Mama yangu kapata stroke mke hataki kumhudumia

Mimi nilichofanya niliacha kumjulisha hali ya mama na nimeendelea kumhudumia mama kwa njia ninayoijua mimi. Just ignore her wewe endelea kumhudumia Mama yetu tu. Tunamwamini Mungu atapona

Samahani mkuu mimi naona nisingeweza kua act kama tuko ok kumbe ndani naungua!!!!
Ningejiona mnafiki
 
Kabla hatujarukia kumsema mkeo kuna mengi hujaweka bayana:
1. Je mkeo ni mfanyakazi au mama wa nyumbani?
2. Kama ni mfanyakazi, je ana dhamana ofisini kwake?
3. Mnaishi nyumba ya kupanga au ya kwenu?
4. Je mna nafasi?
5. Je mna uhusiano imara na mkeo? Maana usitegemee ubabe wako, ubahili wako,kukosekana kwa maelewano kwenu kwa sababu ni mkeo basi lazima amhudumie mama yako.
6. Je mna watoto na wategemezi wengine ndani ya nyumba?

Vitu vingi vinamfanya mkeo pengine akatae. Je mumewahi kukaa naye na kumwuliza kwa utaratibu ni kitu gani kinamuogofia kumhudumia mgonjwa badala ya kumlaumu na kumwona mke asiyefaa?

Binafsi nina rafiki ambaye mama mkwe amepata stroke na yupo kwake ila sasa yeye ni mtu mkubwa ofisini kwao. Cha ajabu mume anamtaka yeye aache kazi akamhudumie mama mkwe wakati ana madada wengi ambao wote wamejikalia makwao hawataki kumjulia mama yao MZAZI hali. Rafiki yangu amemweka msichana wa kazi kwa ajili ya mam mkwe. Anachofanya ni kuhakikisha anarudi mapema na kumtembeza mama mkwe afanye mazoezi ya kutembea. Ila nalo mume hana shukurani maana yeye ameshaachishwa kazi na anamtegemea mkewe. Je upo katika kundi hilo??

Nina ndugy yangu naye mama mkwe alipata stroke. Walichoamua na mumewe ni kutoa nafasi ili aangaliwe pale kwao. Na ndio walikuwa wameanza maisha tu. Ila sasa walikubaliana na wifi zake wawe wanakaa pale wanamwangalia mama mkwe maana yeye ni mfanyakazi. Mawifi walikubali kwa moyo mweupe. Kwa foleni za bongo yeye alikuwa anafika kwake saa 2 usiku. Jumamosi akienda kazini basi akirudi saa 10 na huku apitie saloon kidogo au aende sokoni. Jumapili akitoka kanisani yeye ndio anamwangalia mama mkwe na mambo mengine. Cha ajabu hawakufurahia eti anamkwepa mama mkwe. Maneno yakaanza . Mume kaona watu wanamwingilia ndoa yake basi wakakae kwa kaka yake mkubwa. Hapo ndio maneno yakazidi. Maana yeye ndio mwenye hela kwa nini asimfukuze mke amlee mama yake. Masikini mama akafariki ndugu wala hawakumwambia mdogo wao. Yote haya ni stress ya kumwangalia mgonjwa.

Sasa mdogo wangu (nasema hivi kwa kuwa nahisi wewe utakuwa mchanga kwenye ndoa. Kama la nisamehe), mkeo labda ana experiences kama hizi na ndio maana anaogopa. Kwa nini msiongee mkayamaliza na mkatafuta suluhu. Kwani huna mama zako wadogo? Mama yako hana mawifi? Kuwa mtoto wa kiume haina maana wewe ndio ubebe mzigo wote. Jadiliana na ukoo na familia unaweza ukapata suluhisho. Usimtangaze mkeo kuwa hataki kumhudumia mama yako bila kujua chanzo.

Dunia tambara bovu. Na ndoa ni safari ndefu
Yawezekana ulishawahi kumkatalia na yeye basi analipiza kisasi. Yote hujatuambia. Nadhani katika haya machache niliyoandika jibu utalipata.

