Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Foleni za DAR ZIMEPUNGUA SANA,toka jumatatu hadi leo thursday nimegundua natumia muda mfupi sana ktk foleni za barabarani,
kwa udadisi wangu foleni zimepungua kama inavyokuwa kipindi cha December foleni dar huwa zinapungua sana. naona watu wameenda loliondo.

kama ni hivyo basi watu wa Dar wengi wetu ni wagonjwa wa magonjwa Sugu,inatisha kweli kweli


Bei ya mafuta mkuu!...litre moja buku mbili si mchezo!...safari za kipuuzipuuzi inabidi ufikirie mara nne nne kuzifanya au la.
 
WABONGO jamani wana bongo, kumbe wengi spana mkononi!

Nimeamini kabisa kwamba usianzishe ugomvi ukapigana unaweza kuua. Karibu Wabongo wote ni wagonjwa, ukitaka uthibitisho mwulize Babu wa Loliondo.

Msururu ule wa wazee, vijana, wanawake kwa wanaume, kwenda Samunge ni uthibitisho tosha kabisa, kwamba tulikuwa tunajikausha tu kumbe iko gonjwa.

Vigogo na masikini, sooote maselule tupu. Kikombe cha Babu kimetutanabahishia kuwa kumbe ni ujanja tu, hatuna kitu, nani atabisha kuwa hajakanyaga miwaya, lakini akifika kwa Babu anasingizia kisukari? Wapo wengi wa aina hiyo, tunashukuru Babu hapimi.


Na kama Babu angekuwa na hadubini za kupimia virusi, naamini Wawa Lali asingepiga marufuku haya mapaparazzi kumuhoji na kumpiga picha Babu, kwa sababu hata hivyo nani angejipanga msururu ule kupimwa ngoma? Thubutu!

Watu wanasepa hospitali na kukimbilia kwa Babu, watu wanalipa maelfu kwa maelfu kukimbilia kwa Babu, watu wanakodi helikopta kukimbilia kwa Babu.

Lakini Babu hajui nani ana ngoma, nani ana kisukari wala nani kaoza ini au figo. Fomula ya kikombe ni kupata kaujaze tu na kubwia na kujiondokea, yote yatafanyika kwa imani uliyonayo, ukipona sawa, ukidhani umepona shauri yako na Mungu wako a.k.a. Babu au Kikombe.

Songombingo linaloendelea kuonekana Samunge linatuthibitishia na kutudhihirishia, kuwa hakuna aliye tayari kufa, ingawa hakuna aliye tayari pia kugoma kwenda mbinguni, ingawa daladala la kumfikisha huko ni kifo na hakuna anayetaka kulipanda.

Mimi najiinamia na kujiuliza kwa mshangao, hivi ina maana hospitali sasa hazifai?

Hivi ina maana utafiti unaofanywa na wataalamu wetu haufai na uachwe? Hivi kweli tiba ya Ukimwi imepatikana Loliondo?

Hakuna sababu ya insulini tena hata kwa wazee kama wa Kiraracha? Kama tumefika huko ya nini sasa akina Katotoizi wanamshambulia Babu na kutaka asiwadanganye Wabongo kwa kikombe chake!

Eti wanasema anawadanganya na wala hana tiba ila wao ndio wana tiba ya Neno na si Kikombe. Ina maana upako ni bora kuliko kikombe cha Babu?

Twambieni nasi tujue ukweli wa haya, kwa sababu hata Babu anasema kunywa huku ukiamini, badala ya kunywa ili upone tu bila kuamini.

Maana yake ni kwamba hata ukikamua maji ya mpapai na kunywa huku ukiamini utapona ngoma.

Sijamsikia Ndodi naye anasemaje kuhusu haya kwa sababu naye kila siku namwona na kumsikia akihamanikia tiba yake.

Lakini kinachojionesha dhahiri ni kuwa Babu kawapiga bao wote hao wanaotibu kwa njia zao tofauti, wale ambao walijaza masinagogi kuwaombea walemavu na wasioona, sasa wanaambiwa kutesa kwa zamu.

Hii ni zamu ya Babu kutesa na dala lake la kikombe. Najua wataibuka wengi kufuata nyayo za Babu, lakini wajue kuwa huyu kaoteshwa kutibu magonjwa sugu na ndicho anachokifanya, ingawa utaalamu mh mh!

Wapo walioibuka wengine wakisema jamani nendeni kwa Babu lakini angalieni na utaalamu wa kidhungu! Bugia dawa ya Babu, lakini usisahau kuwa hospitali nazo zipo kukutibia na kumbuka pia kuwa tiba isiyo na utafiti nayo ni zigo kwako!

Tutakunywa vikombe na vikombe, na kujiliwaza, lakini siku ikifika imani ikakutoka ukamkashifu Babu, ndipo sasa madonda yatakapokutoka sidifoo nazo zikushuke na ulishatoroka hospitali, na eiaravii ukazitupa jalalani, ndipo utalia kilio cha mbwa.

Babu katukosea moja tu, angeweka kitabu cha usajili wa wagonjwa na kuwapiga picha zao nasi kuzitundika mbaoni na magazetini, ili tuwajue hao wanaosambaza virusi kwa ndugu zetu kutokana na ukwasi walionao na kuwachukulia hatua.

Au kutusaidia zaidi Babu angekuja na kikombe ambacho kinawagundua wenye virusi na roho mbaya ya kuvisambaza, ili mtu wa aina hiyo akishajipigia kikombe chake tu chali, kikombe kinajichukulia sheria mkononi, yaani kikombe chenye hasira kinamwua.

Hapo hakuna kesi, kwa sababu hata wananchi wenye hasira (walioumbwa nazo) wanapoamua kujiulia mtuhumiwa wao, huwa kunakuwa na vijikesi uchwara tu na kuachiwa kudunda mtaani, kwani huwa wamesaidia kupunguza uhalifu kijijini au mtaani, ndiyo PJ hiyo. Kama huijui niulize.

Hongera sana mjasiriamali nambari wani, Babu, huo ndio ubunifu endelea kutubunia na mengine na mengine zaidi, ili siku moja tupate kikombe cha akili ili watoto wetu wasifeli tena fomu foo kama mwaka huu.

Lakini kuna mshikaji anahoji hivi: “Siku Babu akisema 'ameoteshwa' na Mungu kuwa wale wote waliokwenda kwake na kupata dawa kisha kupona, wanatakiwa kurudi kwake wakiwa na Sh 100,000 na asiyefanya hivyo atakufa ndani ya siku saba, wewe na Serikali mtafanyaje? Alamsiki. Niko nje hapa nasubiri zamu ya kikombe, kinasuuzwa kwanza. (JK).
 
Wakuu nmekuwa nikiyafikiria yale magari yenye atm ya crdb mara nyingi yalikuwa yakipaki pale mlimani city au sabasaba cku izi siyaoni tena. Kwa mtazamo wangu ingekuwa vema sasa yakatumika pale kwa babu loliondo ktk kurahisisha utata wa huduma za kijamii pale semunge.Dr Kimei na dada Tully mwampamba please advice km inawezekana tupieni hiyo kitu pale kati. Nawasilisha
 
Wagonjwa wakwama porini Loliondo Send to a friend Sunday, 20 March 2011 21:37 0diggsdigg


mch%20mwasapile%20loliondo.jpg
Mchungaji Ambilikile Mwasapile

Mussa Juma, Arusha
MAMIA ya wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, ambao walikuwa wanakwenda kupata matibabu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile wamekwama njiani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana na kuharibu barabara.
Barabara ya kwenda katika Kijiji cha Samunge aliko mchungaji huyo inayochepukia eneo la Kigongoni na Selela, Engaruka na Ngaresero, sasa haipitiki kutokana na kuharibika.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema jana kwamba kuharibika kwa barabara hiyo kumesababisha mamia ya wagonjwa na jamaa zao waliokuwa wakielekea Samunge kukwama porini hivyo kukosa huduma muhimu za kijamii ikiwamo chakula na hata usalama wao. Kutokana na hali hiyo, amekiomba Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu, kuingilia kati na kufika eneo hilo kutoa msaada... “Hali ni mbaya sana. Idadi ya watu sasa ni kubwa kuliko kipindi kingine chochote”

Lali aliwataka viongozi wa mikoa inayopakana na wilaya yake kuweka udhibiti wa watu wanaokwenda Samunge kutokana na uharibifu huo wa miundombinu... “Nawaomba wadhibiti watu hadi hawa waliokwama na waliopo Samunge watakapopungua.”

