Mange Kimambi awavaa January Makamba na Ridhiwani, Ajiunga rasmi 'Team Lowassa'

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,121
27,128
Mdada ame speak a lot of sense! Nimemuelewa na ninaunga mkono hoja yake.

1.png
Jamani acheni kusikiliza maneno. Cybercrime sijui cyberbill bado haijapitishwa, JK ameichunia anasikilizia upepo kwanza….hahahaha

Jamani hii bill ni ngumu sana for JK kui sign maana akiisign ita affect nchi vibaya sanaaaaa, Tanzania inategea sana misaada kutoka western countries, hizo western countries haziwezi peleka mikopo au misaada kwenye nchi yenye sheria ya kuziba freedom of speech.

Yani hapa wanampa mtihani tu baba wa watu……. Yani baba yangu JK akisign hii itakuwa ni kwamba kaamua to the hell with Tanzania mie ndo nshamaliza muda wangu ila kama kweli anaipenda Tanzania hawezi kusign hii sheria ya kishenzi…..

Someni gazeti la citizen hapo hapo ujue kwa lugha ya ukweli ni kwamba JK keshachimbwa biti na Western countries kuhusu hii bill..

2.png

Hhahhaa dada enu kama kawa nilishatoa mawazo yangu juu ya hili zamanii..siktuaka tu kuweka kwa blog ila kwa kweli nilichamba….

Yes nilimtarget January Makamba sababu yeye yani ndo alikuwa kiranja wa kutetea hii bill, yani bila yeye na wengine wachache sana from CCM kusimama kidetete na hii bill sidhani kama hii bill ingepita huko bungeni….

Naomba msome tweet zangu alafu naomba mlinganishe na gazeti la citizen limesema nini ndo mjue dadaenu mie kichwa….

Naapa sikuwa naandika kwa vile tu hii bill ingeniharibia hata mie ugali wangu ila pia ni sababu naipenda nchi yangu, hivi kweli tunaelekea wapi kama hii bill ikipitishwa???

kwanza ningeomba kuanzia leo tuache kuiita hii bill cybercrime bill sijui nini naomba tuuite #shutuptanzaniabill

3.png

Mwanzoni dada enu nilikuwa naandika kwa kiswanglish nikapigiwa simu fastaaaa toka Tanzania nikaambiwa niandike in English only ili tweet ziweze eleweka na wahusika wa western countries baada ya tag kufanyika..LOL…

salonge.png

Uwiiiii huyu dada namfagilia sanaaaaa, yani haogopi kituuuu anaongea tu na kuchamba live live. Ila anachamba kistaarabu,hahahahah…

Huyu dada nae alimpa January za uso live live about this issue yani huyu dada kwa kweli apewe hongera….

embu mfollow tweeter uone anavyoongea bila uwoga…Anatumia MariaSTsehai .Yani huyu dada ni mwelewa sana aiseeee….. Na hawa ndo viongozi wanaotakiwa nchini..

a.jpeg


Okay, najua hii yaweza niletea matatizo makubwa ya mahusiano yangu na watu nawaowajali na kuwapenda ila kama na wao wananijali

na kunipenda basi watanielewa…. You guys know kuwa January ni kakangu, na ninampenda sana… Yani mie nilikuwa mmoja wa supporters wake mpaka ilipokuja issue ya hii bill ndo ikabidi nijitoe team January. Kama mnakumbuka hata banner lake niliweka hapa kwa blog yangu tena watu wake wa campaign walitaka kunilipa maana waliniuliza rates zangu nikawajibu kwamba huyo ni kaka yangu siwezi mchaji namuwekea bure…. Ila kama mnakumbuka kuna siku tangazo lilipotea tu, yes thats the day nilipoamua kuwa siwezi kumsupport kiongozi kama huyu…..

Siwezi kumsupport kiongozi ambae anajenga mazingira ya udiktekta ,siwezi kumsupport kiongozi ambae kwenye century hii tunayoishi anasimama kidete kutetea sheria ambayo ita sensor media , siwezi msupport kiongozi ambae anatetea sheria ambayo itamuwezesha yeye kuingoza hii nchi bila kunyooshewa kidole au la sivyo mtu uwe na ushaihidi wa kutosha …

Siwezi kumtetea kiongozi ambae badala asimame kidete kutetea sheria za maana kama vile sheria za copyright za wasanii wetu ila yeye anakuwa selfish anasimam kidete na sheria ambayo inamu affect yeye personally. Siwezi msupport kiaongozi ambae anataka kutuongozi kama makondooo tu. NO ,tukisupport hii sheria tujue tunapoelekea ni mambo pabaya sana….

Kwa kweli kaka yangu January kani disappoint sana ,yani nilikuwa all for him ila dah bora kaonyesha makucha yake sasa hivi… Kinachosikitisha zaidi hana hata watu wa kumshauri vizuri. Unajua this was his chance to play the politics game, January kaka yangu politicians huwa wanaanngalia upepo unapokwenda then ukipata madaraka ndo unatupotezea unaleta mambo yako tena sio ukipata madaraka tu ukishaingia muhula wako wapili ila sio before….

Kama Obama muhula wa kwanza alijitahidi kutouzi watu una muhula wa pili alivyojicetua anajua anaondoka mune msinune atamaliza kipindi chake.Yani kweli washauri wa January walimwambia kuwa its okay mgombea uraisi wa 2015 kusimama kidete kutetea sheria ya kuua freedom of speech? kweli???? hata mie mwenye akili zangu mbili angenipa hata kanafasi ka kupika chai ofisini kwake ningemshauri kuwa bosi hapo you utaharibu ,you need to distance yourself……

Au kama ni politician wa ukweli angefanya opposite ,embu naomba mjaribu ku imagine kama right now JANUARY MAKAMBA angekuwa against this bill alafu ni mgombea uraisi, alafu sio mgombea uraisi tu ni mgombea uraisi ambae daily anakuwa attacked kwenye jamii forums , media zenye kumsupport Lowassa and other media outlets., imagine kama January right now yeye kiongozi ambae hii law ndo itamsaidia kuachwa kusemwa vibaya na media angesimama na kusema kuwa hapana hata kama hii sheria itanilinda na mimi against maadui zangu wanaotumia media kunichafua lazma TANZANIA kuwe na freedom of speech because Tanzania comes first kabla yangu mimi Januar, uwiiii si angekuwa hero sasa hivi jamani???

I mean just imagine guys, politician ambae kutwa anatukanwa na kutungiwa maneno asimame na kusema hata kama mnanitukana endeleeni kunitukana maana ni haki yako wewe kama mtanzania kuongea….UWIIII,Mange kimambi mbona blog yangu ingegeuka Janauary Makamba campaign central???? yani ingekuwa ukifungua hii blog tu unakutana na sura January Makamba ningemfanyia kampeni za online bureeeeee, kina Wema sepetu kina nani wooote huko insta ningewaomba waweke mpaka display za uso wa January maana ni shujaaaa… Ila sasa kaonyesha weakness kubwa mnoooooo na kawadisappoint watu wengi mnooooo…..

Ona hii chat nilikuwa na chat na mtu mmoja wa ndani humo CCM sitaki sema hata influence yake ikoje humo asije stukiwa….hahahaha….

Mie huwa nachat na watu wa maana whatsapp…hahahhhahahha simu yangu ina mapassword mpaka basi maana siku ikipotea isije kuwa tabu…hHAHAHA, Alafu nimeiset kwamba mtu akiingiza wrong password mara fudenge tu ijifute kila kituuuuuuuuuuuu.lol

4.jpg

Hahhhaha chezea vita wewe, uadua tukaweka pembeni tukaungana ili tuwe na nguvu zaidi….Chezea jinsi Jamii wanavyonichambaga ila siku hiyo tulisameheana tukawa kitu kimoja… Umoja ni nguvu utengani ni udhaifu…Jamani media zoooote tuungane hapa… Although we all know ni media zipi haziwezi kuungana na sisi against hili maana waume zao wauza unga wako protected na hii bill….hahahahahahaha..Mmewaona walivyo busy na vibao vyao vya social media…hahahahhaha…..