Pole kwa kuuguza mama.
 
Kwa nini asivunje?????

Kwa sisi wakatoliki, ndoa haivunjwi kirahisi hivyo. Hakuja kumtunza mama yako, amekuja kwa ajili ya wewe tu. Ikitokea akawa mwanamke mwema basi ni bahati. Najua of course kwa kutomhudumia, mke wake ameweka doa kwenye ndoa, naye yakimfika mume hatashughulika.
 
binadamu wengine kazi sana ajiulize ikimtokea yeye akafanyiwa hivyo ......kama una ndugu karibu unaweza mchuku kuishi nae kusaidia kwa muda huku mkifanya mchakato na familia yako namna ya kumtunza mama...pole sana kwa kuuguza

Na asifikiri ni mzaha yatamtokea mabaya zaidi ya hayo na atashangaa hakuna atakayetokea kumsaidia!
Mlioana kwa matamu na machungu ni lazima kuvumiliana. Angekuwa mwepesi basi angetafuta mtu wa kumhudumia mkwewe mapema sio kupandisha kiburi. Si ajabu hata hilo tatizo limesababishwa na yeye.
 
Wadau wenzangu nimeamua kiliweka hill hadharani ilimnipe ushauri.mama yangu mzazi
amepata stroke upande wa kushoto ni MTU wakuhitaji kulishwa kugeuzwa isipokuwa Mke niliye nae hataki kumpa msaada wowote so kumgeuza wala kumuosha.hivyo wadau naombeni ushauri nifanye nini.

Pole sana kwa kuuguza na pole ya mama kwa maradhi yanayomsumbua.

Rafiki yangu anamatatizo ya mgongo yaliopelekea kulazwa hospitali kilomita 120 kutoka kijijini kwao kwa mwaka mmoja sasa, hawezi hata kujigeuza. Desemba iliopita nikiwa likizo nilifunga safari ya kilomita zaidi ya 500 kwenda kumuona, nilikuta anauguzwa na mtoto wa kaka yake ambaye ki umri ni mdogo sana; alikuja kumuona baba yake mdogo miezi mitatu iliopita na kwa hali aliomkuta nayo mgonjwa, alijisikia huzuni kubwa sana iliompelekea kuamua kuwa pale kwa wakati wote huo na kwamba ataendelea kumuuguza baba yake mdogo mpaka siku atakaporuhusiwa; ilikuwa imepita miezi miwili na hakuna ndugu yeyote mwingine aliyekuwa amewatembelea, ingawa mgonjwa ana wazazi, makaka, madada na mashemeji. Wanasaidiwa mahitaji na wagonjwa wengine wenye mioyo ya huruma.

Swala la kuuguza au kusaidia kwa namna yoyote ile ni moyo wa mtu husika,usimlaumu yeyote katika hili; watu hutofautiana kwa namna walivoumbwa, awe mkeo,mtoto wako, mama yako, au ndugu yako yeyote yule. kila mtu yupo tofauti. nakushauri usichukie wala kugombana na mkeo au yeyote yule katika hili, zaidi angalia namna tofauti ya kuweza kumsaidia mama.

dalili za kujua mioyo ya watu waweza kuliona hata kwa watoto wako au kwa ndugu na jamaa zako wa karibu. Kuna watu wanaoguswa na matatizo, na wapo wasioguswa.
 
MKU ACHA UJINGA UNAOAOA TU BILA KUFANYA INTERVIEW HAYA SASA YAMEKUKUTA..weka mfanyakaz wakike amsaidie mama.
 
Pole sana kaka ndivyo wanawake wa kisasa tulivyo.tunapenda ndoa ila yaliyomo kwenye ndoa hatuyataki..huyo mkeo amesahau kiapo alichokitoa cha kuishi kwenye shida na raha..kipindi cha raha mapenzi yanakuwepo cha shida mtafutano.shida ambazo alihaidi kukabiliana nazo hiyo ni moja wapo .tafuta mtu ambaye atakusaidia kumtunza mama.kama ni ndugu au hata mtu baki.wakati ukimshauri mkeo .kamwe usikubali kumwacha mama ateseke.binadamu hujafa hujaumbika leo kwa mama kesho kwake nan atamsaidia.dahhh....

Una hekima sana Mungu akuzidishie...!
 
Nakubaliana na mkeo kabisa ungeumwa wewe akakataa kukuhudumia kweli lkn mama yako, uguza mama yako wewe suala la kuuguza si mchezo mdogo, namtetea huenda mna ndugu wengi lkn mnataka kumtwika yy msalaba wote wa kuuguza, je ingekuwa na mama yake anaumwa ungemuuguza wewe? Wanawaketunapitia ktk mitihani mingi sana mkeo anayakumbuka labda ya zaman sana kuhusu wewe au familia yako ndio anaamua kufanya hivyo kuna mahali kwa namna moja au nyingine wewe na familia yako mlimtenda,timizen wajibu wenu wa kumuuguza mgonjwa sio kumpa misalaba mwan wa mwenzenu
 
Nakubaliana na mkeo kabisa ungeumwa wewe akakataa kukuhudumia kweli lkn mama yako, uguza mama yako wewe suala la kuuguza si mchezo mdogo, namtetea huenda mna ndugu wengi lkn mnataka kumtwika yy msalaba wote wa kuuguza, je ingekuwa na mama yake anaumwa ungemuuguza wewe? Wanawaketunapitia ktk mitihani mingi sana mkeo anayakumbuka labda ya zaman sana kuhusu wewe au familia yako ndio anaamua kufanya hivyo kuna mahali kwa namna moja au nyingine wewe na familia yako mlimtenda,timizen wajibu wenu wa kumuuguza mgonjwa sio kumpa misalaba mwan wa mwenzenu
Naomba ukisome hiki ulichoandika.....inawezekana kabisa ukatetea kitu kama hicho...kwahiyo mipaka ya huyo mke inaishia kwa mmewe tu linapokuja swala la kumhusu mama wa mme si jukumu la mke...labda sijakuelewa........
 
Mleta mada umeulizwa kuhusu mahusiano baina ya mama na mkeo kabla mama hajaumwa naona unapotezea tu, Inawezekana unajua chanzo cha tatizo.
 
I wish ningezaliwa hata na dada au kaka.kuzaliwa pekee ni taabu sana,tena sana

Pole sana mkuu kwa kuuguliwa na mama. Mke wako anakosea sana, hamna anayeomba kuumwa...kwa kuwa umesema ni mtoto wa pekee huna dada wala kaka, si vibaya ukafanya kama wadau walivyoshauri hapo juu kumtafutia mtu wa kumhudumia mama katika kipindi hiki, hata ndugu zako wengine mf. binamu nk.. kama wapo pia. Ila pole sana, Mungu yupo na wewe.
 
Hata kama walikuwa na ugomvi....linapokuja swala la ugonjwa unaweka tofauti zenu pembeni unamhudumia mgonjwa......huyo mwanamke ana roho mbaya tu.....

Unachokiongea ni IDEAL lakini kuki practise ni ngumu sana.
 
binadamu wengine kazi sana ajiulize ikimtokea yeye akafanyiwa hivyo ......kama una ndugu karibu unaweza mchuku kuishi nae kusaidia kwa muda huku mkifanya mchakato na familia yako namna ya kumtunza mama...pole sana kwa kuuguza
Mimi naunga mkoni hoja hii ya huyu bwana n I suggest more more kwakua wewe ndio baba let her know that kupona kwa mama yako mzami ndio tiketi yake ya kusepa ila kama unamoyo hii itasaidia kumuweka akae sawa muulize kama anakumbuka maneno ya kwenye ndoa "KWA SHIDA NA RAHA" sasa yeye anadhani shida ni ipi labda ndoa imemshinda,sikatai ni kazi ngumu but who else can do je angekua mama yake angefurahi??
 
pole sana kwa kuuguza,, usimuoneshe hasira sana
mkeo ila ukiweza muweke mbali maana anaweza kumdhuru mama yako.. pole sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom