange kupitia ukarasa wake wa Instagram tu, jambo ambalo vyama vingi rasmi vya upinzani nchini Tanzania vimeshindwa kulifanya.
Mange ni shujaa.
Shujaa wa matusi.
Shujaa wa "blackmail".

Je Uliandamana?
 
hongera sana Mange kitendo cha mapolice kukaa barabarani ni prove tosha kuwa ni wewe ni mwanamke shujaa... ....kwani nini wangapi wana Instagram account na serikali haiwatambui???? lol
Hapana,

Mange na wafuasi walijua wazi kwenye maandamano ya upinzani lazima polisi watie timu na virungu, mabomu ya machozi na maji ya washa washa.
Yeye aliapa ataandama hadi Magu atoke madarakani..
Polisi wamepita doria siku 1 tu kabla...Mage na wafuasi wake wamenywea kabla hata polisi hawajapiga bomu moja la machozi wala kutumia lita 1 ya maji ya washawasha.

Mange na Mbowe hawana tofauti. Ni waoga.
Mbowe aliitisha maandamano ya Ukuta. Wazee wa kazi wakapita mtaani kuonyesha zana za kazi. Mbowe na Ukuta wakayeyuka.

Mbowe aliitisha maandamano kinondoni. Ile kuona kuna blockade ya Polisi. Mbowe ndio alikuwa wa kwanza kutoroka na kujificha. Aliyeyuka kama moshi. Wafuasi wake wakabaki wameduwaa.

Mange na wafuasi wake hawajaonyesha ujasiri wowote ule. Wamekimbia maandamano waliyopanga dhidi ya dola.

Nimeamini maneno ya Dr. Salmin.. "Chezea ndevu..usicheze na dola".
 
unaniudhi,lol makamanda wanaudhi nao,Mange alipigana mpaka Lissu akapata hela ya matibabu lakini Mange alivyoitisha maandamano wakamkana hawakumpa support,hii nayo ilifanya maandamano kukosa momentum
Wale jamaa ni wanafiki balaa.
Walimjaza Mange upepo afu wakamtelekeza.
Mbowe, Msigwa na hata Lissu mwenyewe wako kimyaaaaaaaa utadhani wamekufa
 
Lakini kajaza askari na vifaa barabarani.Kuna la kujifunza hapa na kesho haiwezi kuwa kama jana!!
Hao ndio Mange alikuwa amepanga kupambana nao tangu mwanzo afu yeye na wafuasi wake wakagwaya.
Kwani kuna maandamano yoyote ya upinzani yasiyo na polisi wa kugawa mkong'oto?
 
General Mabeyo kasikitisha Sana kukubali Mtego wa kuingiza vifaru dhidi ya wananchi ambao ndio wenye jeshi lao mitaaani
Yaani na mkwara wote ule wa Polisi haukutosha hadi kuingiza vifaru
Kawaaibisha hata watangulizi wake
 
Hakuna cha mwiba hapa. Kama anajiamini si aje Tz. Huko kanda ya ziwa kuna msemo " mange ni sawa na kipumulio(kijambio) kinachohamasisha wengine kujamba" halafu kikabaki constant after the reaction. Watanzania wanajua Magu anatupeleka wapi. Yeye aendelee kuwashwa huko insta
mandela alifanywa nini na makaburu?
unajua kwa nini wanaharakati wa SA walikuwa wanakuja kupewa hifadhi Tanzania?
tuanzie hapo we kenge
 
Back
Top Bottom