Mama yake Zitto avamiwa


Kutokana na habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la leo kuhusumajambazi kumvamia Mama Shida Salum na maelezo yake ambayo ameyatoa ni kamaifuatavyo;

i. Lengo kuu ni kuwa Polisi watamkamata Hemed Sabula, ambaye CHADEMA walimtumia kumrekodi Afisa usalama wa Taifa ambaye alikuwaanaanda ushahidi feki wa kumhusisha Lwakatare na ugaidi ……na tayari Polisiwameelekezwa kufanya hivyo kesho .

ii. Usalama wa Taifa , wameamua kulipiza kisasi kwaCHADEMA baada ya kurekodiwa na wanataka kujua walirekodi nini na hichowalichorekodi kipo wapi, hivyo Sabula atateswa sana ili aseme aliwezajekuwarekodi

iii. Zoka Jack , alifanya mawasiliano na ambaowalihusika katika kuandaa na kuandika habari hiyo na mwandishi alikuwaakielekezwa kila kitu, na ndio maana hajawahoji polisi kama suala hilo likokwenye uchungiuzi ama laa , na leo au kesho polisi watatoa tamko kuhusiana nasuala hilo na kuwa wanaendelea na uchunguzi na watamkamata Sabula, swaliatakaloulizwa ni kuwa mbona yeye aliuliza swali kama walivyofanya majambazi haowa kutungwa

iv. Sabula mawasiliano yake ya simu yamefanyiwa kazina baahati mbaya ameonekana kuwa hakumuuliza mama Zitto swali hilo la kuwaanatoa wapi fedha za kuzunguka nchi nzima ,ila alimuuliza juu ya kamaanawafahamu watu hao ama kama alishawahi kuwaona naye akamwambia atarudi kwakebaadae na hakuna ushahidi wa kimawasiliano kama alirejea tena kwake na badalayake akaenda kuongea na vyobo vya habari.

v. Kuhusu kwamba kijana mmoja ni mtu kutoka Tanga ,yupo kijana mmoja anaandaliwa anaitwa Khalid atakamatwa kwa hatua za baadae ,na huyu tayari ameshaandaliwa kimkakati.

Nawashauri CHADEMA wafanye yafuatayo kwa hatua za sasa;

a. Hakikisheni kuwa kuanzia leo mnaweka mawakili wenu kwaajili ya kuhakikisha kuwa Sabula haendi polisi peke yake ili asiteswe

b. Hakikishenikuwa mikanda mliyowarekodi watu wa usalama inawekwa mahali salama kwaniinatafutwa kwa gharama kubwa sana ili iweze kuandaliwa majibu.

c. Wapo watuambao mpaka sasa wanaweza kupoteza kazi kutokana na sakata hili , jiandaenikuwatetea …..

Naishia hapo kwa leo.

bacelona, usicheze mchezo ambao hutaweza kuumaliza. katika kila nchi ukitaka kuchezea vyombo vya usalama basi uhakikishe kuwa wewe ni msafi vinginevyo utajuta kwa nini uliuanzisha
 
haya ni maelezo ya mama zito:siku kazaa kabla ya tukio kunamtu alinipigia simu na alijitambulisha kuwa yeye ni mwanachama wa chadema tawi la tabata relini na kuniomba msaada wa mifuko miwili ya saruji kwa ajiri ya kukalabati jengo la ofisi yao.nilikubali kuwasaidia bila kuwa na fikra kwamba ni watu wabaya hivyo walikuja nyumbani na nikawakalibisha ndani na kuwaeleza kuwa nitawapatia 20000 na wao waongeze 10000,niliposimama kuelekea chumbani kuwachukulia kiasi hicho cha fedha mmoja wao alitoa bastola na kunielekezea kichwani huku akieleza kuwa hawana shida na pesa bali wanatka laptop,flash na simu yangu kwa sababu zinamambo muhimu.
Namheshimu mama Zitto lakini kiukweli hii hadithi mh!!
1)Anasema majambazi wamemvamia saa moja na nusu asubuhi!, anawtambua,ina maana hawakuvaa hata vificha sura..inawezekana?
2)Akatekwa na bastola, wakamwambia tupe laaptop na flash hatutaki hela, anasema nikamwita kijana “AWALETEE“..
Hivi inawezekana jambazi akuteke af akuruhusu kuita watu wengine?
3) yule kijana alipowaona na bastola akakimbilia chumbani nao wakakimbia wakatoroka,
inawezekana hawa majambazi walitegemea huyu kijana awe anatabasamu anapowaletea hiyo computer?
Hawa ni majambazi au wafanya maigizo?
..anyway, najiuliza tu
 