JAMII FORUMS TUKO PAMOJA ILA MPUNGUZE KUNICHAMBA HUMO NDANI JAMANI….DAH!!!

5.png

Mnaona lakini watanzania muache kupelekeshwa meeona eeh hawa politicians hii sheria hawaitetei sababu ya kukujali wewe mtanzania eti usisemwe mtandaoni wanajilinda wenyewe…mmeona eeeeh? kumbe ni game yao wenyewe ya kampeni jinsi ya kudhibitiana influence ya influence ya media… Ila sasa ndo hivyo samaki mmoja akioza ni wote. Kaka alikuwa anawalenga wengine ila ndo hivyo na kina Mange na kina dougiemasta19 pia sheria ikatukamata kooni……hahahahaha

6.png

Yani huyu mheshimiwa alichosema hapa ndo kile nilichokuwa namwambia January kwenye tweeter kuwa that was a really bad move kwa mgombea uraisi…..Huyu jamaa naechat nae kwanza wote mnamjua …hahahha…Atanitukana leo mpaka nidate…..hahahahhaha

Kusema ukweli I dont think January is ready for presidency… Bado sana…Yani just the fact that alidhani kuwa its okay to pass laws za kusensor media jsut a few months before he runs for presidency tells you kuwa bado hajaijua siasa na hayuko tayari na kwamba tukimpa nchi WE ARE IN BIG TROUBLE…. Yani tutafungiwaa na mablog kwa kusema tu kuwa raisi alichelewa kwenye mkutano…hahahahahhahha

Yani inakuonyesha kabisa the kind of president he is going to be….. Ila bado sijaamini kuwa kijana ambae amesomea kwenye nchi inayodhamini freedom of speech kama marekani leo hii anaweza kuwa na guts za kusimama hadharani na kutaka kusensor media….dah..inatisha..

Uwiiii jamani navyoongea kama cherehani January akiwa Raisi inabidi nichukue uraia wa marekani tu la sivyo nikirudi ntakamatiwa airport for treson…ahhahahahahhaha….. Ila ukweli I think he needs 10 more yrs ya kujua jinsi ya kudeal na watu and surrond himself na wao ambao wako kwenye reality na ambao wana guts ya kumwambia ukweli kama mimi hapa. EEh in 10 yrs akija run tena aniweke mie mdogo wake kwenye team yake haki ya nani ntakuwa namwambia ukweli maana it seems he is surruonded na watu wanaomwogopa.

b.jpg


Dah, haki ya nani kweli naipenda Tanzania jamani. Inabidi nije kuwapewa hata uwaziri kwa kuandika posti hii maana Ridhwani ni kakangu yangu wa damu… January ni kaka yangu wa kambo ila Ridhani ni kaka wa tumbo moja chief… Yani we grew up together, very close, tumejuana toka wadogo… Yani baba zetu walikuwa ndugu, wenyewe walikuwa wanaitaka "KAKA" maana walisema washakuwa ndugu so ni brothers only na waliitana kaka mpaka siku my dad anakufa… Yani mpaka watoto wao walikuwa lazma wasome same schools. My young brothers walikuwa same school na the younger kids wa JK.

My dad found out about Kamuzu academy first akasema lazma na watoto wa kakake wasome hapo so walivyokubaliana watoto wao wadogo wote wakaenda hiyo shule. Yani tulikuwa one family kihivyo….So naomba muelewe how hard it is for me kumkosa Ridhwan ila inabidi tu niongeee na kama kweli ni kaka yangu na ananipenda wala hatonimind atanielewa kuwa mie nakipenda sana chama and mostly nampenda yeye kama ndugu yangu ndo maana naongea..Allafu my dad jamani yani alitunyang'anya tonge mdomoni wanaej amani maana he died like 6 months before JK became president ,uiiiiii jamani mie now ningekuwa kwenye royal family mngejutaaaaa….hahahahahahahahhahaha…. You should hear mie na wadogo zangu tukianza kudream kuwa why dad hakusubiria amuone mdogo wake akiwa raisi tule bata refu sieeeeee….. hahahahahahahaha…..

Yani kampenzi za JK toka za uwaziri nyumbani kwetu tulikuwaga hatuna hata gari moja, magari yooote kwenye kampeni, yani my dad kipindi cha kampenzi kwetu ni ilikuwa balaaaaa…hahahha…MY DAD WAS A JK SUPPORTER MPAKA BASI…KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI JAMANI….

Okay back to the topic…. kaka yangu Ridhwani nakupenda sana ujue, ila na wewe umenisikitisha sanaaaa kakangu… Yani nyie vijana wa CCM sijui mna plan gani na nchi yetu jamani mpaka mnataka kupitisha sheria kama hii… Kakka yangu Ridhwani baba yako wakati anakuwa raisi alitupromise watanzania kuwa Tanzania itakuwa na open governance inakuwaje leo wewe mtoto wake unataka kwenda kinyume na baba yako?

JK katukanwa sana ,kapigwa madongo sana na media kuanzia online mpaka magazetini na kavumumilia yote maana alitupromise watanzania kuwa goverment yake ita tolerate freedom of speech. Nimeona some people tweeter wanasema eti JK ndo alietoa aagizo la hii bill kuletwa mezani kwake mimi napinga kabisa maana kama JK angekuwa na akili ya kufanya hivi angefanya mwanzo alipokuwa Raiisi na sio sasa hivi wakati keshamaliza muda wake and he has nothing to loosee hata asemwe mpaka vipi.

Hivi mnakumbuka JK aliwekwa picha ile chafu na yule ze utamu mpaka magazeti wakaingilia wakasema its too much now na kuiomba government iingilie kati Raaisi wetu kudhalilishwa vile, imagine JK wala hakuweka hii sheria kipindi kile. Kweli kipindi ambacho he had everything to loose asipitishie sheria ya kutushutup watanzania then leo hii anaondoka ndo apitishe? nakataaaaaaa..

Alafu JK ana akili nyie hawezi sign hii bill ya kipumbavu anajua implication zake… Uwii can you guys imagine kama January Makamba ndo angekuwa raisi kipindi kile cha JK na ile picha aliyowekwa JK kwenye zeutamu ndo angewekwa January? uwiiiiii,nahisi bloggers mpaka tulioko nje ya nchi tungebebwa tuwekwe selo, tuwe tortured mpaka tuseme blog ni ya nani na nani katengeneza ile picha? uwiii mie navyoogopa maumivu ningemsingizia Shamim fastaaaa…hahahahhhahahahahhahahahaha….Ila serioulsy don't mess na kiongozi ambae weould do anything to protect his image and what people say about him, in short ogopa kiongozi mwenye mentality ya udikteta…..