Kukwama kwa wagonjwa hao, kumekuja takriban siku tatu tangu, Mchungaji Mwasapile alipoiomba Serikali kuharakisha kukarabati barabara hiyo akihofia kukatisha mawasiliano ya kumfikia.
Magari mbalimbali ya abiria yakiwapo mabasi na mengine madogo ya kukodi yamekwama kati ya Vijiji vya Engaruka na Ngaresero na hivyo kutishia afya za wagonjwa wengi.

Mmoja wa madereva waliofanikiwa kupita katika njia hiyo, Jonathan Mrema alisema Serikali isipokarabati barabara hiyo sasa, wagonjwa wengi watakwama hata kupoteza maisha.

Alisema kutokana na ubovu wa barabara hiyo na hivyo wagonjwa kukaa muda mrefu kabla ya kufika kwa mchungaji huyo, amewashuhudia wanne waliofariki dunia juzi na jana.“Watu wanakufa barabarani. Hali ni mbaya sana tunaomba Serikali ikarabati barabara hii japo kwa kiwango cha changarawe,” alisema Mrema.

Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya kukodi magari yanayokwenda Samunge, Saidi Kakiva alisema kutokana na barabara kuharibika nauli zimepanda kwa kiwango kikubwa.“Tunaomba Serikali iwajali hawa wagonjwa. Sasa gharama ya usafiri imefikia kati ya Sh120,000 na 150,000 kwenda na kurudi wakati bei ya awali ilikuwa ni kati ya 35,000 na 80,000,” alisema Kakiva.

Jijini Arusha, nyumba nyingi za kulala wageni zimejaa wateja wengi wakiwa ni wagonjwa na jamaa zao ambao wanataka kwenda huko Samunge Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile.

Baadhi ya wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali nchini wamelazimika kuhifadhiwa katika hospitali na vituo binafsi vya afya wakisubiri usafiri wa kwenda Samunge ambao umekuwa mgumu baada ya baadhi ya magari yaliyokuwa yakiwapeleka kusitisha huduma kutokana na ubovu wa barabara.

Tangu kuanza kutolewa kwa tiba hiyo ambayo imewavutia wananchi wengi wakiwemo viongozi waandamizi wa Serikali, wanasiasa, wananchi na watu wa mataifa mbalimbali, kumekuwa na kilio cha huduma za jamii na miundombinu vitu ambavyo vimekuwa vikikwamisha upatikanaji wa huduma hiyo.
 
...... Tatizo wajinga ni wengi na wazushi ni wengi pia ! ukicheka nao, wamekutia katika ukafiri

Hapa tunajadili uhusiano wa babu na biblia. Je hujifunzi tu kuwa ukristu unaruhusu kupima maandiko na hivyo kutoa uhuru wa mawazo? Try islam and you know what to expect. Yuko wapi Salman Rushdie na yule farmous Danish cartoonist? Uko wapi uzushi? Think, act.
Jesus saves.
 
Mkuu umetibiwa ugonjwa gani ukapona?maana ile si kinga!tujuze after check up hospital

Hapana sijaenda ila nimeshuhudia kupitia kwa jirani yangu!! Hicho ndicho kilichonifanya niufikirie sana ile dawa ya babu na nikaamini kuwa hiyo ni damu ya Yesu Kristu!
 
Ni kweli uponyaji wa Mungu hauhitaji malipo yoyote ya kifedha lakini kama Babu anawatuma vijana kwenda milimani kutafuta hiyo dawa atawalipa na nini. Suala ni je babu anazifanyia nini pesa hizo. Katika Biblia kuna mistari inaongelea kutoa sadaka na ni 10% ya kipato chako.

