Mambo yenye huzuni kubwa duniani

Jul 31, 2022
45
98
1. Kusema "Kwaheri"kwa mtu unayempenda sana.

2. Kumuona unayempenda akifariki mbele ya macho yako.

3. Kumuona mama yako mzazi akilia kwa uchungu.

4. Kumuona baba yako akiteseka kulitafutia "ADA"ili akulipie wewe.

5. Kumpoteza rafiki/ndugu kwa ajali au ugonjwa fulani.

6. Kubezwa au kukandamizwa kwasababu ya Ukanda,ukabila,rangi ya ngozi,ulemavu,Jinsia au Dini.

7. Kuwaona wazazi wako wakiteseka kwa ajili ya kujiinua wewe.

8. Kuhukumiwa na mtu au watu kutokana na ulichokifanya zamani.

9. Kubakwa au kulawitiwa na watu wako wa karibu ambao usingetegemea.

10. Kuwaona watoto wako wakiondoka nyumbani na kuishi maisha yao wenyewe.

11. Kulaumiwa kutokana na maamuzi yako uliyofanya maisha yako yote.

12. Kuua ndoto zako kwa ajili ya kumfurahisha mtu au watu.

13. Kupoteza au kukosa namna ya kutumia kipaji chako na huku akiishi maisha magumu ya kimbuzimbuzi.

14. Kutofikia malengo,ndoto na matamanio yako ukiwa kitandani hujiwezi tena.

15. Kushidwa kutoka katika uraibu au utegemezi wa dawa za kulevya,pombe na sigara.

16. Kumaliza chuo kikuu na kurudi mtaani kwenu bila kupata kazi kwa muda mrefu.

17. Kupoteza vyeti,wallet au pochi yenye vitambulisho vyote.

18. Kufiwa na mtoto wako au kufariki kwa mke/mpenzi wako.

19. Kuitwa majina ambayo huyapendi lakini ni halisi Mfano "Malaya wewe" au "Mwizi" "Mlevi" "Tasa"

20. Kushindwa uchaguzi uliokugharimu au kushidwa kesi na kupoteza haki yako.....Ni huzuni kubwa!!

Unaweza kuongeza nyingine....

Dokezo!!
Maisha ni kitabu,usichoke kufungua kurasa zako.Kitabu cha Safari ya maisha kina furaha na huzuni.Huzuni isikufanye ukate tamaa.Hakikisha unavuka kwa kutokubali kukata tamaa au kukatishwa tamaa.Mshirikishe Mwenyezi Mungu na watu sahihi ambao wanaweza kujutia moyo na kukupeleka mbele na hatimaye kupata mpenyo.

Huzuni haidumu ipo njia ya kutokea.Kumbuka wakati wote tembea juu ya huzuni zako kwa furaha pasipoti kubaki chini.Utaweza kuyamudu maisha.


Kura yako ni muhimu.
Asante.
 
Back
Top Bottom