Kaka yangu ridhwani kila siku uko marekani ,wapi na wapi unaweza kutaka kuleta sheria kama hii nchini? Nilisoma na tweet yako moja umeandika eti " yes no more matusi" hahahahahhahhahaha dah yani kaka yangu kweli iliandika no more matusi? ile sheria haiongelei matusi ya nguoni tuu ile sheria inaongeela mtu kusema chochote kile ambacho hatoweza kuprove mahakamani….which means leo hii tusema Mange nimepewa insdier information na chaumbea kuwa kaka yako Ridhwani ni fisadi basi nisiandike kwenye blog kuwa jamani kuna tetesi kuwa kaka yangu Ridhwan ni fisadi na sio hivyo tu pia nisiapprove comment yoyote ile itakayokusema wewe negatively. Sasa lets say kuwa kweli wewe ni fisadi je mie Mange ntawezaje kuprove hayo? naanzia wapi lakini kwa resources gani nilizonazo kunisaidia kuprove hilo si ndo itabidi niogope hata kuhoji nikae kimya tu? na hao watuma comment si nao inabidi wakae kimya? is that right??Is this the Tanzania we want????

naomba uelewe kaka yangu kuprove kitu mahakamni ni issue ngumu sana hata kama umefanya kweli na nikamtaja alieniambia akiitwa mahakami anaweza kunikana akasema haajsema just because anakuogopa je hapo bado dadako sijafungwa au kutozwa faini ya milioni 50? Kumbuka kuwa O.J simpson kweli alimuua mke wake na boyfriend wake ila kufika mahakani aliachiwa huru sababu tu ushahidi haukujitosheleza ila kila mtu anajua kuwa kweli aliua, je mnavyosema kuwa tusiandike vitu ambavyo hatutaweza kuprove mahakamani iwapo tutakuwa sued si in short mnasema kuwa tusiongee chochote juu yenu.

7.png


Dah kaka yangu hii tweet yako ilinisikitisha sana yani ilinionyesha kuwa wala hukuangalia the bigger picture ya issue yani ulikuwa unajiangalia wewe tu kama Ridhani ila hukuangalia madhara ya hii sheria kwa nchi yako unayotaka kuiongoza…

Kwa vile umesema ambao hatusupport hii bill yenu basi sie tunatetea hawalifu naomba nikwambie kwamba Kati yangu mimi na wewe kaka yangu Ridhwani wewe ndo unaewatetea wahalifu tena wewe unatetea wauwaji , Yani umekuwa selfish mpaja hujaona ni jinsi gani hii sheria yako inatetea wahalifu na nawauwaji….

Kwa mfano mimi dada yako nilishaongeaga na kuweka comments za wadau humu kuwa mume wa Shamim ni muuza madawa ya kulevya na kila mtu anajua kuwa mume wake ni muuza wamadawa ya kulevya na wachangiaji wakatuma comments za kuusema huu mtandao wa madawa kulevya wa mume wa Shamim na wenzie mpaka wengine walijitokeza na kudai kuwa ndugu zao wameshikwa huko nje kwa kubebeshwa madawa na mume wa shamim na wenzie je huoni kwamba hii sheria mnayoitetea nyie wana CCM wenzangu inampa power muuza madawa ya kulevya kama mume wa Shamim kunipeleka mimi mahakamani na kutumia hii sheria yenu kunimliza au kunifanya nisiongee tena kuhusu yeye na wauza madawa wengine.

Kama maaskari wenyewe huwa wanakosaga ushahidi wa kupeleka mahakamani na kuwafanya hawa wauza unga wafungwe je mie blogger ntapata wapi huo ushahidi? Huoni kama hapa wewe na mwenzio January Makamba ndo mnaowatetea wauwaji hawa wanaolimaza taifa? I mean is it really that important kwamba mjikinge nyie and in the proicess muwakinge wauzazi wa madawa ya kulevya criminals wengine ambao huwa wanakuwa outted na social media ? Je maaskari watapata wapi infomation kama hizi? kumbuka kuwa hawa watuma comment ndo wanaishi mitaani na hawa wauza unga so mnapowawekea sheria kama hivi je hili janga linalolimaliza taifa si litazidi kushamiri? Yani sasa hvii wauza unga hawana hata haja ya kututumia watu watufanyizie ni wanatupeleka mahamakani tu na vile pesa wanazo basi sisi wanyonge itabidi tukae kimya tuwaache waendelea kuua ndugu zetu just so nyie viongozi wetu mmeweka sheria ili msisemwe mnapokosea au msikosolewe au msipewe ushauri……

