Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

shiumiti

JF-Expert Member
Jun 4, 2009
435
19
Mafuriko ya watu (weusi na weupe) na misururu ya magari kuelekea kwa babu LILIONDO kwa matibabu!!!!!!.....
 
Attachments

  • zzKUNDI NA WAASIA NO 1.JPG
    zzKUNDI NA WAASIA NO 1.JPG
    17.1 KB · Views: 949
  • zzmagari wakinywa dawa.jpg
    zzmagari wakinywa dawa.jpg
    21.1 KB · Views: 1,037
  • zzzMAMA SHERIA 2.JPG
    zzzMAMA SHERIA 2.JPG
    12.8 KB · Views: 974
  • zzPICHA MAGARI.JPG
    zzPICHA MAGARI.JPG
    19.8 KB · Views: 932
Aiseeee!!!:A S 13:Watu wengi kweli!!Babu wa watu hata hapati kupumua!!!
 
ndugu watu wanye matatizo wapo wengi sana, alafu watu wanabeza eti haiwezekani, hivi kuna kitu kinachomshinda YESU....?? matokeo yake hadi maustaadhi watu wangu wameenda kwa imani watapona na wamerudi kuwashuhudia wenzao, ukienda huko hadi helkopta za matajiri wa kiarabu zinaenda....Kama unamatatizo nenda acha ubishi usio na maana by the way yeye mchungaji a.k.a babu hana anachopungukiwa, hakutangaza magazetini wala redioni ila watu wenyewe wamekua wakiwashudia ndugu zao.....

to god b the GLORY
 
Maajabu ni kwamba, unakunywa kikombe kimoja cha tu cha dawa ambacho ndo kinagharimu Tshs. 500 tu....na mara moja dawa inaanza kufanya kazi. Uruhusiwi kunywa mara mbili..... KWELI DUNIA IMEPETA MKOMBOZI.... TUSUBIRI MPAKA WAZUNGU TOKA ULAYA WATAKUJA...NGOJA TUONEE.!!!!!!!!
 
Mhhh!!!
Huyo babu anatakiwa kuapply demand na supply theory....demand ni kubwa sana, inabidi apandishe bei ili aweze hata kutengeneza mazingira ya kituo chake!
 
Ningekuwa mimi babu naanza na watz wenzangu hao gabachori baadae!!
halafu nilidhani mie tu nina matatizo nilipoona hizi picha naanza kufarijika kuwa sipo peke angu!!
 
Nahisi karing cha udinidini kwako bro? Kweli Yesu hashindwi kitu na ndio maana Tanzania vilema wamepunguwa kutokana na uokozi wa Yesu.
 
Kwani Huyo mbabu anafanya nini? Maombezi au uaguzi?
 
Maajabu ni kwamba, unakunywa kikombe kimoja cha tu cha dawa ambacho ndo kinagharimu Tshs. 500 tu....na mara moja dawa inaanza kufanya kazi. Uruhusiwi kunywa mara mbili..... KWELI DUNIA IMEPETA MKOMBOZI.... TUSUBIRI MPAKA WAZUNGU TOKA ULAYA WATAKUJA...NGOJA TUONEE.!!!!!!!!

ndoto za alinacha!
 
Inamaanisha hao wote waliopo kwenye hio foleni wameathirika na VVU? Duuh tutapona kweli?

Manake nasikia moja ya sharti ya dawa zake lazima uende physicaly, hakuna kumchukulia au kumbebea mtu kwa niaba.
 
Where is the government?, wapeleke JKT au waombe RED CROSS wajenge mabweni ya kujikinga na mvua.
 
Ningekuwa mimi babu naanza na watz wenzangu hao gabachori baadae!!
halafu nilidhani mie tu nina matatizo nilipoona hizi picha naanza kufarijika kuwa sipo peke angu!!

Hao unaosema "gabachori" pengine ni wa Tanzania zaidi yako! Kipi kilichokupeleka kujiona kuwa wewe ni mTanzania zaidi yao? Rangi zao?
 
Aisee babu ana kazi sana kuhudumia umati huo.... Atakuwa halali kabisa!!
 
Jamani sio Loliondo bali ni wilaya ya Ngorongoro mkoa wa Arusha! Loliondo hufiki huko! Lakini yote 9 kweli babu anatibu mimi mwenyewe nimerudi kutokea huko na kwa sasa hivi huwezi kutabiri kua unakwenda huko leo urudi kesho unachotakiwa kujiandaa ni kua uwe na muda wakutosha watu ni wengiii mno inaweza kukuchukua hata wiki mbili ili upatape huduma nimekutana na watu ambao wanamaliza wiki sasa na bado hawajapata huduma.
 
Wizara ya Jamii, Wanawake na watoto iingilie hii huduma na kuratibu kuanzia idadi ya watu wanaolelekea huko. Au wanaoenda huko siyo sehemu ya Jamii inatakiwa kuhudumiwa na hiyo wizara?
 