Babu hachukui hela nyingi yeye anachukua sh mia tu, 200 zinaenda kanisani na 200 za kuwalipa wale watu wanaomsaidia kuchemsha dawa na kutafuta dawa porini.
 
Mungu wa wapi huyo mwenye style moja tu uponyaji, mpaka watu wakachume dawa!! Come on! I cannot reduce the creator of this world to dawa ya mti, hiyo hiyo for the whole country.

Mifano ya uponyaji tunaipata kwa Yesu, alikuwa anademonstrate how rich God is kwenye uponyaji, sio namna moja kwa kila mgonjwa...That's why i am led to believe kuna mungu kamtuma kufanya hivyo lakini si Mungu the creator of this world. He is not that little.

Huwezi kujua kwanini Mungu kaamua kutoa uponyaji wa dizaini hiyo, unaweza ukaniambia kwanini Mungu kachagua njia hiyo ya uponyaji?
 
Jipeni moyo tu ,ooh Hiyo ni damu ya yesu-mtishamba ni damu ya yesu. mauti inawakaribia taratibu poleni sana enyi wenye shingo ngumu.

Mnashindwa kumtafuta mungu wa kweli awafunulie ju ya hiyo huduma,mmekezana tu kibabu,jamani sio nguvu ya mungu,ni roho nyingine hiyo. watu wataanza kufa taratibuuuu!
 
Mkuu umetibiwa ugonjwa gani ukapona?maana ile si kinga!tujuze after check up hospital

Ndio maana watu hawataki kushuhudia kupona, maana hamuishi kuwauliza ugonjwa gani?
Kwanini unautaka ugonjwa wa mwenzio yeye kapona .
Babu kaanisha magonjwa yanayopona nenda ukapate kikombe
 
like it....very constructive idea. have said it well
Kubenea kachemka, tatizo habari zake zingine huwa hazifanyii utafiti wa kutosha! A little home work would have made him come up with a very nice and constructive article, but this was just another crap from him.
 
Huwezi kujua kwanini Mungu kaamua kutoa uponyaji wa dizaini hiyo, unaweza ukaniambia kwanini Mungu kachagua njia hiyo ya uponyaji?

ni wavivu wa kusoma maneno ya Mungu pekee ndio huja na kauli kama hizi. Mungu kafunua kila kitu kwenye neno lake

Glory to God
 
I think you guys are wrong and not sure which world are you belong to!!! The Babu in Loliondo is not doing any business and for that case there are no grounds which could be used to tax him. What he is collecting ni sadaka kama sadaka ya makanisani au misikitini which is also not taxed? By the way which tax were u guys proposing??? VAT, PAYE, Excise, Import, Withholding, Stamp duty, Skilled levy, Corporate?????

JE MAKANISA NA MISIKITI WANALIPA KODI?

You may be right if "Babu" was registered as a church institution, unfortunately, he is not registered; instead he is trading in natural heberlist which means he has to be given TIN Number and Pay corporate tax at individual income taxrates. Also if heberlist is not VAT exempted, he as also to registered with VAT so that each customer pay TShs. 90 above TShs 500 to the Government since his three months' collection exceed 10 million. Government is spending a lot of money to put infrastrure in good order therefore anybody going there should contribute TShs 90 in terms of VAT.
 
Mkuu uko ulimwengu gani wewe, enzi za ukiritimba ilikuwa hivyo sasa hivi ni biashara huria ndio maana unaona mabenki yanajitahidi kufuata watu katika makazi yao na sehemu zenye vyanzo vya pesa.
Kwa wachumi pale kwa babu kunafaa kuwa na agency kwani kunabiashara ya benki tosha. Watu wanaenda kule wanaishiwa wangeweza kusaidiwa kupa t hiyo huduma.
Pia babu vijisenti anavyopata na wafanyakazi wake wangeweza kuwasaidia kuhifadhi kibenki.
 
Back
Top Bottom