Sella turcica
Senior Member
- Oct 13, 2020
- 104
- 193
Kila jambo huwa na zama zake. Kwenye mpira ni hivyo hivyo, clubs hutamba na kupotea. Zama za Man U na Chelsea zimekwisha. Tangu SAF aondoke man u haijafanikiwa kushinda taji la EPL. Usinambie shida ni budget, maana wamiliki wanatoa mpunga wa kutosha tu. Hali kadhalika ndugu yao Chelsea nae yuko hoi. Wametumia pesa nyingi sana kufanya usajili lakini hamna kinachoonekana.
Njoo kwa Man city. Tangu Sheikh Mansour aichukue timu mwaka 2008 wamekuwa wakipiga hatua kwenda mbele. Walitamba kwenye EPL ila kipengele ilikuwa kutamba kwenye UEFA. Wamemvumilia Pep kwa miaka 7 ndipo wakafanikiwa kupata taji la kwanza la UEFA.
Siwezi kuisifia zaidi ila ukweli usemwe kwa sasa man city ni team ambayo inaendeshwa kisasa na kwa weledi. Angalia sajili zao, wachache sana ndo wanashindwa kuonyesha makali kama kina Kalvin Philips. Wengi wao wanafanikiwa kuonyesha potential zao. Fikiria mtu kama Akanji au Alvarez; ni watu walionuniliwa kwa pesa ndogo sana, less than 20 M euros, lakini shughuli zao uwanjani zinaonekana.
Kuna huyu bwana mdogo Doku, amenunuliwa kwa euros 55 M lakini mziki wake mjana mmeuona. Grealish huko aliko anaogopa. Sasa njoo angalia man u walimchukua Anthony kwa euros 85 M lakini anachofanya ni kupiga watu mabuti. Chelsea walimchukua Mudryk kwa 100M euros ila hajaweza kudeliver. Kwa sasa mchezaji kukataa kwenda man city ni sawa na kupishana na gari la mshahara. Harry Kane anaelewa vizuri hili. Nina uhakika city wangempata Kane basi huenda jamaa angetwaa Ballon D’or.
Mchezaji anaweza kuwa mzuri ila akienda Chelsea au man U mnamkataa kabisa. Zile timu ni kama zina gundu hivi.
Arsenal japo wanajitahidi ila bado, hawajafika kwenye levels za kushindania makombe. Mpinzani wa Man city ni Liverpool. Na timu zisipokaa vizuri Pep anabeba tena ile ndoo. Pep anaufanya mpira uonekane rahisi sana. Wapinzani wake wanajaribu kusema anapewa hela za waarabu, wakikumbuka timu zao nazo zimesajili wanaamua kunyamaza. Kama wewe kweli ni mpenzi wa soka safi huwezi kukosa kuangalia game za man city. Tuenjoy zama hizi kabla hazijapita.