LOOK AT THE BIGGER PICTURE, MKIAMUA KUWA VIONGOZI ACHENI KUWA SELFISH…… So my darling kaka RIDHWANI wewe ndo mteteaji mkubwa wa wahalifu , ila I must say you are on the right team angalau wahalifu wa crime ya uuaji kupitia madawa ya kulevya and the like unaowatetea wewe wana mapesa ya kukupa hata ahsante ya kuwasidia ila kina Maria SARUNGI na wana Chadema ni malooser maana wanatutetea sisi wahalifu wa crime ya kuwa too opinionated ,kiherehere,umbea, midomo mirefu na midogo michafu wakati wanajua hatuna hata senti za kuwapa ahsante…..Dada Mariah hutaki kutajirika wewe ???lol

KAKA JANUARY NA KAKA RIDHWANI Nyie ndo mnatakiwa kuwa mfano, nyie ndo mnatakuwa kuleta TRANSPARENCY nchini , nyie ndo mnatakuwa kutupooza watananiza kuwa chama chetu cha ccm hakina cha kuficha, nyie mnatakuwa kutupa sisi moyo wa kuwapigia kura October ila sasa mnatuogopesha kwa kweli. YANI CONFIEDENCE YOOOTE IMETUTOKA NA HOFU ZIMETUJAA…

Nyie vijana ndo mnatakiwa kuwafundisha kina LOWASA how to be leaders in 2015 kwenye miaka hii ya technolojia, kina Lowasa ambao wameijua computer wakiwa na miaka 60 ndo wanatakiwa waogope cyberllying ila sio nyie watoto wa .com , aibuuuuuuuuu ,yani nyie mnataka kueleta leadership za wazee wetu wa ccm wa 20yrs ago leadership ambayo hatuitaki at all….Kusema ukweli kwa vile LOWASSA hakuji associate na hii bill yeni I think ana haki yooooote ya kusimamishwa na CCM la sivyo hata sie wana CCM tutwageuka na kuhamia chadema kwa kweli….Hamuwezi kutupeleka peleka kama makondoooo….

Kaka zangu January na Ridhwani jana usiku niliongea na shemeji yenu Mzungu na kutaka maoni yake kuhusu hii bili na kumuuliza je marekani wana deal vipi na hii kitu ya cyber bullying. Akasema hivi hiyo sheria iliyopitishwa huko Tanznaia inafanana na iliyopo marekani juu ya cyberbullying ila tofauti ni kwamba hiyo sheria kwa hapa marekani haiwezi kutumika kumtetea BEYONCE, AU KIM KARDASHIAN AU OBAMA AU HILLARY CLINTON, wanaweza kujaribu but hardly wata win ndo maana media ya marekani can say as much shit as they want about their leaders and celebrities akaendelea kusema kuwa hiyo law ipo kuwalinda watu wa kawaida.

Ngoja niwaeleze zaidi ni hivi mtu kama Beyonce kaamua kuwa superstar kaamua kuwa kioo cha jamii au tusema mtu kama Obama kaamua kuwa anataka kuwa baba wa taifa well that means akubali kukosolewa na kuongelewa kwa lolote lile in other words ni kwamba maisha unayoamua kuishi kama celebrity au politician ukubali matusi yooote, maneno yote kama ni ya uongo au ya ukweli ukubali tuuu coz it comes with the FREAKING territory.

Ila sasa kuna mtu kama Jane yuko zake kimya hajulikani wala nini mara blogger kaibuka huko anamtukana kwa maneno ya uongo kabisa na kumuharibia maisha yake, Jane akienda mahakamani basi sheria ya cbyerbulling itamlinda sana tu….

uwiiii, watanzania mmeona tofauti hapoo eeeeeh? HII sheria hata nchi za nje ipo ila inaangiliwa nani anaweza kuitumia na kwa situation gani..Ila sasa hawa viongpzi wetu wa Tanzania wamei twist na kuipindisha ili wajilinde wao wenyewe more than hata kukulinda wewe.

Kwanza naomba kuuliza ukimweka Mrs. Sembe pembeni ni watanzania wangapi wana hela hata ya kuweka lawyer akafanya lawsuit ya kumsue MANGE kuwa kamtukana blogini? na ujue mahakani ni process ndefuuuuuu kila siku lawyer anataka pesa na Mange pia hapo ntakupiga counterclaim ya uongo na kweli ili kesi iweeee ndefuuuuu , so kesi utakuta inaenda miaka mpaka mwisho uta give up wewe, waulize mastaaa waliompeleka Shigongo mahakamani kama kuna alieweza na huku Tanzania ina law ya defarmation ya magazeti. Mbona hawamuwezo Shigongo? coz anapesa atakupelekesha kesi inakuwa ndefuuuu mpaka utaacha mweneywe. So hii law wamejiwekea wenyewe viongozi wetu wenye mahela yao ya kuweka lawyer mzuriiiiiiii….

Ni hivi January, Ridhwani na wabunge wengine wa CCM mliotutia aibu wana CCM wote kama Sophia Simba , YOU CAN'T HAVE YOUR CAKE AND EAT IT TOO..(ila Sophia Simba tumsamehe maana ni mzee labda hajui hata kufungua email maskini ukute kaambiwa na kina JAnuary kwenye internet kuna uchawi mtu akiandika chochote about you online kina come true so she should vote YES, simnajuwa wamama wa zamani kwa kuamini uchawi hahaha) Mnataka kua maraisi na mawaziri na hapo hapo hamtaki kukosolewa? it doesnt work like that. you cant have it both ways, kama hamtaki kutukanwa au kusemwa then achieni ngazi ingieni uraiani muone kama kuna mtu atakuwa na time na nyie. ILA kama mnataka uongozi msitake kutufanya mambumbumbu mtuongoze bila sisi kuwasema yani mtupelekeshe tu……

As long as mnataka madaraka vumilieni maneno na matusi … IT'S PART OF THE GAME…..Vya uongo, vya ukweli vumilieni kama hamuwezi kuhandle scrutiny acheni ngazi wenye vifua vya maneno kama kina Mange hapa tuingie madarakani, ahhahahahha uwiii mie mbona ntawawekea na blog ya haters ya kunitukana ila na mie ntataka kuwa na yangu ya kuwajibu maaana sijuagi kukaa kimya…….ahhahahahahhahahahha….. Yani hii sheria yenu ya kipumbavu eti sasa hivi inampa power Wema Sepetu kumpeleka mahakani mimba za majanini kwa kuachia comments za kumsema vibaya pamoja na mwandishi wa hizo comment, hivi does that make sense?

Ynai kweli does it make sense kuwa Wema awe involved na mascandal kila siku mahot hot news ila chombo chochote cha habari kisiandike story ya Wema au kwueka picha ya wema au kuandika jina lake kwa story ambayo mwandikaji hawezi kwenda kuiprove in court iwapo Wema akiamua kumfungulia kesi. Hivi does that even make sense kweli????? KHA!!! Na wachangaiajia kama kina C's mum waliotuma comments za kumuta wema Malaya na tasa basi waende mahakami kuprove kuwa Wema ni tasa na kweli ni Malaya na as long as the comment ipo hewani inasomwa kwa siku zinazidi laki 7….ahahahhha….----- MTUPU…..

Jamani Im about to be team Lowassa Although ameshafanya makosa mengi ila I think he deserves a second chances . Na wahenga wanasema shetani unaemjua hatokusumbua. Bora huyu babu tunamjua weakness zake na strength zake ila hawa vijana wadogo ambao bado hawana busara hapana aiseee. Also lowassa keshatulia pesa zetu za kutosha na keshatajiri sidhani kama tukimpa nchi atatumaliza zaidi atatuonea huruma na pia atakuwa makini coz keshaonja jito ya jiwe ila hawa vijana ambayo ndo wanatafuta utajiri bado tutalia nao nawaambieni….

