Bwana Mziwanda, hayo yote uliyoyaelezea ni uongo mtupu??! Sijui hata hizo info umezitolea wapi?
-kwanza kabisa nyumbu haitwi wild beast? Bali anaitwa wildebeest.
-pia hana michilizi kama ya punda milia,kwani punda milia michilizi yake(stripes)ni Nyeusi na nyeupe.
-kwa jina jingine haitwi zero brain hilo jina umembatiza wewe tu.
- kwa taarifa yako wanyama wanaoliwa(herbivores) hawawaogopi wanyama wanaokula nyama(carnivores) kwani wameishi pamoja miaka nenda rudi.unapomuona nyumba kamkimbia simba na mbele kidogo anasimama haimaanishi kuwa amesahau bali wanachofanya huwa ni ku keep distance ambayo atajiona kuwa yuko salama kwani simba anapotaka kuwinda huwa kuna sign ambazo hawezi kuzificha zitakazo muonyesha mliwa kuwa yuko hatarini hivyo uamuzi wa mliwa ni either kukimbia au kuzidi ku keep distance. Na signal anazo zionyesha simba ni pamoja na concentration, shorten distance,squatting nk. Kwa kufanya hvyo mliwa lazima achukue tahadhali.lkn kama simba anapita zake bila kuonyesha moja ya signal hizo basi huyu mliwa hana haja ya kukimbia kwani wanajuana tokea zamani sna.simba akiwa na njaa ni lazima aonyeshe signal hizo nilizozitaja hapo juu.
- pia pembe hizo sio za nyati bali ni za nyumbu mwenyewe ila zinataka kufanana na za nyati.
Kwa faida ya wengine pia. Huyu nyumbu sifa yake nyingine ni pamoja na kuwa na uwezo wa ku locate mvua umbali ka km 50.wakisha jua hilo eneo linamvua bali huama na kuelekea huko na ndio sababu kati ya maajabu ya dunia kwa Tanzania tuna uhamaji wa nyumbu(wildebeest migration)ambao huama kutoka mbuga ya serengeti na kuelekea Masai mara(Kenya) na idadi yao wahamapo yapata nyumbu milion 3 pamoja na punda milia.
-pia umbali wanao zunguka kuhama eneo moja kwenda jingine wanakimbia umbali wa km 5000(elfu tano) ili kukamilisha mzunguko wote.
-sababu inayowafanya wahame ni utafutaji wa chakula, maji na malisho mazuri.
-nyumbu hawezi fanana na fisi hata sku moja
Karibuni wadau kuhusu kuuliza swali lolote kuhusu wanyama wa porini na sifa zao. View attachment 210146View attachment 210148
apo kwenye kutoogopana ndo kuna swali, kweli nyumbu hamwogopi simba? sasa huwa wanakimbia nini? kizazi cha nyumbu kiko vp? je wanazaana kwa msimu au ni rapid?