Habari kama hizi siyo za kupuuza

Mmmh kweli nimekubali CDM ina mtandao kutokea Ikulu hadi kwa Mwenyekiti wa kitongoji! Lakini njama zote hizo hazitakaa zifanikiwe kwani mungu ni mkubwa kwa majaribu yote chama kiliyoyapitia tungekuwa tunaongea mengine. Mzee wa Vuta Nkuvute upo! Kazi ya Lumumba kwa kushirikiana na TISS na mwaka huu mtaumiza vichwa sana kinachotakiwa ni kutekeleza ahadi mlizowahaidi wananchi na si vinginevyo! Huku Bukoba hatujaona meli aliyoahidi Mzee wa kaya na mpira ndo umebaki dakika 10 refa apulize kipenga sijui 2015 mnakuja na staili ipi tena. Ule mtaji wenu wa kushinda kupitia vijijini nako wameshawastukia. "HUWEZI KUWA NA AKILI TIMAMU UKASEMA UNAIPENDA CCM"
 
Namheshimu mama Zitto lakini kiukweli hii hadithi mh!!
1)Anasema majambazi wamemvamia saa moja na nusu asubuhi!, anawtambua,ina maana hawakuvaa hata vificha sura..inawezekana?
2)Akatekwa na bastola, wakamwambia tupe laaptop na flash hatutaki hela, anasema nikamwita kijana "AWALETEE"..
Hivi inawezekana jambazi akuteke af akuruhusu kuita watu wengine?
3) yule kijana alipowaona na bastola akakimbilia chumbani nao wakakimbia wakatoroka,
hawa ni majambazi au wafanya maigizo?
..anyway, najiuliza tu

Mkuu, hapa kuna-more than 100 questions !
 
Umejiunga leo JF maalum kwa ajili ya ku-preempty tukio hili siyo, tumeshakushtukia . Ni dhahiri kabisa wewe ni mmoja wa walioandaa mkakati wa Mama ZITTO kutekwaa na hata hao unaowataja kuwa watakamatwa huenda mmoja wao ni wewe

mkuu, wanaweweseka sana hawa. naona dili lao limebumbuluka sasa wana anticipate matokeo. huyo sabula lazima akamatwe na mbowe pia awajibike kwa kupanga mpango huo mbaya wa kudhuru watu
 
Kukosa uongozi bora na siasa safi ndio matokeo ya haya yote. Pamoja na kwamba tumebadilisha mfumo wa mawasiliano toka analogia kwenda digitali bado viongozi wetu wa CCM wamekwama kwenye kwenye tope la analogia. Na hata gia ya four wheel drive itashindwa kuwaoa hapo. Hawa vijana wa siku hizi akili zao zina-google,zina-androidi, na kublakiberi fasta fast zinachunguza,zinatenda na kusema fasta fasta. Syndicate za kufanya umafia hawasomi kwenye vitabu ila wanazipata tokaka kwenye mitandao. Mnaona wenyewe mmempeleka Diamond kwenye jukwaa halafu kule hadhira inaridhima kwa uwepo wake! Kdiri mnavyowasingizia na kuonyesha kuwagandamiza ndivyo na wao wanavyotengeneza njia nyingi za kutoa. Nyie mnawaona wameingia kwenye shimo halafu mnavizia mnasimama na marungu hapo juu ya shimo,mnapongezana kwamba hawa wamepatikana sasa.