Aleluyah!

Nimekuwa nikitafakari sana kuhusu huyu Babu wa Loliondo na nguvu alizo nazo za kuweza kuponya maradhi mbali mbali ambayo ni sugu hapa duniani. NIkianza kutafakari neno la Mungu ambalo linasema siku za Mwisho watakuja Manabii wa uongo soma Mathayo sura yote ya 24.

Nimeona watumishi wengi wa Mungu ambao wamekuwa wakitumia Neno la Mungu kufunika matendo yao magumu na ya kichawi tukiambiwa kuwa hawa ni watu wa Mungu. Lakini baada ya Muda imedihirika kuwa ni nguvu za kishirikiana zimekuwa zikitumika. Utakumbuka kuwa Paulo alimtoa pepo mama mmoja ambaye alikuwa ni mjakazi wa mtu ambaye kwa kutumia hilo pepo lake la utambuzi alikuwa akitumika kuagua watu na Mabosi wakewalifaidika sana kimapato kwa kumtumia yeye ingawa yeye alikuwa hafaidiki zaidi ya kuwa mjakazi, na pale paulo alipolikemea na kutoka ikawa ndo mwisho wa mambo ya utabibu wake.

NI kweli nina uhakika kuwa Huyu alikuwa ni Mchungaji kule Imiti babati na leo hii amepewa nguvu za kuweza kutibu magunjwa kwa kutumia dawa ya mizizi. Sasa swali langu ni kitu gani kinachozuia yeye kufanya kazi sehemu nyingine yoyote nje ya eneo lake, je ni kwaninini hiyo dawa lazima akupe yeye kwa mkono wake mwenyewe?
Hii inanipa nafasi ya Kumtafakari pia Mtumishi mwingine aliye kuwa Mchungaji na baada ya kwenda Huko NIgeria na kurudi alirudi na upako wa ajabu sana amabo akikunyooshea mkono tu unaanguka na aliponyesha watu wengi sana lakini siku za hivi karibuni amepoteza umaarufu wote baada ya kujulikana kuwa natumia nguvu za giza kutekeleza hayo yote.

Leo hii natafakari jinsi watu wanavyo kwenda kwa wingi kutoka mikoa yote ya Tanzania na nje ya Tanzania sehemu ambayo haina miundo mbinu na si ajabu leo ukasikia magonjwa ya mlipuko huko Loliondo. Jana nimepewa taarifa kuna Msafara wa magari km 50 wanasubiri huduma hiyo.

Mimi sitaki kumkani huyu babu kwamba yeye ni wa Mungu lakini Neno la Mungu linasema tuzipime hizo roho.

rai yangu watu wa Mungu nisaidieni niweze fahamu ninyi ambao mmesha zipima hizo roho je ni kweli huyu ni mtu wa mungu na siyo anasaidiwa na Mizimu ya mahalia na ndiyo sababu hawezi amishia huduma yake sehemu nyingine? Na hivyo mizimu hii imekuja kwa Sura ya Malaika wa Nuru.

Nisaidieni kwani mimi ni mchanga kwenye Imani nahitaji msaada. Wasi wasi wangu isije kuwa tunakwenda kwa Mganga wa Kienyeji tukuifikiri ni mtu wa Mungu, yaani nalataka ni watu wajue kuwa ile ni nguvu ya Mungu au la ingawa inaponya.

Nawasilisha
Mungu awabarikLi sana!
 
Inamaanisha hao wote waliopo kwenye hio foleni wameathirika na VVU? Duuh tutapona kweli?

Manake nasikia moja ya sharti ya dawa zake lazima uende physicaly, hakuna kumchukulia au kumbebea mtu kwa niaba.

Jifunze kusoma kitu kukielewa kabla hujajibu,

Siyo VVU tu magonjwa sugu, kisukari, kansa nk.
 
Teh teh, wenye mahospitali KCMC etc nahisi maumivu yanawaanza taratibu, wateja wengi watakuwa wameshakimbia mawodini. Huyo Babu anapata hata muda wa kula kweli?
 
Mhhh!!!
Huyo babu anatakiwa kuapply demand na supply theory....demand ni kubwa sana, inabidi apandishe bei ili aweze hata kutengeneza mazingira ya kituo chake!

Amepewa kwa neema na anatoa kwaneema.

Yawezekana walengwa walikuwa ni majirani zake wa kipato cha chini...

Mungu amzidishie ili kila mtu aweze kuaford matibabu..
Big up babu!
 
Serikali makini tayari ingeshakuwa imeanza kuboresha miundo mbinu uko!na kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kupata dawa.
Nasikia kuna meli inatoka ughaibuni imekusanya nyomi la kuja kutibiwa!
 
Back
Top Bottom