safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,169
- 15,851
Kama kweli furaha inatokana na kitu fulani ambacho unakihitaji jee kwa nini baada ya kupata kitu hiko bado kuna vitu vingine vitakukosesha furaha na kukutia stress ?
Yaani utajikuta umepata mtoto tayari,lakini kodi ya nyumba inakunyima raha
,je ni ipi faida ya furaha ya mtoto kama furaha hiyo haiwezi kuondoa hata huzuni ya kudaiwa kodi ya nyumba ?
Ni ipi faida ya furaha ya kuwa na gari kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kazi nyingi ofisini ?
Ni ipi faida ya kuwa na furaha ya kupata nyumba kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kipato kidogo ?
katika haya maisha hicho unachodhani ukikipata kitakupa furaha sio kweli.
FURAHA YA KWELI NI ILE AMBAYO INAKUONDOLEA HUZUNI UNAYOIPATA KATIKA VITU VINGINE.
furaha unayo mwenyewe na wala haipo kwenye vitu unavyovihitaji Kama vile watoto,pesa,nyumba n.k.
Unaweza kutamani gari,ukalinunua na siku za mwanzo ukawa na furaha sana na upya wake.
lakini masiku yakikatika unaliona gari la kawaida hivyo halikupi tena furaha kama ile ya mwanzo,imeenda wapi furaha ile ?
vitu ambavyo tunategemea vitatupa furaha tukishavimiliki tu baada ya masiku kadhaa tunaviona vya kawaida na havitupi tena furaha.
Nilitamani sana kuoa na siku ya kuoa nilikuwa na furaha sana,lakini leo hii sijui furaha ile imeenda wapi na ndoa bado ninayo.
Nilitamani kuwa na mtoto,nilipopata mtoto nilikuwa na furaha sana.
leo mtoto ninaye lakini sijui ile furaha ya mwanzo ya kuwa na mtoto siioni tena na mtoto bado yupo.
Hakuna kitu chochote ambacho ni chanzo cha furaha kwenye maisha yetu isipokuwa sisi wenyewe.
SULUHISHO.
FURAHA TUNATAKIWA KUZITENGENEZA KAMA AMBAVYO TUNATENGENEZA CHAKULA,MAGARI AU NYUMBA.
KUITENGENEZA FURAHA.
furaha tunaitengeneza kwa KUSHUKURU na kutafakari faida ya kitu hicho.
Utakapotafakari faida unazopata kwa kitu fulani na kushukuru basi hapo ndipo furaha utaiona.
Ukiamka asubuhi unaenda kazini kwa daladala sawa hauna gari jee umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa daladala kwako na ukasema asante Mungu..?
Umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa macho yako kwa namna unavyotumia na ukasema asante ?
Je miguu,masikio,pua,mdomo umeshawahi kutakarai kwa ucahche umuhimu wa hivyo vitu kwako kwa namna unavyovitumia ?
Bila kuwa na utaratibu huo utajikuta unaamka kila siku uko bored,hauna mood,hauoni kitu kipya katika dunia na utaanza kudhani kwamba furaha yako kuna sehemu imejificha.
Ukweli mchungu ni kwamba hapa duniani kila kitu sisi ndio tuntengeneza,hata furaha tunatakiwa tuitengeneze wenyewe.