Mnasubiri hapo juu ya shimo ili wakirudi mponde vichwa. Sasa na wao kumbe wanatumia fahamu ya sita, hawakurudi wako ng'ambo ile wanawaangalia wanacheka tu.Hawana mbavu! Kuna mambo viongozi wa CCM mmeanza ya kusingiziasikingizia hivi. Mara udini,mara ufamilia,mara ukanda mara uchagga,mara hawa wanataka kwenda ikulu kwa kumwaga damu. Mdhani kuwa hawa vijana watakubali kweli na hayo mwazo ya ki-ipadi na kiblakiberi? Ni kama mnawaonyesha ili uweze kula nyama unanoa shoka liwe kali kwa ajili ya kukata hiyo nyama. Lakini kwa bahati mbaya wao wanaenda mbele zaidi wananoa kisu kinakuwa kikali. Sasa nani atakula nyama kwa urahisi hapo? Je huu si ndio mkwamo kwenye tope la analogia? Namna ya kupamba na hawa vijana ni kuibana serikali ichape kazi na kusimamia sheria bila upendeleo-aliyeiba billioni 40 EPA na aliyeiba kuku wote wawe lipango. Kuzika "impunity" kama kiongozi akifanya kosa na au akishindwa kuwajibika katika eneo lake la kazi ajiondoe mwenyewe.Hii ni benki kubwa yenye mtaji mkubwa sana kwa CCM lakini cha kushanagaza CCM wanakimbilia kwenye KI-SACCOS kule Tandale kutafuta mtaji!

Nionavyo mimi CCM na viongozi wake wameacha ile misingi iliyokijenga chama tangu uhuru na kukumbatia mambo ya hovyo yanayopingina na misingi yake na ndio maana hata mambo yanayofanywa na viongozi wa CCM sasa hivi ni ya hovyo hovyo. Baada ya miaka hamsini ya uwepo wa CCM inaonekana imerudi nyuma na kuanza kunyonya DOLE GUMBA na lugha tunayosikia ni ile, ya tha !tha! that! Huu ni mkwamo wa kwenye analogia na haya matukio ya kutekana yataendelea tu. Maana hata analogia wakianzisha jambo, hawa google-blakiberi watalipa "perfection". Au wale waingereza wanasema "you get beaten on you own game". Amekeni CCM tokeni kwenye hiyo analogia! Achaneni na kunoa mashoka kwa ajili ya kula nyama, visu(siasa safi na ungozi bora na makini) ndio kifaa sahihi cha kukata kitoweo bila kutumia nguvu kubwa!! Ni ushauri tu
 
Kishili si kweli, zitto kalewa sana sifa mpaka sasa anataka kuharibu chama, kwa taarifa yako zitto anatumika sana na magamba.
 
Yaani hawa jamaa zangu wangekuwa na bidii hii hii katika kutatua matatizo ya watanzania aisseee tungekua mbali
 
Sijui Mh. Zitto amewakosea nini viongozi wenzake wa CHADEMA.

Pumbaf!!

Wewe ndio mmojawapo ya Watanzania majuha wanaotumiwa na CCM kuichafua CHADEMA.
Mambo ni yaleyale ya kina Kibanda kung'olewa kucha na macho halafu anasingiziwa Lwakatare wa CHADEMA!!!!Kweli CCM imejichokea maana kwa sasa inafanya vihoja.

Kwa watu makini na Great Thinkers this is just a CCM game! Believe it or not. Kwamba wamekodishwa vijana kwa kupewa uchache na Mwigulu au Nnepi ili wakamvamie Mama Zitto wakitaka Laptop na Flash na kujifanya kuwa mmoja wao ni KIGOGO wa CHADEMA!!!Ili baadaye ionekana kwamba CHADEMA wanaendeleza ugaidi kwa mama yake Zitto!!

Nasikitika hata kwa Mhe.Zitto kulichukulia swala hilo juujuu kana kwamba na yeye anajua kinacho endelea. Siamini maneno ya Zitto kuwa ni swala la Kipolisi na litashughulikiwa kama matukio mengine...!!!Are you serious Mr. Zitto? Hivi kesi za kina Dr, Ulimboka na Absolom Kibanda zinashughulikiwa vipi na Polisi kama siyo usanii tu huku watu wakiwa wamepoteza viungo vyao???

Ushauri wangu kwa Zitto Kabwe na Uongozi wa CHADEMA ni kwamba haya matukio ya kuvamiwa,kutekwa,kuteswa na hata kuuliwa yanayotokea kwa sasa hapa Tanzania si ya kuupuzia hata kidogo. Tumeshaona kuwa kuna mkono wa Serikali ya CCM katika haya na juzi Steven Wassira amethibitisha kuwa UWT wanawalenga Viongozi wakuu wa Upinzani aidha moja kwa moja au kwa kupitia mtu yeyote wawe wafuasi wa chama,Waandishi wa habari kama Kibanda au Wafanyanyakazi wa kada zingine kama kina Dr.Ulimboka.

CHADEMA msijaribu kupuuzia vitu kama hivi na kuvichukulia lightly kama utani. You have to know kuwa CHADEMA mko vitani na adui yenu amejidhihirisha wazi kuwa ni CCM na Serikali yake. Kwa vile CCM ana dola ana uwezo wa kutumia kila chombo na Mamlaka aliyo nayo ili kuwamaliza. CCM bado ana uwezo wa kupenyeza mashushushu ndani ya CDM kwa kujifanya ni wanachama wanaohamia kutoka CCM kumbe ni maadui au chui waliovaa ngozi ya kondoo!

CHADEMA wake up men and be serious! Kweli mkifanya mchezo mtakwenda na maji maana NGUVU YA CCM NA SERIKALI YAKE IMEELEKEZWA KWA CHADEMA ILI KUISAMBARATISHA KABLA YA UCHAGUZI MKUU WA 2015.

Hiyo ndiyo Habari.
 
bacelona, usicheze mchezo ambao hutaweza kuumaliza. katika kila nchi ukitaka kuchezea vyombo vya usalama basi uhakikishe kuwa wewe ni msafi vinginevyo utajuta kwa nini uliuanzisha

Wewe ni nani??? kwenda huko!!!!Mnatishia watu wasiseme maovu yenu!!!!
 
Niyaonayo katika utunzi wa gazeti la MTANZANIA la leo

"SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe." (Sentensi hiyo haina ubishi. Huyo ni mama yake Zitto, hata Zitto mwenyewe amekiri hivyo, ingawa wakati mwingine anajulikana kama Mama Lulu au Mama Salum)

"Amenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakiwa na silaha za moto." (Kama alivamiwa, inawezekana kweli ni majambazi. Lakini habari inatuambia walikuwa na bastola. Hakuna silaha nyingine iliyotajwa. Lakini ili kutia chumvi, mwandishi anasema walikuwa na "silaha za moto.") Tazama chumvi inayokolezwa. Katika utangulizi wa habari yake, Mtanzania limeandika "watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi". Acha tu nikubali inawezekana ni majambazi, lakini gazeti hilo hilo, katika ukurasa huo huo, linatilia mkazo kuwa watu hao ni "wauaji". Linaandika hivi katika blabu yake: "Wauaji wamdai laptop, flash na simu yake." Sasa gazeti hilo hilo linajichanganya. Majambazi wanaweza kuwa wauaji pia, lakini siyo kila muuaji ni jambazi. Sasa hao ni majambazi au wauaji? Chumvi yote ya nini?

Habari zilizolifikia MTANZANIA Jumatano kutoka kwa watu walio karibu na mama huyo zilieleza kuwa, vijana hao walifanikiwa kumfikia akiwa katika sebule ya nyumbani kwake na kumuelekezea bastola kichwani, huku wakimlazimisha awakabidhi baadhi ya vifaa vyake vya kufanyia kazi na simu yake ya kiganjani. (Vijana hao hawakugonga geti wala mlango. Na mama huyo aliwashtukia tu wako sebuleni.)

"Akizungumza na MTANZANIA Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tukio hilo, mama yake Zitto alisema ni kweli lilitokea na amekwisharipoti katika kituo cha Polisi cha Buguruni." (Mama huyo ndiye aliyepiga simu kwa mwandishi au mwandishi ndiye aliyempigia mama huyo? Ilivyo ni kwamba mama huyo ndiye aliyepiga simu. Na hii ni baada ya kudai kuwa amesharipoti polisi. Kwanini gazeti la Mtanzania na hakupiga kwenye magazeti mengine? Hakuna chombo kingine chochote cha habari kilichopigiwa simu. Hakuna hata namba ya RB ambayo mama huyo alimpatia mwandishi. Na mwandishi huyu alivyo, wala hakuuliza namba ya RB. Ndio waandishi tulio nao sasa. Mwandishi huyo amekosa hata umakini wa kutuambia tukio hilo lilitukia wapi, ingawa ametaja tarehe na saa. Hapa kinakosekana kiungo muhimu sana cha uandishi kinachojulikana kama WHERE).

Mama Zitto alisema siku kadhaa kabla ya tukio hilo alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa mwanachama wa Chadema wa Tawi la Tabata Relini na kumuomba msaada wa mifuko miwili ya saruji kwa ajili ya kukarabati jengo la ofisi yao. (Potelea mbali. Waliomba msaada wa mifuko miwili ya sementi halafu wanakwenda kuibeba na gari lao. Mafuta ni sh. Ngapi na sementi sh ngapi? wana uwezo wa kuendesha gari lakini hawana uwezo wa sh 30,000? Labda hiyo ni mbinu yao ya mauaji.)

Alisema alikubali kuwasaidia vijana hao kwa kuwataka wafike nyumbani kwake mapema siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, kwa sababu alikuwa na ratiba ngumu na ndefu siku hiyo. (Mhhhhhh).

"Lakini niliposimama kuelekea chumbani kuwachukulia kiasi hicho cha fedha, mmoja wao alitoa bastola na kunielekezea kichwani huku akieleza kuwa hawana shida na pesa, bali wanataka laptop yangu, flash na simu yangu ya mkononi kwa sababu zina mambo muhimu … nikamwita dereva wangu, Mtana, alete simu yangu niliyokuwa nikiichaji chumbani na flash ili niwapatie, wakati akielekea kuvichukua aliwaona walivyokuwa wameniwekea bastola, akakimbia moja kwa moja chumbani akajifungia na kuanza kupiga kelele, wakatoka haraka wakakimbia." (Haya. Dereva ndiye anayeitwa na kutumwa chumbani kwa MWANAMKE huyo? Kwanini wamruhusu azungumze na dereva wakati wangeweza kumburuta hadi chumbani na kumnyang'anya walichotaka?

Alisema anaweza kuwatambua watu hao akiwaona na kwamba mmoja wao si mgeni machoni mwake, kwa sababu aliwahi kumuona mkoani Tanga katika moja shughuli za chama hicho. (Si walimpigia simu. Si anasema hawakufanikiwa kuchukua simu yake. Hiyo namba, au hizo namba, walizotumia kumpigia si zipo? Alizikabidhi polisi? Mbona ni rahisi? Waliwasiliana naye na bado walifika kwake na bastola kama walivyoahidiana. Kwanini namba hizo zisiandikwe gazetini?)

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, naye hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni, mahali ambako Mama Zitto ameripoti tukio hilo naye hakuweza kupatikana. (Kweli? Ni kweli haya? Kwanini mwandishi aende kwa Kova wakati tukio liko Buguruni?) Hizi ni propaganda za kuwababaisha wananchi waone kuwa kuna matukio yanayopangwa na Chadema. Nachukia siasa na uchafu wake, lakini wanasiasa wachafu wanaotumia vyombo vya habari nawachukia zaidi. Tusubiri Mtanzania Jumapili na Mtanzania Jumatano kuhusu habari nyingine za Chadema. Hizo ndizo habari pekee walizonazo kwa sababu ya njaa. Nasikia hao jamaa wana njaa sana ndiyo maana wakihongwa kidogo tu wanaandika chochote bila kufuata maadili yao ya uandishi.
 

Kutokana na habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la leo kuhusumajambazi kumvamia Mama Shida Salum na maelezo yake ambayo ameyatoa ni kamaifuatavyo;

HIvi chadema mtajaribu ku-preempty matukio mpaka lini? Na hili nalo? Jamani oneni aibu, matukio haya sasa yamezidi chukueni maamuzi mageumu ndani ya chama badala ya. Kukingia kifua mambo ambayo yako hadharani kiasi hiki
 
Hii ni Mwigulunism kabisa ni mbinu chafu za kutaka watu waamini kwamba Chadema kinamchukia Zitto Kabwe. Hakika siasa ni mchezo mchafu "hata dada aweza kuwa mke" But Zitto alivyotoa tamko lake hao waliodhamiria wangefanikiwa kum provoke Zitto wamegwaya. Safi Zitto
 
Mmmh kweli nimekubali CDM ina mtandao kutokea Ikulu hadi kwa Mwenyekiti wa kitongoji! Lakini njama zote hizo hazitakaa zifanikiwe kwani mungu ni mkubwa kwa majaribu yote chama kiliyoyapitia tungekuwa tunaongea mengine. Mzee wa Vuta Nkuvute upo! Kazi ya Lumumba kwa kushirikiana na TISS na mwaka huu mtaumiza vichwa sana kinachotakiwa ni kutekeleza ahadi mlizowahaidi wananchi na si vinginevyo! Huku Bukoba hatujaona meli aliyoahidi Mzee wa kaya na mpira ndo umebaki dakika 10 refa apulize kipenga sijui 2015 mnakuja na staili ipi tena. Ule mtaji wenu wa kushinda kupitia vijijini nako wameshawastukia. "HUWEZI KUWA NA AKILI TIMAMU UKASEMA UNAIPENDA CCM"

mkuu, kila kitu mnafanya kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. kumbe waziri mkuu Pinda hakukosea aliposema kuwa vichwa vya viongozi wa chadema vimeacha kufikiri kwa kuwaza uchaguzi wa 2015. ndo maana wanataka kumsimamisha mama yake zitto asimfanyie kampeni mtoto wake mikoani kwa vile mbowe anataka aendelee kuwa mwenyekiti wa cdm milele
 
Fumbo mfumbie mjinga mwelevu atlijua tu,sasa chadema naanza kuona kuwa ni chama cha waongo na wazishi huwa sipendi kuzungumzia vyama ila katika hili acha nitaje chadema watanisamehe haiwezekani wanatuchezea akili kama sisi ni ma ndondocha kila siku wanasema zito anawasiliana na viongozi wa usalama wa taifa na ni mamluki eti anatumiwa na ccm na usalama wataifa hasa zoka leo tena mnatuambia eti mpango wa kuvamiwa mama zito umepangwa na usalama sasa urafiki wa zito na zoka umeisha lini?, fumbo mfumbie mjinga
 
Hii ni Mwigulunism kabisa ni mbinu chafu za kutaka watu waamini kwamba Chadema kinamchukia Zitto Kabwe. Hakika siasa ni mchezo mchafu "hata dada aweza kuwa mke" But Zitto alivyotoa tamko lake hao waliodhamiria wangefanikiwa kum provoke Zitto wamegwaya. Safi Zitto

mrembo, kama umekosa kazi nenda kauze mwili wako. hapa watu wanajadili issues. zitto anapaswa kutafakari yanayomtokea badala ya kukimbilia kuwatetea wahalifu. ipo siku atajuta
 
Naona mnacheza muziki msioujua kwa nguvu zote bila kujua kuwa mwisho wa siku mtatakiwa kutafakari kwa mtazamo mpana kuliko kutukanana ndani ya JF! Hii sio thread ya kutupiana matamshi kama ya Seru-rope!
 
Back
Top Bottom