JAMANI I HOPE NO ONE WILL TAKE THIS PERSONALLY, NAIPENDA NCHI YANGU NA SIPENDI UONEVU NDO MAANA NIMEONGEA.

PS: Uwiii vidole vimepinda kwa kutype jamani…. Ngojeni nikapumzike…hahahha…Siweki any update for 2 days ili wote tuweze kuchangia hii topic… Changia kwa raha zako RAISI bado haja sign hiyo sheria….andika chochote unachowaza…


SHERIA YA "SHUT-UP TANZANIA" BADO HAIJASAINIWA NA RAISI
 
ana influence sana kwenye jamii hasa kwa watoto wa kishua wenzie ana watu kama 2000 nyuma yake
 
Lets hope so...ila kama mtu ni mfuatiliaji wa masuala ya kimataifa utajua kuwa donors hawana role kihiiivyo unless umeshikilia maslahi yao...
Kwa hili la kuiweka nchi under surveillance sidhani kama hawajalipenda...mfano US mawasiliano binafsi kwa mtandao hayana usiri anymore...na wangependa nchi nyingine ziwaige ili waweze ku control ugaidi...

Kama bill ni mbaya ni watanzania pekee ndio wa kutegemewa kuikataa...lakini sasa wabunge wetu walikaa kimya wakamwachia Mh Lissu peke yake ajibizane na serikali...
Nsichojua ni uelewa wao au ni kweli wameamua kuitosa nji hii...?

Angalia tu hiyo heading ya The Citizen ndio mtajua kama wanatoa amri au wanajisafisha ili wasije lalamikiwa siku za usoni kuwa walikaa kimya...

Usijeshangaa bill yenyewe imetokana na influence ya donor fulani...ingawa wao wameamua kui extend na ku cover vitu ambavyo hata si vya msingi...
 
Bahati mbaya zaidi wanaosema kuwa bill ni mbaya nao ni kati ya watu walio mstari wa mbele kutukana na kudharirisha wengine!

Kwenye hili bandiko nilitegemea kuona Mange angeonesha japo kwa kiasi kidogo uzuri wa huu muswada! Pamoja na huu muswada kuwa na mapungufu hasa lakini si mbaya kiasi hiki watu wanacho jaribu kuonesha!

Hata hao wazungu hakuna cha siri kwenye data kila kitu cha mtu yeyote wakikihitaji wanakipata...kwa hiyo swala la kusema tutanyimwa misaada kwa sababu ya huu muswada sidhani kama ni kweli!
 
Hatuwezi kunyimwa misaada...
Na hawana ubavu wa kuikemea Tz wakati haya mambo wame copy kwao...

Tatizo ni hapo kwa 'kichaa kupewa rungu'
Tutaweza kuitumia hiyo sheria responsibly au kuficha maovu na kutishana????

Dunia hii ya leo imevurugwa na hao hao so called donors...

Bahati mbaya zaidi wanaosema kuwa bill ni mbaya nao ni kati ya watu walio mstari wa mbele kutukana na kudharirisha wengine!

Kwenye hili bandiko nilitegemea kuona Mange angeonesha japo kwa kiasi kidogo uzuri wa huu muswada! Pamoja na huu muswada kuwa na mapungufu hasa lakini si mbaya kiasi hiki watu wanacho jaribu kuonesha!

Hata hao wazungu hakuna cha siri kwenye data kila kitu cha mtu yeyote wakikihitaji wanakipata...kwa hiyo swala la kusema tutanyimwa misaada kwa sababu ya huu muswada sidhani kama ni kweli!
 
Back
Top Bottom