Mama yetu adhalilishwa

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,706
ny65x5.jpg

Jamani wamama wetu wanaendelea kudhalilishwa...haiwezekani mama yetu kama huyu adhalilishwe kiasi hiki na sisi tunaangalia tu.....imagine watoto wake wanaangalia mama yao anavyodhalilishwa hivi jamani...inatia uchungu sana.....natoa wito wa wamama wana sheria wa kituo cha haki za binadamu kuangalia na hili sio ku deal na kesi yab Lulu tu......
Eti wanasema walikuwa wanacheza mziki wa taarabu...sawa sasa ndio wadhalilishwe hivyo na magazeti ya udaku jamani.....
 
Yo Yo mbona kama amejifunua mwenyewe?
 
Last edited by a moderator:
Sioni kama amedhalilishwa wakati nguo kafunua mwenyewe na alikuwa anajua fika kuwa watoto wapo pale.
 
Utamu wa ngoma sharti Ucheze mama baada ya kunogewa na utamu wa muziki wa Taarabu akaamua kujiachia mwenyewe gazeti la udaku hapa lina makosa gani ????? mwanadamu unapaswa kuwa na Staha katika mambo ya dunia ya leo dunia imepanuka watu wameongezeka wengine hawaoni busara kucheza ngoma mpaka wavue wabaki watupu zote ni burudani wengine wanavaa khanga moja wanaita khanga ndembendembe au khanga moko watu wenye akilizao wanalipa pesa kuangalia hayo madudu na hao ni dada zetu tunaishi nao majumbani mwetu dada zetu mama zetu mama zetu lakini hatuwaulizi haya wayafanyayo ni mazuri kwa jamii ya Kitanzania????????????????kwa vile wao wanayafuraia wacha tuwaone kupitia mitandao ya kisasa.Mujwahuzia
 
Ona hao watoto jamani walivyoshangaa!!!!!! Na nyie waandishi wa habari jamani muangalie na picha za kupiga kwa ajili ya public view, hiyo si haki kabisa huyo ni sawa na mama yako huenda hapo ni pombe ndiyo imem- drive kufanya hivyo, akiona baada ya pombe kumtoka anaweza kuchangayikiwa
 
Ndio, amejifunua mwenyewe. Ni sawa kuwa anajipa raha mwenyewe, lakini anachohoji Yo Yo ni je, jamii inastahili kuwa na michezo kama hii hata kama watu watakuwa wanaicheza kwa hiari ya moyo, hasa inapochezwa hadharani mbele ya watoto wadogo kama hao?
 
Last edited by a moderator:
au na wewe unashabikia mama zetu wapendwa kudhalilishwa hadharani aisee?
Yo Yo mbona wataka kuniunganisha na magazeti ya udaku katika lawama wakati mie nimeuliza tu swali? Wala sishabikii hata kidogo udhalilishaji wa aina yoyote ile. Napata shida tu kuelewa kuwa hapo mbele ya watoto wadogo nani alimfunua huyo dada? Ni magazeti ya udaku au yeye mwenyewe?
 
umesomeka dadake.....
 
Ona hao watoto jamani walivyoshangaa!!!!!! Na nyie waandishi wa habari jamani muangalie na picha za kupiga kwa ajili ya public view, hiyo si haki kabisa huyo ni sawa na mama yako huenda hapo ni pombe ndiyo imem- drive kufanya hivyo, akiona baada ya pombe kumtoka anaweza kuchangayikiwa
Je kama mwandishi ni mwanamke mwenye umri kama huyo mama utasemaje ni sawana mama yake? Hapa suala la msingi ni kwamba huyo mama kajidhalilisha mwenyewe sasa mwandishi ana kosa gani kuwashirikisha wale ambao hawakuwa kwenye tukio? HAPO KAJIDHALILISHA MWENYEWE HANA WA KUMLAUMU
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom